Kanyafu Nkanwa
JF-Expert Member
- Jul 8, 2010
- 849
- 103
Kama ilivyotegemea, uchaguzi umeisha. Lakini jambo moja ambalo ni baya na la kinafiki, ni kitendo cha top brass ya Chadema kujaribu kumtosha mwenzao. Slaa. Kumtosa kwa maana ya kwamba kuteuliwa kugombea Urais, taaisisi ambayo ni ngumu sana kwa mfumo uliopo nchini humu. Haikuweza kufikiriwa kwamba mtu kama Slaa angeingia mkenge wa kuwania Urais ambao kamwe hasingeweza kuupata. Nasema kwamba asingeweza kuupata kwa sababu ni dhahili kuwa maeneo mengi ya nchii hii yamefunikwa sana na CCM kwa namna zote.
Ilikuwa ni jambo la maana sana kwa Chadema na vyama vingine kujaribu kuwaelimisha kwanza watanzania maana halisi ya vyama vingi. Watu wengi nchini mtu akiwa na hela huwa ni 'hero' na kitendo cha Slaa kutumia silaha ya ufisadi kwa namna yoyote ile haikuweza kusaidia chochote.
Tunatambua kuwa ni kweli kulikuwa na matatizo ya kupiga na kuhesabu kura. Pia tunatambua kuwa kulikuwa na uchakachuaji wa hali ya juu sana kutokana na woga wa CCM kushindwa. Lakini ukweli unabakia pale pale kuwa kama ambavyo Slaa anadai, kurudiwa kwa kuhesabu sana sana angeshangaa sana, maana uwezekano wa CCM kupata zaidi ulikuwa ni mkubwa mno.
Tusidanyanyike kwa propaganda za uwongo wakati sisi tuna akili nyingi sana. Ukweli unabakia kuwa Slaa kapigwa chini kabisa. Suala la kuwa watu wachache ndiyo waliopiga kura linachagisha uwezekano kuwa kama wangepiga wote basi CCM ingeweza kupata asilimia kubwa zaidi na si kwa Slaa kushinda.
nafahamu kesho Slaa ataongea. Aongee chochote, bado CCM ndiyo bingwa na ataendelea kuwa bingwa milele kama tukiendelea kuwa wabinafsi kama tulivyoonyesha mwaka huu.