Dr. Slaa, Lipumba, Sendeka na Anna Mghwira

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,197
2,000
Nawaona kama watu muhimu katika serikali ya Dr Magufuli endapo watapata nafasi kwani wamekuwa wakionyesha uwezo wao katika nyanja mbali mbali za kisiasa. Ni mawazo yangu lakini.

Dr. Slaa katika mambo ya kimataifa anafaa sana.

Sendeka pale bungeni anafaa sana katika kujenga hoja

Lipumba katika mambo ya uchumi pia anafaa.

Mghwira katika mambo ya maendeleo ya jamii akishirikiana na Mama Magreth Sitta watasaidiana kutatua changamoto nyingi za jamii.

Nawasilisha.
 
LEGE

JF-Expert Member
Oct 14, 2011
5,107
2,000
KWA serikali ipi ya ccm ?? wataisoma namba.
nafasi zishajaaa washalipana fadhila .

tatizo nchi yetu hatuongozi kwa manufaa ya nchi Bali kwa manufaa ya kulipana fadhila
 
BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,040
2,000
Slaa na Mambo ya kimataifa!!!!! Daah!
After all wameshamalizana,
"They dont know him, He dont know them"
 
Azim Sokoine

JF-Expert Member
Aug 20, 2014
1,027
2,000
mkuu kwani hao uliowataja hapo si washirika wa ccm,dr.slaa alikuwa anafany kazi ya kuuchafua upinzan so lazima ccm ilipe fadhila
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,202
2,000
Nawaona kama watu muhimu katika serikali ya Dr Magufuli endapo watapata nafasi kwani wamekuwa wakionyesha uwezo wao katika nyanja mbali mbali za kisiasa. Ni mawazo yangu lakini.

Dr. Slaa katika mambo ya kimataifa anafaa sana.
Sendeka pale bungeni anafaa sana katika kujenga hoja
Lipumba katika mambo ya uchumi pia anafaa.
Mghwira katika mambo ya maendeleo ya jamii akishirikiana na Mama Magreth Sitta watasaidiana kutatua changamoto nyingi za jamii.
Nawasilisha.
Huyo Slaa na Lipumba tayari walishakabidhiwa chao kwa ajili ya 'special mission' ya kuiangamiza Ukawa, sasa unataka CCM baada ya tayari kupata kile walichokuwa wanakitaka wataona tena umuhimu wa hao watu?
Hao watu hivi sasa wanaonekana kama 'rubbish' ambapo hawahitajiki tena kwenye hicho chama ambacho kina wenyewe.
 
Ngoshanyi

JF-Expert Member
Jun 14, 2013
2,460
1,500
Ccm imekamilika haikodi viongozi wamejaa tele. Mambo ya kukodi ni kwa wachaga kule
 
mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
2,367
2,000
Ana mughwira,amwamwimbie wamuombee kwa ccm amewe ubunge wa viti malumu kupitia viti kumi vya Rais
 
Zungu Pule

JF-Expert Member
Mar 7, 2008
2,218
2,000
Kwa nini tunapenda sana ku-recycle viongozi? Hawa wote uliowataja walishapata nafasi wakafanya walichofanya. Kwa nini tusiwape nafasi watu wengine wenye uwezo zaidi? Kwa nini baraza la mawaziri lisiundwe na technocrats? Kama walivyofanya Kenya? Mama Sitta, Ole Sendeka watatusaidia nini karne hii ya 21 zaidi ya kutupotezea muda? Tufikirie nje ya box. Tusifikiri kwamba nafasi za uongozi serikalini ni kulipana fadhila au zawadi kwa washirika wetu. Hivi kweli bado unaamini tunahitaji hawa watu kama tunataka kujenga uchumi wa kisasa, unaoendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia?
 
Zungu Pule

JF-Expert Member
Mar 7, 2008
2,218
2,000
Ana mughwira,amwamwimbie wamuombee kwa ccm amewe ubunge wa viti malumu kupitia viti kumi vya Rais
Hebu nisaidie kidogo historia ya huyu mama? Naona siku za karibuni amepata sifa nyingi ila sijaweza kujua sifa hizo zinatokana na nini? Na CCM wanampenda sana, pengine kwa kuwa hakuonesha kuikosoa serikali ya CCM? Ukiona wewe ni kiongozi wa chama cha upinzani na CCM wanakusifia, basi ujue hufanyi kazi yako sawasawa.
 
IROKOS

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
8,283
2,000
Kwa nini tunapenda sana ku-recycle viongozi? Hawa wote uliowataja walishapata nafasi wakafanya walichofanya. Kwa nini tusiwape nafasi watu wengine wenye uwezo zaidi? Kwa nini baraza la mawaziri lisiundwe na technocrats? Kama walivyofanya Kenya? Mama Sitta, Ole Sendeka watatusaidia nini karne hii ya 21 zaidi ya kutupotezea muda? Tufikirie nje ya box. Tusifikiri kwamba nafasi za uongozi serikalini ni kulipana fadhila au zawadi kwa washirika wetu. Hivi kweli bado unaamini tunahitaji hawa watu kama tunataka kujenga uchumi wa kisasa, unaoendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia?
Mkuu wapi kitufe cha like??? Yaani huwa nakereka sana na haya mawazo mgando ya viongozi wale wale, eti Olesendeka, mara Slaa, mara Sitta atafaa uspika, mara Shukuru kawambwa anafaa elimu etc. Hivi hapa Tanzania watu wengine wamesoma kwa ajili ya nini?
 
pembe

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
2,065
2,000
Tunaposema ELIMU, ELIMU, ELIMU ndio maanake. Tunataka tuone sura mpya tena vijana kwenye baraza la mawaziri.
 
Top Bottom