Dr. Slaa: Mchakato wa katiba mpya kuanza ndani ya miezi minne nikipewa madaraka

Yale yale ya "Tuko kwenye mchakato". Nadhani angekuwa firm kwa kusema angetupatia Katiba Mpya ndani ya kipindi fulani; uwe mwaka ama miaka miwili lakini eti Mchakato ungeanza baada ya siku 100 bila kutaja ungeisha lini ilikuwa kama danganya toto vile.
Hakuna kitu kinafanyika bila mchakato kwanza, mngempa urais muone kama ilikuwa danganya toto, saa hizi katiba tena ya bei nafuu ingekuwa inaandikwa, sio hii ya bei mbaya ambayo inamaliza mapesa yetu hata hatujui itakuja lini.
 
Kuna watu wanakula na kulala kwa kazi ya umbeya tu.Kama Dr.Slaa aliona uhitaji wa katiba mpya kwa Tanzania ya sasa tangu kwenye kampeni zake za 2010,je Rais Kikwete na magamba wengineo alisema chochote kuhusu katiba mpya? Au alidandia treni kwa mbele! Unaacha kuleta hoja ya ccm kuwa dhaifu kuandaa Ilani zake kisha inapaparakia ilani safi ya CHADEMA kisha vifuasi njaa wa magamba mnakuja kuandama watu JF.Lete hoja tujadili masuala na siyo watu.
 
Hakuna kitu kinafanyika bila mchakato kwanza, mngempa urais muone kama ilikuwa danganya toto, saa hizi katiba tena ya bei nafuu ingekuwa inaandikwa, sio hii ya bei mbaya ambayo inamaliza mapesa yetu hata hatujui itakuja lini.

Mkuu hakika hii katiba ni ya bei mbaya!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom