Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 2, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Tanzania Daima la leo linatuhabarisha ya kuwa Dr. Slaa anamtuhumu JK ndiye mmilki halali wa DOWANS......................hili likiashiria ya kuwa kumbe kashfa nzima ya ufisadi dhidi ya watanzania ilisukwa na kuiva hapo Ikulu chini ya uangalizi mahiri, madhubuti na makini wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...............................je kweli tutafikika kwa hali hii?.................

  Vile vile Dr Slaa anamtuhumu JK kuwa ni muasisi wa kasfa za IPTL................na ya kuwa hana nia ya dhati ya kuandika katiba mpya ila anatutupia changa la moto..........................................  Slaa: JK anamiliki Dowans

  • Asema hana nia ya kuunda Katiba mpya

  na Mwandishi wetu

  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willbrod Slaa amesema kuwa Rais Jakaya Kikwete ni dikteta.

  Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Dk. Slaa, alisema kitendo cha Rais Kikwete, kutangaza kuwa ameunda tume ya kuanzisha mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya na atateua kiongozi na wajumbe kinaashiria kuendeleza udikteta wa uongozi.

  Alibainisha kinachotakiwa kuanzishwa hivi sasa ni Constitutional Assembly au Baraza la Katiba (Bunge la Katiba) ambalo ndilo litakalokuwa na wajibu wa kuratibu kura za maoni ya wananchi juu ya uundwaji wa Katiba mpya.

  Alisema kitendo cha Rais Kikwete, kutangaza kuunda tume ni kiini macho na kinadhihirisha hana nia ya kutaka kuundwa kwa Katiba mpya.

  "Huyu Rais wetu haonyeshi kama yuko 'serious' katika uundaji wa Katiba mpya, anataka kuweka viraka ili aendelee kututawala kidikteta!" alisema.

  Aliongeza kuwa kwa kawaida Baraza la Katiba ambalo hapa nchini halipo ndilo lenye jukumu hilo na linatakiwa lifanye mchakato huo kwa kuishirikisha serikali, Bunge, wadau na wananchi.

  Alisema hakubaliani na tume ya kuratibu mchakato huo, kwani inaweza kufanya kazi kwa utashi wa aliyewateua na hata Bunge pia linaweza likatumbukia kwenye mtego wa kupitisha kitu kisichokuwa matakwa ya wananchi kwa sababu ya wingi wa wabunge wa chama kimoja.

  Alisema katika nchi zote zilizoandika upya Katiba au kutengeneza zilipitia njia ya 'National Constitutional Congress au Convention' (Constitutional Assembly) ambapo ilikubaliwa kati ya serikali, Bunge, wadau mbalimbali na wananchi katika majukwaa yao.

  "Constitutional Congress ni chombo kitakachoratibu maoni ya wananchi na wadau mbalimbali na siyo mtu aliyeteuliwa na Rais ambaye anafanya kazi kwa ajili ya kumfurahisha jambo ambalo ni kuendelea kuweka viraka" alisema.

  Alisema baada ya chombo hicho kuundwa, maoni ya wadau, wananchi mbalimbali hukusanywa kwa njia itakayokubalika.

  Dk. Slaa alisema kuwa 'Constitutional Congress hukaa tena kupitia maoni yote kipengele kwa kipengele na kukubaliana na siyo Rais Kikwete na tume atakayounda jambo ambalo liliwahi kutokea huko nyuma.

  Alisema inawezekana Rais Kikwete, hafahamu au kwa makusudi amepuuza kilio cha wananchi ndiyo maana ameunda tume inayowajibika kwa maslahi yake.

  Alisema kuwa Katiba siyo mali ya Rais wala ya serikali iliyoko madarakani, bali ni mali ya wananchi.

  Dk. Slaa alisema wananchi wanatakiwa kufahamu kuwa wanahitaji chombo chao ambacho kinaweza kuwekewa utaratibu na Bunge, baada ya kupitishwa na Azimio la Bunge, lakini siyo mtu au watu wa tume wanaochaguliwa na Rais.

  "Tume hiyo haikubaliki kabisa tunachotaka tunajua hakitakubalika kwa maana hakuna serikali duniani itakayounda tume ya kujinyonga yenyewe, mabadiliko makubwa kwa vyovyote, hayakupendwa na serikali iliyoko madarakani" alisema.

  Alisema ana imani kuwa tume hiyo haiwezi kuleta Katiba mpya hivyo kutoa nafasi kwa Rais Kikwete kuendelea kuongoza katika sura ya kidikteta kwa kupitia Katiba ya sasa iliyopitwa na wakati.

  Dk. Slaa alisema kuwa inashangaza katika hili ambapo hata Zanzibar wamepiga hatua kwani waliweza kuruhusu kukusanya maoni ya uundaji wa serikali ya kitaifa na si kuundwa kwa tume.

  Alisema Katiba mpya haiwezi kamwe kupatikana kwa njia ya tume hiyo (Constitutional Review Commission) kwani zilishawahi kutokea tume za aina hiyo na hakuna kilichofanyika.

  Alibainisha kuwa jambo hilo halina tofauti na tume zilizowahi kuundwa na Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi pamoja na ile ya Benjamin Mkapa ambapo matokeo yalikuwa ni kuweka viraka kwenye Katiba tuliyonayo hivi sasa.

  "Uzoefu wa Tume za Mwinyi na Mkapa ni kuwa maoni yalikusanywa kwa upendeleo, hojaji zilipelekwa kwenye matawi ya CCM, halmashauri za wilaya vyombo ambavyo vyote ni vya CCM, hatimaye serikali ikatoa mapendekezo ya vifungu vya kurekebishwa na vingine kuachwa, alisema na kuongeza: "hatua hii inawezekana kwa kuwa tume ni ya Rais, na Rais kama alivyosema mwenyewe ndiye atakayepeleka marebisho kwa vyombo husika (Bunge) ambalo karibu lote ni la CCM bado wana wabunge wengi pamoja na kuwa wapinzani wameongezeka sana" alifafanua.

  Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alisema ameshangazwa na kitendo cha Rais Kikwete kushindwa kufafanua kuhusu suala la kulipwa kwa Kampuni ya Dowans sh bilioni 185 na Shirika la UmemeTanzania (TANESCO).

  Alisema fidia hiyo iliyoamriwa na mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya biashara (ICC) hivi karibuni kuwa TANESCO inapaswa iwalipe Dowans fedha hizo baada ya kuvunja mkataba wa kununua umeme.

  Alisema kimsingi uvunjwaji wa mkataba huo na sakata zima ni uzembe ambao unapaswa uwekwe wazi na watu wachukuliwe hatua lakini Rais Kikwete haonyeshi kushtushwa na jambo hilo.

  Alisema kutokana na majibu ya kiongozi huyo inaonyesha kuwa naye ni sehemu ya kampuni ya Dowans.

  Alisema Rais anaonyesha udikteta kwa kuamua kulibeba shirika la umeme nchini (TANESCO) huku wananchi ambao ni walalahoi wakiendelea kunyongwa na upandaji wa gharama hizo.

  "Hasemi kuwa kitendo cha kulipa kampuni hiyo kimesababishwa na uzembe wao wenyewe kwa kuleta mitambo ya Richmond iliyozaa Dowans huku yeye akiwa sehemu ya kampuni hizo ameamua kuficha uovu wao" alieleza.

  Alisema wataendelea kuhamasisha maandamano pamoja na kupinga gharama kwa kuwa vyama vya upinzani havikusajiliwa kwa Rais bali vimekuwepo kwa mujibu wa sheria ili kuhakikisha vinakataa uozo unaofanywa na serikali.

  Dk. Slaa alisema Rais Kikwete amesahau hali ngumu inayowakumba wananchi imetokana na maamuzi mabovu yaliyoanzishwa na wanasiasa wenzake kwa kukubali kufanya mchakato wa IPTL.

  "Eti Rais Kikwete anasema upandaji wa umeme ni suala la kibiashara na wanasiasa wasilizungumzie kisiasa inawezekana hana uchungu na Watanzania wanaoshindwa kununua umeme kwa ajili ya kuendeleza biashara zao" alisema.

  Alisema vyama vya upinzani vina haki ya kujadili masuala mbalimbali na siyo kama anavyodai kufanya hivyo ni kuendeleza malumbano na ikiwa hataki vyama vifanye hivyo basi hana budi kuvifuta.

  Wakati huo huo Chama cha Wananchi (CUF), kimemtaka Rais Jakaya Kikwete, kutekeleza kwa vitendo ahadi yake aliyoitoa juu ya kupata Katiba mpya itakayokuwa na maslahi ya Watanzania wote.

  Naibu Katibu Mkuu wa CUF, bara, Julius Mtatiro, alisema kuwa kitendo cha Rais Kikwete, kukubali kuundwa kwa Katiba mpya kuendane na vitendo hasa kuiunda upya na sio kuifanyia marekebisho kama ilivyokuwa awali.

  Alisema Tanzania imefanya marekebisho mara 14 lakini bado kumekuwa na malalamiko hali inayoweza kuleta machafuko nchini na kuipa nchi doa.

  Alisema ni kipindi kizuri kwa Rais Kikwete kuiga mfano wa Rais wa Zanzibar wa awamu ya sita Amani Karume kwa kuridhia maridhiano yaliyoleta sura mpya ya Zanzibar.

  Alisema suala la Katiba mpya limekuja wakati muafaka, kabla ya kutokea kwa misukosuko inayoweza kuchafua hali ya utulivu na amani ya nchi hatua itakayofanya kupoteza sifa hasa pindi amalizapo muda wake mwaka 2015.

  Hata hivyo chama hicho kilimtahadharisha Rais Kikwete kuhakikisha anatembea katika kauli zake hasa kwa kuunda tume makini itakayokuwa huru na isiyokuwa na upendeleo au agenda ya kuibeba CCM, hasa kwa kufanya maamuzi ya upande mmoja.

  Aidha katika hotuba yake Rais Kikwete aliahidi kuunda Tume Maalum ya Katiba (Constitutional Review Commission), itakayoratibu mchakato kwa kushirikisha wananchi wote ili waweze kutoa maoni yao juu ya yale wanayotaka yaingizwe katika Katiba mpya.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mbona hii iko vivid kabisa?
  Nimekuwa na mashaka siku zote juu ya ukimya wake juu mambo haya...Kwanini aruhusu mizigo mikubwa kama huu kwa mwananchi wake kama hana maslahi nao?

  Kuhusu katiba, huyu ataenda tu kwa shinikizo...Kilichomfanya atangaze nia hiyo juzi ni shinikizo, na kitakachomfanya atekeleze ni shinikizo pia, hivyo apende asipende atashuhudia mabadiliko ya katiba!
   
 3. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hii ndiyo ile ambayo kamati ya Dr. Mwakyembe alisema mengine hawakuyatoa hadharani kwa sababu za kiusalama ( wa Taifa)!!!! Hivi usalama wa Taifa ni usalama wa Kikwete au wa wananchi? Ni usalama gani wa taifa wakati mkulu mwenyewe ndiye anayetusaliti?
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  JK ndo Champion wa kila kitu, huoni hachukuwi hatua yeyyote ile?
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Tuhuma hizi za Dr. Slaa dhidi ya JK inaziunga mkono kwa asilimia mia.........kwa sababu zifuatazo:-

  a) Uteuzi wa Dr. Idrissa Rashid kuongoza Tanesco ulijaa mizengwe ambayo ushahidi mwingi ulibainisha ya kuwa JK ndiye aliyeshinikiza Dr. Idrissa kuwa kibosile pale......................................Dr. Rashid mwenyewe alikwisha diriki kusema ya kuwa hakuiomba hiyo nafasi ila aliombwa kuliongoza Tanesco katika mazingira yanayothibitisha ya kuwa kuna ukiukwaji mkubwa wa maadili ya kitaifa unaongozwa na JK mwenyewe...................Ilikuwaje Dr. Rashid apewe nafasi hiyo wakati waombaji wengi wa nafasi hiyo maombi yao yalitupwa ili kufanikisha mianya ya ufisadi ambayo JK alikuwa tayari ameiandaa..........................................

  b) Aidha uamuzi wa Dr. Rashid kuizuia mitambo ya DOWANS huku akielewa wao na DOWANS hawana mgogoro wowote ulikuwa mpango kamambe wa kuliingiza taifa hili mkenge na kulifanya liingie hasara kubwa ya mabilioni yanayokadiriwa 185 kwa kuvunja mkataba bila sababu za kimsingi..................Mkataba ambao tayari ulikuwa umekwisha hivyo haukupaswa kuuvunja kwa kuzuia mitambo isiyomilikiwa na Tanesco.......Bilioni hizo 185 zinazidi maradufu hata thamani ya hiyo mitambo hata kama leo ingelinunuliwa kuwa mipya...................

  c) Kwa uongozi makini, DOWANS isingeruhusiwa kurithi mkataba wa RICHMOND kampuni hewa na hivyo kulisababishia taifa maumivu makali ya kuendeleza mkataba ambao tayari ulikuwa una nuksi.......................kuanzia awali...................Kama RICHMOND ni kampuni hewa basi mktaba wake iliyourithisha kwa DOWANS nao ni hewa na hivyo hatukupaswa kuuheshimu ila ni ufisadi tu unamwongoza JK kuhalalisha upuuzi huu unaolishushia taifa heshima humu duniani........


  d) JK alikuwa ni Waziri wa Nishati kwenye serikali ya Mwinyi na hivyo alihusika moja kwa zote katika ujio wa IPTL ambayo bei zake za kuiuzia umeme TANESCO zimechangia kwa kiasi kikubwa katika kulifilisi shirika hilo la umma na kuliingiza taifa gizani........................vile vile wakati wa utawala wa JK hapo Wizara ya Nishati ndipo kazi ya uagizaji wa mitambo ya umeme wa dharura iliposhika kasi kama ile mitambo ya Ubungo ambayo uendeshaji wake na bei zake za kuinunulia zilikuwa ni ufisadi mtupu......................

  e) JK baada ya kuona moto wa Katiba Mpya hawezi kuuzima hasa ukizingatia yeye mwenyewe amepoteza uhalali wa kuliongoza taifa hili baada ya kuchakachua matokeo ya Uraisi kupitia NEC na TISS akaamua kuiteka hoja tajwa na kuibinafsisha kupitia Tume yake mwenyewe atakayoiteua ambayo ni marudio ya michakato ya siku za nyuma ya iliyozaa viraka 15 katika katiba yetu.......na ambayo imeshindwa kukidhi mahitaji ya watanzania wa karne hii ya 21.................haya siyo mageuzi hata kidogo na hayashibishi kiu ya mabadiliko katika katiba yetu................................Katiba Mpya itapimwa kama Bunge litapitisha sheria ya kuainisha mchakato huo shirikishi na ambao una nguvu ya kisheria.....................Siyo Tume ya Raisi ambayo haina nguvu ya kisheria na inaundwa na CCM pekee yake badala ya kuwapa nafasi watanzania wenye sifa kujitokeza na kupimwa na kamati maalumu ya Bunge.............kama wana sifa za kuwa kwenye TUME HURU ya kukusanya na kuainisha matakwa ya watanzania juu ya katiba mpya....................Zipo Tume nyingi za Raisi ambazo matunda yake hakuna anayoyafahamu...........Tume ya Nyalali, WHITE PAPER, Tume ya kukusanya maoni ya muundo wa Afrika ya Mashariki ............n.k..................

  Tatizo ni kuwa zimeundwa na Raisi pekee yake ili kuzima uhaja wa mabadiliko nchini na hazina nguvu ya kisheria na hivyo kujifanyia kazi kwa matashi ya yule aliyeziteua.......................UTANi UTANI HUU TUSIURUHUSU KUJITOKEZA KWENYE mchakato wa kuandika KATIBA MPYA...........
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280
  kama Slaa kasema hili wazi huu ndio uanaume na ndio hawa tunaowataka nchi hii!!! PIGA KICHWA! yes siri ya kuua nyoka ni kupiga kichwa tu! Rostam Rostam .... my foot!!!! let our song be Kikwete, Kikwete, then he will feel right temperature in that hot seat in his forced palace

  At least naanza kupata ahueni. Hongera mzee
   
 7. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,517
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Nadhani anamaanisha by implication hana evidence. It is a political game
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280
  Whatever it is! this is a starting point.. you never know some people might bring evidence, but is a good start.... we shake him , others will fall down!
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Tafuteni jingine, kwa hilo mmenowa!
   
 10. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,988
  Likes Received: 3,737
  Trophy Points: 280
  Huu ndio ujasiri unaotakiwa.
  JK anajua sana influence ya Dr Slaa kwa wa-TZ, so am sure this will put a lot pressure on him and he is subsequently likely to end up making panicky (potentially damaging) statements or actions...

  Am urging Dr Slaa to maintain the pressure, and also go a mile further kwa mbunge wenu mmoja kuwasiliha hoja binafsi bungeni on this.

  Tuko nyuma yenu katika kuirudisha nchi hii mikononi mwa wamiliki wake - wananchi!
   
 11. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Huyo ndiyo Dr. Wilbroad Peter Slaa. Mtaumwa matumbo ya kuharisha hii miaka mi5 mtajuta.

  Ndiyo kwanza anaanza.
   
 12. semango

  semango JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  unavyotamka bila kufikiria utadhani hulipi kodi.kama unalipa kodi then inabidi ujumuike ktk harakati maana kodi yako pia imo ktk mabilioni yanayotafunwa na hao dowans wasiojulikana hata walipo......"Daah jk raia 2mekukosea nini mpaka umefikia huko?"!!!
   
 13. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #13
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280
  yapo mengi kaka, Rich, IPTL, EPA, le EPA rais aliyemtangulia kaisha mkaanga na kusema wazi ni JK anahusika! the guy is monster
   
 14. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Waberooooya!
  Thread ya Invisible jana ilinifanya kulala kwa majonzi ila umenichekesha asubuhi asubuhi eti.... Rostam Rostam...my foot!!!!

  At day end you have a point nyoka hafi kwa kupiga mkia. Tumekuwa nakawaida ya kusema Rais wetu anaangushwa na wasadizi wake au wananchi wana imani na Rais lakini hawana imani na serikali yake n.k
  Iweje yeye awe safi halafu wasaidizi wake wawe monsters??????
  Naunga mkono hoja lets change to Mikataba ya madini-Kikwete; Dowans bin RIchmond-Kikwete, IPTL-Kikwete hata kama hatuna ushahidi mkononi ila tuna ushahidi wa kimazingira moyoni.

  Kama JK hahusiki kwenye hii saga ana njia moja tu ya kusafisha jina HAKUNA KULIPA DOWANS. Inashangaza Pinda anawaita Dowans "genge la watu wanaofahamika," sasa kama ni genge kivipi serikali yenye kumiliki majeshi, mizinga na vifaru inaliogopa????

  Enzi za Mwalimu watu wakileta kibri nga kwa kusema "serikali iko mfukoni mwangu" walishukiwa kwa speed ya mwewe!
   
 15. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Dr. Is all about innocent peoples'
  Asante Dr,Hawa walafi lazima watapike vyote walivyokwapua.
   
 16. m

  mpingomkavu Member

  #16
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wananchi tunasubiri nini kumtoa IKULU, hivi taratibu za kumpechi Rais zinasemaje?
   
 17. tunalazimika

  tunalazimika JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  jingine litapatikana wapi_we are the looser kwa dhamana tuliyoijenga kwa familia yenu, Mungu anajua_mtalipwa hapa hapa dunian
   
 18. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Huyu sio Rais, Ila ni mwizi.
  Is a hooligan, thug and a killer of his own people!! Hajawahi kuwa genuine
   
 19. z

  zamlock JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  safi sana dk slaa tulikuwa tuunaumia sana kukuona uko kimya kikwete lazima awajibike na sijui ni kwa nini ajazungumzia dowans
   
 20. tunalazimika

  tunalazimika JF-Expert Member

  #20
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  nusu ya muda wa hotuba yake anatumia kuelezea mafanikio yatakayopatikana Sudan kutokana na uteuz wa mpaka bila aibu wakat ingawa wenzetu wamekuwa kwenye vita ya muda mrefu lkn kimaendeleo hatuwagus kabisa_tusipoangalia hata Burund wanatupita_eti mtu anashindwa ku_address soln ya challenges zinazolikabili taifa anaelezea uteuz wa uzaz wa mpango_safar yetu ni ndefu
   
Loading...