Elections 2010 Dr slaa je nawewe utamchagua jk kuwa waziri katika serikali yako?

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
281
Vikao vya siri vinaonyesha ya kuwa jk amepanga kumchagua slaa kuwa waziri wa nishati na madini iwapo atashinda uchaguzi wake ujao, je na yeye dr slaa akishinda uchaguzi huu ataweza kumchagua jk katika baraza lake ili wafanye kazi pamoja, na nini mitazamo ya wananchi kwa ujumla kuhusu baadhi ya wabunge wa upinzani kuchaguliwa mawaziri?
 
Hii ni swali, utani au ni ombi? Kama haueleweki vile? Tupo ktk vita ya kuikomboa Tanzania ktk mikono ya mafisadi wa CCM halafu linakuja suala la utani. Mpigania Dk Slaa na sote tutafaidika kwa pamoja. Try it and you will appreciate. Umshawishe kila mmoja unayepata nafasi ya kuongea naye mf: mfanyakazi mwenzako, mkeo (kama umeoa), mama, baba, kaka,dada, mdogo wako, mwalimu, mchumba, mpenzi wako na kila mtu awaye yote. Vita vinaendelea. God bless Dk Slaa.
 
Vikao vya siri vinaonyesha ya kuwa jk amepanga kumchagua slaa kuwa waziri wa nishati na madini iwapo atashinda uchaguzi wake ujao, je na yeye dr slaa akishinda uchaguzi huu ataweza kumchagua jk katika baraza lake ili wafanye kazi pamoja, na nini mitazamo ya wananchi kwa ujumla kuhusu baadhi ya wabunge wa upinzani kuchaguliwa mawaziri?

Vikao gani?
Jamani habari nyingine muwe mnaangalia pa kuziweka.
 
Akishinda Slaa, kuna wengi wa kupanda kizimbani. Wote wale wanaonda kutangaza HOFU kwa wananchi.

Watu kama Tumain na Malaria Sugu ni watu wa aina hiyo ambao au baba zao au mabwana zao au ndugu zao/jamaa zao au inaweza kuwa hata wao wenyewe WATAPANDISHWA kizimbani kujibu mashtaka ya kuuza na kuiibia nchi.

Napinga sana watu wanaoandika TUMUOMBE MUNGU.

Kwa sisi Wakristo, biblia imeandika wazi "PIGA HODI, UTAFUNGULIWA." Hii ina maana tusiombe Mungu na kubweteka.
Katika hili, tusipige magoti. Tukimbie huku tukiwa na imani zetu kuwa MUNGU YUPO NA SISI.
Kila mtu na atimize wajibu wake kwa KUMFANYIA kampeni ya nguvu Dr. Slaa.
Ikifika jioni, unapokwenda kulala ndipo unapiga magoti kumuomba Mungu..... AMEN.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.....
 
Tunasema tu maskini kwasababu hatutumii rasilimali zetu, ila tatizo huanzia kutotumia akili kufikiri kama rasilimali ya kwanza kutukomboa. Aliyeweka wazo la utani hapa kuwa vikao vya JK vinafikiria atamteua Slaa kuwa Waziri inaonyesha hatumii akili yake kufikiri ili ajikomboe, uzembe wako wa kutofikiri usiuweke mbele za watu kujidhalilisha.

Kumbuka statement za balzoi wa EU, Tim Clark kuwa anashangaa Tanzanai kuwa maskini kwasababu ina rasilimali ya kulisha Ulaya nzima, inapokea misaada kutoka Ulaya, marekani na Asia lakini haelewi kwanini hatuendelei. Hii ilikuwa tusi kubwa kwetu na wakati wa ukombozi ni sasa.
 
Umetoka kitandani bado una usingizi wewe,
ushauri wa bure
Tanzania ni ya wote na wote wanastahili haki sawa na sio kundi fulani la watu.hali hii itaondolewa na Rais mpya tuu toka chapinzani na ameshapatikana si mwingine ni Mh Dr W.Slaa(JEMBE LA KARATU)
Pole sana amka sasa.
najua ni usingizi ulikuwa unakusumbua tuu bwana mzee.
 
Akishinda Slaa, kuna wengi wa kupanda kizimbani. Wote wale wanaonda kutangaza HOFU kwa wananchi.

Watu kama Tumain na Malaria Sugu ni watu wa aina hiyo ambao au baba zao au mabwana zao au ndugu zao/jamaa zao au inaweza kuwa hata wao wenyewe WATAPANDISHWA kizimbani kujibu mashtaka ya kuuza na kuiibia nchi.

Napinga sana watu wanaoandika TUMUOMBE MUNGU.

Kwa sisi Wakristo, biblia imeandika wazi "PIGA HODI, UTAFUNGULIWA." Hii ina maana tusiombe Mungu na kubweteka.
Katika hili, tusipige magoti. Tukimbie huku tukiwa na imani zetu kuwa MUNGU YUPO NA SISI.
Kila mtu na atimize wajibu wake kwa KUMFANYIA kampeni ya nguvu Dr. Slaa.
Ikifika jioni, unapokwenda kulala ndipo unapiga magoti kumuomba Mungu..... AMEN.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.....

Sikonge ukiacha mambo ya kyela huwa nakukubari sana.
 
mkuu unakua kama malaria sugu na hoja zake za pale kariakoo kwenye vijiwe vya kahawa! sio namsingizia mwenyewe alisema hivyo jamani!
 
Vikao vya siri vinaonyesha ya kuwa jk amepanga kumchagua slaa kuwa waziri wa nishati na madini iwapo atashinda uchaguzi wake ujao, je na yeye dr slaa akishinda uchaguzi huu ataweza kumchagua jk katika baraza lake ili wafanye kazi pamoja, na nini mitazamo ya wananchi kwa ujumla kuhusu baadhi ya wabunge wa upinzani kuchaguliwa mawaziri?

Hakuna muafaka kati ya mafisadi na mpinga ufisadi.Elewa kuwa nuru ni kinyume cha giza
 
Wataibuka na kila hoja; serikali ya umoja wa kitaifa inawezekana; na kitakachotokea ni kuwa

1. Uchaguzi ukifanyika bila haki bado Mgombea na Rais Slaa atashinda; mkwere atatumia jeshi/polisi kupora ushindi; then Slaa atampa Uwaziri mkuu
2. Uchaguzi ukifanyika kwa haki; Dr Slaa ndiye rais wa nchi hii; so Wote inclduing mkuu ni kesi za ufisadi tu kwenda mbele; huwezi kuwapa uwaziri mafisadi
 
Duh!!GODWINE ebu jaribu kutumia basi ata akili kidogo.Najua huna zote ila hata izo kidogo za kuvukia barabara zinatosha.
 
Vikao vya siri vinaonyesha ya kuwa jk amepanga kumchagua slaa kuwa waziri wa nishati na madini iwapo atashinda uchaguzi wake ujao, je na yeye dr slaa akishinda uchaguzi huu ataweza kumchagua jk katika baraza lake ili wafanye kazi pamoja, na nini mitazamo ya wananchi kwa ujumla kuhusu baadhi ya wabunge wa upinzani kuchaguliwa mawaziri?

Hayo yatakuwa maajabu, JK yuko kwenye orodha ya aibu (List of shame) ya mafisadi wa nchi hii ambayo Dr Slaa aliibua pale Mwembe Yanga, hii ina maana JK alitakiwa awe amefikishwa kizimbani kujibu tuhuma za ufisadi, halafu Dr Slaa huyo huyo ampe uwaziri? Fisadi? Hapana Godwine, JK ni fisadi ndiyo maana ameshindwa kuwawajibisha wenzake. Dr Slaa amesema tumpe uraisi aondoe ufisadi,
 
Back
Top Bottom