ISMAIL MKIMBIZI
Senior Member
- Jan 13, 2013
- 192
- 23
Leo ni siku kuu kwa wakazi wa Kasulu, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa, anaanza Ziara yake katika wilaya hii kukagua hali ya kisiasa na kuimarisha demokrasia. Ratiba niliyoipata kutoka Ofisi za Chadema Kasulu inaonesha atakuwa na mikutano miwili leo katika kijiji cha KITANGA na kijiji cha KWAGA.
Kesho atafanya mikutano mingine ya hadhara katika kijiji cha MARUMBA na kisha kumalizia ziara yake Kasulu Mjini kwa kuhutubia wananchi katika viwanja vya shule ya msingi Kiganamo. Habari zinazoendelea katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ni ishu ya Zitto Kabwe na Uamuzi wa Kamati Kuu ya CHADEMA, lakini kwa ziara ya Dr Slaa hilo halina nafasi kwani ni kwa malengo yaliyopangwa toka kitambo hata kabla ya uamuzi huo.
Ninapenda kuona demokrasia ikiimarishwa katika chama CHADEMA wilayani hapa, na Katibu mkuu anayo mamlaka ya kuliwezesha jambo hili. Kwa taarifa ni kwamba kumekuwepo malalamiko na manung'uniko kuwa kuna viongozi wanaodiriki kusema bila wao hakuna CHADEMA Kasulu, na wamejivunia heshima ya woga wa wanakasulu kwa hali ya visenti walivyonavyo.
Wamekuwa wakidiriki kusema wanatumia rasilimali zao, muda wao na fedha zao kukiendesha chama hivyo hawako tayari kuruhusu demokrasia kirahisi rahisi. Mimi ni mwanachama wa kawaida sipati nafasi ya maamuzi katika vikao muhimu, lakini kwa kuwasikiliza wanavyosema viongozi wangu hadharani inaniuma sana. Karibu sana Dr. Slaa, Katibu Mkuu CHADEMA, imarisha demokrasia Kasulu. Amen.