Dr. Slaa: Nikiwa Rais nitamtia Magufuli ndani kwa kuuza nyumba za Serikali

Dr. Slaa akihojiwa na Radio five ya Arusha jioni hii nini maoni yake kuhusu uteuzi wa Magufuli kuwania Urais.

Ameongelea mengi lakini amesema iwapo UKAWA wakimpa nafasi na Watanzania wakampa kura za kutosha kushinda Urais atamtia Magufuri ndani ili kujibu tuhuma za uuzwaji wa Nyumba kwa bei ya kutupa.

Chanzo: Radio five, Arusha

= Magufuli

Kwanza Daktari wa kanoni Padri babu Dr.W.Slaa atueleze jumba la kifahari aliyomjengea hawara yake Josefina kule mabwepande alilijengaje? kwa fedha zipi? akielezea hilo tukaridhika labda na maelezo yake, ndiyo tutamuelewa ya Magufuli.

Isitoshe, nikisoma hapo juu nnaona kuwa babu kisha kata tamaa ya kuwa anaweza kuinusa Ikulu.
 
Last edited by a moderator:
Magufuli hatokuwa na jipya ilani ya chama ndiyo itakayofanya kazi atakuwa si Magufuli yule wa wizara ya ujenzi watanzania msidanganyike ukawa ndio mpango mzima
 
UKAWA ndo nini. Yani tuache kumchagua mtu kama Magufuli tuchague vitu sijui UKAWA labda kama hatujipendi. Tuchague genge la wasakatonge(madaraka) haiwezekani.
 
..hii hoja ikiingia mtaani na kuwa kati ya hoja muhimu ktk uchaguzi huu inaweza kumwangusha magufuli.

..akijitetea kwamba ulikuwa ni uamuzi wa pamoja wa cabinet atakuwa anajiweka ktk nafasi mbaya zaidi. Kitendo hicho kitamfanya aonekane sawa na wala rushwa wengine wa ccm ambao wako tayari kuweka maslahi ya mafisadi mbele, huku wakiweka kando maslahi ya umma.

..lingine linaloweza kumpa shida ni kama na yeye alijimilikisha nyumba za serikali. Kama amefanya hivyo hawezi kusema alikuwa anatekeleza maamuzi ya cabinet.

..kwa upande mwingine nakubaliana na wewe 100% kwamba ukawa watumie muda mwingi kunadi SERA na ILANI yao. Wajifunze toka kwa Mrema ambaye alitumia muda mwingi kuzungumzia kashfa ya chavda badala ya kuwaeleza wapiga kura nini anataka kufanya ikiwa atachaguliwa. Matokeo yake Mrema alishindwa ktk uchaguzi ule.

cc Mkandara, Kimweri, Nguruvi3
..i concur with you joka....ni kweli hoja ya ufisadi ni ya msingi...nadhani kuliko hoja zote...maana ufisadi imekua kama alama ya ccm....Nachokazia ni kwamba isiwe inazungumziwa peke yake...maana kuna issues chungu mzima ambazo umma wa tz hauzijui kuhusu ilani/sera ya UKAWA...in fact watu hawajui kama UKAWA watasimamia sera gani kwa umoja wao....kwa maana ya kwamba sijui kama wame harmonize sera za vyama vyao na kuzifanya kitu kimoja cha kupigania kwa pamoja...Hili ndilo jambo litakalowapambanua dhidi ya magufuli na ccm yake...

....ikumbukwe kuwa hata JK aliyeshinda Dr. Slaa hapo 2010 alikuwa miongoni mwa "list of shame" ya Dr. Slaa ..kwa maana ya mmoja wa mafisadi....lakini hoja hii pekee haikutosha kumpa ushindi Dr. Slaa dhidi ya JK na ccm yake....Kwa hiyo ni wazi kwamba hoja ya ufisadi pekee haitoweza kuwapiga ccm na magufuli....

...hatujui ilani ya ccm inasema nini...lakini inaweza ikaja na mambo haya yoote yanayozungumzwa sana na wapinzani...na ikiwa hivi itakuwa kazi kweli kweli kwa UKAWA wasipojipanga...maana hadi sasa ccm wako mbele yao...kwa maana tayari wana mtu wao wa urais....na soon watakuja na ilani (ambayo seems wameamua ku modify zaidi pia majuzi kwa kuiachia NEC imalizie hiyo kazi)....All said....UKAWA needs to also modify its strategy.....
 
- Kwa hili Slaa hana hoja zaidi ya makelele hewa, uamuzi wa kuwauzia nyumba Wastaafu ulikuwa ni wa Bunge na Serikali ya awamu ya Tatu, ndio maana hata Marehemu Makani aliyekuwa Makamu wa Mwenyekiti wa Chadema na yeye alinufaika na mpango huo uamuzi haukuwa ma Magufuli ila wa Serikali, labda aifungulie mashitaka Serikali na Wabunge wote wa Jamhuri.

- Dr. Slaa angejitahidi sana kuonyesha mahesabu ya Chadema na ruzuku zetu Wananchi walipa kodi badala ya kulilia non ishu!!

Le Mutuz

hivi wewe mbaba na degree zako una sena tatu mbona fikra zako dhaifu kama chatu alie shiba?by tje way nenda kapige picha na mabebez huku hakukufai
 
ccm wana udhaifu mkubwa hata kama nyerere angefufuka na kusimama nadhan angekosa kura za kutosha
 
..hii hoja ikiingia mtaani na kuwa kati ya hoja muhimu ktk uchaguzi huu inaweza kumwangusha magufuli.

..akijitetea kwamba ulikuwa ni uamuzi wa pamoja wa cabinet atakuwa anajiweka ktk nafasi mbaya zaidi. Kitendo hicho kitamfanya aonekane sawa na wala rushwa wengine wa ccm ambao wako tayari kuweka maslahi ya mafisadi mbele, huku wakiweka kando maslahi ya umma.

..lingine linaloweza kumpa shida ni kama na yeye alijimilikisha nyumba za serikali. Kama amefanya hivyo hawezi kusema alikuwa anatekeleza maamuzi ya cabinet.

..kwa upande mwingine nakubaliana na wewe 100% kwamba ukawa watumie muda mwingi kunadi SERA na ILANI yao. Wajifunze toka kwa Mrema ambaye alitumia muda mwingi kuzungumzia kashfa ya chavda badala ya kuwaeleza wapiga kura nini anataka kufanya ikiwa atachaguliwa. Matokeo yake Mrema alishindwa ktk uchaguzi ule.

cc Mkandara, Kimweri, Nguruvi3

Ushauri wa BURE kwa UKAWA.

Magufuli mwepesi sana. Wambane kwenye mambo mawili.

Moja, UBOVU wa Miundombinu aliyosimamia na kujenga. UKAWA wakusanye taarifa za barabara zote zilizojengwa kwa kiwango cha chini wakati wMAGUFULI, ili kuwaonesha kuwa huyu bwana sio msimamizi wa ubora, yeye anajali quantity. Yu can coin a catchphrase ya barabara zake which can resonate with people.

Mfano mnaweza kuziita "barabara za kata" or whatever jargon that your stratergists can come up with. From this point sasa, mwananchi wa kawaida inaanza kumuingia akilini kuwa, kumbe magufuli anajenga chini ya kiwangoo, maana wote wanajua shule za kata ni shule zenye elimu ya kuunga unga. Mkishamuweka on the defensive kwenye barabara basi, amekwisha, hana kingine anachoweza kusema ame-stand out, kwani he is such a one dimensional politician. Hana kauli nzuri, hana busara za kueleweka, na pia maamuzi yake ni ya kukurupuka. Hapa mnaweza kumpin down kama CCM walivyomgeuzia Kibao Lowassa na safari yake ya matumaini. kwa kuwawekea wananchi mfano mwepesi wa wao kufuata. Mfano mnaweza kusema Mkimchagua Magufuli mjiandae kwa "Maamuzi ya hovyo" huku, mkitoa mifano halisi ya maamuzi yake kama ile kesi ya samaki na sheli ya mwanza. at the same time you corelate na umuhimu wa Raisi kuwa na resilience hasa kwa mambo ya kukurupuka,jinsi gani yanaweza kuiingiza nchi matatizoni. Mnaweza waambia wananchi, akichaguliwa Magufuli kuna hatari ya kuingizwa vitani (mungu epusha), kwani Huyu bwana ni mbabe. hapa mnaonesha jinsi gani maraisi wababe wa nchi jirani wameziingiza nchi zao matatizoni kwa kutoa mfano wa Kenya(uamuzi wa kuingia somalia) n.k

By the time wanajipanga kupangua hoja hizi ,matakuwa mmetoka kwenye defensive zone, sasa mnaanza ku-attack Mfumo uliomuweka hapo Magufuli, mkimuunganisha kuchaguliwa kwake kama plan B ya JK kumkomoa Lowassa na kwamba hafai kuwa raisi, kwani hata hiyo nafasi amependelewa, hapo mnachagiza tena kauli mbiu kama "Mgombea wa Goli la Mkono" au Jargon yoyote inayouzika, kuonyeshwa huyu kabebwa.

Mkishaweza kuwaaminisha wananchi kuwa Magufuli kawekwa pale kwa kupendelewa, mtakuwa mmepandikiza mbegu kuwa hakujiamini kupambana na wagombea wenzie kwa uwazi ndio maana walimkata Lowassa,Mwandosya na wagombea wengine tishio kama kina jaji ramadhani, hapa sasa mnaanza kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa wagombea waliokuwa hawana madudu kama kina ramadhani.

mkimaliza hapo lazima Lumumba watafutane.
Tumaini Makene, JokaKuu, Nguruvi3
 
Sijui kama hawa UKAWA wanasoma haya!

Niongezee, huku Sofia akiwakusanya wanawake kumnadi Magu, ni huyo huyo hakukubaliana na maamuzi ya CC.

Ukiunganisha na UWT ilivyo chombo cha wanawake wa wakubwa, akina mana wanabeba bendera na kuzalia juu ya matenga! ile nguvu ya kundi hili inayoyoma.

At the same time wawepo watu watakaoeleza wao watafanya nini mbadala na kwa njia zipi tofauti.

Kampeni ziwe za kisasa, wawepo watu wenye uwezo wa kuangalia mambo, kuunganisha dot na kupeleka mashambulizi ya maana non stop
 
Umeongea la maana, wanahitaji kuwa stratergic sana. Magufuli zitakazomtia matatni ni hizo hizo barabara zake. Miaka -5 anabwabwaja kuhusu flyovers, tatizo la foleni n.k, hajatimiza.Most likely atasema akipewa nchi zitajengwa mara moja. Sasa UKAWA wanatakiwa kumuwahi na kusema alikuwepo wizarani miaka mi-5 hawajajenga flyovers, ila atakuja kujinadi mmumpe kura ndio ajenge.kwa kuwa ziko kwenye mchakato, obviously Magufuli atasema hivyo kwenye kampeni, hence haiwi tena point ya magufuli,inakuwa pre-empted.

watafute wataalamu wa takwimu na hesabu, wawasaidie kutengeneza informatics zinazoeleweka kuonesha jinsi gani bajeti ya barabara ni kubwa lakini barabara ni chache na zenye kiwango cha chini, wanaweza pia kutazama viashiria vingine vingi. Inahitajika timu ya watu makini kukaa chini na kuzichambua taarifa, na kuziweka kwenye lugha nyepesi.

Kuna vitu kama kazi nyingi za barabara kupewa makampuni ya nje, hasa wachina, na watanzania kuishia kuwa vibarua au subcontractrs tu, hili nalo linaweza kuwa turned against magufuli with the right spinning.Narudia tena, huyu bwana akishawekwa kwenye defensive, tayari kazi inakuwa rahisi, yeye kurudi level moja na wagombea wengine, na hapo UKAWA watapata fighting chance.

kingine sio kila political attack kwenda kwa magufuli zitoke ukawa, wanaweza kutafuta fringe candidate nje ya ukawa kazi yake ikawa kusema yale ambayo hayajakaa sawa kwa mgombea serious wa UKAWA kuyasemea, au yako controversial.

MAGUFUFLI kama walivyo watu wengi kutoka mikoa ya kanda ya ziwa,imani ya kishirikina zina mizizi mizito. Mikoa kama shinyanga, mambo kama "mwana malundi", "Gambosh", "wazee wenye macho mekundu kuuliwa" ni vitu vya kawaida. Kutokana na hilo alikuwa mmoja kati ya viongozi wa CCM waliokwenda kwa babu wa loliondo. Nina imani alienda kule kwa kuwa ni mtu anayeamini sana imani zetu za kiafrika. hili lina mema na mabaya yake. Mema kwamba anadumisha mila, mabaya yake ni kuwa Imani hizi zimechangia sana vifo vya ma-albino. Sasa ukimfanya Magufuli aonekane Pro-vifo vya maalbino by association, hapo tayari umemuweka kwenye Huge hurddle, kwani hawa wanaharakati wa ma-albino ni wapiga kelele wazuri.Hili linahitaji umakini mkubwa sana lakini, kwani,ni issue delicate, lakini inauwezo wa kuondoa machachari yote ya Magufuli.

Mimi naamini kuwa MAGUFULI hana jipya kama kiongozi,na sifurahii aina yake ya uongozi, kiutendaji sawa, lakini sio kiuongozi overall.CCM wamemuweka kwa kuwa viongozi wao wazuri hawauziki.

Mwisho kabisa, kama Dr.Slaa aliweza kumfanya sitting president JK kushinda kwa asilimia 60 tu, na wakati huo mafisadi wakiwasaidia CCM, UKAWA hawatakiwi kumuogopa protege wake Magufuli, ambaye kisiasa hamfikii master wake JK hata kwa asilimia 10.Hence, UKAWA< kama wakituliza vichwa wakawa na gameplan nzuri, CCM 50% wataisikia kwenye bomba.

I don't care CCM kushinda au kushindwa, what i care for the most ni hawa wap*uzi wa CCM kutokuwa na majority Bungeni ya kupitisha kila upuuzi wanaotaka. This has to stop ili nchi iendeleee. Ninaamini Raisi wa CCM atakayekosa majority atakuwa kiongozi mzuri kwa taifa, kuliko raisi wa CCM mwenye majority.
 
(1)Umeongea la maana, wanahitaji kuwa stratergic sana. UKAWA wanatakiwa kumuwahi na kusema alikuwepo wizarani miaka mi-5 hawajajenga flyovers, ila atakuja kujinadi mmumpe kura ndio ajenge.kwa kuwa ziko kwenye mchakato, obviously Magufuli atasema hivyo kwenye kampeni, hence haiwi tena point ya magufuli,inakuwa pre-empted.

(2)watafute wataalamu wa takwimu na hesabu, watengeneza informatics zinazoeleweka kuonesha jinsi gani bajeti ya barabara ni kubwa lakini barabara ni chache na zenye kiwango cha chini, wanaweza pia kutazama viashiria vingine vingi.

(3)Inahitajika timu ya watu makini kukaa chini na kuzichambua taarifa, na kuziweka kwenye lugha nyepesi.

(4)Kuna vitu kama kazi nyingi za barabara kupewa makampuni ya nje, hasa wachina, na watanzania kuishia kuwa vibarua au subcontractrs tu, hili nalo linaweza kuwa turned against magufuli with the right spinning.

(5)Narudia tena, huyu bwana akishawekwa kwenye defensive, tayari kazi inakuwa rahisi, yeye kurudi level moja na wagombea wengine, na hapo UKAWA watapata fighting chance.

(6)kingine sio kila political attack kwenda kwa magufuli zitoke ukawa, wanaweza kutafuta fringe candidate nje ya ukawa kazi yake kusema ambayo hayajakaa sawa kwa mgombea serious wa UKAWA kuyasemea, au yako controversial.

(7)MAGUFUFLI kama walivyo watu wengi kutoka mikoa ya kanda ya ziwa,imani ya kishirikina zina mizizi mizito. Mikoa kama shinyanga, mambo kama "mwana malundi", "Gambosh", "wazee wenye macho mekundu kuuliwa" ni vitu vya kawaida. Kutokana na hilo alikuwa mmoja kati ya viongozi wa CCM waliokwenda kwa babu wa loliondo. Nina imani alienda kule kwa kuwa ni mtu anayeamini sana imani zetu za kiafrika. hili lina mema na mabaya yake.

Mema kwamba anadumisha mila, mabaya yake ni kuwa Imani hizi zimechangia sana vifo vya ma-albino. Sasa ukimfanya Magufuli aonekane Pro-vifo vya maalbino by association, hapo tayari umemuweka kwenye Huge hurddle, kwani hawa wanaharakati wa ma-albino ni wapiga kelele wazuri.Hili linahitaji umakini mkubwa sana lakini, kwani,ni issue delicate, lakini inauwezo wa kuondoa machachari yote ya Magufuli.

(8)Mimi naamini kuwa MAGUFULI hana jipya kama kiongozi,na sifurahii aina yake ya uongozi, kiutendaji sawa, lakini sio kiuongozi overall.CCM wamemuweka kwa kuwa viongozi wao wazuri hawauziki.

(9)Dr.Slaa aliweza kumfanya sitting president JK kushinda kwa asilimia 60 tu, na wakati huo mafisadi wakiwasaidia CCM, UKAWA hawatakiwi kumuogopa protege wake Magufuli, ambaye kisiasa hamfikii master wake JK hata kwa asilimia 10.Hence, UKAWA wakituliza vichwa wakawa na gameplan nzuri, CCM 50% wataisikia kwenye bomba.

(10)I don't care CCM kushinda au kushindwa, what i care for the most ni hawa wap*uzi wa CCM kutokuwa na majority Bungeni ya kupitisha kila upuuzi wanaotaka. This has to stop ili nchi iendeleee. Ninaamini Raisi wa CCM atakayekosa majority atakuwa kiongozi mzuri kwa taifa, kuliko raisi wa CCM mwenye majority.
Mkuu tuanzie na hoja namba (10).
Wananchi watambue,nguvu ya CCM ni bunge si wananchi au serikali. Tumeona miswada ikipitishwa'bila' kujadiliwa.

Mswada wa gesi na mafuta unawezaje kujadiliwa kwa masaa kwa kuzingatia umuhimu wake? UKAWA wangekwenda kuwauliza wananchi, je wanafahamu miswada inasema nini? Kama hawajui ni kwanini.
Na je, wapo tayari kuendelea kuburuzwa au ni wakati wa kupeleka wabunge kuzuia ulaghai!

Hoja namba(8) Magufuli ni administrator siyo leader. Ndio maana anajivunia utendaji na si ungozi.
Hana historia ya kusimama kama kiongozi, husimama kama mtendaji.

Madudu ya serikalini hawezi kusema alifanya hivi au pale nilipinga kile au kushauri vile

Hoja namba (7), akiwa mbunge na waziri, yeye kama yeye amesimama wapi na lini kuonyesha njia za kukabiliana na mauaji ya Albino na vikongwe?

Haoja (6). Tumesema kuhusu &#8216;attacking dog' sasa atakaposimama M-KAWA kujibu hoja za Samia, inampa nafasi Magufuli.

Kusimama na mwanamama tayari ni kosa kabla ya hoja(ndivyo jamii ilivyo).

Tumeuliza wale wa kukabiliana na Samia wapo wapi? Ukawa wanawake wapo wapi?

Watu wanakumbuka Sarah Palin na Trump kuhusu birth certificate ya Obama?
Wanamkumbuka Joe the plumber, hawa walikuwa wavurugaji Mcain akimwaga sera

Hoja (5), ukimlinganisha na mgombea mwingine, Magufuli ni 'vulnerable'

Maamuzi mengi alishiriki hata Hansard zinaonyesha msimamo wake. Hizo tu zinampleka katika &#8216;defensive'

Hoja (3), hilo neno lugha rahisi ni muhimu sana. Wakienda Magoroto au Mtimbira ukaongelea GDP nani ataelewa?

Lakini , wakiongelea huduma za afya na jinsi zinavyoweza kuboreshwa watakuelewa.

Watumie takwimu rahisi , misamaha ya kodi na wizi inavyoonyeshwa n.k.
Halafu weka gharama dhidi ya hasara kwa lugha rahisi

Waonyeshe tatizo,na kisha ufumbuzi na wanafikiria kufanya nini tofauti

Wakieleza watu wanachangia maabara kwasababu pesa za maabara zimetolewa kama misamaha ya kodi , wataeleweka.

Kwamba michango yao ya maabara ingeweza kujenga chumba kingine cha hospitali, badaa yake imejenga maumbo

Timu iwe ya watu wenye weledi wa siasa, mawasiliano, uchumi, na sayansi ya jamii, siyo wanaozungumzia global warming

Mwananchi aliyeshinda na njaa ili anunue kidonge cha asprin hana habari na global warning
 
KAWADANGANYE WATOTO WADOGO NA WAZEE VIJIJINI. HEBU TUAMBIE ATATUMIA SHERIA GANI KUVUNJA MIKATABA YA MAUZIANO? OFFER ikishakuwa ACCEPTED IT CAN NOT BE REVOKED.

Mikataba yenye nia mbaya ni batili. Isitoshe nyumba zinaweza kutaifishwa na fedha zikarudishwa.
 
Hoja namba (7), akiwa mbunge na waziri, yeye kama yeye amesimama wapi na lini kuonyesha njia za kukabiliana na mauaji ya Albino na vikongwe?

It will be pathetic to invoke the albino killings for political tussle of votes. Bila ya kuwa na ushahidi wa yeye binafsi kuhusika, sidhani kama ni hekima kumjumuisha yeye katika matendo hayo ya kinyama, kisa siasa.

Last edited by a moderator:
It will be pathetic to invoke the albino killings for political tussle of votes. Bila ya kuwa na ushahidi wa yeye binafsi kuhusika, sidhani kama ni hekima kumjumuisha yeye katika matendo hayo ya kinyama, kisa siasa.

Nakataa, CCM wameshindwa kuzuia mauaji ya ALBINO, sio CHADEMA. Hili sio kosa la CHADEMA. kama weakness ni CCM kushindwa kuzuia maalbino wasiuliwe, kwa nini CDM wasiliongelee?

Implication ya Magufuli, ni kitendo cha yeye, kuamini waziwazi imani za kishirikina(kama zinavyoitwa). Hawezi kujitenga na hili, kwani yuko on record, akiongelea issue ya mbuyu kushindwa kukatwa hadi wazee walipoombwa.Huyu ni mtu anayeamini sayansi yetu ilee.

Magufuli anajinasibisha na wasomi, halafu alikuwa kwenye msururu wa kikombe cha babu, sasa huu usomi au vituko. Huyu ni jamii ya wanasiasa na wasomi wa Kitanzania, ambao bado imani za pata potea zimeshamiri mioyoni mwao. siko hapa kumuhukumu kwa hilo. Niko hapa kuweka mwanga kwenye hii side ya magufuli, aache unafki.

Tuache unafki, sayansi yetu ya jadi ndio sababu kuu ya mauaji ya albino.MAGUFULI hawezi kuchomoka hapa, kama wakiweka attack dog anayejua kubwabwaja hasa na akapewa proper air time. hii karata UKAWA waicheze vizuri, kwani imani zetu hizi ni sehemu muhimu ya jamii yetu, ingawa ndio hizo zinaleta maafa kwa maalbino. Kwa mfano, hii hoja sio ya kuiongelea Mikoa ya kanda ya ziwa, kwani kule mambo kama gambosh yako kwenye damu ya watu. kila mtu anaamini bibi mwenye mifugo mingi wale ni misukule wake n.k, this is fact sio hadithi.

Hoja ya kumdisown magufuli kutokana na imani za kishirikina inatakiwa iongelewe kwa wapiga kura progressive, sehemu za mijini hasa miji kama morogoro,arusha,kilimanjaro, dodoma, dar es salaam n.k, ambako ushirikina haujafikia kiwango kikubwa sana.

Hoja hii ikiongewa kwa proper channels, hasa social medias, inatosha kabisa kupunguza kura za wasomi kwa magufuli.

Niko hapa ku-incite UKAWA walete proper fight, hata kama kutakuwa na under the belt blows. UKAWA Wasijidanganye kuwa wakisimamisha mgombea wao, CCM will always play clean, hawana historia hiyo.
 
Unamaanisha nini unaposema mikataba yenye nia mbaya? Bila shaka unajua migogolo ya ardhi ilivyo mingi na serikali imeshindwa kuitaifishwa ardhi iliyochukuliwa na wawekezaji kwa uhalali kupitia serikali za vijiji na hatimaye wawekezaji wakapata hati kutoka ofisi za ardhi makao makuu. sio rahisi kiasi hicho kutaifisha mali ya mtu.
 
JokaKuu,

Mkuu unajua haya maswala ya Ufisadi yameshafika mwisho wa kuzungumziwa, sio tishio tena kisiasa ni sifa kwa wadanganyika (Lowassa) kwa hiyo mimi nadhani mgombea mzuri ni yule atakaye pindua pindua sera za CCM. Kuichambua ILANI ya CCM ambayo kwa kiwango kikubwa bado ni tegemezi japo JK kaweka madai yake kuwa wamekata utegemezi kwa kiango kikubwa, mfumko wa bei ambao pia JK kasema umepungua sio Uhalisia! (siamini). Huduma za AFYA, ELIMU, AJIRA, KODI, USALAMA, USAFIRI na MAWASILIANO inatakiwa data kamili maadam Magufuli anasifika kwa takwimu, mgombea lazima awe pia mtu wa takwimu na haswa kumbana Magufuli katika QUALITY na sio QUANTITY (kama ulivyosema).

Kama kulikuwa na mwaka ambao Upinzani wangeweza kuchukua nchi kwa kupitia UFISADI basi ilikuwa mwaka 2010 lakini CCM walitafuta penyo z akutokea na hizo ndio iwe kazi kubwa ya Upinzani kuondoa hiyo mitija ilivujisha Uchaguzi wa mwaka 2015 laa sivyo yatakuwa yale yale. Ufisadi ni swala la kulaaniwa kimya kimya, ukiingia ndio unawashangaza watu sio sifa tena imeshakuwa hadith hadith...

Tatizo la Kutupiana madongo na kuchafuana limekosa uzito kwa sababu bado sheria inawlainda baadhi ya watu. Penye KASHFA watu watasema ni TUHUMA, hivyo utahitaji Ushahidi. lakini KASHFA haina ushihidi maadam kiongozi katika wizara yake kumetokea Ufisadi anakuwa Accountable for kwa sababu kama kashindwa kuongoza wizara moja tu atawezaje kuongoza wizara 20 na kitu.

Ndio maana Dr.Slaa anasema akiwa rais atamtia Magufuli ndani kwa kuuza nyumba, lakini ukweli ni kwamba huwezi kushinda uchaguzi kwa kutegemea NIKIWA (IFs).. Ili uwe rais ni lazima uwaonyeshe kwanza wananchi utawafanyia nini zaidi ya kushughulikia majina ya watu. Ufisadi ni mpana zaidi ya Magufuli, onyesha unachoweza kufanya Magufuli hakiwezi.

Kwa Dr.Slaa kusema kweli safari hii sitompa nafasi ya Ushindi kwa sababu kapata mshindani mzito zaidi yake. Magufuli ana nyota, ni aina ya kiongozi wananchi walimtaka kwa muda mrefu sana, ni mfano wa Kagame wa Tanzania na yawezekana kabisa walomchagua wakaja jutia maamuzi yao. UKAWA kusema kweli walisha chemsha, nilisema toka mwanzo probability ya ushindi kwenye Wabunge na Urais ni hakuna ila wanaweza kupata wabunge wengi kuliko mwaka 2010, Bila shaka wataongeza mfuko wao wa ruzuku na Uheshimiwa lakini ktk Uhalisia hakuna USHINDI..
 
Mkandara,

..kilichonifurahisha ktk statement yz dr.slaa ni kwamba hamuogopi magufuli.

..wakati wengine tayari wanafikiria baraza la mawaziri la dr.magufuli, dr.slaa anafikiria kumsweka ndani kwa tuhuma za ufisadi.

..that is a big plus for me. That is the candidate i wanna vote for.

..magufuli amezoea kunyenyekewa, kuogopwa,kusifiwa, na kushangiliwa. He has not been tested.

..mimi naamini ukawa wanaweza kushinda uraisi na kupata wabunge wengi. Wanachotakiwa kufanya ni kuweka mjenga hoja mzuri atakayeweza kupambana pound-for-pound na magufuli ktk kunadi sera za ukawa.

..naamini Dr.Slaa au Tundu Lissu wanaweza kuleta ushindi kwa ukawa.
 
Last edited by a moderator:
Kiongozi pekee mfano wa Kagame aliyepita Tanzania ni Marehem Edward Moringe Sokoine.It is very unfortunate kwamba hakuwahi kuuona urais.Sijui kama muanzisha kamba alikuwepo miaka ile lkn kama sio basi nimuambie Sokoine hakuwa na doa hata moja na wanaokumbuka statement zake wanajua.Hakuwa anao e haya mpaka wakongwe ktk chama chake.Huyu atatishatisha tu Wakandarasi ,wezi na wala rushwa ndogo ndogo sijui manesi police lkn sio yale ma syndicate makali kama madawa ya kulevya,ujangili ,kashfa kali za wizi km escrow,kagoda agriculture,iptl,songas.Naona watu washaweka matumain makubwa kwake .Angewekwa Jaji Augustino ningesema sawa lkn huyu jamaa sijamkubali na atafail tu
 
Back
Top Bottom