Dr Slaa: Mama Salma ni mama wa nyumbani!

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,120
2,000
Katika mikutano yake inayoendelea mkoani Kagera mkuu wa msafara wa Ukawa ambaye pia Katibu mkuu wa Chadema Dr W. Slaa amesema waliambiwa na IGP wakati wa kikao cha makatibu wa vyama vinavyounda Ukawa kwamba RPC wa Lindi na Mtwara walijifungia ndani kupata taarifa ya Mama Salma anafanya mikutano kinyume na amri ya kuzuia mikutano ya kisiasa mikoani humo.

"Hawa mapolisi wanashangaza sana, wamefikia hatu hatua ya kutetemeka wanapomuona mama huyu , huyu si mama wa nyumbani tu?" alisema na kuwafanya umati kuangua kicheko huku wengine wakishangilia kwa nguvu. Alisema kitendo cha Mama Salma kuachwa afanye mikutano sehemu iliyozuiliwa ni kitendo cha kuonyesha kwamba kuna watanzania daraja la kwanza na la pili.

Source: Mi mwenyewe katika msafara na sasa tunaingia Ngara.
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195

Bila hata kutafuta ushahidi, ni wazi kwa sasa taifa letu lina madaraja ya kutosha. Siyo karibia na usahihi kuhisi kuna wananchi wa daraja la kwanza na la pili. Kuna zaidi ya hapo.

Ndiyo maana, kuna wengine wanaiba, wanaambiwa wao sheria za kukamatwa na kufikishwa mahakamani haziwahusu. Warudishe walichoiba, waende zao. Ndiyo maana wakati wengine wanabanana hospitali na vitanda havitoshi, kuna wengine wakijisikia mafua, vipimo wanaenda kufanyia India, kama nasingizia mwulizeni Lukuvi. Ndiyo maana wakati barabara zenu zinajengwa leo zinaharibika miezi minne ijayo, kuna mitaa wana barabara bomba na hazina shida! Na tena ndiyo maana wakati nye shule zenu hazina walimu, maabara za majaribio ya kisayansi na maktaba, wakati nyie mnaambiwa watoto wenu hawajafeli, wamepata division five, wa wengine wako nje ya nchi kwani division five hazina maana kwao! Kuna haja ya kubisha kuwa kuna madaraja?

Kama hakuna madaraja, ni mara ngapi Waziri mkuu amelalamikiwa kwa kudanganya bunge na hajachukuliwa hatua? Ni kwamba kanuni za bunge zimemshindwa? Ni mara ngapi amelalamikiwa kwa kutoa kauli zinazovunja katiba na ameachwa tu? Au ni mara ngapi Viongozi flani wa CCM wamekuwa wakilea vikundi vya kuvuruga amani huku serikali ikiwa inajua lakini wala hawaulizwi?

Ni kweli madaraja yapo, Kuna ya watwana (wananchi) na Untouchables (watawala na familia zao), hata yale ya polisi na wahalifu wanaolindwa ni madaraja. Kwa hiyo asipoteze bure mshangao wake. Aendelee mbele kwa kuja na namna ya kuondoa madaraja yaliyopo, kwani tayari yapo.

cc. Dr.W.Slaa
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Kwa vile yeye ni mwanaume tena wa UKAWA, hawezi kujua maana ya first lady. Hivi utamlinganisha na wanawake wengine huyu mama anayelala Ikulu?

Dr Slaa kama hqjui umuhimu wa First Lady, amuulize Josephine

Mkuu, kwangu namuonaga Dr Slaa ni mtu aliyefilisika kisiasa

Hoja siyo "umuhimu wa first lady" hoja ni double standards katika kutekeleza amri ya serikali ya "kutofanya mikutano ya kisiasa mikoa ya kusini" Nadhani hakuna ubishi kuwa Mama Salma analala wapi. Wala kauli haikosei kusema ni Mwanamke wa nyumbani. Nayo ni sahihi pia.

Swali ni kwa nini anakiuka maagizo ya serikali? Na kwa nini anaangaliwa tu? Cha ajabu ni vipi Law upholders (polisi) wanajificha badala ya kusimamia maagizo? Nadhani haya ndiyo ya kujadili hapa.
 
Mkulia

JF-Expert Member
Apr 26, 2012
375
225
Kwa vile yeye ni mwanaume tena wa UKAWA, hawezi kujua maana ya first lady. Hivi utamlinganisha na wanawake wengine huyu mama anayelala Ikulu?

Mungu ninaomba uibariki Tanzania na watu wake!
Hivi ni kweli kuwa Salma aachwe afanye atakavyo maadamu yeye analala na kuamka ikulu au kwa kuwa ni 1st lady? Kama watanzania akili zetu zimefikia hapo basi ni hatari.
 
xenaxena

JF-Expert Member
May 20, 2014
2,237
1,500
Mungu ninaomba uibariki Tanzania na watu wake! h
Hivi ni kweli kuwa Salma
aachiwe afanye atakavyo maadamu yeye analala na kuamka ikulu au kwa kuwa ni 1st lady?:fear: Kama

watanzania akili zetuzimefilia hapo basi ni hatari.
Aeleze bajeti yake ya shirika lake iko wapi?, je,mfuko wa mama mkapa alikabidhiwa?
 
bendaki

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
954
250
Kwa vile yeye ni mwanaume tena wa UKAWA, hawezi kujua maana ya first lady. Hivi utamlinganisha na wanawake wengine huyu mama anayelala Ikulu?

Nini shuguli za first lady? Anaruhusiwa kuendesha siasa? Nitofauti na wanawake wengine je ni mwana siasa. Katiba inalisemeaje la mke wa rais?
 
Hansard

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
838
225
Dr Slaa atuambie ile safari yake ya kujifunza nchini Marekani kwanini Josephine Mshumbusi alilipiwa gharama zote na Chadema? Chadema ilimlipia Joesphine Mshumbusi kama nani ndani ya chadema?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom