Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
Wakati huohuo Joseph Senga kutoka Chunya anaripoti kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa, amewataka maaskofu kutohubiri amani na badala yake wahubiri kwanza kupatikana kwa haki.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kanga, wilayani Chunya, jana, Dk. Slaa alieleza kushangazwa kwake na viongozi hao wa dini ambao wanahubiri sana suala la amani ambalo ni tunda la haki. "Nawaomba hawa maaskofu wanisamehe tu, kuhubiri amani wakati hakuna haki haitoshi," alisema Dk. Slaa.
Alisema kuwa maaskofu wanashutumu vyama vya siasa vinaharibu amani wakati amani ni zao la haki. Amesema baadhi ya maaskofu na masheikh wamekuwa wakiunga mkono yanayotolewa na viongozi mbalimbali ambao wao wana maslahi katika hilo.
"Yesu alihubiri haki kwanza, na hawa wanatakiwa kuzingatia hilo kwani amani haiwezi kuwepo bila haki," alisema.
Tanzania daima