Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

Naunga mkono.

Baada ya uchaguzi wote wameanza maandalizi ya uchaguzi ujao. Wananchi tumebaki yatima, hakuna kiongozi hata mmoja mwenye kuweza kufikilia kama weye mkuu.

Thnks ubarikiwe
 
Mimi nawashauri watanzania wote waipige chini hii ccm ili wote tumiliki nyumba bora wote kwa kununua Mfuko 1 wa cement kwa shs 5,000/
 
In government,i need peopke like you bhana...big up japo inatia uchungu,hasara ya Tsh 15000/= nzima for nothing...
 
Hapo bado upo India halafu uulete Tanzania uuze kwa bei ya Slaa ya 5,000/= kwi kwi kwi teh teh teh!

huyu zomba naona hajasoma vizuri hii thread..naomba uuweke utanzania pembeni alaf usome tena utaona salma ameonesha tofauti ya utengenezaji huko india na hapa tz..raw materials wanazo tumia kule wanazinunua lakini sisi tunazo hapahapa nchini
 
big up sana mama,tatizo hii ni Danganyika state,na Wadanganyika wamekubali kudanganyika kwa kila jambo.Tujifunze kwa wenzetu wa Kenya,hawakubali kuburuzwa na watawala walafi wa madaraka.Angalia Zambia kilo moja ya sembe ikipanda watu wanaingia barabarani lakini sisi vichwa vya wendawazimu kial fisadi ana jifunzia kuibia.
 
Hicho kiwanda si kilikuwa cha umma mkashindwa kukiendesha? kachukuwa singa singa, mambo swaafi kabisa. Ndio maana mkaambiwa maendeleo ya mtu huletwa na yeye mwenyewe. Nyinyii mlishindwa nini tena umma mzima, singa-singa mmoja kaweza. Aibu.

Sema vizuri!chama lako hilo la majizi ndilo lililoendekeza ulafi mpaka likakosa hela ya kununulia Mifuko!!ambayo ndiyo material pekee inayoingia kutoka nje ya geti,aibu gani hii mmetuletea watanzania?nakuombea kwenye jeneza la ccm nawe uwepo ndani yake,na mfe kwa aibu kama yule masikini muliyemdhulumu anavyoishi kwa aibu.
 
Sema vizuri!chama lako hilo la majizi ndilo lililoendekeza ulafi mpaka likakosa hela ya kununulia Mifuko!!ambayo ndiyo material pekee inayoingia kutoka nje ya geti,aibu gani hii mmetuletea watanzania?nakuombea kwenye jeneza la ccm nawe uwepo ndani yake,na mfe kwa aibu kama yule masikini muliyemdhulumu anavyoishi kwa aibu.

Chama ndio wanaendesha kiwanda? kwani hujui viwanda vyote vya umma vilianza kufa kabla havijaingiza faida? kuna mali ya dhulma ikaendelea?
 

Nikaenda mbali kidogo na kujiuliza kwanini India cement ni bei rahisi. Nikagundua kwamba, kasheshe kubwa ya kutengenza sement iko kwenye maandalizi yake hasa hasa uzalishaji wa vijiwe vidoho vigumu sana vinavyoitwa Clinker. Mchakato wa Kutengeneza malighafi hii clinker ndio mgumu na ghali zaidi. Kwa utafiti mfupi nilioufanya nimegundua utengenezaji wa Clinker Kule India Ni Ghali sana Kulinganisha na hapa kwetu TZ. Nilibahatika kutembelea kiwanda cha Lafarge Mbeya Cement maarufu kwa kutengeneza Cement ya Mnyama (TEMBO CEMENT). --Simba ni Tanga na Twiga ni DSM.

SALMA2015, nilikuwa naelewa kwamba Twiga Cement uimport clinker toka nje ya nchi ili kufidia mahitaji yao ya clinker. Sijui kama wameanza kutengeneza clinker ya kutosheleza mahitaji pale kiwandani (ingawa nafahamu walikuwa wana mpango wa kuboresha uzalishaji wa clinker katika KILN No. 3) . Na nakumbuka mara kwa mara wamekuwa wakilalamika juu ya gharama kubwa za uzalishaji zinazochangiwa na uagizaji wa clinker toka nje.

Pia kuna hili suala la Portland and Pozzolana Cements; hiyo portland (imechukua jina hilo kutokana na kufananishwa na jiwe linaloitwa portland, jiwe linalopatikana katika kisiwa kidogo cha Portland kilichopo Uingereza) cement ndiyo maarufu kuliko pozzolana (pia jina lake linatokana na eneo linaloitwa Pozzuoli lililoko Italia, ambako ndipo inasemekana majivu jivu ya ki-pozzolanic ndipo yalichimbwa na kugundulika kwanza) cement.

Sasa hiyo pozzolana cement inasemwa kuwa ni imara zaidi ya portland cement; kwa kuwa pozzolana cement pale inapokuwa ngumu (imekauka vizuri) ina sifa ya kutofyonza na kutopitisha maji kwa kiwango (lower porosity) kikubwa kama portland cement, sifa ambayo inafanya iwe imara pia dhidi ya kuvunjikavunjika (breaking into fragments/small pieces). Na sasa nasikia makampuni makubwa duniani yanachanganya pozzolanic materials na portland cement katika kufaidika na sifa za cement hizo mbili.

Hii pozzolana inapatikana kwa wingi sana Mbeya na pia maeneo ya karibu na Mlima Meru (tena kulikuwa na mradi wa kuchimba na kutumia majivu ya volcano yaliyokuwa yanapatikana karibu na Mlima Meru miaka ya 1970). Sasa sielewi kwanini viwanda vyetu havitumii hii pozzolana katika kuzalisha simenti, sijaweza kufahamu shida ya pozzolana, labda kama kuna mdau anaelewa, anaweza kunisaidia.

Sasa kwa mtazamo huo, ni hakika kwamba kama viwanda vyetu vikiweza kutumia hii pozzolana katika uzalishaji wa simenti, basi naamini kwa kiwango kikubwa bei za simenti zitashuka sana. Na hivyo kupelekea wazo la Slaa kuwa linalotekelezeka.
 
Last edited by a moderator:
Kwanza saluti sana kwa mleta mada,ameleta mjadala wa muhimu sana hapa,wale wenye akili mgando za kimagamba ndio hawaamini kua cement inaweza uzwa kwa bei hiyo.mimi kitu kimoja kimenishangaza cement ya pakistan inauzwa bei moja na ya tz na ubora ni wa juu kuliko hata ya tz,hapa kuna tatizo tutafakari na tuchukue hatua tuwakatae wanaokumbatia wawekezaji wanyonyaji hii si enzi ya binadam kuishi nyumba ya udongo juu mpaka chini kama wanyama,Mungu alituambia tuje kuitawala dunia na vyote vilivyomo
 
Halafu hiyo hesabu yako mfuko mmoja ni shillingi ngapi? ukiweka gharama za usafiri wa meli (zilizo sawa, hiyo ya dola 400 kwa container la futi 40 ni porojo), gharama za bandari? usafiri wa nchi kavu? gharama za kuhifadhi (storage)? gharama za kuuza (sales cost)? kwi kwi kwi teh teh teh, bado ni elfu tano tu kwa mfuko? sasa wewe mbona juu huko kwa gharama porojo na unauza 10,000 kwa mfuko? umempita bei Slaa kwa 100%, sasa nani porojo zaidi wewe, au yeye?

Hivi inakuingia akilini cement inatengenezwa km 17 inauzwa zaidi ya sehemu ya km 800.fanya nawewe utafiti wako so kupinga kila kitu.
 
Vitu makini kama hivi vikisemwa na wengine mara utasikia habari za udini, ukanda, upadri nk.. kweli watanzania utafikiri tumelogwa, hakika inawezekana cement kuuzwa kwa bei ya chini hata chini ya 5000.
 
Kabla ya miaka 5 Kikwete alishasema anashughulikia hili tatizo la simenti na naam, hivi karibuni tutaona ushindani mkubwa kwani kuna viwanda vipya vinne sehemu tofauti Tanzania viko katika ujenzi, vingine vimeshaanza mpaka uzalishaji wa majaribio.

Tegemeeni kushuka kwa bei ya simenti lakini sio kwa kiwango cha Bi Salma cha 2,500/= kwa mfuko wa kilo 50 au cha Slaa cha 5,000/= huko ni kujidanganya.
 
Umaskini wetu unasababishwa na mibwege kama akina zomba.. hebu fikiri serikali ikiwa na watendaji wa aina ya zomba unatarajia nini kama si kuyumba kama tuyumbavyo?
 
Back
Top Bottom