Dr Slaa ni Kiboko; Serikali yaamuru Bei za saruji, nondo zishushwe, sera za Chadema! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa ni Kiboko; Serikali yaamuru Bei za saruji, nondo zishushwe, sera za Chadema!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Not_Yet_Uhuru, Oct 25, 2010.

 1. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  SERIKALI YATEKELEZA KAULI ZA DR SLAA NA SERA ZA CHADEMA TAYARI!!

  Serikali ya CCM wanakimbiana kutokana na Nguvu na ukweli wa Uwezo wa Dr Slaa, yaogopa kila kitu kinachosemwa katika Sera za CHADEMA. Sasa imefikia kujikanyaga hadi kuamuru waziri wake afanye jinsi ashushe bei za Saruji, nondo na bidhaa nyingine...Aibuu!  WanaJF, taarifa ya nipashe ipo chini hapa....

  ----------------------------------
  NA GAZETI LA NIPASHE
  20th October 10

  Serikali: Bei za saruji, nondo zishushwe

  Richard Makore


  Serikali imeviagiza viwanda vya saruji na nondo nchini kuhakikisha vinapunguza bei ya bidhaa hizo kwa kuwa hakuna sababu yoyote ya msingi inayochangia zipande mara kwa mara.
  Agizo hilo lilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara Viwanda, Biashara na Masoko, Joyce Mapunjo, alipozungumza na NIPASHE kuhusu upandaji holela wa bidhaa hizo.
  Alisema uzalishaji wa saruji na nondo ni mkubwa lakini hajui kwanini wazalishaji hao wanazipandisha na kuwafanya wananchi wa kawaida kushindwa kuzinunua.
  Aliahidi kufuatilia kwenye viwanda hivyo ili aelezwe sababu zinazowafanya wazidi kupandisha bidhaa zao kwa mauzo ya jumla na hivyo kuwafanya wauzaji wa rejareja nao kupandisha bei.
  Bei ya nondo yenye milimita 10 yenye urefu wa futi 40 kwa sasa ni Sh.10,000 kutoka Sh. 8,000 milimita 12 Sh. 13,000 badala ya Sh. 12,000 na bei ya mfuko mmoja wa saruji hivi sasa ni Sh. 13,000 badala ya Sh. 12,000.
  Na katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Wakala wa Serikali Biashara na Leseni nchini (Brela), Esteriamo Mahingila, aliwataka wazalishaji na wakulma kujiwekea malengo ili kuhakikisha wanaziwekea nembo bidhaa zao zote wanazozalisha.
  Mahingila alikuwa akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wataalamu wa masuala ya hakimiliki duniani ambao wanahakikisha bidhaa zinakuwa na nembo na alama kabla ya kuuzwa.

  ------------------------------------
  CCM TUNAWAARIFU UKWELI HUU! Subirini KIDOGO muone nchi inavyoongozwa kuanzia hapo baada ya kura hapo 31 Oct. Wananchi watafumbuka macho na gharama zitakuwa chini wafurahie maziwa na asali katika nchi yao. Mtasahaulika mara moja katika historia!!
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hata wakishusha cement hadi 8000/= hawachaguliwi na mtu!
  Wakubali tu kuwa wanatoa harufu ya muozo, hatuwataki!
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Hizi ni chechemea za mshindwa kamwe hatuwezi kupokea danganya toto.........
   
 4. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mh! hili sijui,
  Lakini si ajabu mbona mambo mengi tu ya Dr. Slaa huwa wanasema hivyo hivyo kuwa mwongo hayatekelezeki halafu wanafanya.
  huko ni kutapatapa ili kuwahadaa wananchi, maana watapandisha kesho tu, na hao wapiga kura wake walie
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Walisema watapeleka umeme Busanda waliposhinda hawakupeleka hatuwapi ushindi tutampa slaa kumbe inawezekana kumbe hata elimu bure tutaweza tunaomba wagombea wote wa Upinzani wawaeleze wananchi kwamba hiyo ni rushwa kutoka serikali kwenda kwa wanachi baada ya uchaguzi hakuna kitu kitattekelezwa
   
 6. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  CCM kwa rushwa mbona kawaida yao, Lkini mwaka huu ushenzi wao imekula kwao,
  Wamelikoroga, lazima walinywe
   
 7. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135

  Rutaaaaaaaa upo weye? umeshanunua suti ya kushangilia ushindi wa cham chetu?
   
 8. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Serikali haitakiwi iagize viwanda inatakiwa utoe kodi kwenye hizo bidhaa automaticaly bei zitapunguza bila ya kutoa ushuru haiwezekani................
   
 9. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  CCM kimebaki chama cha COPY and PASTE!! - Chadema ndiyo wanaongoza nchi hii - kila DR Slaa anachosema wanatekeleza na bado utasikia wanafuta ada zote za shule.

  Wanakumbuka shuka kumeshakucha.
   
 10. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mbona nimesikia nadhani leo asubuhi kwenye mapition ya magazeti kuwa CCM inatoa elimu bure tayari......Sikumbuki ni gazeti gani ila anayekumbuka anaweza kunisaidia.
   
 11. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naam Rais akinguruma nchi inatetemeka. Tunataka saruji 5000/= bila cent
   
 12. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mi nasubiri tu uongozi mpya nianze ujenzi fasta. Nyumba za kupanga zimenichosha
   
 13. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Wanampigia Dr. Slaa kampeni hivyo. Watanzania watajua kumbe ilikwa inawezekana, lakini haikuwa hivyo mpaka Dr. Slaa alipotamka. Watanzania watajua kuwa mtetezi wao ni nani hasa!
   
 14. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Hata kama Saruji itauzwa Sh. 5,000/= leo, CCM haifai kupewa kura kwani itakuwa danganyatoto.
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Wanatapatapa, sa hivi hatujengi hadi baada ya uchaguzi!
   
 16. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hata wafanye vp haja sijisaidii n'go, ccm wakujisitiriiii kwa fweza za walipa kodi mmetuletea ukatiliii..
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hata washushe mfuko wa cement ufike buku shi tano na bati mia 2 hawapati kura
   
 18. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hivi vitu vinawezekana ni basi tu hawataki kukubali!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
   
 19. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280

  Nakumbuka pia kwamba sisiemu waliiba sera ya CUF ya kufuta kodi ya maendeleo iliyokuwa ni mzigo kwa wananchi. Ilikuwa ni enzi zile Mramba akiwa waziri wa fedha. Sisiemu kwa copy and paste hawajambo!
   
 20. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #20
  Oct 25, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yuko wapi yule Kilaza Kamalaaaaa, nchi hii bwna bila mtulinga haiendi.
   
Loading...