Dr. Slaa ni mjamaa, gumzo kuhusu anavyoishi Canada linathibitisha ujamaa wake

Mbona unajichanganya sana unasema Dr Slaa ni mjamaa na mtu makini lakini wewe ulikataa kujiunga Chadema kwa sababu ya itikadi yao sio ya kijamaa so ilikuaje mjamaa makini akawa Katibu Mkuu wa chama kisicho cha kijamaa?
Huyu mwandishi aitwae Majjid Mjengwa huwa hana logical consistence kwenye maandiko yake mengi.Ni mtu mnafiki mwenye kujikomba upande wenye maslahi.
 
ujamaa ulimshinda nyerere, ni falsafa ya kufikirika

Who is Nyerere in this world? Tunaposema siasa za dunia hii hatutakiwi kujikita kwa binadamu mmoja aliyeishi eneo dogo sana hapa duniani linaloitwa Tanzania.

Kazi ya kujikita tuwache waumini wa huyo jamaa ambao nao ni wachache sana hapa duniani na hawasikiki kokote zaidi ya hako ka-eneno kanakoitwa Tanzania?
 
You must be kiddin' me. Babu anabeba boksi kwa $10 per hour Costco, na ni wazi ame-surrender to capitalism sababu hawezi pata ajira mbadala inayolipa zaidi pamoja na (relative) IQ yake kubwa halafu unakuja na rhetorics za mjamaa na ujamaa as if its a virtue or virtuous?
huwa nawashangaa wajamaa, kujisifu kwingi lakini wanaenda kutalii na kupiga picha nchi za kbepari,

mjamaa anaenda kuwa shopkeeper kwenye nchi ya kibepari .

huyu majidd! kama ccm wanamtegemea kujenga hoja wamepoteza
 
Maggid sitaki kupinga sifa zote ulizomwagia Dr. Slaa kwani hata mimi mbali na mapungufu yake bado naheshimu mchango wake kwa cdm, upinzani na siasa za nchi yetu kwa ujumla. Hivyo najizuia kumkashifu japo sijakubaliana na kitendo chake cha kususia kile alichokipigania ila naheshimu msimamo wake. Sasa naomba nikuulize, hivi sheria za Canada zikoje? Wanaajiriwa hata watu wa umri wake? Maana nijuavyo Slaa kwa umri alio nao ni wa mstaafu, sasa iweje kapata ajira kwa umri huo? Hebu nisaidie isije ikawa tunaingizana mjini kwa kuwa hatujui sheria za ajira nchini Canada.

Halafu hii zana kwamba watu hawataki kazi, kuna viwanda au ajira zilizo wazi na watu hawataki kwenda kujaza hizo nafasi? Mnaposema watu hawataki kufanya kazi huwa mnamaanisha nini? Nijuavyo mimi kama hujapata kazi ya ajira ili ufanye shughuli nyingine unapaswa wangalau kuwa na mtaji, je mtu kapuku anapata wapi mtaji wa kufanya biashara? Je mmewahi kujiuliza watu waliokopa kisha biashara kuanguka kutokana na sababu mbalimbali wanaishije? Kama kweli Dr. Slaa au wewe unamuwekea maneno mdomo atume nafasi za kazi zilizoko kwenye hiyo supermarket huko Canada aone kama kesho haijajaza watu kwa usaili.
 
Ujamaa uzungumzwao hapa ni ktk ngazi ya taifa, Halafu muwe mnasoma na vitabu sio tu kukaririshwa. Inaonekana hadi leo hata hujui tofauti kati ya Ujamaa, socialism na communism, kwako tofauti ni lugha yaani Ujamaa ndio socialism.

Wengine tunaposema tu Wajamaa na zaidi Social Democrat inahusu itikadi yenye kuangalia maslahi ya wengi. Hata kama Kuna masheikh wamethibitishwa kula nyama ya nguruwe, Waislamu hawawezi ama kuhalilisha nguruwe au kuukana Uislamu. Hivyo, itikadi ya mtu ni imani ya mtu kwenye itikadi, na inapotokea kuna wenye kwenda kinyume na itikadi haimaanishi itikadi ni mbaya kwa ujumla wake. Bila kusahau, itikadi iliyo imara ni ile yenye kuendana na mabadiliko ya wakati bila kuacha misingi yake. Nina furaha na najivunia sikuzaliwa kwenye nchi ya kibepari. Kwa kusema hayo sina maana pia kwenye Ujamaa hakutakiwi kuwepo na mabepari, isipokuwa, mabepari watozwe kodi stahiki kusaidia kuwainua walio chini ikiwamo kupata huduma bora za afya, elimu na mawasiliano.
 
...hata msemeje lakini all in all charity begins at home....huwezi kukimbia family nyumbani ukaenda nje ya nchi ukajifanya sijui mchapa kazi mara mzalendo na bla bla nyingine....mfano bora huonekana nyumbani.... I mean kwenye family...hayo mengine yote ni unafiki tu....
 
Mzee mbona umearibu kikubwa hivyo...
Unaongelea kujitegemea kwenye ujamaa kweli bora ulikataa kwenda cdm maana ungewadanganya wananchi
 
Mimi Dr nitaendelea kumheshimu kwa jinsi alivyojitolea ili kuleta mabadiliko ya kweli ktk siasa za nchi hii (Tz).
Katika watu ninaowadharau mmoja wao ni huyu Dk Slaa. Ni mtu asie na msimamo, amejaa mambo ya hovyo, mara kalikimbia kanisa mara kakwapua mke wa mtu, mara kawasaliti wenzake kwenye siasa. Matokeo yake kaishia kuuza kiduka cha masufuria na vikombo, zambi ya usaliti haitamwacha salama huyu babu. We na uzee ule bado unafanya kibarua cha kuosha masufiria.
 
Mleta thread mnafiki tu hamna kitu, na huyo Slaa wake hawatofautiani kwani hakuwa na uwezo wa kwenda kuishi Canada kama isingekuwa hongo aliyopewa na ccm.
 
Mleta thread mnafiki tu hamna kitu, na huyo Slaa wake hawatofautiani kwani hakuwa na uwezo wa kwenda kuishi Canada kama isingekuwa hongo aliyopewa na ccm.
Nyanjo Migire, hujajibu hoja wala kuleta hoja mpya. Umeishia kunishambulia mimi mtoa hoja. Sina tatizo na hilo. Shukran.
 
Ndugu zangu,

Jana na leo kwenye gazeti la Mtanzania kuna habari kumhusu Dr Slaa na anavyoishi akiwa ughaibuni.

Inasemwa, kuwa kuna wenye kumshangaa Dr Slaa kufanya kazi ikiwamo ya kwenye duka kubwa huko aliko.

Dr Slaa kupitia majibu yake kwa mwanahabari wa gazeti hilo ameweza kuweka wazi umuhimu wa kazi na kuthamini kazi. Umuhimu wa kujitegemea na kusimamia kanuni zinazokuongoza mwanadamu katika maisha.

Ameliona pia tatizo kubwa tulilo nalo sasa na kutaadharisha tabia ya Watanzania kutafuta njia za mkato kwenye kupata mafanikio.

Amenukuliwa akisema; " Kila mara nimekuwa nikiwataka Watanzania na vijana wafanye kazi, kwani fedha haziji kwa kukesha kwenye mitandao wala propaganda."

Dr Slaa huko aliko ajue tu, siku hizi huku nyumbani vijana wamejikita pia kwenye kucheza kamari/ kubeti na kuigeuza kuwa ndio ajira.

Dr Slaa aliachana na siasa za vyama Julai 28, 2015 kwa madai ya kuona misingi ya chama alichoshiriki kukijenga imepotoshwa. Ni pale CHADEMA ilipomkaribisha Mheshimiwa Edward Lowassa. Dr Slaa aliweka sharti akiitaka Chadema imtake Lowassa kujisafisha kwanza dhidi ya tuhuma ya kashfa ya Richmond aliyohusishwa nayo akiwa Waziri Mkuu.

Nakumbuka nilimsikiliza Dr Slaa akiongea na Taifa akitangaza rasmi kuachana na siasa. Nikaandika, kuwa binafsi naamini Dr Slaa hajaachana na siasa, bali siasa za vyama.

Kwamba siku zote, kiongozi makini ni yule anayejijua na kuujua wakati unaomzunguka. Nikampongeza ndugu yangu Dr Slaa kwa maamuzi yake yaliyotokana na kusukumwa na dhamira yake. Mchango wake kwa ustawi wa nchi yetu utaendelea kuhitajika.

Nilivyokutana kwa mara ya kwanza na Dr Slaa..

Juni , 2004, nilitambulishwa mara ya kwanza kwa Dr Slaa na ndugu yangu na Mjamaa mwenzangu, Zitto Kabwe. Nikiwa ofisini kwake pale Mtaa Togo, Ndugu yangu Zitto alinishawishi sana nijiunge na Chadema, nikamwambia, asihangaike sana, hilo haliwezekani.

Chadema kwangu ni chama chenye kufuata itikadi ya Kihafidhina ( Kibepari) na mimi ni Mjamaa, na zaidi Social Democrat. Isitoshe mimi naamini mtu anaweza kushiriki siasa hata bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Naamini pia, kuwa kushiriki uongozi si lazima mtu uwe Diwani au Mbunge.

Mathalan, siwezi katika maisha yangu kufikiri kuwa kwenye msafara wa chama kilichokaribishwa kwenye kongamano la chama rafiki cha Republican cha Donald Trump!

Kwa siku mbili, Desemba 31, 2010 hadi Januari Mosi, 2011, nilipata fursa ya kuwa na Dr Slaa pale Mikumi National Park. Ilitokea tukakutana pale, mimi nikiwa na familia yangu na yeye na familia yake. Ilikuwa ni mapumziko ya Krismasi na Mwaka Mpya.

Nilipata kuongea kwa kirefu sana na Dr Slaa. Nilimfahamu zaidi Dr Slaa katika siku zile mbili tukiwa pamoja kwenye mazingira ya kawaida kabisa na ya kifamilia.

Dr Slaa ni mtu makini sana. Ana uzoefu wa mambo mengi. Ni mcheshi na hakujisikia vibaya hata nilipomkosoa kwenye baadhi ya mitazamo ya Chadema.

Kwangu mimi Dr Slaa ni Mjamaa mwenye kuamini pia kwenye kujenga misingi ya kujitegemea. Ni Social Democrat pia kwa maana ya ni mtu mwenye mwenye kufikiri zaidi kwenye ustawi wa jamii pana badala ya ustawi wa wachache. Dr Slaa ni Social Democrat pia katika kuamini kwenye misingi ya uwepo wa demokrasia na kuruhusu uhuru wa fikra.

Nakumbuka, mama wa familia moja iliyokuja Mikumi kwa mapumziko alikuja na binti yake na kukaa jirani na nilipokaa mimi na Dr Slaa.

Mama yule akasema;

" Mheshimiwa, mimi na mume wangu ni Wana-CCM, lakini binti yangu huyu anaipenda sana Chadema kwa sababu yako!"

Dr Slaa, alifurahi sana na akamwambia mama yule;

" Tafadhali naomba nipige nae picha!"

Na ni nani wa kuipiga picha hiyo, kama si mimi ' Mwenyekiti Wenu!"

Naam, huyo ndio Dr Slaa ninayemfahamu mimi, maisha yake anayoishi huko aliko ni sehemu ya mafundisho kwa wananchi wa kawaida na viongozi.

Tuthamini kazi, tuhimize watu wetu kufanya kazi, na kwamba hakuna njia za mkato katika kujipatia mafanikio, iwe kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla.

Maggid Mjengwa.

0688 37 36 52 ( Whatsapp)
Huyu Mzee ni mpumbavu kweli, sijui hata Elimu yake imeshindwa kumsaidia anateswa na laana ya usaliti,Tanzania kuna kazi gani? Eti watu wanashinda mtandaoni, alitaka washinde wapi? Watu Watu wanapiga pesa nyingi FOREX, eti anaponda watu. Hata Ku bet kuna pesa nyingi kuliko kufungua duka, asifundishe watu namna ya kuishi, maisha ni namna yoyote, bora tu usiibe au kudhulumu MTU.

Huyu Mzee ni mpumbavu kweli, sijui hata
 
Ujamaa ni msingi wa maisha unaoharibu uchumi.

Halafu, ukiongelea ujamaa, hutakiwi kuongelea kujitegemea. Kwa sababu kujitegemea ni kinyume cha ujamaa.

Ujamaa ni kutegemeana, sasa utaongeleaje kujitegemea katika kutegemeana?
Power.
 
Back
Top Bottom