Dr Slaa kugombea Urais, mafisadi wajipanga kummaliza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa kugombea Urais, mafisadi wajipanga kummaliza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paparazi Muwazi, Nov 14, 2009.

 1. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tetesi toka vyanzo vya kuaminika vinaeleza kuwa Dr Slaa anatafakari kugombea urais kutokana na shinikizo toka kwa wananchi ndani na nje ya chama chake.

  Habari zinaeleza kuwa hata uamuzi wa viongozi wakuu wa chama hicho na wabunge kufanya kikao cha pamoja Dodoma ilikuwa ni sehemu ya hatua kuelekea maamuzi hayo.

  Taarifa zaidi zinaeleza kuwa wakati CCM ikifanya kikao na wabunge wake Dodoma na Kamati ya Mwinyi, wakati huo huo kikao cha Mbowe na wabunge wa CHADEMA na wakurugenzi wa chama hicho kilikuwa kikiendelea.

  Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kambi ya Lowassa na Rostam Aziz kupata taarifa hizo sambamba na kikao cha kawaida cha kuidhibiti kambi ya Sitta na Malecela palifanyika kikao cha kuidhibiti CHADEMA na kuzima azma ya Dr Slaa kugombea urais kupitia chama hicho.

  Mtoa habari wetu anaeleza kuwa katika kikao hicho iliamuliwa kama mkakati wa muda wa awali uwepo mkakati wa kuvunja imani ya wananchi kwa Dr Slaa kupitia kuvunja imani ya CHADEMA na utendaji wa Dr Slaa kama katibu mkuu.

  Chini ya mkakati huo iliamuliwa kwamba magazeti ya Mtanzania na Rai yaendeshe propaganda za kudumu yenye dhamira ya kuonyesha kwamba CHADEMA ni chama cha udini, ukabila na ubadhirifu wa matumizi ya ruzuku. Kama sehemu ya mpango huo habari za mara kwa mara ziandikwe kumhusisha Chacha Wangwe na Zitto Kabwe na masuala mbalimbali yanayojitokeza ndani ya CHADEMA.

  Kwa upande mwingine, gazeti la Mwananchi ilikubaliwa kwamba liibue suala la Dr Slaa kugombea urais. Tayari gazeti hilo katika toleo lake mojawapo la wiki hii limeshamtaja Dr Slaa kama mgombea urais wa mwaka 2010. Mkakati huo pia utahusisha kuhoji jitihada zote za Dr Slaa za kupambana na ufisadi zikihusisha na nia yake ya kugombea urais na kuelezea vita hiyo kuwa ni ajenda ya kusaka madaraka. Habari hizo pia zitahoji utendaji wa Dr Slaa ndani ya CHADEMA na kutaka aondolewe kama ambavyo kuna shinikizo la kutaka Makamba aondolewe kwenye nafasi hiyo ndani ya CCM. Habari hizo zitahusisha kuhoji baadhi ya watu na hata pale watakapokosekana habari zinazoitwa za kiuchunguzi zitaandikwa.

  Mtoa habari anaeleza kuwa uamuzi wa kambi kuishughulikia CHADEMA na Dr Slaa hautokani tu na ukweli kuwa Orodha ya Mafisadi iliyotolewa naye Sept 15 mwaka 2007 bali unatokana na hofu kubwa ya ushirikiano wa kiajenda kati ya viongozi wakuu wa chama hicho na wabunge wa ndani ya CCM wanaojiita makamanda dhidi ya ufisadi.

  Inatarajiwa kwamba mkakati huo utaweza kuzalisha mgogoro na makundi ndani ya CHADEMA lakini pia utaleta mgawanyiko wa kiajenda ndani ya chama hicho kama ilivyo kwa CCM. Kama mkakati huo ukishindwa kuleta mgogoro ama mgawanyiko basi inatarajiwa walau mkakati huo utasababisha Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu wake Dr Slaa washindwe kukiongoza chama hicho kutokana na mivutano ya moja kwa moja na hivyo chama kupoteza nguvu yake kinapoelekea mwaka 2010.

  Chaguzi za marudio za Tarime, Mbeya Vijijini, Busanda na Biharamulo ambazo kwa sehemu kubwa wagombea wake kwa upande wa CCM walitoka kambi inayoitwa ya mafisadi zimetoa ishara kwao kuhusiana na nguvu za CHADEMA kwenye ngazi za ubunge kuelekea uchaguzi wa mwaka 2010. Hivyo, namna ya kuvunja nguvu hizo ni kuhakisha chama hicho kinavurugika ama wananchi wanapoteza imani nacho mapema.

  Tayari viongozi wakuu wa chama hicho wamekuwa na misimamo tofauti katika hoja zinazohusu ufisadi hali inayoashiria kuanza kwa mpasuko wa kiajenda katika chama hicho. Kwenye masuala hayo mbalimbali Mwenyekiti Freeman Mbowe amekuwa na msimamo sawa na Katibu Mkuu wake Dr Slaa huku Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe akiwa na msimamo tofauti nao.

  Baadhi ya masuala yanayotajwa ni pamoja na kuingia kwenye Kamati ya Madini(Bomani), hoja ya Mkapa kustakiwa, Mitambo ya Dowans, taarifa ya Kamati teule kuhusu Richmond na suala la Dr Mwakyembe kuhusu mradi wa kufua umeme Singida. Katika siku za karibuni viongozi hao wametofautiana kimsimamo kuhusu kutenguliwa kwa uteuzi kwa maafisa wa chama hicho David Kafulila na Danda Juju. Wakati Mwenyekiti Mbowe na Dr Slaa wametoa msimamo mmoja wa kupinga utovu wa nidhamu ya kiutendaji na maadili ya uongozi wa maafisa hao, Zitto amemtetea Kafulila pekee akieleza kwamba hatua hiyo imemwonea ikimlenga yeye na kwamba itaathiri nafasi ya Kafulila kugombea ubunge wa Kigoma Kusini ambapo yeye amemwandaa kwa muda mrefu kuwa mbunge.

  Dr Slaa amekuwa akikanusha mara kwa mara kuwa hakusudii kugombea urais na kwamba yeye anapendelea zaidi kuwa mbunge wa Karatu. Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe ambaye aligombea urais mwaka 2005 tayari ameshatangaza kutogombea urais mwaka 2010 na ameelekeza nguvu zake kurejea bungeni kupitia jimbo la Hai ambalo ameliongoza mwaka 2000 mpaka 2005. Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe, yeye ametangaza kugombea urais siku za baadaye. Wadadisi wa mambo wanaeleza kuwa kwa umri wake, hatakuwa amefikisha umri wa kugombea urais mwaka 2010 hata hivyo anaweza kugombea urais mwaka 2015. Wachambuzi wengine wa mambo wanaeleza kuwa mvutano ndani ya CHADEMA kama ilivyo ndani ya CCM unaweza kutokana na nia za wanaotarajia kugombea urais mwaka 2015 ndani ya vyama hivyo.

  PM
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tunasikia.....unaweza fanya vizuri zaidi ya huu upupu wa KUSIKIA
   
 3. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  lazima utakuwa mpenzi wa timu ya Yanga wewe, kwa ubishi!! Lol

  Ila safi sana.
   
 4. K

  Kilian Senior Member

  #4
  Nov 14, 2009
  Joined: Apr 26, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Amekula pesa za kanisa gani? unaweza kufafanua na kutoa ushahidi? msiropokeropokea bila kujua mnachoongea.
   
 5. M

  Mzee wa Kale Member

  #5
  Nov 14, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninao uhakika hata ukiona watoto wanaporomosha mawe kwenye mti lazima yapo matunda yanapatikana katika mti huo, hivyo majaribu yote haya yanayoelekezwa kwa CHADEMA sishangai hata kidogo ila kwayo ni changamoto na pia kuna njia ya kujifunza ndani yake, bado zinatupa umakini na kujiweka sawa katika safari ndefu za kumkomboa Mtz masikini.
   
 6. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Chadema 'asa hawajuwi kujipanga bana weshaanza kuniboa.
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Loh! Fisadi Slaa!
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,860
  Trophy Points: 280
  Dawa ya Malaria sugu inapatikana
   
 9. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  LOL, hiyo dawa yako ni ya kichina haitaki
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Nov 14, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hongera Dkt Slaa, saizi yako ni Kikwete ambaye ameamua eti "kuongea na watoto" huku mambo ya ufisi-adi yamewekwa kapuni! Kesho atadai eti hajui kwa nini Tanzania ni maskini!
   
 11. M

  Magezi JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Slaa kama akigombea urais angeweza kupata kama wananchi wangekuwa wameelewa na kama vyombo vya usalama vingekuwa vinapenda mabadiliko. Lakini kwa sasa inaonyesha bado vyombo vya usalama havipendi mabadiriko kwa sababu maafisa wengi ktk idara za usalama ni vihiyo na wala rushwa.
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  hana jipya huyo Padre mstaafu na aliyewahi kuwa katibu wa baraza la maaskofu wa kanisa katoliki Tanzania.

  Hana jipya zaidi ya UDINI na UKABILA. dalili ya mvua ni mawingu mnaona sasa ameshaanza ubaguzi wa kufukuza watu wasio wa North.

  Anafanya kazi kwa maagizo ya kanisa tu.

  Sijui kama ataambulia zaidi ya 4% ya jura za urais za watanzania.
   
 13. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #13
  Nov 14, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,850
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280
  "ccm wote hakuna asiye fisadi"- sophia kondo simba.
   
 14. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #14
  Nov 14, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Kweli kuna mtu anaweza kuthibitisha humu kuwa kwa hali ya sasa Slaa anaweza kuwa tishio akashika urais??

  Wananchi hawa hawa wanaowabeba na kuwatandikia mazuria mafisadi?

  Kuna wabunge wangapi, na wapinzani wako wangapi bungeni?

  Natamani iwe hivyo, ila naona kazi kubwa bado haijafanyika, Chadema is wasting time on her own issues rather than spreading good news to voters
   
 15. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #15
  Nov 14, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ficha Upumbavu wako usifiche Hekima Yako
   
 16. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #16
  Nov 14, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hapa umenikosha hasa
   
 17. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #17
  Nov 14, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Wote wakati fulani tulikuwa ccm akiwemo huyu mgombea wenu. Acha ku=generalise, Unajuaje labda wengine wameungama madhmbi yao?
   
 18. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #18
  Nov 14, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kama wameungama madhambi yao na watoke huko...huwezi kumkataa shetani ukiishi nyumba yake
   
 19. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #19
  Nov 14, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Dr Slaa akigombea uraisi nikupoteza mda wake tu na kwa manufaa ya nchi ni vizuri angebaki bungeni hili aendeleze kuleta hoja moto moto.hakuna uchaguzi wa haki sasa kwanini anataka kugombea uraisi? huu mchezo wa viongozi wa wapinzani kutaka uraisi ndio unatufanya kila siku tunayumbishwa na ccm.wapeleke nguvu zao zote kwenye ubunge na waweke mgombea mmoja tu wa uraisi kama kweli wana nia ya kuleta mabadiriko kwenye nchi yetu.wakiliteka bunge kwa kishindo basi itakuwa raisi sana kuchukua kiti cha uraisi hapo baadae.
   
 20. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #20
  Nov 14, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Date::11/14/2009 Dk Slaa atajwa kugombea urais mwakani [​IMG] Na Mussa Juma, Arusha

  VUGUVUGU la kupata mgombea wa urais mwakani ndani ya Chedema linadaiwa kuanza huku Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa akipendekezwa kuchukua nafasi hiyo.

  Habari zilizolifikia Mwananchi Jumapili zimeeleza kuwa Dk Slaa ametajwa kuwania nafasi hiyo akipambana na kiongozi mmoja wa juu serikalini ambaye ni mwanachama wa Chadema.

  Mchakato wa kutafuta mgombea huyo, umeanza kutokana na uamuzi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuamua kugombea ubunge katika Jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro hivyo kukosa sifa kikatiba kugombea urais.
  Â
  Habari zilizothibitishwa na mmoja wa viongozi wa Chadema ambaye hakutaka kutajwa gazetini, zinaeleza kuwa suala hilo limekuwa likijadiliwa katika vikao vya juu vya chama bila mwafaka.
  Â
  “Ni kweli kuna viongozi wanamtaka Dk Slaa agombee pia kuna kigogo mmoja ameonyesha nia ya kuja Chadema na kugombea na kuna wanasiasa wengine maarufu hawajatoa uamuzi, lakini mapema mwakani nadhani tutakuwa katika hali nzuri ya kujua nani atagombea,”alisema kiongozi huyo.
  Â
  Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa, Chadema imekuwa na wakati mgumu kumtangaza Dk Slaa kuwa atagombea urais mwakani hasa kutokana na hofu ya kupoteza Jimbo la Karatu.

  Pia hofu nyingine inatokana na baadhi ya wana CCM kuanza kuonyesha nia ya kuondoka katika chama hicho kujiunga na Chadema, kutokana na mgogoro unaoendelea kukitafuna chama chao.

  Inaelezwa kuwa kutokana na mgawanyiko mkubwa uliopo ndani ya chama hicho, huenda makada maarufu wakaamua kujitoa na kujiunga na upinzani, hali ambayo inaweza kuwafanya wakapata mgombea urais.

  Akihutubia wananchi wa Karatu wakati wa kufunga kampeni za serikali za mitaa, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Phillemone Ndesamburo aliwataka wananchi wa jimbo hilo kumchagua mtu ambaye ataletwa badala ya Dk Slaa kwa sababu chama kimeamua kumpa majukumu mengine.

  Hata hivyo, kauli hiyo ilipingwa na umati wa watu waliohudhuria mkutano huo, akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Titus Lazaro ambaye amekuwa akitajwa
  kutaka kumrithi Dk Slaa.

  Alisema hadi sasa anaamini hakuna mtu wa kumrithi Dk Slaa Karatu hivyo ni
  bora akaachwa aendelee kuwa mbunge wa jimbo hilo.

  Lazaro ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alisema kuanza kutafuta mrithi wa Dk Slaa sasa kunaweza kulipoteza jimbo hilo ambalo limekuwa likinyemelewa na CCM.

  “Mimi sijafikiria kugombea ubunge kama Dk Slaa akigombea urais kwani najua ugumu wa jimbo hili na mikakati mingi ya CCM kulitaka jimbo la Karatu”alisema Lazaro.

  Hata hivyo,kwa upande wake Dk Slaa aliliambia gazeti hili kuwa bado hajaamua kugombea urais mwakani.

  “Mimi huwa sipendi kuzungumza bila ya kufanya utafiti..ni kweli watu wanasema nigombee ila bado sijaamua na jambo hili linahitaji utafiti kwanza,”alisema Dk Slaa.

  Dk Slaa ambaye katika siku za hivi karibuni, amekuwa mmoja wa viongozi wanaoheshimika na wenye msimamo mkali ndani ya chama hicho na bungeni, alisema muda wa kutangaza kugombea urais haujafika na suala la urais ni zito sio la kusema bila kuwa na mikakati.

  Umaarufu wa Chadema katika miaka ya hivi karibuni, umekuwa ukiongezeka hasa kutokana na kuanzisha Operesheni Sangara nchi nzima ambayo imekifanya chama hicho kupata wafuasi wengi.

  Chadema ilianza kuweka mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 ikimsimamisha kuwania kiti hicho, Freeman Mbowe ambaye pia alisimama mwaka 2005, huku ikiweka rekodi ya chama cha upinzani kutumia helikopta katika mikutano yake ya kampeni.

  Mkakati wa kumsimamisha Dk Slaa ni kutaka kuongeza idadi ya wabunge baada ya kumtumia Mbowe mara mbili.
  Source: Mwananchi Kesho

  Ama kweli PM wewe ni Noma
   
Loading...