Elections 2010 Dr. Slaa nyanda za Juu Kusini: Songea, Iringa, Mbeya (picha na habari)

Duh!
umati unatisha huo, Tunashukuru PG kwa picha, umezipiga vizuri sana

sio mimi , kaka ni kwa msaada wa FRANCIS GODWIN MZEE WA MATUKIO, yule aliyepokea simu ya vitisho baada ya kuripoti, kuhusu kutimuliwa kwa ridhiwani, iringa
 
sio mimi , kaka ni kwa msaada wa FRANCIS GODWIN MZEE WA MATUKIO, yule aliyepokea simu ya vitisho baada ya kuripoti, kuhusu kutimuliwa kwa ridhiwani, iringa
Hivi walimtisha? .....very insecure!
 
Mgombea urais kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) Dk Willibrod Slaa amesema kuwa iwapo serikali ya CCM imejiandaa kwa ajili ya kuchakachua matokeo itachakachuliwa yenyewe kwa nguvu za umma.

Amesema kuwa CCM itafikiri kuwa watanzania ni wajinga kiasi cha kudanganywa kwa kila jambo na kuwa sasa watanzania wamebaini kuwa wanadanganywa na hivyo lazima isubiri kupata anguko la karne katika uchaguzi huu utakao fanyika octoba 31 mwaka huu.

Asisitiza kuwa serikali ya Chadema ikiingia madarakani elimu ,afya ni bure kwa watanzania wote kwa kutumia kodi za watanzania ambazo kwa sasa zinachezewa.

Dk Slaa amesema kuwa sehemu kubwa ya watanzania wanatibiwa kwa waganga wa kienyeji huku serikali ikiendelea kujitapa kuwa imeboresha afya
 
Kama mambo yenyewe ndo hivi, Ningekua JK Mi na familia yangu wala tusingejipa shida tungeenda zetu ULAYaa kula Raha,
Kwani TZ hatuna chetu.
 
CCM watajuta kumwengua Mwakalebela. teh,Teh,Haaa haaaa,nicheke mie.
Wamejimaliza weeeenyewe.

Juhudi za Ridhiwani kuwapatanisha Mwaka na Mbega nazo zimegonga mwamba. Haruuuu!!!!!!!!!!

CCM mnalo hilo.
 
Kama mambo yenyewe ndo hivi, Ningekua JK Mi na familia yangu wala tusingejipa shida tungeenda zetu ULAYaa kula Raha,
Kwani TZ hatuna chetu.

Anajifanya mjeshi king'ang'anizi, lakini matokeo ya mwaka huu lazima aanguke tena pamoja na ulinzi aliopewa na bamchawi.
 
Hivi walimtisha? .....very insecure!

Mwandishi aliyeandika, kutimiliwa kwa ridhiwani iringa , apokea simu za vitisho

September 30, 2010

SITAZIBWA MDOMO KWA VITISHO ,NIPO TAYARI KUFA KWA KUSEMA KWELI DAIMA........


Mmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin

UPO usemi kuwa ukitaka kazi ya jeshi usiogope kufa na siku zote mkweli hutengwa wa waongo kama hivyo ndivyo basi kwa mara ya kwanza leo kwanza ninapenda kuanza kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ambaye amepata kunileta duniani na kuniongoza kwa kila jambo na kunilinda na maadui wangu kwa kuwapa roho ya upendo na huruma mwingi.

Pia napenda kuwapongeza wanahabari wenzangu wote wa Tanzania ambao tumekuwa nao bega kwa bega katika kuipasha habari jamii ya kitanzania kulingana na uwezo wetu kweli nawapongeza wote bila kuwasahau wakurungezi wenzangu ambao tunamiliki vyombo vyetu yaani Blog na Website .

mimi Francis Godwin kama mmiliki wa mtandao huu na mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima napenda kutumia uwanja wangu huu wa kujidai kueleza masikitiko yangu kwa wale wote ambao wameendelea kunipigia simu za vitisho kuhusiana na habari hii chini ya japo sijapokea simu ya wahusika wenyewe ila wapambe wa nje wameendelea kuwa na nguvu hata kutoa vitisho dhidi yangu kuwa iwapo nitaendelea kujifanya mkweli siku zangu zinahesabika .

Napenda kupingana na wote walionipigia simu nakutoa vitisho kama hivyo huku nikiamini kuwa kifo kwangu ni mipango ya Mungu na sitoogopa wala kuingia katika dhambi ya kusema uongo kwa jambo la ukweli hivyo ni heri kuteswa hata kufa kwa kusema ukweli kuliko kuliangamiza taifa langu kwa kuendekeza rushwa na kusema uongo kwa faida ya wachache .


Pia ninapenda utambue kuwa habari hii iliyopewa nafasi ya mbele katika gazeti la Tanzania Daima la leo na katika mtandao huu ndiyo ambayo imeonekana watu hata wale ambao ni rafiki zangu wakubwa na viongozi wangu ninao waheshimu zaidi kuninyoshea vidole na bila uchunguzi wakinituhumu kuwa mimi ni Chadema japo si dhambi kuwa chadema wala chama chochote cha siasa kwa mtanzania ila ni vema watambue kuwa mimi ni kada wa CCM na nimepata kugombea ubunge kupitia CCM na hapa nilipo ni mjumbe wa halmashauri ya CCM wilaya ya Iringa vijijini japo taaluma yangu haina chama ,dini wala kabila​
 
Dah! inatia moyo saaaana! Wacha chama filisi cha mafisadi waanze kuingia kiwewe na kuliita jeshi liwasaidie katika wizi wa kura. Shime Watanzania wakati wa kukiondoa chama filisi cha mafisadi umewadia. Wakati ni huu!
 
Watu wa kyela tunawategemea, fanyeni kama wenzeni wa iringa, yaani ni balala, TUNATAKA KUISHANGAZA CCM, OCT 31
 
Huyu jamaa kweli ni mwandishi makini, anaandika hali halisi ilivyo , ndiyo maana kwenye blog yake kuna picha kibao tu za JK kwenye kampeni zake na zikionyesha idani ya watu anaovuta, vile vile za chadema .

Ni tofauti na blog ya michuzi ambaye yeye anajaribu kuripoti mabaya tu ya chadema,mara slaa kapora mke..mara sijui nini, mpaka niliamua kuimwaga, maana inaonyesha hajui taaluma yake ,ushabiki kaweka mbele sana hadi anapitiliza.
 
iringa.JPG
pencil.png
 
Back
Top Bottom