Dr Slaa Kutoonekana kwenye mazungumzo ya CDM na Rais Je ni kuepuka utabiri wa Marehemu Sheikh Yahya

Status
Not open for further replies.

Amakando

Senior Member
May 9, 2011
158
27
Wana jamvi nimetafakari swala la kutokuhudhuria kwa Dr Slaa katika kikao cha wajumbe wa CDM na Rais Kikwete sambamba na mambo yaliojiri nikapata majibu kuwa huenda Marehemu Sheikh Yahya alikuwa mtabiri wa Ukweli kwa sababu zifuatazo.

a) Alitabiri kuwa Dr Slaa na Kikwete watakaa pamoja na kukumbatiana kabla mwaka haujamalizika.
b) Mwitikio wa haraka wa Mheshimiwa Rais wa kukubali kukutana na wana CDM hasa ukizingatia kuwa Dr Slaa alikuwa miongoni mwa majina tajwa katika kamati iliyoteuliwa na CDM kumuona Rais japo hakutokea, je inawezekana Rais nae alikuwa ana kumbukumbu za utabiri huu.
c) Kwa kuwa hakuna sababu maalumu mpaka sasa ya kutokuwepo kwa Dr Slaa katika kikao kile nafikiri Dr aliona asitekeleze kwa makusudi ili kuepuka utabiri kutimia kikamilifu.
d) Katika utabiri alisema kuwa hawa wanasiasa wakionana hali itakuwa shwari na hii inanielekeza kuamini hivyo kutokana na kauli ya Mh Freeman Mbowe kuwa baada ya makubaliano kwa sasa hakutakuwa na maandamo tena.

Wanajamvi nawasilisha.
 
Swala ni kwamba ilitabiriwa na inataka kufanana, kwenye u ccm siko wala CDm
 
Naona kama kuna mrithi wa sheikh hapa!! Ngoja nichape zangu usingizi......
 
Taarifa iliyotolewa ni kwamba Dr Slaa alitoa udhuru wa kuuguliwa...........stoooooop ramli
 
Sababu alizotoa Dr. Slaa:

1. Alitoa udhuru ya kuuguliwa,
2. Jana nimemuona mimi kwa macho yangu huku Arusha, yupo kwa ajili ya kesi yao inayoendelea leo nadhani,

So, kama hukuyajua hayo, bora ungekaa kimya kulikoni kuleta ushirikina humu jamvini!
 
Mie nimeeleza kile kilichotabiriwa jinsi inavyotaka kufanana na ukweli kwa swala la unabii sijafikia level hiyo
 
He might have been strategically absent, si unajua kwenye mazungumzo huwa mnaletewa chai na maji "Polonium"!!Sijui kama hawa makomando walikunywa maji/chai?
 
7bu mbona zmetolewa! Kuwa isingekuwa rahic kuwepo kwenye mazungumzo hayo coz alifiwa na ndg yake wa karibu na taarifa hzo alizipata tiyari akiwa ameshatinga Ikulu.
 
Mie nimeeleza kile kilichotabiriwa jinsi inavyotaka kufanana na ukweli kwa swala la unabii sijafikia level hiyo
Acha ushirikina ndugu. hautakusaidia kitu. huyo sheikh amekufa pamoja na uchawi wake, kumbe we bado unamkumbuka? inawezekana ulikuwa mteja wake wewe. ushirikina hautakiwi hapa, hatutaki utabili wa kishetani, wala majini ya sheikh marehem yahaya hapa..
 
He might have been strategically absent, si unajua kwenye mazungumzo huwa mnaletewa chai na maji "Polonium"!!Sijui kama hawa makomando walikunywa maji/chai?

Tuliwashauri wasinywe wala kula chochote huko. Kikwete na genge lake la mafisadi hawaaminiki.
 
acheni imani za kishirikina basi, japo upo, lkn c popote. yaani kikwete awaroge timu yotei le iliyoenda kwake!
 
Sababu alizotoa Dr. Slaa:

1. Alitoa udhuru ya kuuguliwa,
2. Jana nimemuona mimi kwa macho yangu huku Arusha, yupo kwa ajili ya kesi yao inayoendelea leo nadhani,

So, kama hukuyajua hayo, bora ungekaa kimya kulikoni kuleta ushirikina humu jamvini!
Kwanza hata kama angekuwa hana udhuru Dr. Slaa hakustahili kwenda kuonana na wasanii pale Ikulu. Level yake siyo ya kujadiliana na wasanii.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom