Dr. Slaa: Mambo makuu matatu nitakayofanya nikichaguliwa kuwa Rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa: Mambo makuu matatu nitakayofanya nikichaguliwa kuwa Rais

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by n00b, Aug 23, 2010.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2010
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  [​IMG]
  MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willibrod Slaa akiongea leo

  [​IMG]

  Na Waandishi Wetu

  MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa ameeleza vipaumbele vyake katika muda mfupi, kati na mrefu akianza na mambo makuu matatu endapo atashinda nafasi hiyo.

  Dkt. Slaa alieleza hayo Dar es Salaam jana katika mahojiano maalumu na gazeti hili juu ya mipango yake na jinsi atakavyoitekeleza, endapo atapata ridhaa ya Watanzania kuwa kuongoza serikali ya awamu ya tano.

  Mambo hayo ni mabadiliko ya katiba, kurejesha taifa katika misingi ya maadili na uzalendo iliyopotea na uwajibikaji serikalini, ambayo yatatekelezwa ndani ya siku 100.

  "Tutakapozindua kampeni zetu tarehe 28 tutazindua na ilani yetu pamoja na action plan (mpango wa utekelezaji). Huu ni uchaguzi utakaotupeleka kwenye mabadiliko makubwa," alisema.

  Kwa mujibu wa Dkt. Slaa mpango huo utaonesha jinsi ya kufanya mabadiliko hayo, ili kulirejesha Taifa katika mstari kutokana na kupoteza uadilifu na kuendesha nchi kwa misingi ya kubaguana.

  Alitolea mfano wimbo maarufu wa CCM uanaohubiri 'kuwaleta wapinzani, kuchanachana na kuwatupa' kuwa unaimbwa hata mbele ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho lakini hawasemi lolote wakati unahubiri dhana ya mauaji.

  Akizungumzia utendaji wa serikali, mgombea huyo alisema kwa sasa serikalini hakuna uwajibikaji wala maamuzi na kero za wananchi zinatatuliwa kisiasa.

  Dkt. Slaa alitumia muda mrefu kuzungumzia mabadiliko ya katiba, huku akiainisha vipengele vyenye matatizo kwenye katiba ya sasa, hasa madaraka makubwa aliyopewa rais, yanayompa nafasi ya kuteua watu wengi, ingawa si rahisi kwake kuwafahamu wote.

  Alisema atakapoingia ikulu ataunda serikali ndogo yenye ufanisi ya mawaziri wasiozidi 20 ili kupunguza matumizi ya serikali yasiyokuwa ya lazima.

  Kwa mujibu wa mgombea huyo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Serikali ya sasa yenye mawaziri 47 ni mzigo kwa walipa kodi, katika mishahara, marupurupu, magari na huduma nyingine.

  Alitoa mfano wa Uingereza yenye watu zaidi ya milioni 70, ina mawaziri wasiozidi 20.

  Akizungumzia baadhi ya gharama zinazoendesha serikali, alitoa mfano wa magari (mashangingi) ambayo yanauzwa sh. milioni 200 kila moja, akisema kila waziri anatembea na zahanati nne zinazogharimu sh. milioni 50 kila moja.

  "Hiyo anasa hatuiwezi, lazima tuachana nazo...Mtu asitarajie akienda serikali ya CHADEMA anakwenda kula. Hili tutaanza nalo kwa katiba ya sasa na baadaye kuliingiza katika katiba tutakayounda, ili idadi ya mawaziri wanaotakiwa ijulikane, asijekutokea rais mwingine akaweka anaowataka kwa kuzingatia uswaiba," alisisitiza.

  Mgombea huyo alitoa mfano wa Wilaya ya Karatu ambako chama chake kilikuwa kinaongoza serikali na CCM kuwa wapinzani, kuwa waliweka watendaji ndani ya miezi mitatu walifungwa karibu wote kwa ulaji.

  Mambo mengine ambayo Dkt. Slaa anatarajia kuweka mfumo wa utawala utakaopunguza matumizi na kuongeza uwajibuikaji, kama kuondoa nafasi za wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa na kazi zao kurejeshwa kwa wakurugenzi wa Halmashauri na baadaye katika majimbo, kuongeza uwajibikaji kwa mawaziri kuthibitishwa na bunge, mawaziri kutokuwa wabunge na rais kushinda kwa zaidi ya nusu ya kura.

  Pia CHADEMA kinakusudia kuruhusu matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani, kuweka mipaka ya kiutendaji katika mihimili mitatu ya serikali, bunge na mahakama, kuainisha shughuli za usalama wa taifa na kuunda tume huru ya uchaguzi.

  Vile vile Dkt. Slaa alisema wanakusudia kuondoa dhana potofu kuwa kila kitu kuhusu jeshi ni siri, bali lijulikane kuwa ni huduma ya umma, bali siri ni mbinu, mikakati na vyombo vyake, lakini si masuala kama ya kashfa ya Meremeta, iliyofishwa kwa sababu ya kuhusisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.

  Alisema pia wanakusudia kuwa na jeshi dogo lenye vifaa vya kisasa na lenye ufanisi. Pia watafufua kikosi cha nyumbu ili jeshi litumike kutengeneza magari na vifaa vingine.

  Akidokeza juu ya kampeni yake, alisema asingeweza kuweka wazi mikakati, lakini wanayo mambo mengi ya kuzungumza, zikiwamo nyaraka mbalimbali za ufisadi na jinsi serikali inavyotumia fedha za walipakodi kuisaidia CCM.

  "Uchafu ndani ya serikali uko kila sehemu, tunazo documents (nyaraka), kwenye serikali za mitaa huko ndo usiseme ufisadi wao ninaujua kila sehemu. Kwa ufupi serikali nzima imeoza na haina uwezo wa kujisafisha," alisema.

  Kuhusu ajira, Dkr. Slaa alisema serikali yake itahakikisha kila bajeti inayopangwa inalenga kuongeza kiwango fulani cha ajira badala ya kusubiri wawekezaji ndio walete ajira.

  Katika kipango ya muda wa kati ndani ya miaka mitatu, Dkt. Slaa alisema kilimo cha zalishaji wa chakula ama kwa kutumia uwezo wa serikali au kwa kutangaza tenda za kimataifa ili kuondoa aibu ya kila mwaka ya kuomba chakula kwa wahisani.

  "Mfano yale mabilioni ya JK yalifanya nini, Kina Kapuya (Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Juma) wanatoa takwimu kuwa watu 44,000 wamenufaika. Watu 44 elfu ni kitu gani kati ya milioni 40? fedha kama hizo zingeweza kutumika kuinua kilimo cha umwagiliaji na taifa likajitegemea kwa chakula," alisema.

  Alitumia nafasi hiyo kuziponda trekta ndogo (powertiller) kuwa zimenunuliwa bila utafiti katika baadhi ya maeneo, na matokeo yake zimeshindwa kulima kwa kuwa zinatumia nguvu ya binadamu.

  Vile vile Dkt. Slaa alisema ni mipango yake mingine miji na kuweka miundombinu ya umma itakayopunguza msongamano wa magari mijini.

  Alisema kwa sasa ujenzi unaondelea ni wa majumba makubwa lakini hakuna miundombinu ambayo muda wake muafaka ni sasa, kwa huko baadaye itakuwa si rahisi kulipa fidia.

  Kwa upande wa elimu alisema serikali lazima igharamie masomo hadi kidato cha sita badala ya kufuta tu mchango wa UPE ikasema kuwa imegharamia elimu.

  Akizungumzia maisha binafsi, Dkt. Slaa alikiri kuwa aliwahi kuwa padri na vyeo alivyowahi kushika ndani ya kanisa Katoliki, kama Makamu wa Askofu, Mkurugenzi wa Maendeleo na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu.

  Alitumia nafasi hiyo kumtambulisha mke wa sasa, Josephine, na kuweka bayana kuwa kuanzia mwaka jana alitengana na Rose Kamili ambaye katika maisha yao, bila kufunga ndoa kikanisa, walipata watoto wawili.

  CHANZO: Haki Ngowi Blog
   
 2. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Haya haya.......kipenga ndo kimeshapulizwa....Sie twasubiri hayo mabomu kwa hamu kubwa.....
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  hayaa tunasubri Siraha's move
  Go Slaa
   
 4. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli jamaa ana mikakati mizito. Ngoja tusubiri.
   
 5. v

  vuvuzelaorigina New Member

  #5
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mikakati ipi Mizito zaidi ya kusema habari ya EPA ambao ndio wimbo wake.Urais sio Kuitaja EPA kila dakika.Rais anachaguliwa kwa Mambo mengi.Slaa mtaji wake ni EPA.
   
 6. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,190
  Likes Received: 996
  Trophy Points: 280
  .
  Nani alikuambia urais ni kuchakachua mafisadi, yupi alinipa mgao(kagoda) asishtakiwe na yupi hakuna mgao(maranda) ashtakiwe? Subiri wakati ndio huo unawadia kama babako kafisadi, kiboko yao Slaa huyooo anakuja. Mahakama zitakua safi kama paji la uso, na polisi mishahara yao ya kuwatosha na wala hawatahitaji kujipendekeza kwa fisadi awaye yote.
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Aug 24, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nimeshindwa kuelewa hapa... yani atapunguza idadi ya wanajeshi, na kisha ataongeza ajira? Mhh...!
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  lovely...
   
 9. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,835
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mungu alipotaka kukutana na wana wa Israel alimtuma Musa akamwambia waambie wana wana Israel wajitakase na wafue nguo zao, na wawe tayari siku ya tatu" I pretty understand that I should not be talking about this metaphor to the secular and liberal audience of this platform, but my point is CHADEMA you are about to go out to meet Tanzanian! GET CLEANED YOURSELF FIRST!

  Any blemish that would distract your campaign should be cleared now! First impression has a huge impact is persuading the undecided! Right now Tanzanian need to hear the message of hope, something different beyond the obvious.

  Tanzanian have been blinded by CCM for so long! Their mind have been made so feeble and to many peace is enough "Mengine ni majariwa". When I hear that I see no future. Many have given up! Who would rekindle that spirit of patriotism and awaken a new zeal and hunger for change?

  It takes more than a hovering helicopter, more than the list of Mafisadi neither than operation sangara nor mocking the ruling part! We need first to win the attention of the audience, then enlighten them! How? Get to know the audience! THEN THE MAGIC POWER OF WORDS! I'm taking about speeches! Dr you need a speech writer, we need speeches that will send the correct tone! the tone strong enough to break and smash the crusting mantle of fear and thick stumbling blocks that have blinded us for so long! and comes a new hope and anticipation that will keep us going!

  God bless Tanzania! God bless your servant Dr Slaa, so that he can brace through the hurdles and when the sun goes down we shall celebrate the triumph of our democracy!
   
 10. A

  August JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Katika kipindi hichi cha amani, ambako hakuna taifa linalo taka kupigana, kwani nguvu za kiuchumi haziruhusu hivyo, wanajeshi wengi wa nini?

  Tunahitaji watu wengi kwenye shughuli za kiuchumi, kama uzalishaji viwandani, mashambani, kwenye tafiti, usafirishaji, kuhifadhi, na vitu vinavyo elekeana na hivyo.
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kwa nchi yetu Tanzania na kwa system ya sasa ya Tanzania jeshi ni mzigo mzito. Linatumia pesa nyingi zaidi kuliko linavyoingiza, na even worse sasa limekuwa part ya ufisadi nchini. Kwa mwenye akili timamu anajua kuwa jeshi linatakiwa kupunguzwa sana, lipewe uwezo wa kisasa na liwe highly mobile.

  Jeshi la wananchi, jeshi la polisi na hata magereza, si sehemu nzuri za kutumia kuongeza idadi ya ajira.
   
 12. T

  Tom Lyimo Member

  #12
  Aug 24, 2010
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi namtakia kila la heri na maombi tele ili atimize ndoto zake!!
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Dr Slaa hafai kabisa. Yaani Wasanii hatatujengea Studio kubwa zaidi ya REMASTERING? Ruge angelifaidi.

  Halafu akimaliza foleni za barabarani, alama gani itaonyesha kuwa sisi Watanzania ni Matajiri?

  Mashangingi lazima yanunulike Dr maana Mjomba ndiyo Mlo wake na nyumba zake ndogo.

  Ukiziba sana Dr., wengine itakuwa kasheshe maana TUMEZOEA VYA KUNYONGA .........

  Ahhh, sasa wewe utatuleta nini? Spain? Holland? Au Pweza Paul?

  Lete wala Argentina ili tukuze Utalii.......
   
 14. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu sidhani kama ni kweli kuwa mtaji wa Slaa ni EPA, yeye ni mgombea wa CHADEMA anakuja na sera za chama sidhani kama kuna anti-EPA policy kwenye manifesto ya CHADEMA.

  Lakini ni lazima tutambue kuwa ufisadi ni tatizo kubwa Tanzania, watu miloni 40 tunafanya kazi lakini Kadogo na wenzake kumi ndio wanakula pesa hizo. Ni sawa na kufanya kazi ya kujaza maji kwenye ndoo yenye tundu kubwa, kama huna sera ya kuziba tundu hilo, maana yake ni kuwa kazi yote ya kujaza maji itakuwa bure.

  Kikwete hawezi kutuambia lolote kuhusu kudeal na ufisadi maana tumeona uwezo wake.
   
 15. A

  Awo JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Mimi nimependa ya katiba mapya. Namshauri Dr Slaa amtumie salamu za pongezi Rais Kibaki na Waziri Mkuu Raila tarehe 27/08/2010 wakati wa uzinduzi wa katiba mpya. Awaambie Wakenya kuwa Watanzania wanatamani wapate nao nafasi ya kuingia mkataba mpya (katiba mpya) na watawala wao. Njia pekee ya kufanya hivyo ni kuiondoa CCM madarakani kwa sababu wameshindwa kutambua hilo na kuendelea kukumbatia katiba iliyoandikwa hovyo hovyo kwa manufaa yao.
   
 16. N

  Nyanzura Member

  #16
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hii ni babu kubwa nimeipenda, haya mambo ni mazuri yametulia, ushauri wangu kwa CHADEMA, kwenye Kampein zenu tumieni lugha rahisi ya kawaida kabisa isiyo na misamiati migumu ambayo wananchi wa kada zote watawaelewa mnachotaka kufanya pindi mkiikamata hii nchi (Lugha iendane na kundi la watu mnaoongea nao). Wakielewa itakuwa rahisi kwao kueleza wenzao ambao hawakupata nafasi ya kuwasikiliza.

  Ni sawa Jeshi letu ni kubwa lakini, hiyo sera ya kulipunguza haitawafanya wanajeshi waogope kumuchagua Dr. Slaa kama kamanda mkuu? Watu wasije hofia kumwaga unga hapo.

  Go Dr. Slaa in you we Trust!!!!
   
 17. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Oh Yes!
   
 18. F

  Fanfa JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2010
  Joined: Sep 25, 2009
  Messages: 538
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sera na mtazamo kama huu ndio tunaoutaka ili nchi hii iendelee. Tunasubiri ilani ya CHADEMA kwa hamu. Mungu akusaidie uwe rais wa nchi hii
   
 19. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #19
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Mkakati huo wa uongozi ndio unaotakiwa Tanzania. Kuwa na serikali inayozidi ile ya Uingereza huku viongozi wakilipwa sawa na wale wa uingereza kwenye uchuni huu ndiyo maana serikali inaishia kuwa ya kuombaomba misaada, huku raia wetu wakiishi maisha ya mapangoni
   
Loading...