Dr. Slaa kuzindua kampeni za ubunge Chalinze leo Jumapili tarehe 16.03.2014

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Leo ni leo katika kata ya Miono ambako ni nyumbani kwa Marehemu Said Bwanamdogo ,uzinduzi wa kampeni za Chadema utaanza kuanzia saa nane mchana leo , hamasa ni kubwa sana Miono na hasa baada ya jana CCM kuzindua kampeni zao kwenye eneo hilo na kudoda.

Hapa , ni nyumbani kwa Wazigua ambao wana hasira sana baada ya kifo cha utata cha kijana wao Said Bwanamdogo, ambaye alikuwa ni Mzigua wa kwanza kuwa mbunge wa Chalinze, kwani Chalinze imekuwa chini ya utawala wa Wakwere kwa kipindi chote tangu uwepo, leo CHADEMA wanapeleka Mmasai ambaye ni Mwenyeji,CCM wameamua kumpeleka mwana mfalme , eti sifa yeye ni mtoto wa Rais , baba yake amekuwa mbunge wa Chalinze kwa miaka 15 , ila ameshindwa kutatua changamoto za Jimbo husika, mtoto ataweza kuziattach kweli!

CHADEMA , leo wanataka kushangilia ushindi wa Kalenga Chalinze , wanataka kuwa onyesha wananchi wa Chalinze kuwa ni watu muhimu sana kwao ndio maana wanazindua leo....

Nitawaletea live updates ya kinachojiri ....
 
Miono na wana jimbo wote wa Chalinze hili ni fursa adhimu kwenu kuonyesha kuwa jamii ya Pwani iko tayari kwa mabadiliko baada ya mdororo wa kuogopa kufanya maamuzi kwa muda mrefu dhidi ya chama tawala ambacho kimedhihirisha kuwa chaguzi ndogo ni kwa ajili ya watoto wa vigogo kwenye chama hicho.

Jimbo lina changamoto kubwa ya maji wakati liko kwenye chanzo kikubwa cha maji (WAMI) kwa mikoa ya pwani na dsm, inasikitisha kukuta jamii za wafugaji na wakulima wana shear maji na wanyama hususani kata ya Ubena zomozi na ile ya kibindu. Nimeshangazwa CCM kuanza kutengeneza barabara ambazo zilikuwa hazipitiki tangu miaka 3 iliyopita! Walikuwa wapi hadi wasubiri uchaguzi ndio ndio watengeneze barabara ya kwende kijiji cha Mkoko ambacho walikidharau siku nyingi?
 
Chadema badala ya kujikita kwenye sera na kuwaeleza watu wa Chalinze mtawafanyia nini mnajikita kwenye siasa za fitna kujadili kifo cha mbunge.
 
Dunia iliumbwa ili tuitawale na kufanya mabadiliko ya Kweli ndio maana tukapewa akili za kujua mema na mabaya pia kusoma nyakati, America walifanya maamuzi magumu kumchagua mtu mweusi BARACK OBAMA kwa tija, huko ndiko binadamu anapoonekana ANA fikiria na sio kukariri, CCM haina lolote zaidi ya kutapatapa sasa hivi haina uwezo zaidi ya kusimamisha watoto WA marehemu Baba zao na Chalinze mtoto WA Mshua ni Aibu sana' Tafakari kwa undani utaona kama mfanyabiashara, biashara haitoki ila anakula Mtaji mwisho WA siku anafunga duka hao ndio CCM.
 
Tukishirikiana kwa pamoja tutaishangaza dunia,yu wapi mkuu wa kanda ya pwani? Gwiji la siasa,nguli wa sheria,wakili msomi mabele malando pamoja na prof wa sheria,mwanasheria wa kujitegemee wengi twamwita Mwalimu wa sheria Prof safari kwa heshima na taadhima naomba wasimamie kanda yao ili twende sawa naikibidi waweke kambi kabisa,wapenda sifa wa mujini hasa matajiri wenye ukwasi wameapa kutupa hela mpk mtoto wa mkuu awe mbunge wa JMT,kwa sisi rushwa sio jadi yetu twendeni tukawaelimishea wakwere kuwa "Kula ccm,Kura cdm" wapokee hela zao ila kura wazipeleke kwa mgombea wa cdm
 
Chadema badala ya kujikita kwenye sera na kuwaeleza watu wa Chalinze mtawafanyia nini mnajikita kwenye siasa za fitna kujadili kifo cha mbunge.


Ndo sera ya chama kusema ukweli, tulieni watu waelezwe ukweli, maana vifo vya viongozi wengi vimekuwa vya utata ili ama kutoa kikwazo ktk ufisadi au watoto wa vigogo wapate nafasi. Sasa lazima watu wafunuliwe macho. Kwa nini unapiga mayowe?
 
Kumbe cdm walishazindua mbona hatukuona mbwembwe zao au mambo magu sana.
 
Walilemewa na zigo la kipigo cha kisiasa walichokuwa wanakipata katika Jimbo la Kalenga!.

Kwa sasa husikii hata kiongozi wa juu wa chama akiwa Chalinze pamoja na kuzindua kampeni ya CHADEMA jumapili iliyopita. Dr. Slaa alifungua kampeni na kukimbia haraka kurudi mtaa wa Ufipa.
 
Walilemewa na zigo la kipigo cha kisiasa walichokuwa wanakipata katika Jimbo la Kalenga!.

Kwa sasa husikii hata kiongozi wa juu wa chama akiwa Chalinze pamoja na kuzindua kampeni ya CHADEMA jumapili iliyopita. Dr. Slaa alifungua kampeni na kukimbia haraka kurudi mtaa wa Ufipa.

Dr. Slaa Ana kazi zaidi ya kampeni , Kinana hana kazi nyingine ndio maana anarandaranda Chalinze kila uchwao.......
 
Dr. Slaa Ana kazi zaidi ya kampeni , Kinana hana kazi nyingine ndio maana anarandaranda Chalinze kila uchwao.......
Yes, you are right.

Hivi unategemea kiongozi anayefanya kazi na timu asiyoiamini atafanya nini zaidi kama siyo kufanya kazi zote.

Hili hata halina ubishi. CHADEMA ni chama chenye viongozi wasioaminiana katika majukumu ya kiutendaji. Hakuna delegetion of power. Katibu Mkuu, Dr. Slaa anataka kufanya kazi zote hata zile ambazo zingefanywa na junior political officer kwa sababu hawaamini na kikubwa kabisa, hataki madudu yaliyojificha kuhusu utendaji wa ofisi yake wafanyakazi wengine wayafahamu.

Viongozi wa CCM wamegawana majukumu na katika kugawana majukumu, ndiyo maana unawaona wame relax katika kazi zao kwa sababu wanaaminiana na katika kuaminiana, ndiyo delegation of power inapofanyika. wewe unaona ni kuranda randa, wakati hiyo katika CCM inaitwa, spread the work burden.

Hivi chama ambacho hakina hapa ofisi katika wilaya zote nchini achilia mbali katika vijiji kinaweza kikawa na majukumu mengi zaidi ya chama chenye ofisi katika vijiji karibia vyote nchini?. Give me a break!.
 
Dr.w. slaa ana penda posho sana yani hadi za chalinze ambako walipaswa kujitoa amelazimisha kuweka mgombea.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom