Dr slaa,ndesamburo: Ni viongozi makini au wachochezi mahiri?

jamani...kwani hamjui zomba amekula ban jana ....anazo ID nyingi na pia hazitumiki muda..... angalia profile ya Dos Santos



Join Date: Mon Nov 2010

Posts11

Thanks0
 
Hoja ya nini kilitokea Arusha na nani alisababisha inaweza kujieleza vizuri kama tutafuatilia mchakato mzima kabla na baada ya tukio lenyewe.Tayari CHADEMA walishafanya mawasiliano ya kutosha na polisi na ngazi ya wilaya ambayo ndio tukio halisi la maandamano lilipokuwa litokee walishatoa baraka zote.Majadiliano ya maandamano yalikuwa ni mlolongo wa vikao na maongezi toka Dec 22,2010.Sasa kilicholeta tafrani ni ile haki ya watu kuandamana kupingwa na jeshi la polisi tena kwenye vyombo vya habari kwa kisingizio cha taarifa za kiintelijensia.Na hata katika taarifa iliyosomwa na jeshi la polisi wanasema walifikia kutumia risasi za moto kwa sababu watu walitaka kuvamia kituo cha polisi.Ukweli ni kwamba Denis Michael Shirima alipigwa risasi maeneo ya kaloleni karibu na baa maarufu picknick.Kutoka sehemu hiyo shirima alipopigwa risasi mpaka kituo cha polisi ni wastani wa km moja na nusu.Ismail Omari alipigwa risasi maeneo ya philips ambapo ni wastani wa km moja narobo kufikia kituo cha polisi.nae raiya wa kenya Paulo Njuguna alipigwa risasi akiwa maeneo ya Jogoo house karibu na kituo cha mabasi cha arusha na benki ya CRDB.Kwa mantiki hiyo wote hawakuwa wamesogelea kituo cha polisi.

Kuhusu nani amesema nini na kikapelekea nini haiwezi kubadili sura kwa chanzo chote cha machafuko haya ni kuingiliwa kwa vyombo vya ulinzi ambavyo kimsingi ni vya wananchi.vikaingiliwa na wanasiasa ili kuzuia maandamano ya amani ya Chadema.Tena walikuwa wameandamana kwa karibu kilometa 2 walikuwa wamebakiza moja tu ndipo polisi wakaanza kupiga na hata kuua.Walifanya hivyo ili kauli ya mkuu wao isionekane ni ya uongo.
Hizi ndio habari muhimu ambazo Dunia inapaswa kufahamishwa. Haya ni mauaji ya kukusudia kabisa.
 
Mandela,Kenyata,Samora,Kabila na wengine wengi tu waliitwa ni wachochezi na waliokuwa madarakani kwa wakati huo.Sisi tuliwaita ni wapigania uhuru na mashujaa.Kwa hiyo wewe waite wapambanaji wetu vyovyote utakavyo,ukweli hautabadilishwa kwa namna utavyowaita.

Asante
 
Back
Top Bottom