Dr Slaa jaribu UKWELI na UUNGWANA utakusaidia

KAMARADE

Member
Nov 18, 2009
63
3

Wote tunajua kuwa moja ya sababu kubwa ya watanzania wengi hasa wale wenye upeo wa kiasi fulani kuhusu siasa zetu na historia ya harakati za demokrasia ya vyama vingi hadi sasa kushindwa kuamini katika ukombozi wa CHADEMA ni sura ya chama hicho inayowakilishwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe.

Kwa mtazamoa wa wengi wajuvi wa siasa zetu lakini hata wale wengine wasio na kujua sana, Freeman Mbowe si mwanasiasa bali mjasiria mali ambaye kwake siasa ni mtaji wa biashara zake. Lakini zaidi biashara zake hasa lile danguro la Mbowe na baadae Bilicannas, ni mzigo mkubwa kwa Chadema katika jitihada zake za kujenga imani miongoni mwa watanzania wenye nia ya dhati ya kutaka kuona tunakuwa na MBADALA BORA utakaoweza kuondoa na kutufanya tusahau HISTORIA mbaya ambayo CCM imetupitisha katika miaka ya hivi karibuni.


Hata hivyo moja ya vitu vilivyokuwa vinatupa imani kwa kiasi na CHADEMA ni kuwepo kwa mtu kama Dr Slaa ambaye wengi tulikuwa tunadhani kuwa ni mtu muungwana na muadilifu na pia wa kiasi fulani hasa upande wa vijana ni umahiri wa wabunge wake vijana wakiongozwa na Zitto Kabwe.

Wote hawa walikuwa nguzo muhimu za imani ya watanzania kwa CHADEMA. Nasikitika kusema kuwa tangia uchaguzi uliopita kuanza, nguzo hizi zimeanza ama kuregea ama kubomoka kabisa.

Ukianzia baadhi ya matamshi ya Dr Slaa wakati uchaguzi, Sakata ama kashfa ya hawara ama mke wa mtu, ukaja hoja za kutomtambua rais bila ya kutoa ama kuonyesha ushahidi wa kutosha na sasa haya yanayoaandikwa kuhusu Zitto Kabwe kwa upande mmoja na kauli za Dr Slaa zinazojaribu kukwepa ukweli kuwa msimamo wa Kamati Kuu ya Chadema ni tofauti na ule waliouita msimamo wa chama hapo awali, yote haya yanaelekea kubomoa imani kiasi ambayo watanzania waliweka katika CHADEMA.

Hapa chini ni kile kinahodaiwa kuwa ndio msimamo wa CHADEMA uliotolewa na Dr Slaa kuelezea sakata hili la sasa la Msimamo wa Kamati Kuu Vs Msimamo wao ambao inaonyesha wazi kuwa Dr Slaa anakwepa kukubali kuwa msimamo wa awali ulikuwa tofauti na msimamo wa sasa ambao umetolewa na kamati kuu.



Msimamo wa Chadema haujabadilika

by Dr. Wilbrod Slaa on Tuesday, December 14, 2010 at 7:29pm

Kuna taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na kuripotiwa na vyombo vya habari ambavyo zinaashiria kuwa Chadema tumebadili msimamo wetu kuhusu masuala ya uchaguzi.

Hakuna mahali popote Chadema imebadili msimamo wake na kusema kuwa Kura hazijaibiwa au kuchakachuliwa. Taarifa niliyotoa jana kwa TBC ilieleza wazi kuwa Kamati Kuu, ilipokea na kujadili na kuridhia mapendekezo yote yaliyowasilishwa na Sekretariat ya Chama kuwa Chadema imekataa matokeo ya Uchaguzi kutokana na irregularities 15. Chadema inaamini kuwa iwapo Katiba ya nchi isingelikuwa imezuia kuhoji matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Rais mahakamani, matokeo hayo yangeliweza kubatilishwa. Kwa vile Katiba inakataza kuhoji matokeo kuhojiwa mahakamani, basi japo Kikwete's Presidency ni Lawful it is Illegitimate.

Chadema ilitumia maneno ya kiingereza kuonyesha tofuati kubwa kati ya maneno hayo mawili. Huo ndio msimamo wa Chadema toka mwanzo na haijawahi kuyumba, japo maneno ya kiswahili yamekuwa yakipewa tafsiri tofauti na watu mbalimbali. Ni kwa msingi huo, Kamati Kuu ikasisitiza " Kuundwa kwa Tume Huru" kuchunguza Dosari " Irregularities" hizo kubwa katika uchaguzi. Nasisitiza, Chadema ni Chama ambacho toka mwanzo ilisisitiza kuwa "Haiko Tayari kuingia Ikulu kwa kumwaga Damu ya Watanzania".

Inawezekana wanaopenda na kufurahia vurugu, Chadema haiko tayari kwa hali hiyo. Tunasukumwa sana na wapenzi na wanachame wetu kutoka mitaani na kuandamana, na ndicho pia wanachotaka ndugu zetu akina Mwanakijiji. Maandamano, (ya amani au ya kushinikiza), kwa watu wanaojua mchakato wa demokrasia ni hatua ya mwisho kabisa baada ya njia zingine zote kushindikana. Pili, ili Tanzania isiingie katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 kwa Katiba na Sheria mbovu kama tuliyonayo leo, Chadema inasisitiza upatikanaji wa Katiba mpya, Shirikishi na ya Wananchi.

Upatakanaji wa Katiba hii utakuwa na mchakato, na kama Serikali haitaki, basi Chadema kwa kushirikiana na wadau na watu mbalimbali wakiwemo wananchi itatutumia njia zote zinazoweza kuipatia nchi Katiba ya Wananchi. Yote haya ni mchakato, na kwa mtu yeyote anayoamini kuwa mchakato huchukua muda, basi atakuwa mvumilivu. Hakuna sababu ya kutumia lugha kali, kukashifiana na kutukanana japo jamvi letu ni mahali ambapo "we dare to speak". Tukivumiliana na kuheshimiana tutafika salama bandarini.

Tukikurupuka tunaweza pia tusifikie lengo tunalotaka. Hekima na busara vikitawala na kuongoza matunda yatakuwa mazuri kwa Taifa letu. Taifa ni letu tukilibomoa hatuna pengine pa kwenda, labda tukiamua kulowea penginepo. Tukikurupuka tunaweza kuwaumiza wanaohusika na wasiohusika. Uvumilivu na Busara daima huvuta heri.


Source: Gonga hapa Msimamo wa Chadema haujabadilika | Facebook




Itakuwa vizuri kama tutajikumbusha kauli hizi hapa chini ambazo zilitolewa hapa Jamiiforum kwa kutumia ID ya Dr Slaa...

Ya kwanza ni hii ambayo ilitolewa siku ya pili baada ya wabunge wa CHADEMA kususia hotuba ya JK yaani tarehe 18/12/2010. Hi ilikuwa kama transcription ya taarifa ya Dr Slaa redioni jioni tu ya siku ile ya kumsusia JK.



Ndugu zangu Watanzania, pamoja na ndugu zangu wote waliokuwa wanafuatilia matukio ya bungeni leo. Aaah... ni kweli nimepata watu wengi wakiulizia, aah.. ni kwanini wabunge wa CHADEMA walitoka ndani ya ukumbi wa bunge, wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano alipoanza kutoa hotuba yake. Eeenh... moja ni kwamba CHADEMA ni chama chenye msingi, kinachofuatilia, eenh na kuhakikisha kwamba daima kiko consinstent yaani kinatekeleza kile ambacho kinasimamia, aah kwa kuwa tulikwisha kukataa kutambua matokeo ya uchaguzi, na vilevile baada ya kukataa kutambua matokeo tulikataa vilevile kumtambua rais aliyepatikana kwa mchaka.. eenh kutokana na mchakato huo ambao hatuutambui, basi ni dhahiri kabisa aah matendo yetu yaendane na kile tunachoamini.

Wabunge wetu wapo kwenye forum ambayo inasimamia kile ambacho CHADEMA inakiamini. Bunge ni mahali ambapo wabunge wana nafasi ya kubeba bendera ya CHADEMA, na mahali pa kwanza pa kuonyesha kwamba hatumtambui rais ni dhahiri basi ni kwamba ni ndani ya bunge. Kitendo cha leo kilianzia asubuhi, kwa wabunge wetu kutohudhuria hafla ya kumuapisha Waziri Mkuu, kwa sababu isingekuwa na maana kwenda kuhudhuria hafla ambayo inasimamiwa na rais ambaye kimsingi hatumtambui, lakini vilevile ni ishara kwa watanzania kwamba bado eenh tunataka maelezo ya kina kutoka serikali kuhusu kauli tulizokwishakuzitoa.

Baada ya kususia hafla ya leo asubuhi , hatua ya pili ilikuwa kususia hotuba ya rais, na jambo hilo lilifanyika, na hatua ya tatu ni kususia hafla ambayo inatokea leo usiku, ambayo tulikubaliana pia wabunge wetu wasihudhurie. Hizi ni ishara muhimu katika siasa, kupelekea kuipeleka kwa serikali kwamba kuna malalamiko ya msingi ambayo tunayo kuhusu mchakato wa uchaguzi, na ni dhahiri kwamba kama serikali ni makini, kama serikali ni sikivu basi itasikiliza kauli hiyo ya wenzetu ambao huko bungeni. Lakini kauli hizo hazitaishia pale, kama tulivyokwishakutoa katika press conference yetu, tulisema tutatumia forum ndani ya bunge, na forum inje ya bunge kupiga kelele mpaka serikali itusikilize.

Ni nini tunachokihitaji ? Tunahitaji, aah, demokrasia ya kweli katika nchi yetu, tunahitaji uchaguzi ambao utaendeshwa kwa misingi ya misingi ya demokrasia ya kweli. Tunahitaji tume huru ya uchaguzi. Eenh.. tunahitaji sheria mbovu ziweze kurekebishwa, ili chaguzi zisiendelee kuchakachuliwa kama ilivyotokea safari hii. Kwa hiyo haya ni mambo ya msingi ambayo hakuna mtu yeyote atatuambia tusiyadai, kwa sababu tumelalamika mara nyingi juu ya kat.. ya marekebisho ya katiba, serikali imekuwa si sikivu haitaki kusikiliza, tumedai kuhusu tume huru, serikali imekataa kutusikiliza, tumedai marekebisho ya sheria mbalimbali ambazo ni kandamizi serikali haitusikilizi, tumedai serikali iache kutumia vyombo vya dola hasa polisi na FFU katika uchaguzi serikali haitusikilizi. Kwa hiyo namna pekee ya kudai haki, ukiona mazungumzo ya kistaarabu hayafanyiki basi unapiga kelele. Na hii ni namna mojawapo ya kupiga kelele.Tukumbuke kwamba CHADEMA tumesema hatuhitaji vurugu, hatuhitaji kuwaambia wananchi waende mitaani kwa maandamano - hata kama ni ya amani kwa hatua ya awali - tukitegemea kwamba serikali itatusikiliza, tukae pamoja au ituahidi kwamba itafanya haya marekebisho kabla ya uchaguzi wa 2015. Bila ya kuchukua hatua kama hizi, 2015 tutarejea kwenye mchezo huo huo mchafu, kura zitaendelea kuchakachuliwa, vyombo vya dola vitaendelea kutumika, watanzania wataendelea kunyanyasika, na ukombozi ambao tumewaahidi watanzania hautaweza kupatikana.

Kwa hiyo kimsingi yaliyotokea ni tafsiri ya press conference ambayo tulifanya siku chache zilizopita pale Dodoma, inawezekana Watanzania wengi hawakuelewa ile press conference. Sasa hii ni tafsiri ya ile press conference, na tunawaomba Watanzania watuelewe kwamba tuliposema tutatumia ukumbi wa bunge, na tutatumia eenh.. fora nyingine nje ya bunge, hii ndiyo maana yake. Inje ya bunge tumesusia hafla mbalimbali, ikiwemo hii ya waziri mkuu kuapishwa, kikiwemo ya chakula cha rais, lakini nahafla zingine zitakazoendelea ambapo rais ataendelea kuwa ndiye mwenye hafla hiyo. Eenh, lakini vilevile tumesema kwamba tutakwenda kwa wananchi kuwaeleza sasa ni nini kimetokea.

Kwa hiyo watu wasishangae kwamba tunafanya mikutano yenye sura ya kufafanua zaidi hatua zetu maana yake ni nini, nadhani hii ni kitu ambacho kila mtanzania anaielewa, na kwa simu tulizopokea mpaka sasa hivi, sms ambazo nimekuwa nikizipokea mpaka sasa hivi, watanzania wengi sana wametusifu , wamepongeza wabunge wetu. Ninaomba Watanzania wote wenye nia njema watuunge mkono katika kilio hiki, lakini tukizingatia kwamba yote tunayofanya yawe kwa msingi ya amani, tusitoke mitaani kama tulivyokwishakuwaomba. Watanzania kama wa Shinyanga ambao wamechakachuliwa kura za mbunge wao waziwazi, Watanzania kama wa Mbozi ambao wamechakachuliwa kura zao waziwazi, Watanzania kama Segerea ambao wamechakachuliwa kura zao waziwazi, tunaendelea kusisitiza kwamba, mazungumzo daima ni njia bora ya kuondoa migogoro. Kwa hiyo tusingependa katika hatua hii eeenh yale yaliyotokea yaendelee kutokea.

Ninawaomba amani, ninawaomba utulivu lakini tuendelee kudai haki zetu kwa njia ambazo zinaweza kuzaa matunda.


Ya pili, ni hii iliyotolewa tena katika ID ya Dr Slaa siku iliyofuata yaani tarehe 19/12/2010.



Mkandara,

Thanks. Nadhani message ya Wabunge na ya kwangu iko very clear isipokuwa kwa mtu anayetaka tu kui spin au kuibadilisha kwa sababu anayoitaka mwenyewe. Naomb kurejea mambo ya msingi kwa wale ambao kwa bahati mbaya yamewapita na wana nia ya kuelewa ili spinning hii isiwabughudhi.

Mara baada ya uchaguzi, tarehe 3 November, 2010 Dr. Slaa alifanya Press Conference Makao Makuu ya Chadema kama Mgombea Urais ambaye hakuridhika na mchakato wa uchaguzi na Matokeo yaliyokuwa yakitolewa kupita Vituo vya TV na Jaji Lewis Makame, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Katika Press Conference hiyo Dr. Slaa alitaja dosari nzito katika mchakato wa uchaguzi na hasa katika hatua ya kujumlisha na kutangaza Taifa ambapo matokeo yaliyokuwa yakitangazwa na NEC yalitofautiana kwa kiwango kikubwa sana na yale yaliyotangazwa na Wasimamizi wa Uchaguzi (W) pale ambapo zoezi hilo lilifanyika. Nikatoa Mfano wa Geita.

Pili, nilieleza kuwa Katika majimbo takriban 25 zoezi la majumlisho halikufanyika kama inavyotakiwa na sheria na hivyo matokeo kutangazwa na wasimamizi kwa utaratibu kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi. Tatu, nilieleza kuwa katika maeneo mengine kama Kinondoni masanduku yapatayo 25 ambayo tunayo namba zake tunazo yalipatikana katika ghala la Shule ya Sekondari ya Biafra Jijini Dar-Es-Salaam ambayo hayajahesabiwa na matokeo yamekwisha kutolewa.Nne, Siku ya tarehe 28 October, Tume ya Taifa ya uchaguzi ilialika Wataalam wa IT wa vyama, na kuwa mbele ya Wataalam hao mfumo wa computer uliokuwa unatumika uli "collapse" na Tume kuwajulisha Wataalam kuwa wataita LapTop zote kutoka nchi nzima zirejeshwe Dar kwa matengenezo ya program husika. Ni kuwa wataitwa tena kujulishwa kama zimetengenezwa. Hawakuitwa tena. Hivyo mfumo wa Computer uliotumika kukusanya matokeo na upeleka Taarifa NEC unatia mashaka makubwa.Hata hivyo,baadaye tulipokea Barua kutoka NEC ya tarehe 28/10 ambayo ililetwa kwa Dispatch Makao Makuu Chadema tarehe 5 November, ikisema " Watalaam walikuwa na kukagua mfumo wa IT unaotumika na Tume na waliridhika" .

Ni dhahiri barua hii inatia mashaka kwanini barua ya tarehe 8/10 iletwe kwa dispatch na ifike siku takriban 8 baadaye? Hali hii inatia mashaka kuwa barua hii imekuwa backdated kwa Tume kuficha ukweli wa Scandal kubwa iliyotokea katika mfumo ambao uligharimiwa kwa fedha nyingi na UNDP. Iwapo Tume inaweza kudanganya katika swala kama hili tutatukuwa na imani gani na Tume tena. Kutokana na dosari hizo kubwa (pamoja na mambo hayo yaliyojitokeza baadaye)

Dr. Slaa, kama Mgombea aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifanye mambo yafuatayo:

i) Kusimamisha Zoezi la Kutangaza matokeo hadi uchunguzi kamili utakapokuwa umefanyika ili kuondoa hisia na tofauti zilizoanza kujitokeza. Ikumbukwe kuwa Tofauti hizi kimsingi ziligundulika na Wananchi wenyewe kutokana na Tarakimu alizosoma Jaji Makame kutofautiana na zile zilizotangazwa na Wasimamizi katika maeneo yao. Matokeo yake wananchi waliingia mitaani kupinga hali hiyo. Hayo yalitokea Geita, Shinyanga, Mbozi Mashariki na kadhaa. Matokeo yake wananchi hao waliokuwa wanadai haki zao walipigwa mabomu na polisi. Njia ya Busara ilikuwa kuitaka Tume kusitisha zoezi hili ili lisilete athari zaidi, japo hawakufanya hivyo. Chadema tulifanya jitihada za ziada kuwasihi wananchi wetu wasiingie mitaani kuepusha shari.

ii) Kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufuta uchaguzi na kutangaza upya marudio ya uchaguzi kwa kuwa Tofauti zilizoko ni kubwa sana, na nikatoa mfano wa Tarakimu za Geita CCM 17,792 CDM 3,789 ( Iliyotangazwa na RO Geita CCM 30,960 CDM 22031) Ni wazi kilichotokea hapa ni kuchakachua kwa lengo la kupunguza kabisa kura za Dr. Slaa, japo za JK nazo zimepunguzwa). Jimbo la Hai CCM 35,910 CDM 18,513 (Iliyotangazwa Hai na RO CCM 20,120 CDM 26,724 = Uchakachuaji uliofanyika hapa ni wa kumwongezea JK kwa zaidi ya kura 15,000 na kupunguza za Dr. Slaa kwa zaidi ya 8,000). Nilitoa pia mfano wa Ubungo ambapo kwa mujibu wa CCM 68,727 CDM 65,450(iliyotangazwa na RO CCM 70,472 CDM 72,252 hapa nako uchakachuaji ulioafanyika ni wa kupunguza kura za Dr. Slaa kwa Takriban 8,000 na kupunguza za CCM kwa kama 2000 hivi) Katika Jimbo la Bunda CCM 20,836 CDM 571 ( Iliyotangazwa na RO CCM 20,836 CDM 18,445 = Tarakimu za Bunda zimerekebishwa katika Taariffa ya mwisho ya NEC. Taarifa hii inaonyesha kuwa Dr. Slaa alipewa kura za Lipumba). Jimbo la Karatu ni kichekesho zaidi kwani kwa mujibu wa Taarifa ya awali ya NEC iliyonukuliwa na Mwananchi CCM 24,364 CDM 41 ( iliyotolewa na RO CCM 24,364 CDM 43,137. Taarifa ya mwisho ya NEC imerekebishwa kufanana na ya RO Karatu. Tume ilikiri kuwa imekosea Taarifa ya Geita japo hadi leo haijarekebisha Taarifa hiyo.

Hadi leo hii tarehe 19/11 Tume haijatangaza matokeo ya Geita, Tumbe, Tunduru Kaskazini, na Vunjo kwenye Website yake. (Tume ilikiri siku ya kujumlisha matokeo Taifa kuwa Vunjo kulikuwa na Taarifa mbili na ikaamua kutumia ile ambayo haikusainiwa na mawakala na kutumia ambayo haina saini ya mawakala. Ni akili ya kawaida tu kujua kuwa kuna jambo hapo.
Hivyo basi kutokana na Dosari hiyo kubwa mgombea yeyote anayekubali kupokea matokeo atakuwa mwendawazimu. Ndiyo maana nikakataa kutambua matokeo na kumtambua Rais aliyepatikana kwa matokeo hayo.

2:Tarehe 15 November, katika Press Conference iliyofanyika Dodoma, Dr. Slaa, alikabidhi rasmi majukumu kwa Chama kwa kuwa kazi ya Mgombea Urais imefikia mwisho wake Baada ya Rais kutangazwa kwa mujibu wa Katiba (Mbovu) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa chombo ambacho kilikasimiwa madaraka na Kamati Kuu ya Chama ( Sekretariat) mbele ya Wabunge wa Chama. Chama kilipokea majukumu na kuelekeza utekelezaji na ufuatiliaji maazimio hayo ya kukataa matokeo na kumkataa Rais kufanyika kuanzia siku hiyo na Vyombo mbalimbali na ngazi mbalimbali za Chama, na Wabunge wa Chama. Hivyo kilichotokea Bungeni ni utekelezaji wa maamuzi ya Chama hadi pale ngazi za juu za Chama zitakapobariki au kubadilisha msimamo huo. Ni dhahiri basi,

i) Wabunge wetu wala Dr. Slaa, hawakuhitaji kurudia madia ya msingi ikiwa ni pamoja na kurudia uchaguzi. Madai ya Mabadiliko ya Katiba au Katiba ya Wananchi na kudai Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kujiuzulu na Kuundwa kwa Tume ya uchunguzi ni madai yaliyotolewa katika Press Conference ya Tarehe 15/11. Hata hivyo, msisitizo wa awali ni kwa kuundwa kwa Tume ya Uchunguzi ambayo inaweza kutupelekea kwenye yote hayo. Mtu yeyote asiyemakini kufuatilia mtiririko huo anaweza kupotosha na kusababisha vurugu na uchochezi ambao Chadema, pamoja na jitihada zake za kudai haki zake na za wananchi waliochakachuliwa kura zao inapenda kufuata njia za kistaarabu na za amani. Ni vema yeyote anayetaka kufanya analysis ya hatua za Chadema kwanza akajielimisha vizuri badala ya kuweka hisia zake (hakuna sababu ya kuandika na mate wakati wino upo, na wakati wowote Chadema tuko tayari kutoa ufafanuzi utakao hitajika, isipokuwa ule unaopaswa kupitia kwenye vyombo vyetu vya maamuzi kama chama cha kidemokrasia.


Jamani. Uungwana nao waweza kuwa mtaji mkubwa kisiasa. Jaribuni hili la kukubalia kuwa tulikosea na sasa tupo tayari kujisahihisha. Hapa sio Kabwe tu atakayekuwa mshindi, Chadema na haswa Dr Slaa atarudisha na kulinda heshima yake lakini sio huu mchezo unaofanyika sasa ambao ni tofauti na fikira zetu kuhusu Dr Slaa.
 
mkuu be panoramic you have no justifications or what soever...... and if i will say and prove that your wife is a traitor..... would you write all this blatant propaganda
 
I can read your minds..... they can, at least based on these statements you have written be hardly trusted.
 
Mkuu, waingereza husema 'You are trying too hard' Kwa kuweka post ndefu haina maana ndo ushawishi. Naomba utumie logical flow na kuquote sehemu za tamko unazotaka kutumia kama uthbitisho wa hoja yako.
Vinginevyo machoni kwangu, nasoma tamko na sioni mabadiliko ktk msimamo, tofauti ni msamiati tu.
Ni hayo tu!
 
Thanks for this long post, I wish we could also track statements tata za wakuu wetu ambazo in one way or another zimetugharimu...for Dr Slaa,I never expected an angel out of him, even Obama was haunted by his various speeches he made some contradicting and all, the main point was none was at the expense za wapiga kura, so Dr Slaa pls come in and contribute to the thread..btw I still support him until when he loses my vote of confidence...
 
Watu wanavunjwa mbavu huko Arusha we unakuja na posti za kijinga kutaka kumsafisha mtu hujaona wajasirimali duniani wakawa wnasiasa mbona husemi Lowasa ,makamba JK,Rostam,Mramba Yona Chenge Abooud,Diallo ,Ridhiwani,salma,Bashe,beno na wengi wengi tu wote hao huwaoni ila Mbowe katufute glasi ya mvinyo ulale usingizi mnono usitusumbue hapa
 
kamarade,

Thank you for such a long and difficult post to follow!!!

Binafsi sioni chochote kibaya au unafiki au kigeugeu cha dr. slaa... ninachoona ni ukweli na mambo yanavyoendelea with time. this is the person i still admire kwani kila usomacho hapo ni mwendelezo wa tukio fulani

sitegemei slaa awe mpumbavu na chadema wawe wapumbavu wa kungangania kila walichosema tar 2 november; hayo yatakua si maisha na kwa ujumla jamii itakua jiwe

ningependa kulinganisha ukomavu huu wa slaa na chadema na ule wa rais kikwete wa kusema kigoma itakua dubai, kuahidi uwanja wa ndege shinyanga na bila kuwa realistic na time bound kwenye ahadi na objectives zake za kusadikika

given a chance, i would say JAKAYA, JARIBU UKWELI NA UUNGWANA, UTAKUASIDIA"
 
Watu wanavunjwa mbavu huko Arusha we unakuja na posti za kijinga kutaka kumsafisha mtu hujaona wajasirimali duniani wakawa wnasiasa mbona husemi Lowasa ,makamba JK,Rostam,Mramba Yona Chenge Abooud,Diallo ,Ridhiwani,salma,Bashe,beno na wengi wengi tu wote hao huwaoni ila Mbowe katufute glasi ya mvinyo ulale usingizi mnono usitusumbue hapa

ahsante sana..... Silvio bellusconi... Hariri`s of Lebanon... the kings of jordan..Tokyo Sikwelle of South Africa......
 

Ukianzia baadhi ya matamshi ya Dr Slaa wakati uchaguzi, Sakata ama kashfa ya hawara ama mke wa mtu, ukaja hoja za kutomtambua rais bila ya kutoa ama kuonyesha ushahidi wa kutosha na sasa haya yanayoaandikwa kuhusu Zitto Kabwe kwa upande mmoja na kauli za Dr Slaa zinazojaribu kukwepa ukweli kuwa msimamo wa Kamati Kuu ya Chadema ni tofauti na ule waliouita msimamo wa chama hapo awali, yote haya yanaelekea kubomoa imani kiasi ambayo watanzania waliweka katika CHADEMA.

Hapa chini ni kile kinahodaiwa kuwa ndio msimamo wa CHADEMA uliotolewa na Dr Slaa kuelezea sakata hili la sasa la Msimamo wa Kamati Kuu Vs Msimamo wao ambao inaonyesha wazi kuwa Dr Slaa anakwepa kukubali kuwa msimamo wa awali ulikuwa tofauti na msimamo wa sasa ambao umetolewa na kamati kuu.

Hakuna mahali popote Chadema imebadili msimamo wake na kusema kuwa Kura hazijaibiwa au kuchakachuliwa. Taarifa niliyotoa jana kwa TBC ilieleza wazi kuwa Kamati Kuu, ilipokea na kujadili na kuridhia mapendekezo yote yaliyowasilishwa na Sekretariat ya Chama kuwa Chadema imekataa matokeo ya Uchaguzi kutokana na irregularities 15. Chadema inaamini kuwa iwapo Katiba ya nchi isingelikuwa imezuia kuhoji matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Rais mahakamani, matokeo hayo yangeliweza kubatilishwa. Kwa vile Katiba inakataza kuhoji matokeo kuhojiwa mahakamani, basi japo Kikwete's Presidency ni Lawful it is Illegitimate.

Chadema ilitumia maneno ya kiingereza kuonyesha tofuati kubwa kati ya maneno hayo mawili. Huo ndio msimamo wa Chadema toka mwanzo na haijawahi kuyumba, japo maneno ya kiswahili yamekuwa yakipewa tafsiri tofauti na watu mbalimbali. Ni kwa msingi huo, Kamati Kuu ikasisitiza " Kuundwa kwa Tume Huru" kuchunguza Dosari " Irregularities" hizo kubwa katika uchaguzi. Nasisitiza, Chadema ni Chama ambacho toka mwanzo ilisisitiza kuwa "Haiko Tayari kuingia Ikulu kwa kumwaga Damu ya Watanzania".





Itakuwa vizuri kama tutajikumbusha kauli hizi hapa chini ambazo zilitolewa hapa Jamiiforum kwa kutumia ID ya Dr Slaa...

Ya kwanza ni hii ambayo ilitolewa siku ya pili baada ya wabunge wa CHADEMA kususia hotuba ya JK yaani tarehe 18/12/2010. Hi ilikuwa kama transcription ya taarifa ya Dr Slaa redioni jioni tu ya siku ile ya kumsusia JK.



Eeenh... moja ni kwamba CHADEMA ni chama chenye msingi, kinachofuatilia, eenh na kuhakikisha kwamba daima kiko consinstent yaani kinatekeleza kile ambacho kinasimamia, aah kwa kuwa tulikwisha kukataa kutambua matokeo ya uchaguzi, na vilevile baada ya kukataa kutambua matokeo tulikataa vilevile kumtambua rais aliyepatikana kwa mchaka.. eenh kutokana na mchakato huo ambao hatuutambui, basi ni dhahiri kabisa aah matendo yetu yaendane na kile tunachoamini.
Kitendo cha leo kilianzia asubuhi, kwa wabunge wetu kutohudhuria hafla ya kumuapisha Waziri Mkuu, kwa sababu isingekuwa na maana kwenda kuhudhuria hafla ambayo inasimamiwa na rais ambaye kimsingi hatumtambui, lakini vilevile ni ishara kwa watanzania kwamba bado eenh tunataka maelezo ya kina kutoka serikali kuhusu kauli tulizokwishakuzitoa


Ya pili, ni hii iliyotolewa tena katika ID ya Dr Slaa siku iliyofuata yaani tarehe 19/12/2010.


Chama kilipokea majukumu na kuelekeza utekelezaji na ufuatiliaji maazimio hayo ya kukataa matokeo na kumkataa Rais kufanyika kuanzia siku hiyo na Vyombo mbalimbali na ngazi mbalimbali za Chama, na Wabunge wa Chama. Hivyo kilichotokea Bungeni ni utekelezaji wa maamuzi ya Chama hadi pale ngazi za juu za Chama zitakapobariki au kubadilisha msimamo huo


Jamani. Uungwana nao waweza kuwa mtaji mkubwa kisiasa. Jaribuni hili la kukubalia kuwa tulikosea na sasa tupo tayari kujisahihisha. Hapa sio Kabwe tu atakayekuwa mshindi, Chadema na haswa Dr Slaa atarudisha na kulinda heshima yake lakini sio huu mchezo unaofanyika sasa ambao ni tofauti na fikira zetu kuhusu Dr Slaa.

Usishangae huyo ndiye kiongozi makini kwa defn ya mashabiki mabubusa wa chadema
 
MKUU KAMARADE NI BORA KWANZA WEWE UANZE KUJARIBU KUWA MKWELI NA MUNGWANA KABLA YA KUATTACK WATU WENYE CREDIBILITY ZAO BILA KUWA TAFITI SAHIHI. SASA KABLA SIJAONGOLEA CHADEMA, MBOWE, SLAA NA ZITO NAOMBA NIKUPE USHAURI HUU.

1. NI VEMA KUFANYA UTUMWA WAKO VIZURI BAADA YA KUWASAFISHA KWANZA WALIOKUTUMA-UKIZUNGUMZIA UCHAFU HAKUNA WACHAFU KAMA SISIEM UKIANZIA NA WAKUU WAKE AMBAO WANAVIMADA KILA KONA YA NCHI NA NJE YA NCHI, HAPO HATUONGELEI KASHFA ZA BABU SEYA, LIYUMBA NA WENGINE WENGI WANAOTAFUNA MALI ZA NCHI KWA SABABU TUU NI VIBURUDISHO VYA WALIOKUTUMA.

2. NI VEMA KUFANYA UTUMWA WAKO KWA KUNAGALIA KWANZA JE KUNA MABEPARI WANGAPI NDANI YA SISIEM? ANZA NA LOWASA, MKWERE NA MAFISADI WOTE AMBAO WAMEPATA MALI ZAO KWA KUWANYONYA WATANZANIA-LAKINI BADO NI WANASISIASA NA WANAONGOZA NCHI -HIVI KUNA MTU MCHAFU NA MNYONYAJI WA MALI YA NCHI HII KAMA ROSTA? HEBU ANGALIA ILE CC YA SISIEM UTUAMBIE NANI SIYO BEBERU? UKIANZIA KINANNNNNNN SEMBSE MBOWE AMBAYE NI KWELI NI MJASILIAMALI HALALI BILA KUHUJUMU UCHUMI???

3. CHADEMA NI TAASISI NA NI MWIBA KWA MASULTANI NA WATAWALA MADIKITETA ITAENDELEZA MOTTO WAKE. KWA SASA CHADEMA INAONGOZWA NA KAMATI KUU CHINI YA KIONGOZI FREEMAN MBOWE KAMA MWENYEKITI NA SLAA(PhD) KATIBU MKUU. HAWA NI VIONGOZI PIA BINADAMU WANAKASORO ZAO NI KWA KUELEWA HILO KAMATI KUU IPO, KATIBA YA CHAMA IPO NA KANUNI MBALIMBALI-HOJA ZAKO KWA INDIVIDUAL IS BASELESS KAJIPANGE UPYA.

3. UKITAFUTA MKWELI NA MUNGWANA NCHI HII KWA WAKATI HUU HUTASITA KUMPATA SLAA(PhD) AKIONGOZA -AMEEPUSHA VURUGU KWA KUCHAKACHULIWA NA KUAMUA KUTUMIA NJIA SAHIHI -JE KUNA MUNGWNA ZAIDI YA HUYO??? MTAJE WEWE-NI MKWELI ALISEMA KUNA WIZI BOT -EPA IKATHIBITIKA, ALISEMA KUNA WIZI TANESCO=RICHMOND -IKATHIBITIKA, ALIWATAJA WEZI 11 MAPAPA WA WIZI WA MALI YA UMMA-HAKUNA ALIYEENDA MAHAKAMANI PAMOJA NA MWENYEKITI WA CCM, NA VIGOGO AMBAO WENGINE WAPO MAHAKAMNI, JE KUNA MKWELI ZAIDI YA HUYO??? MTAJE WEWE WALIMFUNGULIA KESI YA MKE WA MTU MPAKA LEO YUKO NAYE NA WAMENYWEA -HIVI UNATAKA MKWELI GANI????? ACHA UNAFIKI

4. CHADEMA NI TAASISI NA SIYO YA MTU MMOJA -HAKUNA AMBAYE YUKO JUU YA SHERIA-ZITTO AMEKIKOSEA CHAMA NA WABUNGE WENZIE AMEKIUKA KANUNI ZA CHAMA KIONGOZI -AMESHUGULIKIWA KIKANUNI KWANINI TUTAFUTE MCHAWI??? KILA MTU ANAJUA KOSA LAKE NA HATA YEYE MWENYEWE ANAJUA -BORA UKAJIPANGE UPYA KAMARADE USIVAMIE HOVYOHOVYO UTAUMBUKA MAANA YAKE TUTASEMA KILE TUNACHOJUA KWA UKWELI BILA MSUKUMO WA FIKRA CHANYA SIYO HASI KAMA WAKO.

PAMOJA TUTAIKOMBOA NCHI HII KUTOKA KWA WAKOLONI WEUSI NA KUANZA UPYA.

SASA NIKUJIBU HOJA ZAKO;
1. SLAA (PhD) NA CHADEMA HAWAWAHI KUBADILI MSIMAMO WEWE NDIO UNAUBADILI -UWE GREAT THINKER, WANASEMA KURA ZILICHAKACHULIWA NA ILI KUTHIBITISHA HAYO SLAA AMETAJA WAHUSIKA MBONA HAWAJAMPLELEKA MAHAKAMNI KAMA ANASEMA UONGO -MANAKE ATAKUWA ANAVUNJA KATIBA, SLAA KAWAAMBIA NA AKAWAOMBA WAENDE MAHAKAMANI-CHADEMA INAAMNI NA INAUSHAHIDI KURA ZILICHACHACHULIWA NA KWA KUWA KATIBA IMEZUIA KUHOJA NJIA NYINGINE ILIKUWA NI KUFANYA KILE -
 
Hujaweza kuoainisha katika quotetion ulizonukuu tofauti za misimamo ya wabunge na cc ya chadema.
Halafu kwa jinsi ulivyoanza na maelezo yalio ni mawazo yako inadhihirisha wewe kama sio kilaza wa ccm ni mwathirika wa kundi la kale la kina Kafulila ama mlamba viatu vya mh Zitto.
Sioni haja ya great thinkers kujisumbua kufanyia kazi propaganda zilizo siasa za maji taka ulizotumbukiza hapa wakati huu wa amani (uchaguzi umekwisha mamisuli ya nini)?
.
 
MKUU KAMARADE NI BORA KWANZA WEWE UANZE KUJARIBU KUWA MKWELI NA MUNGWANA KABLA YA KUATTACK WATU WENYE CREDIBILITY ZAO PASIPOKUWA NA TAFITI SAHIHI.

SASA KABLA SIJAONGELEA CHADEMA, MBOWE, SLAA NA ZITO NAOMBA NIKUPE USHAURI HUU.

1. NI VEMA KABLA YA KUFANYA UTUMWA WAKO VIZURI-HAKIKISHA KUWASAFISHA KWANZA WALIOKUTUMA-UKIZUNGUMZIA UCHAFU HAKUNA WACHAFU KAMA SISIEM UKIANZIA NA WAKUU WAKE AMBAO WANAVIMADA KILA KONA YA NCHI NA NJE YA NCHI, HAPO HATUJAONGELEA KASHFA ZA BABU SEYA, LIYUMBA,VIKY NA WENGINE WENGI WANAOTAFUNA MALI ZA NCHI KWA SABABU TUU NI VIBURUDISHO VYA WALIOKUTUMA.

2. NI VEMA KABLA YA KUFANYA UTUMWA WAKO -KWANZA KUANGALIA JE KUNA MABEPARI WANGAPI WAPO NDANI YA SISIEM? ANZA NA LOWASA, MKWERE NA MAFISADI WOTE AMBAO WAMEPATA MALI ZAO KWA KUWANYONYA WATANZANIA-LAKINI BADO NI WANASISIASA NA WANAONGOZA NCHI -HIVI KUNA MTU MCHAFU NA MNYONYAJI WA MALI YA NCHI HII KAMA ROSTA? HEBU ANGALIA ILE CC YA SISIEM UTUAMBIE NANI SIYO BEBERU? UKIANZIA KINANNNNNNN NA ZANTEL,

3. CHADEMA NI TAASISI NA NI MWIBA KWA MASULTANI NA WATAWALA MADIKITETA ITAENDELEZA MOTTO WAKE. KWA SASA CHADEMA INAONGOZWA NA KAMATI KUU CHINI YA KIONGOZI FREEMAN MBOWE KAMA MWENYEKITI NA SLAA(PhD) KATIBU MKUU. HAWA NI VIONGOZI PIA BINADAMU WANAKASORO ZAO NI KWA KUELEWA HILO KAMATI KUU IPO, KATIBA YA CHAMA IPO NA KANUNI MBALIMBALI-HOJA ZAKO KWA INDIVIDUAL IS BASELESS KAJIPANGE UPYA.

3. UKITAFUTA MKWELI NA MUNGWANA NCHI HII KWA WAKATI HUU HUTASITA KUMPATA SLAA(PhD) AKIONGOZA -AMEEPUSHA VURUGU BAADA YA KUCHAKACHULIWA KWA MAPINDUZI YA NEC NA KUAMUA KUTUMIA NJIA SAHIHI -JE KUNA MUNGWNA ZAIDI YA HUYO??? MTAJE WEWE- DR SLAA NI MKWELI ALISEMA KUNA WIZI BOT -EPA IKATHIBITIKA, ALISEMA KUNA WIZI TANESCO=RICHMOND -IKATHIBITIKA, ALIWATAJA WEZI 11 MAPAPA WA WIZI WA MALI YA UMMA-HAKUNA ALIYEENDA MAHAKAMANI PAMOJA NA MWENYEKITI WA CCM, NA VIGOGO AMBAO WENGINE WAPO MAHAKAMNI, JE KUNA MKWELI ZAIDI YA HUYO??? MTAJE WEWE WALIMFUNGULIA KESI YA MKE WA MTU MPAKA LEO YUKO NAYE NA WAMENYWEA -HIVI UNATAKA MKWELI GANI????? ACHA UNAFIKI

4. CHADEMA NI TAASISI NA SIYO YA MTU MMOJA -HAKUNA AMBAYE YUKO JUU YA SHERIA-ZITTO AMEKIKOSEA CHAMA NA WABUNGE WENZIE AMEKIUKA KANUNI ZA CHAMA KIONGOZI -AMESHUGULIKIWA KIKANUNI KWANINI TUTAFUTE MCHAWI??? KILA MTU ANAJUA KOSA LAKE NA HATA YEYE MWENYEWE ANAJUA -BORA UKAJIPANGE UPYA KAMARADE USIVAMIE HOVYOHOVYO UTAUMBUKA MAANA YAKE TUTASEMA KILE TUNACHOJUA KWA UKWELI KWA MSUKUMO WA FIKRA CHANYA SIYO HASI KAMA WAKO.

PAMOJA TUTAIKOMBOA NCHI HII KUTOKA KWA WAKOLONI WEUSI NA KUANZA UPYA.

SASA NIKUJIBU HOJA ZAKO;
1. SLAA (PhD) NA CHADEMA HAWAWAHI KUBADILI MSIMAMO WEWE NDIO UNAUBADILI -UWE GREAT THINKER, WANASEMA KURA ZILICHAKACHULIWA NA ILI KUTHIBITISHA HAYO SLAA AMETAJA WAHUSIKA MBONA HAWAJAMPLELEKA MAHAKAMNI KAMA ANASEMA UONGO -MANAKE ATAKUWA ANAVUNJA KATIBA, SLAA KAWAAMBIA NA AKAWAOMBA WAENDE MAHAKAMANI-CHADEMA INAAMNI NA INAUSHAHIDI KURA ZILICHACHACHULIWA NA KWA KUWA KATIBA IMEZUIA KUHOJA NJIA NYINGINE ILIKUWA NI KUFANYA KILE -
 
non-sense...

1. Hivi ukitaka kuwa mjasiriamali kwenye nchi hii utachagua nini kati ya CCM na CHADEMA??
2. Kama Mbowe hafai je kukaa pembeni ili Slaa agombee uraisi na CHADEMA wapate wabunge wengi... weka ukinzani hapo??? Angalia CUF wanatoka kura 1.3mil kwenda laki 6... Who is the best hapa katika vyama vyoote nchini???
3. Unasema SLaa ni geugeu.. Hivi kwwa akili yako unajua maana ya msimamo?? Huko si kubadili msimamo bali ni mtego kwa CCM na sasa wanaweweseka na katiba mpya na tume Huru... Huoni kama ni CHADEMA yooote hayo...
4. Unasema Mbowe ana Bilicanas hivi unajua JK ana hoteli nchi ipi?? Mkapa jee? Lowassa Je?? Ridhiwani je?? Karamagi je?? Makamba je?? Rubantizigwa je??? Chenge je?? Sitta je?? wengine je?? Hvi unajua Anna Makinda alikopa sh ngapi benki na kazipeleka wapi??
Hivi unajua pale serengeti kuna Hoteli ya mkuu imejengwa sehemu isiyoruhusiwa kabisa?? Hivi unafikiri TICTS wanapodai hawataki mpinzani kwenye biashar.. Jeuri wnaapata wapi?? Hivi unawajua wamiliki wa VODACOM tz???

5. Mimi ngoja nikae pembeni tukuchekeeee weee mpaka tuchoke... Hivi unajua adhabu yakusaliti CCM kawauulize wenzako....

hahhahahhahahhahhhhhhhhhhhhhhhhaaaaaa mwehu mwehu ni mwehu tuu labda angeumbwa miguu mitatu tumjue huku mitaaani
 
Kamarade, umeeleza vizuri na kinaga ubaga. Anaejifanya hajakuelewa huyo hataki tu kukuelewa.

Uliyoandika ni ukweli mtupu na anaepinga ni kwa jazba tu na kwa kuwa hataki kuamini kuwa at the end ukweli ndio siku zote una prevail.
 
Siwezi kukubali mpuuzi akimshauri mweledi. Unamwambia ajaribu ujinga unaosema kwako ni Uungwana wakati wewe unatumia maneno ya matusi kwa wakuu. Kumbuka ho ndo viongozi wako wa gov.2015. Acha matusi waheshimu wakubwa!
 
Hata Dikteta Hitler alikuwa ni kiongozi,pia Iddi Amin.Kwa hilo hata JK ni kiongozi
 
Back
Top Bottom