Elections 2010 Dr. Slaa nyanda za Juu Kusini: Songea, Iringa, Mbeya (picha na habari)

USHUHUDA NI MUHIMU:

Wiki hii nilikuwa Kigoma mjini, Kasuru na Kibondo. watu niliokutana nao kati ya 50 na 100, kulikuwa na watu kama 50% yao ambao walikuwa tayari kutopiga kura kwa sababu walizodai kuwa " hawakuwa wanaona wa kumchagua wakati Dr. Slaa alipokuwa hajapitishwa, lakini sasa, tumepata wa kumpigia."

So, wengi kadi wanazo na wengine walikuwa wameisha kata tamaa ya kupiga kura lakini sasa wakumpigia yupo Dr. Slaa.

kula 5. Napenda kusikia habari kama hizi
 


Ewaaaah kwanza nina nia mathubuti juu ya hiyo familia na niko CCM,

Moja ndani ya UVCCM lazima nikafanye mapinduzi ya hali ya juu subiri utaipata habari na nitaanza na RizOne kumweka benchi na fitna ya hali ya juu maana huku nyamagana alichokuja kukileta ndicho kitakacho mgharimu 2015
YOU HAVE A POINT ccm inahitaji mabadiliko makubwa saana!
 
rostam_election.jpg


Slaa_Songea.jpg


Angalia tofauti ya picha hizi.....

Picha ya juu yaonyesha hamna darasa linalotolewa na huyo cheupe badala yake anauza sura na kujisifia kuwa ana pesa.Lakini pia wale wanaohutubiwa nao hawana umakini kwani hakuna cha kusiliza kwani haja yao imetimizwa kwa kupa Njano na kijani
Kura yako kwa dr.slaa
 


mi nakubaliana nawe kwa kiasi fulani kuwa maneno yanawaingia safi, ila kwa kusoma alama za nyakati nikuwa hii yote ni kwa maaandalizi ya 2015 ndipo hali itakuwa ndio siasa imepamba moto

mean while tu angaze macho yetu kwenye katiba ya JAMUHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA kwa umakini ili huko tuendako tupate maisha bora sasa na elimu bora zaidi na matibabu safi

Mkuu Huamini kama Rais ajaye ni Slaa? Hebu jaribu kimpigia kuara.
 
Mimi nawashauri sana Chadema wafike hadi zanzibar (Unguja na Pemba) kumnadi Dr.Slaa na mgombea mwenza kwani ktk kura za Rais wa Muungano Wazanzibar pia watakuwa na mchango mkubwa sana ktk kura zao.

Ifahamike tu kwamba Zanzibar wanaweza mchagua Sief Hamad kama rais wa Zanzibar na kumchagua Dr.Slaa kama rais wa Jamhuri wakitambua muafaka wa kwanza baina ya Chadrema na CUF kuhusiana na Utawala wa visiwani ambao unawapa nguvu zaidi CUF kuongoza kuliko huo wa mseto na CCM.

MI huwa nashangaa sana watu wanaong'ang'ania Slaa aende ZNZ. Simaanishi muungano uvunjike, ila kama ikibidi hata ukifunjika poa. My point ni kuwa ZNZ kuna wapiga kura wangapi? Mfumo wetu wa kura ni wa kujumlisha, mtu mmoja kura moja! Kura za ZNZ japo ni muhimu lakini haziwezi kumzuia Slaa kupata URAIS endapo atapata hata 47%% za kura za Bara.

Wanaosizitiza Slaa akubalike ZNZ nadhani ni wana CCM na wanataka akapoteze Muda wake Kule. MBONA KIKWETE HAJAENDA ZNZ?
Tuwe makini hapa tusipotezane, Slaa atakuwa ni Rais wa Tanzania Bara (Tanganyika) na Sio ZNZ. Kule wana rais wao! Na Kura zao ni Kidogo sana kama za jimbo la Ubungo TU!
 
Picha ya juu yaonyesha hamna darasa linalotolewa na huyo cheupe badala yake anauza sura na kujisifia kuwa ana pesa.Lakini pia wale wanaohutubiwa nao hawana umakini kwani hakuna cha kusiliza kwani haja yao imetimizwa kwa kupa Njano na kijani
Kura yako kwa dr.slaa

Ukiangalia vizuri, Polisi wa Picha ya juu (ya CCM) hawafuatilii hotuba, lakini hapo chini polisi wote wanaonyesha kusahau kazi yao na wamelegea kabisa ready kupokea ukweli. Inaonyesha hotuba ya Slaa imewagusa.

Mimi naamini, 31 Oct mambo yatakuwa ya mshangao kwa wengi. Hawa polisi ambao leo wanashurutishwa kuwakingia CCM kifua wakati wa Kampeni, Watawageuka na kutetea Haki siku ya usimamizi wa kura!
Ni kuendelea kuwaelimisha tu kuwa Slaa si ADUI bali ni Mtu anayetaka kubadili maisha ya Watanzania wote, wao kama Polisi na familia zao pia! Mana Hata ukiwa polisi matatizo ya maji, shule na afya ni ya wote!
 
tehetehe
na utakuta watu hawa hawa wanajitokeza kwa wagombea wa vyama vingine. na kama unavyosema haijulikani ni wangapi wana kadi za kupigia kura. ni vigumu ku judge matokeo ya uchaguzi kwa kuangalia tu umati wa watu
Jethro na Ng'azagala, Kama hiyo ni sababu zenu za kuwatia wasi wasi kwa nini sisi m huwasomba kwa malori ili waje kumsikiliza Kikwete? Penye mzoga ndipo tai ukusanyika! Hata tukisema kuwa nusu ya wahudhuriaji wa mikutano yote ndio wenye shahada, na hao ndio watapiga kura bado Dr Slaa atashinda.
 
Nilikuwa kwenye mkutano wa Slaa songea,mkutano huu ulifanyika viwanja vya shule na msingi songea kata ya majengo.Ukweli watu walikuwa wengi na walijitokeza kwa mapenz yao na mji wote wa songea ulitetemeka.yafuatayo ni mapungufu ambayo yalitokea na km sio mapenz ya dhat ya wananchi kwa slaa na mbunge wao Edson mbogoro bac mkutano ulishaharibika.1)mikutano mingi ya slaa mkoa wa ruvuma ilivunjika jana kutokana na helikopta kukwama songea mjin kutokana na gari ambalo lilibeba mafuta lile fuso big sound kukwama njombe na kushindwa kufika songea hivyo kumlazimu slaa asafiri kwa gar toka songea had mbinga na kufanikiwa kufanya mkutano mmoja tu mbinga mjini,na mikutano zaid ya mitatu ambayo ingebid ifanyike ktk vijiji tofauti vya jimbo la mbinga magharibi haikufanyika kutokana na muda wa kusafir na gari,hali hii imewakasilisha sana wananchi wa mbinga kwa kuwa watu walifika ktk maeneo ya tukio toka hasubuh wakimsubiri dokta Slaa,hali hii pia ilitokea katika jimbo la songea mjini kulipangwa ifanyike mikutano miwili eneo la majengo na eneo la yule ya Tanga nje kidogo ya mji wa songea,lakini ulifanyika mkutano mmoja tu eneo la majengo na kuwaacha wanakijiji waliojitokeza kwa wingi katika eneo la shule ya Tanga ambao toka asubuh walikuwa wakisubiri mkutano wakilalamika kwa kuwa kilichofanyika ni kwamba dr slaa hakushuka pale,alizunguka tu na helikopta ktk eneo na kuwaomba radhi wananchi kwa kupitia kwa viongoz,lakin kwa hali halic wananchi hawakuelewa.baada ya hapo slaa alipitiliza moja kwa moja ktk viwanja vya majengo tena kwa kuchelewa.2)viwanja alivyofanya mkutano slaa hapa songea mjin vilifulika watu weng kuanzia majira ya saa saba mchana lakini cha kushangaza lile fuso la big sound halikufika na viongoz wa mkoa waliambiwa waandae mkutano wa shule ya tanga na huyu mgombea wa ubunge aliuandaa vizur kuanzia jukwaa na sound kwa ujumla,lakin huu wa majengo ulikuwa unashughulikiwa na makao makuu na waliwaambia viongoz wao wa songea kuwa big sound yan lile gar linalotumiwa km jukwaa na limebeba sound system kwamba linakuja na litatumika majengo,lakin wananch walijaa uwanjan na had saa kumi na robo gar hilo lilikuwa halijafika na uwanja ulikuwa hauna muziki wala jukwaa na waratibu wa kampen wakikaa kimya.Hal hii ilimlazimu mgombea ubunge mwanasheria edson mbogoro kunusuru haibu kwa kuleta majukwaa ya dharura kwenye majira ya saa kumi na nusu.saa kwenye maspika na vipaza sauti ndio ilikuwa balaa,yaan watu walifulika weng lakin hawasikii kitu hasa wale waliokaa mbal na jukwaa,hata dr alikuwa anaumia sana kwa kuwahutubia watu weng kupitia vipaza saut hafifu vitumikavyo kwenye magar ya matangazo.Hakika wasaidiz wa slaa sasa wanaanza kumuhujumu slaa..hizo ndizo kasoro kubwa zilizokea songea..hakika chadema tupo nyuma yenu bac jipangeni il muctuangushe.


Libasket Asante sana kwa ujumbe,

Kwa kweli inasikitisha sana, na naamini CHADEMA watashughulikia kwa makini Swala hili, na kama kuna namna wanaweza Kujibana watafute siku nyingine moja wakafanye hiyo Mikutano 'sina uhakika inaruhusiwa na NEC'


Kitu cha Muhimu kuliko Vyote, CHADEMA wanatakiwa wawe na plan B, katika kila wanachokifanya, huu si wakati wa kusikia eti Vipaza sauti vilikuwa na matatizo, haa.., at least kila anakoenda Dr. Slaa inatakiwa wawe angalau na System Tatu, fully equiped..
 
Huo umati namba zao za kadi za mpiga kura zilishachukulia na mabalozi hinyo idadi kubwa ya majina yao hayatatokea kwenye orodha ya wapiga kura hivyo japokuwa watafika kwenye vituo vya kupigia kura hawatapata fursa ya kupiga kura, CCM itaendelea kutawala for the next five years.
 
Habari za kuaminika ni kuwa Dr Slaa atakuwa akifanya mikutato ya kampeni katika mji wa kyela kesho tar 3-10-2010. Kabla ya mikutano ya Dr slaa itakayofanyika vijijini, atafanya mkutano mkubwa Kyela mjini. Wote wenye mapenzi mema na Tanzania mnapaswa kuja kumsikiliza.
 
Habari za kuaminika ni kuwa Dr Slaa atakuwa akifanya mikutato ya kampeni katika mji wa kyela kesho tar 3-10-2010. Kabla ya mikutano ya Dr slaa itakayofanyika vijijini, atafanya mkutano mkubwa Kyela mjini. Wote wenye mapenzi mema na Tanzania mnapaswa kuja kumsikiliza.

Juzi juzi baada ya Mwakyembe kumnadi JK alizomewa, wakadai "tunamtaka Dkt Slaa!" Dkt Slaa pale ni kwako, kawasalimie watu wako tu sio kuomba kura!
 
kila la kheri next prezdaaa!! Wanakyela msituangushe huko japo vyombo vya habari vinatubania.
 
IMG_2096.JPG

Mgombea urais kupitia Chadema Dr Willibrod Slaa akishangaa umati mkubwa wa wakazi wa jimbo la Iringa mjini ambao wamefika katika uwanja wa Mwembetogwa Iringa mjini kumsikiliza katika mendelezo wake wa mikutao ya kampeni za chama hicho ,
IMG_2055.JPG

umati wa wananchi wa jimbo la Iringa mjini ambao wapo uwanjani wakimsikiliza Dr.Slaa uwanja huu ambao CCM imekuwa ikifanyia mikutano yake na ndipo mgombea mwenza wa JK Dr Bilal alihuhudia mpasuko wa wana CCM
IMG_2047.JPG

Ulinzi wa kutosha uwanja wa Mwembetogwa Iringa
IMG_2034.JPG


IMG_2037.JPG

Wananchi wakitazama Helkopta ya Dr Slaa



'LIVE' DR SLAA AMPA MTIHANI SHIMBO WA JWTZ ,ASEMA CCM IMEPANGA KUCHAKACHUA KURA



IMG_2093.JPG

Wananchi wa Iringa mjini wakirekodi hotuba ya Dr Slaa kwa kumbukumbu zao

IMG_1943.JPG

Helkopta ya mgombea urais wa Chadema Dr.Slaa ikitua katika uwanja wa mkutano asubuhi hii

IMG_1958.JPG

Wananchi wa Njombe wakiipungia mikono Helkopata ya Dr Slaa
IMG_1949.JPG

Dr Slaa akipokelewa na viongozi wa wilaya ya Njombe mara baada ya kuwasili dakika chache kuanzia sasa
IMG_1941.JPG

Helkopta ya Mgombea Urais wa Chadema ikiwa hewani ikijiandaa kutua uwanja wa Mdete Njombe mjini
IMG_1958.JPG

Mgombea urais kwa Chadema Dr Willibrod Slaa amemshukia mkuu wa mnajimu mkuu wa majeshi nchini Bw Shimbo kuwa ndani ya siku 10 awe amewakamata wale wote ambao wanatuhumiwa kumwaga damu na vinginevyo hatua itachukuliwa dhidi yake.

Pia Dr.Slaa amesema kuwa CCM imepanga kuchakachua matokeo ya uchaguzi mkuu na ndio sababu ya kuanza kutumia vyombo vya habari vya umma ,majeshi na usalama wa Taifa kuweka kinga na kuwa kama CCM imepanga kuchakachua matokeo basi itachakachuliwa yenyewe .

Hata hivyo ameonya jeshi la Poliso kupitia wakuu wa polisi wilaya kuwa kama wanapewa taarifa na kuchanwa mabango ya wagombea bila kuchukua hatua ni mwanzo wa jeshi la polisi kuchochea vurugu na kuwa Chadema kamwe haitafanya fujo labda fujo zitoke CCM.

Dr.Slaa ambaye anaendelea na hutuba yake viwanja wa Mdete mjini Njombe anaema kuwa hatautamani Urais wa Tanzania kama damu ya watanzania itamwagika katika uchaguzi na kuwa Chadema imejipanga kulinda amani na kuwa Green gadi ya CCM ni mwanzo wa fujo katika uchaguzi agiza polisi kuwakamata

 
Pay God big up. Tunakushukuru kwa picha, mafisadi na mawakala wao roho zitawauma sana ila ndio jimbo la Iringa mjini linaondoka hivyo.
 
Back
Top Bottom