Dr Slaa na sekratariet yako. wajibikeni katika hali... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa na sekratariet yako. wajibikeni katika hali...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Oct 25, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Oct 25, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mimi kama mwanachama wa kawaida wa CDM, siingii katika vikao vya juu vya chama, hivyo naamini ni sahihi nikitumia jukwaa letu hili pendwa kufikisha ujumbe kwa viongozi wangu.

  Dr. Slaa, tunatambua na kuheshimu sana kazi kubwa unayofanya ya kuuza chama, lakini kuna hii homework ambayo bado haijafanyiwa kazi.
  Tatizo ni kwamba, hadi sasa CDM katika baadhi ya maeneo (nadhani maeneo mengi), haina watu wenye 'uwezo' wa kuongoza, kutenda na kugombea nafasi mbalimbali.

  katika uchaguzi uliopita, tulishuhudia kuwa katika maeneo mengi CDM ilishindwa sio kwa sababu haikupigiwa kura za kutosha, au sio kwa sababu haikuwa inapendwa, bali kwa sababu haikuwa na wagombea na watendaji wenye mvuto, uwezo wa kuongoza na/au uwezo wa kusimamia kura.

  Wapiga kura wanashawishiwa majukwaani, lakini wapigiwa kura wanapikwa (groomed). Wenzetu CCM wanaiba ndio, lakini pia wanatuzidi pia kwa kuwa na wapigiwa kura 'wenye uwezo' zaidi. Nilishasema hapa, tungechukua majimbo 100 yenye wagombea wa CDM in random, alafu wagombea wa CCM katika majimbo hayo wakachukua kadi za CDM, then tukafanya kura za maoni, sio zaidi ya majimbo 20 kati ya hayo watakayochaguliwa waliokuwa wagombea wa CDM tokea mwanzo. CCM wanawa-groom wagombea wao mapema. Sio vibaya tukaiga kwao kama ni jambo jema.

  watu wanaweza kudhani kuwa hii itacompromise demekrasia wakati wa kura za maoni; no, kama kuna mtu ameshapikwa katika jimbo au kata husika, then wakati wa kura za maoni akatokea mwingine mwenye sifa zaidi, then well anachukuliwa mwenye sifa zaidi. Hii ina maana kuwa demekrasia inazingatiwa.

  Katika uchaguzi uliopita tulishuhudia (kwa wale tulioshiriki) katika baadhi ya maeneo tukiwa na wagombea wabovu na maeneo mengine tukiwa hatuna wagombea kabisa. Huu ni udhaifu ambao kwa gharama yeyote hatutakiwi tuende nao katika uchaguzi wa 2015, au uchaguzi wowote mdogo utakaojitokeza tena hapa katikakti.

  Dr Slaa anza kusajili timu yako mapema, sio vizuri kuwa kama Arsene Wenger...
   
 2. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  well said, lakini mimi naona ni juu ya watu wanaotaka kugombea kuanza maandalizi mapema ya kukijenga chama maeneo wanayotaka kugombea. Nadhani kitakuwa kigezo pia kwa mtu kuteuliwa kugombea kama atakuwa amechangia kukuza chama jimboni kwake. Haya maandalizi ni muhimu sana ili kuhakikisha mgombea asije akawa ni surprise kwa wapiga kura kwa kuwa hata hawamjui. Watu humpenda kumchagua mtu aliyekaribu nao kuliko aliyembali hata kama technically ni mzuri.

  Amkeni wale mnaofikiria kuomba kupeperusha bendera ya cdm 2014 and 2015.
   
 3. j

  jajii02 Member

  #3
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sawa mkuu but kuna maeneo cdm haijawi kutia hata maguu km jimbo la mkono msoma vjjn wapite angalau mar 1 wahamasishe watu
   
 4. Mwanakilimo

  Mwanakilimo Member

  #4
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jimbo la Musoma vijijini na mfano wa maeneo yaliyokuwa na wagombea dhaifu. Unakumbuka yule dogo aliyeteuliwa, kisha yeye na wenzake watano wa vyma vingine wakajitoa siku moja baada ya kutangazwa wagombea na NEC. Hizo ndo hali tunazopaswa kujiepusha nazo 2015.

  Hongera mkuu kwa kumkumbusha Slaa...
   
 5. Ryaro wa Ryaro

  Ryaro wa Ryaro JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 2,663
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ni kweli viongozi Ufundwa/upikwa kutegemeana na mazigira ya kisiasa na ilikuwa inawezekana sana kwenye mfumo wa chama kimoja hilo 100% nakubaliana na wewe. lakini takika mzaingira haya ya sasa itakuwa ngumu ie. Mimi nikaa nje ya nchi kwa miaka mingi kidogo na sikuweza kuwa mwanachama wa chama chochote cha kisiasa na wakati wa uchaguzi 2010 sikupata muda wa kushiriki uchaguzi huo. Msimamo wangu ni kwamba iwe iwe je 2015 kama nipo hai nitagombea jimbo hilo ulilolisema la Musoma Vijijini na Chama si Kingine ni CHADEMA. Sina kadi ya CHADEMA hadi sasa kwa sababu nimerudi nchi pude tu lakini naamini time will tell na ninauhakika tutakayesimama nae anayokazi maana nimejipanga na watu wangu nawajua na wananijua.Na kama viongozi wa CHADEMA watasikia ushauri wako wakamuandaa mtu basi kazi ni ngumu sana.. Naamini mzee Mkono ametumiakia vya kutosha inabidi apumzike kwa heshima maana alipofikia inabidi atoe kijiti kwa mwingine. 2015 si mbali lakini ukweli ni kwamba NIA ninayo, uwezo wa kuongoza ninao na ni muda wangu kuwatumikia watu wangu.
  Kama kuna mwanaCHADEMA mwenye nia basi kazi hiyo tutawaachia Secretarete itaamua muda ukifika na mimi nitakuwa nipo wazi...iwe iweje nitagombea na nimejiandaa katika hilo kwa kila khali.
  Asante sana.
   
 6. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2011
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hongera kwa maamuzi yako sahihi.

  Kuongezea maoni ya mtoa mada, katika yale majimbo ambayo CDM ilisimamisha wagombea wazuri na hawakutangazwa washindi mf. Kigamboni, Kibaha, Arumeru Mashariki, Segerea, Kule shinyanga, Sumbawanga, na kwingineko. Wale wagombea wafanye kazi ya kuimarisha chama kuanzia sasa. Uchaguzi wa serikali za mitaa wagombea makini wajitokeze!

  Inawezekana!
   
 7. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mawazo yako ni mazuri na yenye nia njema kabisa kwa mustakabali wa chama kushika uongozi wa nchi ili kuwaletea wananchi ustawi bora wa maisha yao.

  Lakini litakuwa jambo la msingi sana kama watu mbalimbali wazalendo wa kweli na wenye sifa wakaanza kujiandaa wao wenyewe. Ni vizuri kujitolea mapema ili kukiimarisha chama na kuongeza mtandao wa chama kwa kuongeza wanachama ambao ndio nguzo ya chama chochote.

  Sisi wengine tumeshaanza juhudi za kukijenga na kukiimarisha chama ili kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 tuanze rasmi kazi ya kuelekea magogoni hapo 2015. Kazi ni kwenu ambao bado hamjaanza kuchukua hatua, karibuni tuunganishe nguvu.
   
 8. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Nililishuhudia hili Monduli.
  Mgombea alikosa mvuto kwa watu,alikuwa hana kabisa uwezo wa kujenga na kutetea hoja,mwisho wa siku alikimbia bila kujua ni nani anaenda kusimamia uhesabuji kura.Vijana wengi hasa wa chuo cha ualimu monduli waliojitolea kusimamia kura walikuwadisapointed sana.
  Tafadhali Dr.Sla fanyia kazi huu ushauri.
   
 9. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2011
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,142
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  CDM kina wapenzi wengi ila wanachama wachache sana !
  Ni jukuma la kila mpenzi wa CDM kuanza kujenga mtandao wa chama ,
  Ila uongozi wa CDM inabidi utoe elimu zaidi kuhusu faida za kuwa mwanachama hai wa CDM
   
 10. S

  Stany JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hili wazo ni zuri mno! Dr take note.Kuna sehem ambazo hamna hata ofisi,kad hazpatikan kwa wepes hivyo inakuwa vigumu mtu pmj na kukipenda cdm na kuwa na nia ya kugombea akakosa sifa ya kutokuwa mwanachama.ie hana kad.
   
 11. R

  Ramos JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2011
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kuna jimbo moja la mjini tena, jamaa alienda kutaka kugombea na CCM, akafika akaambiwa kule competition ni kubwa, akavaa shati ambalo sio la kijani, akaenda ofisi za CDM akapewa fomu na akawa mgombea (hakuwa na mpinzani). Alifanya kampeni dhaifu sana lakini akapata 42% ya kura...

  Viongozi wa juu wa CDM, tunaomba kama kuna mnaloweza kufanya, lifanyeni sasa...
   
Loading...