Dr slaa,ndesamburo: Ni viongozi makini au wachochezi mahiri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr slaa,ndesamburo: Ni viongozi makini au wachochezi mahiri?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dos santos, Jan 19, 2011.

 1. d

  dos santos JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Nilikuwa naangalia kipindi maalumu(kimeandaliwa na wizara ya habari) kilichokuwa kinarushwa katika televisheni,kilichokuwa kinaelezea tukio zima la maandamano ya wafauasi wa CHADEMA wakipambana na jeshi la polisi mjini Arusha.Ni picha ambazo sikuwahi kuziona katika chombo chochote cha habari,wakati wanaripoti tukio la ghasia za huko Arusha.
  Nilistuka sana kwanini vyombo vyetu vya habari havikuonesha namna viongozi wa CHADEMA walivyokuwa wanawahamasisha wafuasi wao kuvamia kituo cha polisi kuwatoa baadhi ya viongozi waliokuwa wanashikiliwa na polisi.Aidha zilioneshwa picha za mkutanoni viongozi wa chadema walivyokuwa wakiwahamasisha wafuasi wao kufanya fujo eti kwa kuwa baadhi ya viongozi wao walikuwa wamekamatwa.
  Alioneshwa Philemon Ndesamburo(mbunge-Moshi Mjini) akizungumza maneno na lugha ambayo haifanani na umri wake.Maneno yake yalijaa uchochezi,yalikosa chembe ya busara ya utu uzima aliokuwa nao.Maneno yake hayakuwa na adabu,hayakutofautiana na mtu aliyekuwa amepata kilevi.Ametia aibu, ametia kinyaa kwa watu wa umri wake na hata kwa familia yake.Ameonesha si mzee wa kupigiwa mfano mzuri katika maamuzi na maneno ya busara.Ni fursa kwa wazee wenzake kumkalisha chini na kumuelekeza namna ya kufikisha ujumbe au kudai haki kwa maneno yasio na matusi.
  Pia katika mkutano huo alioneshwa wilbrod Slaa(Katibu Mkuu-CHADEMA).Huyu nae alionesha mfano mbaya wa Kiongozi.Hakuonesha umakini bali umahiri wa kuchochea.Alikuwa na hasira kupita maelezo.Pengine mmoja wa waliokamatwa ni HAWARA yake (first lady wa kuazima).Alionesha kana kwamba amani ya Tanzania ipo mikononi mwake.Ni kiasi cha yeye kuamua iwepo amani ama la.Alionesha ni kiongozi aliyejisahau na anayedanganyika na shangwe za wale wanaomsikiliza anapozungumza.Na hili limewaponza wanasiasa wengi wasio makini Tanzania.
  Hakuonesha kama ni kiongozi makini pale linapotokea jambo zito lenye kuhitaji maamuzi ya busara.Hakupima uzito wa kuhamasisha wananchi kwenda kuvamia kituo cha polisi na matokeo yake.Huu ni udhaifu wa viongozi wetu,hutafakari baada ya kutenda.
  Viongozi hawa wawili si mfano wa kuigwa hata kidogo,ni wa kulaaniwa na kukemewa na wapenda amani.Ni viongozi wenye kupenda kutimiza kiu na malengo yao hata kwa gharama ya damu za watanzania.Watanzania wenzangu, tuamke wanasiasa wasitumie damu zetu kwa maslahi yao.Mabadiliko yanawezekana si lazima kwa damu zetu.Tutahadhari sana na viongozi ambao hawana njia mbadala ya kufikia malengo yao ya kisiasa isipokuwa kwa kuchochea ghasia na vurugu.
  Kiongozi mmoja mashuhuri sana na mwenye akili sana aliwausia watu wake kwamba, "UKITAKA KUFANYA JAMBO KWANZA ANGALIA MWISHO WAKE, LIKIWA LINA HERI BASI LIFANYE NA LIKIWA LINA SHARI BASI LIACHE"
  Tuwe mbali na viongozi mahiri wa uchochezi na si makini wa maneno na maamuzi yao.Watanzania wenzangu tutafakari kabla ya kutenda na si kutenda kabla ya kutafakari.Mwenye macho haambiwi tazama.
  Nawasilisha
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Tuwekee maneno waliyosema sio kutuuliza suali kwa mujibu wa tafsiri yako
   
 3. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Wewe kweli umelegea!Ulichokieleza ni toilet paper.
   
 4. K

  Kiwete JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 281
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  Mandela,Kenyata,Samora,Kabila na wengine wengi tu waliitwa ni wachochezi na waliokuwa madarakani kwa wakati huo.Sisi tuliwaita ni wapigania uhuru na mashujaa.Kwa hiyo wewe waite wapambanaji wetu vyovyote utakavyo,ukweli hautabadilishwa kwa namna utavyowaita.
   
 5. jcb

  jcb JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2011
  Joined: Jul 6, 2010
  Messages: 281
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tafuta jingine hili limepita Halina mashiko
   
 6. Elly B

  Elly B JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 1,194
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nilitegeme tutofautiane kwa sababu najua na wewe una itikadi yako kisisasa au labda kuna hisa humo.Sijui sana, lkn sikutegemea hoja hii kutoka kwa mtu anayeona akafikiria.MABADILIKO NI MUHIMU NA LAZIMA KWA AJILI YA TANZANIA NZURI YA KESHO! HUU NI UKWELI HATA KAMA KUNA WENZETU HATAKI. Hata kule Bondeni kulikuwa na Buthelezi! But No offence!
   
 7. n

  notradamme JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,015
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  acha ulevi...... wakati kipindi kinaonyeshwa ulikuwa kwenye KILABU unakunywa mbege,,,, ndio maana unapitwa na kila jambo..............
   
 8. a

  arasululu Senior Member

  #8
  Jan 19, 2011
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umetumwa na wanadowans KAMA SII DAWANS wee mwehu katapikie huko si hapa ninaaa!! television gani hyo mbona hujaitaja kama si uswahili unakusumbua kakaange vitumbua na waswahili wenzako. tuache tukomboe taifa letu hata kwa kumwaga damu haki aiombwi tulikuwa tunaomba ndo maana wametufikisha hapa tulipo sasa hv hatuaomba tena haki tunaidai kwa nguvu ya UMMA... PIPOOOOOOOOOOS. YOU WIL DIE NOISLESS
   
 9. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  wewe mwnyewe umeandka maneno yasiyo na busara. Vp kuhusu babu yako makamba anayoyaongeaga yanaendana na umri wake? Au na ww umetokea kilabuni?
   
 10. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  big Thanks. Ungekuwa karb yng nngekupa bonge la zawadi!!
   
 11. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wewe ndiye umetokea kilabuni na kuja ku2andkia upupu. Usilo lijua litakusumbua. To hel wth ur post. Hujahc aib wkt unaandka huu ujinga??
   
 12. K

  Kishalu JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 850
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Sasa wewe upo upande upi maana hata kama walitoa maneno ya hasira je walioleta hasira walikuwa akina nani?

  Tafakari maana mafisadi bado wanatumaliza na kutunyima haki ya kuandamana maana kama wasingezuia hayo maandamano vurugu zingetoka wapi?

  kama hujatumwa na mtu basi mada yako inalenga kutetea kundi mojawapo kati ya CCM na Polisi ambao ndiyo chanzo cha matatizo yote
   
 13. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Faraja unayoipata ni kuona post yako inasomwa. Kujibizana na wewe haina maana. Ulichofanya ni kuwatukana watanzania million 2+ waliompigia kura dr slaa. Pia wanaKaratu waliomchagua kuwa mbunge wao mpaka alipogombea uraisi. Umewatukana wakazi wa Moshi mjini waliomchagua Ndesamburo kwa vipindi vyote. Wewe na TV uliyoangalia ndio wenye busara zaidi.

  Kama ni kijana jiulize, Ndesamburo ana miaka 77 je malengo yake ni yapi? Anautajiri wa kutosha anamiliki hoteli, majumba, amenunua helcopter nk bila kuhusishwa na wizi wa rasilimali zetu akiwa mpinzani anataka nini zaidi? Lengo lake analotaka damu imwagike litimie ni lipi?

  Mbona hujasema ulichoona wakati polisi wanapiga watu? Wakati wanawalenga kwa risasi waliokufa na waliojeruhiwa? Wakati wanaenda kwa baba yake marehemu Ismail kumshawishi asipeleke mwili uwanjani? Wakati polisi anaiba simu ya Mh. Lucy Owenye na kuhamisha credit kwenda kwenye simu ya polisi mwingine? Hayo yote uliyaona? Sema na hayo pia!
   
 14. a

  arasululu Senior Member

  #14
  Jan 19, 2011
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata ungekuwa wewe hasira zingekuwepo wazee wale walipgwa mabomu bila kosa lolote wakiwa uwanja nmc wakiutubia! alafu unataka ammbembeleze kikwete amshikeshike? mbona kama kuna watu wamo huku ni -0?
   
 15. a

  ablood8 Senior Member

  #15
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Kuna watu wengine kazi yao ni kujipendekeza tuuuuuuuu bila hata ya kutumwa ili siku nao ikifika angalau ikiyokea post basi nao wafikiriwe. Hawajali ni kwa kiasi gani Taifa ili limefilisiwa na watu wachache kwa miaka yoote hii hasini ya Uhuru, rasimali zoote za nchi wamejineemesha wao peke yao huku mamilioni ya waTZ wakitaabika na ufukara wa kila aina.
  Mimi na nasema mabadiliko ni lazima,hata wao wakuchukulia kuwa ni uchochezi lakini tutaendelea kudai mabadiliko ili hawa vibaraka wachache tuwaondoe madarakani. chi inakuwa kama imelaaniwa, yaani tuna gas,makaa ya mawe,mito, Uranium, na sijui upepo then kila kukicha migao ya Umeme,waziri akija kwenye press confrence anatoa mimacho eeh tatizo hili ni mtambo wa sijui wapi umeharibika, mara mgao ni historia then utasikia tena mgao haukwepeki. IPO SIKU
   
 16. m

  mob JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  samahani hii imenitia wasiwasi kumbe kuna watu wanashabikikia vitu vya ajabu. wewe kama ungelikuwa makini ukaangalia picha zilizprushwa tokea tarehe 5 na zilizoonyesha kwenye kipindi cha pambanua ungekuwa umeona mbali. watunza ulinzi na usalama walichukua jukumu la kuvunja viooo vya magari kumkamata mwanamke na kumweka chini ya ulinzi ili hali wao ni wanaume pasipo hiyo kazi kufanywa na mwanamke. je kama kweli wao wanafuata sheria iweje kiongozi gari lake lina bendera anavamiwa na kuumizwa kwa mtanzania wa kawaida asiye na bendera atafanyiwa nini
   
 17. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #17
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,739
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Dear Dos Santos: Makamba is always proud of your bigotry and work. Delivered
   
 18. nginda

  nginda JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 745
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unamlinganishaje na Mkwere ambaye yuko buzy kufungua shule za msingi zisizo na madawati wala waaalimu?
   
 19. B

  Baba Tina Senior Member

  #19
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umesema mengi sana lakini ukweli unabaki palepale kwamba kitendo cha polisi kuyavuruga maandamano ya amani ya chadema ambayo awali yalikua yameruhusiwa na kamanda wa polisi wa mkoa tena yakiwa yamekaribia kufika viwanja vya NMC ndicho kilichosababisha maafa ya arusha. Wazo la kuvamia kituo cha polisi ambalo polisi wanalitumia kama sababu ya wao kutumia risasi za moto lisingekuwepo kama polisi wangeyasindikiza maandamano hayo hadi viwanja vya NMC. Polisi hawawezi kukwepa lawama za mauaji ya arusha. IGP mwema aliingilia mamlaka ya kisheria isiyokua ya kwake..na kusababisha mauaji ya raia wasiokua na hatia. Afahamu kwamba damu za wahanga hao zinamlilia.
   
 20. M

  MushyNoel Senior Member

  #20
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hoja ya nini kilitokea Arusha na nani alisababisha inaweza kujieleza vizuri kama tutafuatilia mchakato mzima kabla na baada ya tukio lenyewe.Tayari CHADEMA walishafanya mawasiliano ya kutosha na polisi na ngazi ya wilaya ambayo ndio tukio halisi la maandamano lilipokuwa litokee walishatoa baraka zote.Majadiliano ya maandamano yalikuwa ni mlolongo wa vikao na maongezi toka Dec 22,2010.Sasa kilicholeta tafrani ni ile haki ya watu kuandamana kupingwa na jeshi la polisi tena kwenye vyombo vya habari kwa kisingizio cha taarifa za kiintelijensia.Na hata katika taarifa iliyosomwa na jeshi la polisi wanasema walifikia kutumia risasi za moto kwa sababu watu walitaka kuvamia kituo cha polisi.Ukweli ni kwamba Denis Michael Shirima alipigwa risasi maeneo ya kaloleni karibu na baa maarufu picknick.Kutoka sehemu hiyo shirima alipopigwa risasi mpaka kituo cha polisi ni wastani wa km moja na nusu.Ismail Omari alipigwa risasi maeneo ya philips ambapo ni wastani wa km moja narobo kufikia kituo cha polisi.nae raiya wa kenya Paulo Njuguna alipigwa risasi akiwa maeneo ya Jogoo house karibu na kituo cha mabasi cha arusha na benki ya CRDB.Kwa mantiki hiyo wote hawakuwa wamesogelea kituo cha polisi.

  Kuhusu nani amesema nini na kikapelekea nini haiwezi kubadili sura kwa chanzo chote cha machafuko haya ni kuingiliwa kwa vyombo vya ulinzi ambavyo kimsingi ni vya wananchi.vikaingiliwa na wanasiasa ili kuzuia maandamano ya amani ya Chadema.Tena walikuwa wameandamana kwa karibu kilometa 2 walikuwa wamebakiza moja tu ndipo polisi wakaanza kupiga na hata kuua.Walifanya hivyo ili kauli ya mkuu wao isionekane ni ya uongo.
   
Loading...