Elections 2010 Dr. Slaa nyanda za Juu Kusini: Songea, Iringa, Mbeya (picha na habari)

Habari za kuaminika ni kuwa Dr Slaa atakuwa akifanya mikutato ya kampeni katika mji wa kyela kesho tar 3-10-2010. Kabla ya mikutano ya Dr slaa itakayofanyika vijijini, atafanya mkutano mkubwa Kyela mjini. Wote wenye mapenzi mema na Tanzania mnapaswa kuja kumsikiliza.

Strategy nzuri sana hii, lazima CHADEMA wapite sana huko ili wavune kura zote za vijijini huko.
 
Kuna kajanja kamoja kachwara kanadai kanatoka Iringa kamethubutu kutoa tathmini ya Uchaguzi wa October 31 kuwa Dr. Slaa ataambulia nafasi ya tatu baada ya Kikwete na Lipumba ! - sidhani kama hiyo Iringa yake ndio hii tunayoishuhudia hapa. Shame on you Maggid Mjengwa. Hata hivyo tusimpuuze, hapa kuna ajenda ya siri kwani matamashi ya jana ya Shimbo yanathibitisha hilo. Pamoja na hayo nina hakika mipango hii miovu ya kutaka kuleta machafuko nchini kamwe haitaweza kufua dafu mbele ya nguvu ya Umma kama giza lisivyoweza kustahimili mwanga.

Peoples Power will always prevail !

Please katendee haki. Kape jina stahili; ni kapuuzi fulani hivi.
 
Mbeya ni jimbo la Chadema na CCM wanalijua hili vyema kabisa. Na hii ndiyo sababu iliyowafanya CCM kupiga kambi ya nguvu Mbeya hadi bwana mdogo Rizone kupewa uchifu bandia. Mbeya ni jimbo la Chadema. Mwakyembe unafanyanini huko CCM?.
 
Ninafikiria sijui nishone suti ya rangi gani ya kuvaa siku ya kuapishwa kwa Dr Slaa. Nisaidieni jamani nivae rangi gani?
GO SLAA GOOOO....!!!
 
Pole sana PayGod. Vitisho kwa wasema ukweli ni kawaida hapa Tanzania. Tunawakumbuka waandishi kama yule wa BBC, mh. Kolimba na wengine waliosema ukweli waliuawa lakini mpaka leo tunawakumbuka. nadhani hofu imewazidi.

hATUDANGANYIKI.JPG
 
Mwandishi aliyeandika, kutimiliwa kwa ridhiwani iringa , apokea simu za vitisho

September 30, 2010

SITAZIBWA MDOMO KWA VITISHO ,NIPO TAYARI KUFA KWA KUSEMA KWELI DAIMA........

Mmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin

UPO usemi kuwa ukitaka kazi ya jeshi usiogope kufa na siku zote mkweli hutengwa wa waongo kama hivyo ndivyo basi kwa mara ya kwanza leo kwanza ninapenda kuanza kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ambaye amepata kunileta duniani na kuniongoza kwa kila jambo na kunilinda na maadui wangu kwa kuwapa roho ya upendo na huruma mwingi.

Pia napenda kuwapongeza wanahabari wenzangu wote wa Tanzania ambao tumekuwa nao bega kwa bega katika kuipasha habari jamii ya kitanzania kulingana na uwezo wetu kweli nawapongeza wote bila kuwasahau wakurungezi wenzangu ambao tunamiliki vyombo vyetu yaani Blog na Website .

mimi Francis Godwin kama mmiliki wa mtandao huu na mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima napenda kutumia uwanja wangu huu wa kujidai kueleza masikitiko yangu kwa wale wote ambao wameendelea kunipigia simu za vitisho kuhusiana na habari hii chini ya japo sijapokea simu ya wahusika wenyewe ila wapambe wa nje wameendelea kuwa na nguvu hata kutoa vitisho dhidi yangu kuwa iwapo nitaendelea kujifanya mkweli siku zangu zinahesabika .

Napenda kupingana na wote walionipigia simu nakutoa vitisho kama hivyo huku nikiamini kuwa kifo kwangu ni mipango ya Mungu na sitoogopa wala kuingia katika dhambi ya kusema uongo kwa jambo la ukweli hivyo ni heri kuteswa hata kufa kwa kusema ukweli kuliko kuliangamiza taifa langu kwa kuendekeza rushwa na kusema uongo kwa faida ya wachache .

Pia ninapenda utambue kuwa habari hii iliyopewa nafasi ya mbele katika gazeti la Tanzania Daima la leo na katika mtandao huu ndiyo ambayo imeonekana watu hata wale ambao ni rafiki zangu wakubwa na viongozi wangu ninao waheshimu zaidi kuninyoshea vidole na bila uchunguzi wakinituhumu kuwa mimi ni Chadema japo si dhambi kuwa chadema wala chama chochote cha siasa kwa mtanzania ila ni vema watambue kuwa mimi ni kada wa CCM na nimepata kugombea ubunge kupitia CCM na hapa nilipo ni mjumbe wa halmashauri ya CCM wilaya ya Iringa vijijini japo taaluma yangu haina chama ,dini wala kabila​

Ahsante sana na kazi nzuri mkuu... Unatuonyesha spirit ya Mkwavinyika. Tunahitaji wana habari na watanzania wengi kama wewe ambao wanaiweka nchi mbele bila kujali vitisho vya mafisadi. Mungu atakulinda kaka.
 
Mlioko Kyela tunaomba mtuletee na picha za mabasi na malori yatakayo wabeba watu kuja kwenye mkutano wa Dr. slaa kama alivyofanya memba mwenzetu wa kule Tabora kwenye mkutano wa Jk
 
Ama kweli watu wanaonyesha kuichoka CCM. Ndo maana wanafurika sana kwenye mikutano ya Dr. Slaa, wakizingatia cheche zake alipokuwa bungeni wananchi wengi wanamatumaini naye kuwa ni mwanamageuzi wa kweli. Nashauri watanzania tumwunge mkono Dr Slaa, ili apate kupambana na mafisa wanoitesa nchi yetu.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Yah leo ndo niliipata iyo kuwa kumbe Ridhiwani alikoswa koswa kupigwa mawe na wananchi wenye hasira pale walipotaka kufanya kikao kwenye moja ya shule pale ipogolo CHADEMA wakaju juu bse kwanza walitumia darasa ambalo wanafunzi waliambiwa waende nyumbani.
CCM wehu kweli
 
DR SLAA IN IRINGA 010.jpg Watu walikuwa maeneo ya mwembetogwa toka mida ya saa tisa wakimngoja.
Kulikuwa na burudani za apa na pale na ilipofika mida ya 10:20 gari la mziki likaondoka kwenda kuraki bwana Slaa maeneo ya Kihesa.
Cha kushangaza baada ya gari la mziki kuondoka nilidhani watu wangeondoka kwa kuwa jukwaa lilikuwa tupu ila watu wakaendelea kuwepo eneo la uwanja.Wengine walisikika wakisema ingekuwa CCM apa kungekuwa na wasanii mbalimbali wa kuwakeep bize watu.
Mida ya 10:32 helcopter ya Mh raisi mtarajiwa ikaonekana kwa mbali inakuja watu wakaanza kelele za RAISI RAISI RAISI ilipiga round kama mbili ivi hewani kuuzunguka mji.Na ratiba ya kwenda Kihesa ikabadilika kunako majira ya 10:41 helcopta 5H-MWK ikashuka uwanaja wa Mwembe Togwa IKITOKEA Makambako ili kuokoa mda ukizingatia kampeni mwisho saa 12
Nilihoji kwa baadhi ya wananchi kwa nini uwanja wa SAMORA haukutumika kama alivyokuja JK nikaambiwa uwanja ule ni wa CCM na tena leo kwa makusudi ndo wanazindua michuano ya mpira wa miguu ya wilaya ili mradi tuu uwanja uonekane uko bize.
Baada ya kutua helicopter vumbi lilitimka watu wakawa hawaonani na ata baada ya mkutano ikabidi kwenda shushia glass ya maziwa fresh kuondoa vumbi ingawa Dr aliwaomba radhi watu kwa Vumbi na watu hawakujali vumbi na kumjibu kuwa hamna shida wamekuja kumsikiliza.
Mjumbe wa kamati kama sikosei alikuwa Chiku alikaribishwa na mwenyekiti wa wilaya kumkaribisha Dr.Unaweza hoji mwenyekiti yuu wapi eti kumbe amepewa mrungula na akina Lukuvi kukisubortage CHADEMA walivyomstukia wakamtimua.
Uyu mama aliongelea namna familia ya JK ilivyo bize na kampeni kana kwamba familia ndio chama
Kunako majira ya 11:16 Raisi Mtarajiwa akasimama kuanza kuongeza na watanzania waliokuja kwa miguu yao kuja kwa mkutano.Kwanza kabisa aliomba utulivu kwa kuwa zilikuwa zimebaki dk 45 kumaliza kampeni.Pili akagusia tamko la mnadhimu wa jeshi kuwa amempa wiki kuwakamata watu anaodai kuwa wanataka mwaga damu la sivyo watamfungulia mashitaka ya uchochezi.Saa 11:21 mitambo ikazima watu walisikika wakisema CCM hao wameingilia mungu si athumani baada kama ya Dk mbili mitambo ikatengemaa na dr akaendelea kuunguruma.
Dr atoa angalizo kuwa mapenzi ya mungu na nguvu ya umma ndo vya kuvitegemea na si polisi wala jeshi hayo yote kwake ilikuwa ni utangulizi tuu then akaanza rasmi ILA alitoa angalizo kuwa ahadi zake ni za kiinchi na si vinginevyo kama elimu,afya,kuuondoa umaskini na si kama JK ambaye anotoa ahadi maharia ambazo nyingi hatazitimiza kwa uwingi wake
i. JK ni afisa mipango-ahadi anazozitoa JK zinamfanya abandikwe jina ilo na akatolea mfano anaaidi ujenzi wa barabara na kutaja kiasi cha fedha wakati ata feasibility study haijafanywa.
ii. Umasikini-aliongea kwa kirefu kuwa ni 50 years nchi yetu haina mbele wala nyuma.Akaisisitiza kuwa uchaguzi wa mwaka huu uwe wa tathmini ya kule tutokako,tulipo na tuendako.Nyumba duni wanazoishi watanzania ni ushaidi tosha ya umaskini wakati akina Ridhiwani wakimiliki magorofa pamoja na kundi la mafisadi wangine.Akaahidi ili kuboresha nyumba akiingia madarakani bati na cement ni 5000ths ili wengi wajenge.Akatoa mfano kuwa OCD analipwa laki 5 ukiona kajenga ujue ni rushwa imemfikisha apo,vivyo ivyo kwa walimu shs 120,000
iii. Elimu-akaahidi elimu bure kuanzia nursery mpaka form 6 na kuwaasa CCM waache kujivuna kwa idadi ya madarasa na matundu ya vyoo uku ubora wa elimu ukiwa washuka.Na watakaofaulu kwenda chuo nao watasoma bure.Akasema iyo inawezekana kwa kuwa na matumizi sahii ya bajeti ya serikali(karibu tril 9 za bajeti zimewekwa kwa ajili ya anasa za serikali )mfano wa matumizi ni kwa forged receipt ya ndege alioitumia Salma na uhoji kasma ya 42 wameitoa wapi?kama serkali inaforge vitu wananchi hamtakiwi iamini na kuhakikisha madini yanatuneemesha(kwa sasa katika kila sh 100 twaambulia shs 3 kwenye madini).Aakitolea mfano yeye mwenyewe kuwa amesoma bure na kama ingekuwa kulipa baba yake alikuwa mpishi kwa wazungu iyo elimu asingeipata.
iv. AFYA-akaahidi afya bure kwa wote ili wote waweze pata tiba Mf kuutibu mkono wake pale muhimbili ametumia mil 4 je kama angekuwa hanazo mkono ungekuwa wa kukatwa au kuwa kilema milele.
Baada ya apo akamsimamisha mgombea ubunge Mch Msigwa ambaye alipewa dk tano kujinadi kwa kuwa mda ulikuwa waenda mbio na baadae madiwani.
Hatimae akamsimamisha mkewe ambaye aliahidi kumtunza mumewe ili awe na afya njema mda wote wa kampeni.
Kwa kumalizia Slaa akawaambia watu wakunje ngumi na kutupa mkono juu na kujibu hatudanganyikiiiiiiiii na kusema JK bye bye.
MC aliwaambia watu ili kupata ring tone ya chadema kwa kuandika neon BUY na kutuma kwenda 15577
Vilevile aliwaambia watu kuichangia CHADEMA KUPITIA vikapu vilivyokuwa vikipita ambapo name nikachangia kuonyesha msisitizo.
Mkutano uliisha kunako mida ya saa 12:02 Dr akiwa ametumia Dk zisizozidi 45 kwa ajili ya kampeni.Baada ya mkutano watu wakaanza kuondoka kwa miguu yao wenyewe kama walivyokuja na Dr kuondoka kwa gari kwa kuwa Helcopta ilishaondoka eneo la tukio na kwenda kupaki mbali na maeneo ya mwembe togwa
AOB
i. Na akahoji bajaji alizoahidi kama 400 zitapita wapi wakati hatuna barabara za kuaminika.
ii. Pia alingaka kwa kusema atakufa na watu waliokula billion 21 watu wakapiga makofi.
iii. Jk alitangaza stimulus package akiwa mlimani city na mbaya zaidi hela izo nyingi zimeishia kwa watuna makampuni yao.Apo Dr akangaka kuwa JK akanushe kama yeye ni mwanaume,watu wakapiga yowe.
iv. Alimkebei JK kwa majigambo yake kuwa alikuwa raisi wa kwanza afrika kumwona Obama akihoji nchi imefaidika na nini katika ilo au ndo izo net mbilimbili?
v. JK amejialika kuudhulia sherehe za walimu kule Songea na Dr akasema iyo ni rushwa kwa kipindi ka iki cha kapeni

ANGALIZO
Dr alisema karibu nusu ya watu wa TISS wanampa report hivyo akawahakikishia wananchi kuwa hakuna uchakachuaji wa kura na kusisitiza damu ya mtetea haki za wanyonge mungu ataisimamia
VITUKO
Jamaa alikuwa na radio zile za national kubwa akirecord mkutano uku akiwa ameweka tape.
Mwandish wa habari wa TBC alipoteza kamela yake ya digital kama ilivyotangazwa na MC moyoni nkajisemea wasije wakagoma kushoot mkutano kisa kamela imepotea
Defender 2 na kruza mkonge moja zilikuwa zimejaa FFU wakizunguka eneo la mkutano ambao mpaka mwisho hakukuwa na hata chembe ya fujo hasa baada ya Dr kuwaasa wananchi kuwa fujo hazifai
MC aliwaambia watu washike vichwa alafu akasema CCM watu wakajibu huuuuuuuuuuuuuuuuuuu kama kuashilia wameichoka.
Slaa alimwanuru Msigwa avue kofia kwa kuwa wananchi ni mabosi wake
Aliwakebei askali kuwa wanalipwa mishahara mdiogo na ndo maana wako bize na rushwa na kuishi katika nyumba ambazo haziendani na hadhi yao.
NB:Mniwie radhi kwa uandishi wangu si unajua ni fani za watu izi ila lengo langu ni kushare na wale ambao hawakuwepo.

DR SLAA IN IRINGA 011.jpg
 
mbona hatuoni malori wala mabus hapo?

Si unajua CHADEMA hawana staili za kubebezana kwenye Ma-Fuso. Wewe kama unataka kusiliza sera za serikali ijayo itakayo-kutibia bure na kukusomeshea mtoto wako mtaji wako ni "mguu" tu wako ukufikishe kwenye mkutano wa kampeni.
 
slaa_iringa.jpg

Si mwingine ni Dr W.Slaa

Watu walikuwa maeneo ya mwembetogwa toka mida ya saa tisa wakimngoja.

Kulikuwa na burudani za apa na pale na ilipofika mida ya 10:20 gari la mziki likaondoka kwenda kuraki bwana Slaa maeneo ya Kihesa.

Cha kushangaza baada ya gari la mziki kuondoka nilidhani watu wangeondoka kwa kuwa jukwaa lilikuwa tupu ila watu wakaendelea kuwepo eneo la uwanja.Wengine walisikika wakisema ingekuwa CCM apa kungekuwa na wasanii mbalimbali wa kuwakeep bize watu.

Mida ya 10:32 helcopter ya Mh raisi mtarajiwa ikaonekana kwa mbali inakuja watu wakaanza kelele za RAISI RAISI RAISI ilipiga round kama mbili ivi hewani kuuzunguka mji.Na ratiba ya kwenda Kihesa ikabadilika kunako majira ya 10:41 helcopta 5H-MWK ikashuka uwanaja wa Mwembe Togwa IKITOKEA Makambako ili kuokoa mda ukizingatia kampeni mwisho saa 12

Nilihoji kwa baadhi ya wananchi kwa nini uwanja wa SAMORA haukutumika kama alivyokuja JK nikaambiwa uwanja ule ni wa CCM na tena leo kwa makusudi ndo wanazindua michuano ya mpira wa miguu ya wilaya ili mradi tuu uwanja uonekane uko bize.

Baada ya kutua helicopter vumbi lilitimka watu wakawa hawaonani na ata baada ya mkutano ikabidi kwenda shushia glass ya maziwa fresh kuondoa vumbi ingawa Dr aliwaomba radhi watu kwa Vumbi na watu hawakujali vumbi na kumjibu kuwa hamna shida wamekuja kumsikiliza.

Mjumbe wa kamati kama sikosei alikuwa Chiku alikaribishwa na mwenyekiti wa wilaya kumkaribisha Dr.Unaweza hoji mwenyekiti yuu wapi eti kumbe amepewa mrungula na akina Lukuvi kukisubortage CHADEMA walivyomstukia wakamtimua.

Uyu mama aliongelea namna familia ya JK ilivyo bize na kampeni kana kwamba familia ndio chama

Kunako majira ya 11:16 Raisi Mtarajiwa akasimama kuanza kuongeza na watanzania waliokuja kwa miguu yao kuja kwa mkutano.Kwanza kabisa aliomba utulivu kwa kuwa zilikuwa zimebaki dk 45 kumaliza kampeni.

Pili akagusia tamko la mnadhimu wa jeshi kuwa amempa wiki kuwakamata watu anaodai kuwa wanataka mwaga damu la sivyo watamfungulia mashitaka ya uchochezi.Saa 11:21 mitambo ikazima watu walisikika wakisema CCM hao wameingilia mungu si athumani baada kama ya Dk mbili mitambo ikatengemaa na dr akaendelea kuunguruma.

Dr atoa angalizo kuwa mapenzi ya mungu na nguvu ya umma ndo vya kuvitegemea na si polisi wala jeshi hayo yote kwake ilikuwa ni utangulizi tuu then akaanza rasmi ILA alitoa angalizo kuwa ahadi zake ni za kiinchi na si vinginevyo kama elimu,afya,kuuondoa umaskini na si kama JK ambaye anotoa ahadi maharia ambazo nyingi hatazitimiza kwa uwingi wake

i.
JK ni afisa mipango-ahadi anazozitoa JK zinamfanya abandikwe jina ilo na akatolea mfano anaaidi ujenzi wa barabara na kutaja kiasi cha fedha wakati ata feasibility study haijafanywa.

ii.
Umasikini-aliongea kwa kirefu kuwa ni 50 years nchi yetu haina mbele wala nyuma.Akaisisitiza kuwa uchaguzi wa mwaka huu uwe wa tathmini ya kule tutokako,tulipo na tuendako. Nyumba duni wanazoishi watanzania ni ushaidi tosha ya umaskini wakati akina Ridhiwani wakimiliki magorofa pamoja na kundi la mafisadi wangine.Akaahidi ili kuboresha nyumba akiingia madarakani bati na cement ni 5000ths ili wengi wajenge.Akatoa mfano kuwa OCD analipwa laki 5 ukiona kajenga ujue ni rushwa imemfikisha apo,vivyo ivyo kwa walimu shs 120,000

iii. Elimu-akaahidi elimu bure kuanzia nursery mpaka form 6 na kuwaasa CCM waache kujivuna kwa idadi ya madarasa na matundu ya vyoo uku ubora wa elimu ukiwa washuka.Na watakaofaulu kwenda chuo nao watasoma bure. Akasema iyo inawezekana kwa kuwa na matumizi sahii ya bajeti ya serikali(karibu tril 9 za bajeti zimewekwa kwa ajili ya anasa za serikali )mfano wa matumizi ni kwa forged receipt ya ndege alioitumia Salma na uhoji kasma ya 42 wameitoa wapi?kama serkali inaforge vitu wananchi hamtakiwi iamini na kuhakikisha madini yanatuneemesha(kwa sasa katika kila sh 100 twaambulia shs 3 kwenye madini). Akitolea mfano yeye mwenyewe kuwa amesoma bure na kama ingekuwa kulipa baba yake alikuwa mpishi kwa wazungu iyo elimu asingeipata.

iv. AFYA-akaahidi afya bure kwa wote ili wote waweze pata tiba Mf kuutibu mkono wake pale muhimbili ametumia mil 4 je kama angekuwa hanazo mkono ungekuwa wa kukatwa au kuwa kilema milele.

Baada ya hapo akamsimamisha mgombea ubunge Mch Msigwa ambaye alipewa dk tano kujinadi kwa kuwa mda ulikuwa waenda mbio na baadae madiwani.

Hatimae akamsimamisha mkewe ambaye aliahidi kumtunza mumewe ili awe na afya njema mda wote wa kampeni.

Kwa kumalizia Slaa akawaambia watu wakunje ngumi na kutupa mkono juu na kujibu hatudanganyikiiiiiiiii na kusema JK bye bye.

MC aliwaambia watu ili kupata ring tone ya chadema kwa kuandika neon BUY na kutuma kwenda 15577

Vilevile aliwaambia watu kuichangia CHADEMA KUPITIA vikapu vilivyokuwa vikipita ambapo name nikachangia kuonyesha msisitizo.

Mkutano uliisha kunako mida ya saa 12:02 Dr akiwa ametumia Dk zisizozidi 45 kwa ajili ya kampeni.Baada ya mkutano watu wakaanza kuondoka kwa miguu yao wenyewe kama walivyokuja na Dr kuondoka kwa gari kwa kuwa Helcopta ilishaondoka eneo la tukio na kwenda kupaki mbali na maeneo ya mwembe togwa

AOB

i. Na akahoji bajaji alizoahidi kama 400 zitapita wapi wakati hatuna barabara za kuaminika.
ii. Pia alingaka kwa kusema atakufa na watu waliokula billion 21 watu wakapiga makofi.
iii. Jk alitangaza stimulus package akiwa mlimani city na mbaya zaidi hela izo nyingi zimeishia kwa watuna makampuni yao.Apo Dr akangaka kuwa JK akanushe kama yeye ni mwanaume,watu wakapiga yowe.
iv. Alimkebei JK kwa majigambo yake kuwa alikuwa raisi wa kwanza afrika kumwona Obama akihoji nchi imefaidika na nini katika ilo au ndo izo net mbilimbili?
v. JK amejialika kuudhulia sherehe za walimu kule Songea na Dr akasema iyo ni rushwa kwa kipindi ka iki cha kapeni

ANGALIZO
Dr alisema karibu nusu ya watu wa TISS wanampa report hivyo akawahakikishia wananchi kuwa hakuna uchakachuaji wa kura na kusisitiza damu ya mtetea haki za wanyonge mungu ataisimamia

VITUKO

Jamaa alikuwa na radio zile za national kubwa akirecord mkutano uku akiwa ameweka tape.

Mwandish wa habari wa TBC alipoteza kamera yake ya digital kama ilivyotangazwa na MC moyoni nkajisemea wasije wakagoma kushoot mkutano kisa kamera imepotea

Defender 2 na kruza mkonge moja zilikuwa zimejaa FFU wakizunguka eneo la mkutano ambao mpaka mwisho hakukuwa na hata chembe ya fujo hasa baada ya Dr kuwaasa wananchi kuwa fujo hazifai
.

MC aliwaambia watu washike vichwa alafu akasema CCM watu wakajibu huuuuuuuuuuuuuuuuuuu kama kuashilia wameichoka.

Slaa alimwanuru Msigwa avue kofia kwa kuwa wananchi ni mabosi wake

Aliwakebei askari kuwa wanalipwa mishahara midogo na ndo maana wako bize na rushwa na kuishi katika nyumba ambazo haziendani na hadhi yao.

NB: Mniwie radhi kwa uandishi wangu si unajua ni fani za watu izi ila lengo langu ni kushare na wale ambao hawakuwepo.
 
Attachments

  • DR SLAA IN IRINGA 009.jpg
    DR SLAA IN IRINGA 009.jpg
    1.3 MB · Views: 62
View attachment 14592Watu walikuwa maeneo ya mwembetogwa toka mida ya saa tisa wakimngoja.
Kulikuwa na burudani za apa na pale na ilipofika mida ya 10:20 gari la mziki likaondoka kwenda kuraki bwana Slaa maeneo ya Kihesa.
Cha kushangaza baada ya gari la mziki kuondoka nilidhani watu wangeondoka kwa kuwa jukwaa lilikuwa tupu ila watu wakaendelea kuwepo eneo la uwanja.Wengine walisikika wakisema ingekuwa CCM apa kungekuwa na wasanii mbalimbali wa kuwakeep bize watu.
Mida ya 10:32 helcopter ya Mh raisi mtarajiwa ikaonekana kwa mbali inakuja watu wakaanza kelele za RAISI RAISI RAISI ilipiga round kama mbili ivi hewani kuuzunguka mji.Na ratiba ya kwenda Kihesa ikabadilika kunako majira ya 10:41 helcopta 5H-MWK ikashuka uwanaja wa Mwembe Togwa IKITOKEA Makambako ili kuokoa mda ukizingatia kampeni mwisho saa 12
Nilihoji kwa baadhi ya wananchi kwa nini uwanja wa SAMORA haukutumika kama alivyokuja JK nikaambiwa uwanja ule ni wa CCM na tena leo kwa makusudi ndo wanazindua michuano ya mpira wa miguu ya wilaya ili mradi tuu uwanja uonekane uko bize.
Baada ya kutua helicopter vumbi lilitimka watu wakawa hawaonani na ata baada ya mkutano ikabidi kwenda shushia glass ya maziwa fresh kuondoa vumbi ingawa Dr aliwaomba radhi watu kwa Vumbi na watu hawakujali vumbi na kumjibu kuwa hamna shida wamekuja kumsikiliza.
Mjumbe wa kamati kama sikosei alikuwa Chiku alikaribishwa na mwenyekiti wa wilaya kumkaribisha Dr.Unaweza hoji mwenyekiti yuu wapi eti kumbe amepewa mrungula na akina Lukuvi kukisubortage CHADEMA walivyomstukia wakamtimua.
Uyu mama aliongelea namna familia ya JK ilivyo bize na kampeni kana kwamba familia ndio chama
Kunako majira ya 11:16 Raisi Mtarajiwa akasimama kuanza kuongeza na watanzania waliokuja kwa miguu yao kuja kwa mkutano.Kwanza kabisa aliomba utulivu kwa kuwa zilikuwa zimebaki dk 45 kumaliza kampeni.Pili akagusia tamko la mnadhimu wa jeshi kuwa amempa wiki kuwakamata watu anaodai kuwa wanataka mwaga damu la sivyo watamfungulia mashitaka ya uchochezi.Saa 11:21 mitambo ikazima watu walisikika wakisema CCM hao wameingilia mungu si athumani baada kama ya Dk mbili mitambo ikatengemaa na dr akaendelea kuunguruma.
Dr atoa angalizo kuwa mapenzi ya mungu na nguvu ya umma ndo vya kuvitegemea na si polisi wala jeshi hayo yote kwake ilikuwa ni utangulizi tuu then akaanza rasmi ILA alitoa angalizo kuwa ahadi zake ni za kiinchi na si vinginevyo kama elimu,afya,kuuondoa umaskini na si kama JK ambaye anotoa ahadi maharia ambazo nyingi hatazitimiza kwa uwingi wake
i. JK ni afisa mipango-ahadi anazozitoa JK zinamfanya abandikwe jina ilo na akatolea mfano anaaidi ujenzi wa barabara na kutaja kiasi cha fedha wakati ata feasibility study haijafanywa.
ii. Umasikini-aliongea kwa kirefu kuwa ni 50 years nchi yetu haina mbele wala nyuma.Akaisisitiza kuwa uchaguzi wa mwaka huu uwe wa tathmini ya kule tutokako,tulipo na tuendako.Nyumba duni wanazoishi watanzania ni ushaidi tosha ya umaskini wakati akina Ridhiwani wakimiliki magorofa pamoja na kundi la mafisadi wangine.Akaahidi ili kuboresha nyumba akiingia madarakani bati na cement ni 5000ths ili wengi wajenge.Akatoa mfano kuwa OCD analipwa laki 5 ukiona kajenga ujue ni rushwa imemfikisha apo,vivyo ivyo kwa walimu shs 120,000
iii. Elimu-akaahidi elimu bure kuanzia nursery mpaka form 6 na kuwaasa CCM waache kujivuna kwa idadi ya madarasa na matundu ya vyoo uku ubora wa elimu ukiwa washuka.Na watakaofaulu kwenda chuo nao watasoma bure.Akasema iyo inawezekana kwa kuwa na matumizi sahii ya bajeti ya serikali(karibu tril 9 za bajeti zimewekwa kwa ajili ya anasa za serikali )mfano wa matumizi ni kwa forged receipt ya ndege alioitumia Salma na uhoji kasma ya 42 wameitoa wapi?kama serkali inaforge vitu wananchi hamtakiwi iamini na kuhakikisha madini yanatuneemesha(kwa sasa katika kila sh 100 twaambulia shs 3 kwenye madini).Aakitolea mfano yeye mwenyewe kuwa amesoma bure na kama ingekuwa kulipa baba yake alikuwa mpishi kwa wazungu iyo elimu asingeipata.
iv. AFYA-akaahidi afya bure kwa wote ili wote waweze pata tiba Mf kuutibu mkono wake pale muhimbili ametumia mil 4 je kama angekuwa hanazo mkono ungekuwa wa kukatwa au kuwa kilema milele.
Baada ya apo akamsimamisha mgombea ubunge Mch Msigwa ambaye alipewa dk tano kujinadi kwa kuwa mda ulikuwa waenda mbio na baadae madiwani.
Hatimae akamsimamisha mkewe ambaye aliahidi kumtunza mumewe ili awe na afya njema mda wote wa kampeni.
Kwa kumalizia Slaa akawaambia watu wakunje ngumi na kutupa mkono juu na kujibu hatudanganyikiiiiiiiii na kusema JK bye bye.
MC aliwaambia watu ili kupata ring tone ya chadema kwa kuandika neon BUY na kutuma kwenda 15577
Vilevile aliwaambia watu kuichangia CHADEMA KUPITIA vikapu vilivyokuwa vikipita ambapo name nikachangia kuonyesha msisitizo.
Mkutano uliisha kunako mida ya saa 12:02 Dr akiwa ametumia Dk zisizozidi 45 kwa ajili ya kampeni.Baada ya mkutano watu wakaanza kuondoka kwa miguu yao wenyewe kama walivyokuja na Dr kuondoka kwa gari kwa kuwa Helcopta ilishaondoka eneo la tukio na kwenda kupaki mbali na maeneo ya mwembe togwa
AOB
i. Na akahoji bajaji alizoahidi kama 400 zitapita wapi wakati hatuna barabara za kuaminika.
ii. Pia alingaka kwa kusema atakufa na watu waliokula billion 21 watu wakapiga makofi.
iii. Jk alitangaza stimulus package akiwa mlimani city na mbaya zaidi hela izo nyingi zimeishia kwa watuna makampuni yao.Apo Dr akangaka kuwa JK akanushe kama yeye ni mwanaume,watu wakapiga yowe.
iv. Alimkebei JK kwa majigambo yake kuwa alikuwa raisi wa kwanza afrika kumwona Obama akihoji nchi imefaidika na nini katika ilo au ndo izo net mbilimbili?
v. JK amejialika kuudhulia sherehe za walimu kule Songea na Dr akasema iyo ni rushwa kwa kipindi ka iki cha kapeni

ANGALIZO
Dr alisema karibu nusu ya watu wa TISS wanampa report hivyo akawahakikishia wananchi kuwa hakuna uchakachuaji wa kura na kusisitiza damu ya mtetea haki za wanyonge mungu ataisimamia
VITUKO
Jamaa alikuwa na radio zile za national kubwa akirecord mkutano uku akiwa ameweka tape.
Mwandish wa habari wa TBC alipoteza kamela yake ya digital kama ilivyotangazwa na MC moyoni nkajisemea wasije wakagoma kushoot mkutano kisa kamela imepotea
Defender 2 na kruza mkonge moja zilikuwa zimejaa FFU wakizunguka eneo la mkutano ambao mpaka mwisho hakukuwa na hata chembe ya fujo hasa baada ya Dr kuwaasa wananchi kuwa fujo hazifai
MC aliwaambia watu washike vichwa alafu akasema CCM watu wakajibu huuuuuuuuuuuuuuuuuuu kama kuashilia wameichoka.
Slaa alimwanuru Msigwa avue kofia kwa kuwa wananchi ni mabosi wake
Aliwakebei askali kuwa wanalipwa mishahara mdiogo na ndo maana wako bize na rushwa na kuishi katika nyumba ambazo haziendani na hadhi yao.
NB:Mniwie radhi kwa uandishi wangu si unajua ni fani za watu izi ila lengo langu ni kushare na wale ambao hawakuwepo.

View attachment 14591

Ahsante sana kwa mukhatari huu wa matukio wa habari hizi njema zenye matumaini. Habari za Wokovu wa M-Tanzania hapo Oct 31, 2010. Usijali ndugu yangu CHADEMA ikishachukua nchi fursa zitakuwepo za wewe na wengine kwenda kuisomea fani ya Uandishi ikibidi. Kwani nchi itarudi kwenye mikono yetu wenyewe Watanganyika.
 
Kuna kajanja kamoja kachwara kanadai kanatoka Iringa kamethubutu kutoa tathmini ya Uchaguzi wa October 31 kuwa Dr. Slaa ataambulia nafasi ya tatu baada ya Kikwete na Lipumba ! - sidhani kama hiyo Iringa yake ndio hii tunayoishuhudia hapa. Shame on you Maggid Mjengwa.

Hata hivyo tusimpuuze, hapa kuna ajenda ya siri kwani matamashi ya jana ya Shimbo yanathibitisha hilo. Pamoja na hayo nina hakika mipango hii miovu ya kutaka kuleta machafuko nchini kamwe haitaweza kufua dafu mbele ya nguvu ya Umma kama giza lisivyoweza kustahimili mwanga.

Peoples Power will always prevail !

Majjid Mjengwa is a huge disgrace
 
Namuunga mkono slaa, lakini kwenye swala la Afrika mashariki sikubalini nae 100%.
Pia sidhani swala la afya bure na elimu bure kama litaboresha huduma kwani si swala la bure tuu, kuna mambo mengi ya kuangalia.Kama akishinda litakuja kumaliza kisiasa.
Bure huleta kuto kuwajibika na kutokujali kinachoitajiaka kwenye swala la afya ni la kiutendaji zaidi, swala la gharama, wananchi walipie kutokana na uwezo walio nao, sio bure.
Siamini bure, na wala sikubaliani na bure, itashindikana tuu.
 
Back
Top Bottom