Dr. Slaa kuzungumza na Vyombo vya Habari, Serena Hotel - Septemba 1, 2015

Status
Not open for further replies.
Hatimaye katibu mkuu wa Cham cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Wilbrod Slaa ameamua rasmi kuachana na siasa baada ya tafakari ya muda mrefu.

Kesho Slaa anatarajiwa kutangaza uamuzi wake huo ndani ya 'Dar es Salaam Serena hotel' ambao utakuwa ni pigo kubwa kwa vyama vinavyounda UKAWA.

Katika hatua nyingine mwanachama wa CHADEMA anayeamini katika siasa za Dr. Slaa, G Sam ameamua kumuunga mkono kutokana na mizengwe ya uteuzi wa mgombea urais ndani ya chama hicho.

"Nitapiga kura kwa Halima Mdee na mgombea udiwani wa Chadema ila siyo kwa Edward Lowassa" anasema G Sam.

G Sam anamuona Edward Lowassa kama mgombea dhaifu sana asiyeweza kwenda sambamba na kasi ya chama hicho. Aidha G Sam anakiri kuwa hana tatizo na Edward Lowassa kuhusu mambo ya ufisadi bali ni kutokana na udhaifu unaoonekana waziwazi juu ya mgombea huyo.

Jambo moja lilo wazi ni kuwa Chadema hawapendi kabisa Dr. Silaa afungue msomo.
Kumekuwa na mada na posts kibao za kumwomba akae kimya...afunike kikombe..
Lakini waliokatwa huko kwa magamba wanapiga kelele nyingi wahame kambi.
Kwa jinsi ukimya wa Silaa ulivyokuwa unaombwa...naamini wanajua wamekosea nini na kwa sababu gani..
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: nao
Dr Slaa staafu tu baba! Umejenga chadema kwa ukimya wa Lowassa! Leo Lowassa ameongea ukweli kuhusu ufisadi anaolazimishwa nao! Ukweli huo umemweka huru na kuaminiwa na vyama vyote vya siasa kupeperusha bendera yao ya urais 2015!

Sio Ikulu sio Kikwete aliyewahi kukana ukweli aliobainisha Lowassa kuhusu richmond. Hii maana yake ni kwamba Lowassa kaongea ukweli mtupu!

Sasa wewe unasusa nini? Unataka Lowassa asiseme ukweli?

Mwombe radhi Lowassa kwa kumbebesha mzigo mkubwa wa ufisadi aliotakiwa kubebwa na Bosi wake! Ukimya wa Lowassa ni hekima toka kwa Mungu! Mungu ni mkimya! Kwa kumuomba radhi maana yake Mungu naye atakusamehe. Japo ni siasa lakini Mungu bado ana nafasi kuu. Usibeze maana kila mtu hulipwa sawasawa na maneno na matendo yako!

Kikwete ndio fisadi sio Lowassa!
 
Kwa matapishi haya ya Slaa tusitegemee CCM kufurahi kesho' Aidha,Dokta Slaa alisema kitendo cha Ufisadi huo kutokea na Idara ya Usalama wa Taifa kushindwa kulinda nchi kwenye ufisadi huo ni wazi idara hiyo imeshindwa kazi. “Usala wa Taifa upo kila Barozi inashangaza sana kuona Idara hii inashindwa kuona utaperi wa mmiliki wa IPTL au tutegemee nini ndio maana hata kwenye Ufisadi wa EPA,tuliona Jinsi Kampuni iliyokuwa ikimilikiwa na Ofisa wa Usalama wa Taifa ilivyochota pesa unategemea nini”
“Na hata Kikwete alivyosema mara baada ya kutua uwanja wa ndege alipotoka kutibiwa anavyosema alijui sakata hili kutokana na yeye kuwa kwenye matibabu , ni kuwadanganya watanzania kwani baada ya masaa mawili kutoa uwanja wa ndege hapo,niliona email aliyekuwa akitumiana na bwana Rugimalira,sasa huyo ni kiongozi kweli”alihoji Dokta Slaa
Maumivu anayopata Dr Slaa kwa sasa ni makali kuliko hata hayo maneno. Kama Sumaye alisema kuwa CCM wakimteua Lowasa yeye anahama chama lakini cha kushangaza leo wapo pamoja, utashangaa vipi ya Dr Slaa?
 
Maumivu anayopata Dr Slaa kwa sasa ni makali kuliko hata hayo maneno. Kama Sumaye alisema kuwa CCM wakimteua Lowasa yeye anahama chama lakini cha kushangaza leo wapo pamoja, utashangaa vipi ya Dr Slaa?

Leo Dr. SLAA amekuwa mzuri kwako hahahahaa ngoja tusubiri kesho Faiza Foxy atasema nini
 
Huu ni usajili wa kuvunja rekodi ya dunia kama sio tz


Usajili unaendelea dirisha bado halijafungwa!!!!
 
keshokutwa Headlines za English n papers zitakuwa like:
* Slaa defects to CCM
* Slaa's U-turn to CHADEMA
-Insists he was on leave
-Declare support to incumbent UKAWA presidential candidate.
*Slaa quit politics. - Speaks out about Opposition Parties status
- Says UKAWA grinds opposition politics to a halt.
* Slaa in dilemma. - Says he'll reveal his stance after October poll
* Slaa adds Opposition momentum as he declare his comeback.
Etc

u wrie good english big up
 
Mimi kura ya Udiwani Chadema, Ubunge Chadema ila Urais ACT Wazalendo yule mama jana amenikosha sana.!

Kwa Mafuriko ya kura za Lowasa mwaka huu, wewe nenda tu mwalimu unaturushia stimu tu,
Kiboko ya ccm ni Lowasa, upadre alioupitia Dr Slaa ilikuwa ni kikwazo sana kupata kura za waislamu waliojaa ujahidina.
 
Mkuu angalia historia ya mtu, Lowasa ni kiongozi wa kuzaliwa! Kama umefatilia hostoria yake ITV utathibitisha haya! Udhaifu pengine unaotokana na maradhi ni jambo ambalo hata Dr.Slaa lingeweza kumfika wakati wowote maana na yeyeni mwanadamu!

Lakini tukiwaweka kwenye mizani ya uongozi bado Lowasa ni kiongozi japo Dr.Slaa pia ni kiongozi lakini kuna tofauti! Lowasa ana kitu ambacho Dr.Slaa hana! Lowasa ni mtu wa watu wote lakini Dr.Slaa hamfikii katika hili! Nasema hili wazi kwamba kuna watu wengi walikuwa wanamwogopa Dr.Slaa kwa sababu wanasema ni mkali mno!
Kweli ukawa ni malofa. Lowassa ajitengenezee sinema yake itv, halafu mijinga humu inaitumia kama benchmark. Hii nchi ujinga wake ni mzito kuliko mwezi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom