Elections 2010 Dr. Slaa, Mpendazoe Kunguruma Tabata - Liwiti Jumapili Nov 14

Angalizo, huruhusiwi kubadili neno/herufi ndani ya post ya mwenzako ulichotakiwa ni kuandika masahihisho nje ya post.

Kamanda angalia hoja za msingi achana na vitu vidogo kama hivyo . . . . Mods wapo na kazi zao wanazijua.
 
I ama very happy this BONGO FLAVOR generation didn't win.They are just angry without understing the real life.They must know that government will never make them rich.They will make themselves welloff.
 
Sasa hivi kinachotakiwa ni kumwunga mkono ili kujenga TZ imara.Yuko radhi kufanya kazi na watu wote bila ya kujali itikadi zao.TZ imara ni nzuri kwako na kwangu na kwa watanzania wote.
 
Ndugu yangu hayo mawazo yako ya ukoko hapa hayawezi kufanya kazi. Chadema kamwe haitaweza kuungana na Cuf kusimamisha mgombea urais kwanza kabisa Cuf haina mgombea urais, Lipumba tayari ameshapauka na hana mpya zaidi ya lecture za uchumi pili Cuf haina sera makini za kuwakomboa watanzania, tatu Cuf ni tawi la CCM au niite CCM(B) kwa mawazo hayo mgando nakushauri ujiunge na chadema ili kuongeza nguvu katika kuleta ukombozi nchini.
cuf hawana shida yakusimama wala kuungana na chama chochote,cuf itasimama kama cuf na daima cuf itaendelea kuwepo,hao chadema nimoto wakifuu unalipuka unazimika gafla,ngoja zito nambowe waanze kuparurana kuwania uenyekiti na hao kina mbowe na wachaga wake wanajifanya miungu watu ktk chadema kilakitu wanataka wao,hata uongozi waupinzani
bungeni alitakiwa awe zito,udikteta wakina mbowe wakang'ang'ania kwaulafiwao,chadema kunabomu litalipuka wakati wowote,tuvute subira natumuombe mola atupe uhai mtayaona mengi yanakuja,
 
naam, ndio, mh. 'rais wa wananchi na mbunge halali' wanasubiriwa kwa hamu kubwa hapa. kuna vikundi vya ngoma na majigambo vinatanguliza burudani ya aina yake kabla wateule hawajafika na mkutano kuanza rasmi. watu kibao wanawasili. tupo makini tunasubiria.
 
Asante Kamnda, tunakusoma.

Tunafuatilia endelea kutuhabarisha.
 
asante kwa taarifa za mkutano wa slaa. Kikubwa ni hilo bomu atakalolitoa ni muhimu kupost!
 
naam, ndio, mh. 'rais wa wananchi na mbunge halali' wanasubiriwa kwa hamu kubwa hapa. kuna vikundi vya ngoma na majigambo vinatanguliza burudani ya aina yake kabla wateule hawajafika na mkutano kuanza rasmi. watu kibao wanawasili. tupo makini tunasubiria.

Msaki;

Bado mnamsubiri?

Kuna mkutanao kweli?
 
baada ya madiwani wa chadema kukaribishwa na kila mmoja kumwaga shukrani... kwa sasa ndio mh. mbunge halali anamwaga shukrani na mikakati ya baadaye kulikomboa jimbo la segerea...
 
baada ya madiwani wa chadema kukaribishwa na kila mmoja kumwaga shukrani... kwa sasa ndio mh. mbunge halali anamwaga shukrani na mikakati ya baadaye kulikomboa jimbo la segerea...

Kamanda Dr. Slaa yupo?
 
Mkutano upo, ni ukweli, ila kwa 'rais wa wananchi' kuja sina uhakika sana naana nimepata msg kuwa 'rais wa watu' hataweza kuja maana yupo dodoma na wapambanaji -wabunge, anawapa 'somo la ukomavu' kuelekea kulikomboa taifa letu.
 
fred anamwaga sana mikakati, amesema ni wauati wa watanzania kubadilika toka moyoni, watu waache woga, mfano wa watumwa wa zamani walikuwa 400 wakiwa wanalindwa na waarabu wa2 na gobore tu, kumbe wangetambua udhaifu wa gobore wangejinasua toka utumwa, ndio wananchi wajikomboe. ametoa namba yake kwa ajili ya kumchangia kwa kukamilisha kesi. namba yake ni wa 0717 050335. katoa pia ya zain, sijaweza kuinasa.
 
Ndio amefunga sara mkutano. amesema wapambanaji wema wameshamchangia sh. milion 5, na bado wengi wanajitokeza.
hapa wananchi wana hamasa sana! watu wengi sana, umati wote unapiga makeleke, watu wanagombania card za chadema kama njugu, nchi inakubali mabadiliko. mamia ya wananchi wanapiga mayowe kuunga mkono kesi na wameahidi kuhudhuria kwa wingi siku ya kesi.
 
Sasa ndio 'mbunge wa segerea anaondoka taaratib, watu wanamfuata, wengi wanamzuia, msafara mkubwa. nadhani vyombo vya habari vitaitoa hii kesho, tufuatilie.
Sijaweza kutuma picha, simu inanitoa nishai kidogo, sijui wameichakachua!

naomba kuwahakikishia, wananchi kibao wanalisukuma gari la mbunge kwa furaha. wamfunga mitaa na barabara, ndio tunaondoka,

nawasilisha
 
Back
Top Bottom