Dr Slaa: Maggid, Umetuchukia CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa: Maggid, Umetuchukia CHADEMA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Dec 25, 2010.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Tukiwa Kikoboga Camp, Mikumi, jana na leo nimepata bahati ya kuongea kwa karibu na Dr Willibrod Slaa, Katibu Mkuu ( CHADEMA). Leo kabla ya mlo wa mchana tuliongea kwa kirefu. Mazungumzo yalikuwa ni ya kirafiki sana. Tulikumbushana tulipokutana mara ya kwanza, mwaka 2004 mwezi Julai. Wakati huo, rafiki yangu Zitto Kabwe ndiye aliyenitambulisha kwa Dr Slaa pale zilipo ofisi za CHADEMA, Kinondoni.

  Dr Slaa: " Maggid, umetuchukia CHADEMA, tangu nikuone wakati ule hujaja tena kwetu!"

  Mimi: " Hapana Dr, naishi Iringa, ni mbali na Dar. Ningependa nionane mara kwa mara na wanasiasa, lakini nashindwa. Hata Mzee Makamba nimeonana nae mara moja mwaka 2007. Mpaka hii leo hatujakutana tena. Nimemwona leo hapa mbugani akiwa kwenye gari, nimempungia mkono tu".

  Wakati nikimpa majibu hayo Dr Slaa, kichwani nafikiria, hata Profesa Lipumba nimeonana nae mara moja tu, mwaka 2005, tangu wakati huo hatujatiana machoni. Na James Mbatia namsoma tu magazetini, ningependa nikutane nae siku moja.

  Kisha Dr Slaa na mimi tunajikita kwenye mazungumzo ya siasa. Namweleza Dr Slaa;

  " Dr, naamini tumefanya kosa kubwa kama nchi mara ile tulipoingia kwenye mfumo wa vyama vingi bila kuifanyia marekebisho katiba ya nchi yetu. Tuliwaamini wanasiasa wetu, lakini sasa tunaona, kuwa wanatuangusha. Ufisadi umetamalaki, baadhi yao ndio wenye kushiriki ufisadi huo, na Katiba inawalinda. Tunahitaji marekebisho makubwa ya Katiba yetu".

  Dr Slaa: " Ni kweli kabisa".

  Kisha Dr Slaa anachambua kwa undani kwa kutoa mifano. Mazungumzo yamepamba moto. Iko siku nitarejea mazungumzo yangu na Dr Slaa kuhusu hili la Katiba na mengineyo.

  Picha zaidi: http://mjengwa.blogspot.com
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Umesema Makamba umemuona kwenye gari umempungia mkono tu mbona kwenye picha umepiga nae au hiyo ilikuwa 2007????
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 5. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  huyo dogo kwenye picha ni nani
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  hizo picha zinaonekana kabisa kuwa hazijapigwa siku moja
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  tunayangojea kwa hamu, sasa sijui itakuwa lini
   
 8. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #8
  Dec 25, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Mtoto wa Maggid... Kwani hujui Bw.Maggid ana wakwe Uswidi???
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  MJENGWA heshima yako mkuu.. umemuuliza DR kwa nini yeye hakukomaa kama Alassane Quattara wa ivory cost?
   
 10. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #10
  Dec 25, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii story imebeba jambo fulani. Na bado wengi tu watajisalimisha!
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  mgao wa umeme umeshampata naye lol!
   
 12. m

  maggid Verified User

  #12
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ivuga,
  Bahati mbaya, swali hilo sikuliuliza!
   
 13. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #13
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  no comment.
   
 14. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #14
  Dec 26, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Nashukuru sana bwana Maggid kwa utangulizi mzuri,nimeutazama kwenye blog yako na nimependa ulivyoanza lakini tatizo lako ndugu yangu ni kuwa mara nyingine huwa unaanza simulizi kwa mbwembwe kisha unapotea na hutoi sababu za kutomalizia simulizi zako,hali hiyo inatuvunja moyo sana wale tunaofuatilia makala zako.Kwa mfano unaweza kutueleza tu ni kwa sababu gani hukumalizia ile makala yako ya kifo cha mzee Mwamwindi?Au walikuzuia wenye nchi?Kwa hiyo basi naomba na hii nayo utakapoianza basi ujitahidi mtiririko wake ufike mwisho na sio kuishia njiani.

  Asante sana:Ni mimi mfuatiliaji wa makala zako.
   
 15. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #15
  Dec 26, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hahahahahaha,kumbe sometimes muongo pia eh
   
 16. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #16
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  ???
   
 17. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #17
  Dec 26, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sasa mi sijaelewa, what is the story here?
   
 18. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #18
  Dec 26, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Acha unafki Maggid wapi sijui toto ya jk hukupiga nayo picha:frusty::frusty::frusty::frusty:
   
 19. Kibaraka

  Kibaraka JF-Expert Member

  #19
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Natamani hili sawali Maggid angelijibu.
   
 20. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #20
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280

  Majid ni mnafki tu kama walivyo wanafki wengine, nilikuwa namuheshimu sana na nilikuwa navutiwa na makala zake, lakini lah wapi! njaa na akili haviwezi kwenda pamoja hata siku moja. yaani sasa hivi ndio wanajifanya wamezirudisha akili zao kwenye vichwa vyao kutoka kule walipoziacha kipindi cha kampeni. hawa mtaji wao ni kalamu na camera tu, hawana lolote. HYPOCRITES.
   
Loading...