Dr. Slaa: Niko tayari kula mihogo Ikulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa: Niko tayari kula mihogo Ikulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Oct 15, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Joyce Mmasi | Friday, 15 October 2010

  MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Wilbroad Slaa alisema akichaguliwa kuwa rais, serikali yake itaondoa matumizi yote ya anasa na kifahari serikalini, akisema kuwa yuko tayari kula mihogo Ikulu kuliko mayai na mapochopocho huku wananchi wakifa kwa kukosa dawa hospitalini.

  Dk Slaa, ambaye amekuwa akipinga kitendo cha serikali kutenga fedha nyingi kwa ajili ya kukirimu wageni, amesema atafyeka kabisa bajeti hiyo aliyoiita ya chai na vitafunwa ambayo alisema kiwango chake cha fedha huzidi vya baadhi ya wizara muhimu.

  Dk Slaa alisema hayo jana katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika Bunazi, nje kidogo ya mji wa Bukoba ambako alisema ni aibu na fedheha kwa bajeti moja ya chai na vitafunwa ya serikali kutengewa Sh30 bilioni wakati bajeti ya wizara muhimu kama ya Maji na Umwagiliaji ikitengewa Sh29 bilioni.

  "Huu ni ufisadi mkubwa; ni jambo la aibu na fedheha kubwa kwa wizara muhimu kama ya Maji na Umwagiliaji kutengewa bejeti ndogo ukilinganisha na ile chai na vitafunwa ambayo inaizidi kwa bilioni moja zaidi... angalieni wenyewe aibu hii. Nikiingia Ikulu, jambo la kwanza nitalimaliza tatizo hilo," alisema.

  Alisema ataondoa magari ya anasa kwa kuhakikisha watendaji, wakiwemo mawaziri, wanatumia magari aina ya Toyota Land Cruiser-Hardtop maarufu kama mkonge, ambayo alisema bei yake ni Sh60 milioni tu badala ya magari aina ya Toyota Land Cruiser VX ambayo alisema moja hugharimu Sh200 milioni.

  "Nipo tayari kwenye kula mihogo ikulu, badala ya mayai na mapochopocho mengine huku wananchi wangu wanakufa kwa kukosa dawa hospitalini. Serikali ya Chadema itasamehe starehe na anasa zote ili iwatumikie wananchi," alisema.

  Akizungumzia suala la afya, Dk. Slaa alisema Bunge la kwanza la bajeti la serikali yake litatenga fedha za kutosha kwenye sekta ya afya ilio huduma zitolewe bure kwa kila Mtanzania tofauti na hali ilivyo sasa ambayo wenye uwezo wa kiuchumi tu ndio wenye uhakika wa matibabu bora.

  "Mfano ni mimi mwenyewe. Nilivunjika mkono wangu huu (alinyoosha mkono wa kushoto juu), lakini ndani ya kipindi cha mwezi mmoja nimepona na kuweza kuendelea na maisha. Mimi nimeweza kwa sababu nina uwezo wa kulipa zaidi ya Sh4 milioni MOI (Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Muhimbili) Muhimbili. Je ni Watanzania wangapi wenye uwezo kama wa Dk Slaa," alihoji.

  Alisema kutokana na bajeti ndogo ya wizara ya afya, Watanzania wengi wanahukumiwa hukumu ya kifo kwa kuendelea kusumbuliwa na hata kufa kutokana na magonjwa ambayo yanatibika na yalishafutika duniani kote.

  Alitoa mfano ugonjwa hatari wa Malaria ambao unaoongoza kwa vifo vingi nchini licha ya kuwa ni ugonjwa unaotibika na kwamba hata katika maeneo mengine duniani ikiwemo, kisiwani Zanzibar umetokomezwa kabisa.

  "Ni ajabu sana, na ni uthibitisho wa kukosa vipaumbele vya taifa kwa serikali ya CCM kujisifu kuwa inagawa vyandarua. Sasa hivi wanatangaza wanatoa viwili kwa kila familia. Sasa najiuliza, kwa familia yenye watu zaidi ya saba watafanya nini? Hii inamaanisha kuwa wale wengine waendelee kuumwa na mbu na kufa kwa malaria," alisema.

  Wakati huo huo, helkota iliyokuwa ikitumiwa na mgombea huyo wa Chadema katika kampeni zake imetengemaa baada ya kupata hitilafu ya kiufundi na kusababisha mgombea huyo kufanya kampeni zake kwa kutumia magari katika mkoa wa Kigoma. Sasa itaanza kuchanja mbuga wakati Dk Slaa akielekea Mwanza kuendelea na kampeni zake.
   
 2. S

  So Perfect Member

  #2
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Mimi nimeweza kwa sababu nina uwezo wa kulipa zaidi ya Sh4 milioni MOI (Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Muhimbili) Muhimbili. Je ni Watanzania wangapi wenye uwezo kama wa Dk Slaa," alihoji. Awagiwie sasa huo uwezo wake hao masikini ili awe nao sawa yeye si mpenda usawa? adhihirishe kwa vitendo!
   
 3. S

  So Perfect Member

  #3
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Nipo tayari kwenye kula mihogo ikulu". UONGO WA KITOTO HUO
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Aangalie tu asije uziwa mihogo bei ya ikuru, maana wa tz!
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu, kweli wee ni Great Thinker and So Perfect.....................
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mbona Sean Paul hadi leo chakula chake kikuu ni SAMAKI na WALI?

  Huu ushamba wa umepanda ngazi basi unajifanya kuvuta Cuban Ciger na kunywa Whisky Black Label ni ushamba tu.

  Kama anapenda Mihogo na Chai asubihi, kwa nini asile?

  Nina ndugu yangu aliishi sana nje ya Tanzania (Europe/USA). Ila akiwa nyumbani, asubuhi anatununulia mikate na yeye anakula mihogo. Ilidi zipite siku nyingi sana ili nifahamu kwa nini alikuwa akifanya hivyo. Sasa hivi mwenyewe pia ni mla mihogo au kiporwa cha wali asubuhi na mikate huwa naipisha mbali kwa wakuja kama wewe....................
   
 7. d

  dkn Senior Member

  #7
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tatizo kubwa kwa wana-forum wengine ni uwezo wa kutafsiri, Dr. Slaa anaposema kula mihogo siyo kuwa ataishi kwa kula mihogo tu hapana, hapa ina maana fedha zinazotumika na serikali kwa sasa kwa wageni sijui chai nk. ni kubwa sana na yeye akiwa Rais atapunguza hayo matumizi kwa gharama mbadala. Hapa ujumbe mkubwa ni bilioni zilizotumika kwa hayo wanayosema chai nk. yanazidi hata budget ya wizara fulani.

  Tusiangalie uCCM au uCHADEMA au uCUF na vyama vingine bali tuangalie jinsi serikali ya Kikwete inavyofuja fedha za walipa kodi na mfano wa kuigwa ni serikali ya Kenya kila kitu kiko wazi sasa na sisi tuige hayo, kweli kuna ufisadi lakini Kikwete anaweza kutuahidi nini kuhusu wala rushwa wa serikali yake, matumizi mabaya ya fedha atayakomesha vipi..si unaona kina Mramba bado wapo na wana kesi lakini bado wanabebwa.

  Tunahitaji mapinduzi ya kweli sasa, iwe Kikwete au Dr. Slaa wafanyie kazi wananchi siyo urafiki ulikidhiri katika CCM. Afadhali hata Kikwete angegombea kama mgombea binafsi kama sheria ingeruhusu na baraza la mawasiri liwe na watu wenye upeo mkubwa wa kumsaidia siyo kuiba na kumdhalilisha raisi wetu.
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mmmmh NO COMMENT
   
 9. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  dkn

  hii ni tafsiri yako si ya dr slaa wala wanajf wote. Kila mtu anaruhusiwa kuja na tafsiri yake. Acha kuweka maneno yako mdomoni mwa dr slaa unaweza kupotosha maana halisi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  anaposema atakula mihogo hamaaanishi ni mihogo hii
  mnayokula hapo nyuma ya bilicanas
   
 11. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kwani kula mihogo ni maajabu ya dunia?
   
 12. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Wasikuumishe kichwa hawa -- ni mazao ya sekondari za kata. wamedumazwa akili na CCM na hivyo IQ yao kuwa ndogo sana.
   
 13. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  kweli kunawatanzania wavivu wa kufikilia! Yaani hata hilo linakushinda kufikilia duuu!!
   
 14. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tumeijaribu ccm kwa miaka 49,sasa tujaribu chadema kwa miaka mitano.
  ccm imekuwa madarakani kujaribu kuongoza bila mafanikio yaliyotarajiwa,sasa kama wanaona wameshindwa kuleta maisha bora kwa watanzania kwanini wanang'ang'ania Ikulu?vijembe na matisho kwa Kiongozi aliyejitolea mhanga kuleta unafuu wa maisha ya watanzania kweli watanzania bado tunampiga vita?Kweli ukistaajabu ya musa utaona ya firauni.
  Tumpe suport Dr Slaa aweze kupambana na mchwa wa rasilimali za watanzania.
  NINAUNGA MKONO HARAKATI ZA DR SLAA KATIKA MAPAMBANO YA UMASKINI WA WATANZANIA.
  TUNAMUHITAJI NA TUNAMWAMINI NI FALSAFA ITAKAYOKUMBUKWA MILELE DAIMA.TUSIPOTEZE HII LULU.
   
 15. d

  dkn Senior Member

  #15
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mama Porojo..kweli unaporojo. Mfano wa tafsiri ni kama huu "Nitasoma kufa na kupona nifaulu".... hii haina maana atasoma afe, hapana ila inaweza kuwa inamaana atafanya bidii kadri ya uwezo wake afaulu. Sasa sisi tusiangalie haya maneno madogo madogo bali tuangalie ujumbe mkuu kama utendaji wa kazi na facts.... umeshasikia CCM wamekanusha kuwa hizo bilioni hazikutumika Ikulu? zilitumika na document zilikuwa bungeni wakati wa budget na inabidi wafunge midomo..na mengi yameshasemwa na yapo hata nyaraka zinazosambazwa kwa wabunge na Dr. Slaa anaongea facts na zina ushahidi, CCM itabaki ikitumia propaganda bila ku-defend yanayosemwa na upinzani. Mwingine mwenye facts ni Prof. Lipumba
   
 16. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #16
  Oct 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kumbe kuna watu humu wakiambiwa kuwa ni ni rahisi kwa ngamia kupenya kwa tundu la sindano kuliko...... wengi watafikilia tundu la sindano na ngamia kumbe kuna ujumbe mzito apo.
  Mihogo hakumaanisha kama wengi mdhaniavyo jamani khaaa.
  To me means kushiriki na watanzania wengine katika umaskini wao na bse Mihogo kwa watanzania wengine ni zao la wakati wa njaa.
  So chukulia when mhogo unaliwa,jamani watu wako Philosophical
   
 17. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Nasikitika kwa sababu nafahamu kuwa Dr Slaa na Prof Lipumba ni watu makini sana na wenye taarifa hai, na wanajua kutumia taarifa katika kuleta mabadiliko. Kinachonisikitisha ni kuwa kati yao hakuna atakayeshinda kiti cha urais mwaka huu. Kibaya zaidi, hawatakuwepo bungeni ambako Dr Slaa alifanya kazi nzuri mno kwa miaka 15 aliyokuwa bungeni.

  Kitakachofanya Dr Slaa na Lipumba washindwe uchaguzi huu ni idadi ndogo ya wanaowaunga mkono kwa dhati. Upinzani unaungwa mkono kwa dhati na jamii ya wasomi, ambao ni wachache sana Tanzania, hawafiki 10% ya wapiga kura wote. Kama nakumbuka sawasawa, idadi ya watanzania wanaopata elimu ya chuo kikuu ni kama 1% ya wale walioanza pamoja darasa la kwanza. Hawa ni wachache mno kuleta mabadiliko kwa mfumo wa 'one man one vote'. Wengi wanaojazana katika mikutano ya kampeni ni opportunists, wale Kikwete anaowaita 'wafuata upepo', hawana mapenzi ya dhati na wagombea. Hii ndio sababu Dr Slaa anaongoza katika kura za maoni za mtandaoni na za wasomaji wa magazeti, wakati kura kama hiyo miongoni mwa watu wenye viwango duni vya literacy na elimu ya ujumla ndipo JK anapoongoza, na bahati mbaya huko ndiko kwenye wapigakura wengi.

  Nimewahi kuandika kuhusu mawazo yangu ya 'qualitative voting' nikipinga dhana ya 'one man one vote', kwamba dhana ya kura zote kuwa na uzito sawa ni potofu kabisa. Kura inatokana na uamuzi, ambao pia unatokana na uwezo wa mtu kuchambua taarifa zilizoko mbele yake na kufanya 'informed choice'. Uwezo wa kuchambua una uhusiano mkubwa sana na elimu. Upigaji kura wa sasa ni purely quantitative procedure ambayo inapuuza kabisa thamani iliyoko ndani ya kila kura, inachukulia kuwa kila kura ina thamani sawa, jambo ambalo si kweli. Kura iliyotokana na tafakuri ya kina ya masuala makubwa ya taifa hili haiwezi kulingana hata kidogo na ile iliyotokana na zawadi ya khanga au ya kufurahishwa tu na sura ya mtu au hamasa ya muziki wa 'bongo flava'.

  Kura za watu makini zitachukuliwa kwa uzito sawa na zile za wasio makini, na kwa kuwa wasio makini ndio wengi, basi walio makini watashindwa. Validity. Tunahitaji kuangalia upya validity ya mfumo wetu wa kura.
   
 18. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hili alilolisema Dk Slaa kwamba yupo tayari kula mihogo Ikulu halihitaji tafsiri yoyote. Hakuna ubaya wowote kwa Rais kula mihogo akiwa Ikulu, ili mradi kama atafanya hivyo kwa lengo la kubana matumizi ili wananchi wake waneemeke. Huyu ni mtu anayedhihirisha jinsi anavyokerwa na umaskini wa Watanzania na yupo tayari kupambana ili kuuondoa. Kwa maoni yangu huyu ndiye aina ya RAIS anayehitajika katika Tanzania ya leo.
   
 19. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2013
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  WanaJF!

  Huu ni moja ya usanii wa Dr Slaa katika siasa zake zilizo sheheni ulaghai kwa watanzania.

  Dr Slaa ni kinara wa makatibu wakuu wa vyama vya siasa nchini wanao ongoza kwa kuwa na matumizi makubwa ya binafsi kupitia pesa za chama, iweje atoe ahadi kuwa eti mpaka afike Ikulu ndio apunguze matumizi?

  Dr Slaa ni miongoni mwa wapiga kelele kuhusu anasa ya manunuzi magari ya kifahari aina ya shangingi (VX), ila jambo la kushangaza yeye ndiye mtoa pendekezo na msimamizi wa ununuaji magari ya aina ya shangingi baada ya chama kuongezewa ruzuku (hapa ana maanisha mashangingi ndio kipamumbele kwenye chama).

  Dr Slaa amehadaa wana CHADEMA kwa kujifanya mbunifu wa mavuguvugu kama vile operesheni sangara, operesheni okoa kusini na huu mradi mpya M4C kwa kuaminisha watu kuwa operesheni hizi zitajenga chama na kukiimarisha, ila Dr Slaa amezibuni kwa lengo la kuombea misaada.

  Kama Dr Slaa kweli hapendi anasa na kuteketeza pesa, kwanini yeye asishinikize kamati kuu ya chama kuachana na mpango wa Mbowe wa kufanya chama hicho kiwe kwenye nyumba ya kupanga milele, badala yake wafanye mpango wa ujenzi wa jengo la chama?

  Dr Slaa hii nchi ina wenyewe!
   
 20. T

  TECH WIZ JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2013
  Joined: Jun 7, 2013
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wewe lazima utalitafuta tatizo kwa Dr Slaa hakuna siku uliowahi kuzungumza zuri kuhusu huyu Rais mtarajiwa.Sasa sijui 2015 akichukua Nchi utahamia Nchi nyingine?Ila usiwe na shaka 2015 baada ya Dr Slaa kutwaa Ikulu nishtue tu kama utataka kuhamia Nchi nyingine ili nikuchangie pesa ya kununulia one-way ticket na usirudi tena.
   
Loading...