Dr. Slaa: Lowassa alijieleza kwetu tukamuelewa, pia wapo wengine wanakuja

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Katibu mkuu wa Chadema Dr. Willbrod Slaa amebainisha kuwa Edward Lowassa alijieleza mbele ya kamati kuu na akaeleweka vyema.

Aidha Dr. Slaa amewataka wana Chadema na watanzania kwa jumla kuwa wavumilivu kwani wao kama viongozi wa Chadema wanajua wanachokifanya wana uhakika wa100% kushinda uchaguzi mkuu ujao katika ngazi zote kama UKAWA.

Aidha Dr. Slaa amesema kuwa swala la Lowassa kujimuika Chadema pia liliridhiwa na UKAWA kwani kwa sasa ni wamoja na wanashirikiana kwa kila jambo.

Dr. Slaa amesema kuwa mgombea urais wa UKAWA atatangaza rasmi agost 5. Na sasa kila shauri kuhusu mgawanyo wa madaraka UKAWA lipo vizuri
 
Hivi kwanini mnawafanya watanzania wote wapumbavu..
Mbowe jana kasema walimpigia magoti Fisadi PAPA lowassa na kumuomba ajiunge nao.
Sasa wa kujieleza ni nani hapo.

Nasubiri kauli yake nichome kadi au la.
 
Dr. Slaa Je umemfuta kwenye list of shame na kumuingiza list of fame?/ hilo ndilo tunalolihitaji toka kwako na UKAWA
 
Hatuwezi kuua chama cha wakulima na wafanyakazi tukaacha chama cha majambazi kushika dola, ccm mbele kwa mbele
 
Sijui nicomment nini kwa jinsi nilivyosuuzika roho yangu kutokana na speech hii ya Dr!!!! Mola akujaalie sana Dr. Slaa!!!!!
 
Back
Top Bottom