Elections 2010 Dr. Slaa in Mbeya (picha)

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Sorry mods, naona wengi wanaziulizia picha hizi lakini nimeona niwaletee kipekee bila kuingiza kwenye ile ya nyanda za juu kusini, mnaweza kufanya hivyo baadae baada ya wadau kuziona na kutoa maoni yao kwa hali hii ya Mbeya.

Mabango_slaa_mbeya.jpg

Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Mbalizi mkoani Mbeya, wakiwa na mabango yenye ujumbe mabli mbali, wakati wa mkutano wa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa. (Picha na Joseph Senga)

slaa_akihutubia_mbalizi.jpg

Mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mbalizi mkoani Mbeya, kwenye Uwanja wa Stendi ya Mabasi. (Picha na Joseph Senga)

sugu_mbeya.jpg

Mgombea ubunge katika jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Mbilinyi "Mr Sugu", akiwatumbuiza wananchi wa mji wa Mbalizi, wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi ya Mabasi. (Picha na Joseph Senga)
 
Nasikia kufarijika. Luteni Jenerali A. Shimbo, ujumbe unaupata ? Daily News, ujumbe unawafikia ? CCM, Watanzania wamewachoka ! Kikwete, wewe pamoja na familia yako anzeni kufungasha mrudi Bagamoyo msubiri kuwajibishwa kwa kushirikiana na mafisadi kuliibia taifa.
 
polisi_slaa_mbeya.jpg


Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiwa katika ulinzi wakati wa mkutano wa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi ya Mabasi mjini Mbalizi mkoani Mbeya. (Picha na Joseph Senga)
 
Omar Ilyasi akiona hivi anatamani kujinyonga ... waberoya ndiye kabisaaaa kaaamua kuanza mbele ya safari
 
Omar Ilyasi akiona hivi anatamani kujinyonga ... waberoya ndiye kabisaaaa kaaamua kuanza mbele ya safari

Hivi mbona mimi niki attach file kinatokea kipicha kidogo sana, kuna pics nyingi nimetumiwa na Watu wa Mbeya lakini nashindwa kuziweka hapa katika mapana yake
 
slaa_akihutubia_mbalizi.jpg

Mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mbalizi mkoani Mbeya, kwenye Uwanja wa Stendi ya Mabasi. (Picha na Joseph Senga)

Duh hawa ni binaadamu au nzi?
 
Bye bye CCM, new era to Tanzania and to Tanzanian. New hope is just arrived.
Thanks GOD
 
Hivi mbona mimi niki attach file kinatokea kipicha kidogo sana, kuna pics nyingi nimetumiwa na Watu wa Mbeya lakini nashindwa kuziweka hapa katika mapana yake
Mkuu, wewe wasiliana na mods watakusaidia kwa haraka. Tuma kwenda support@jamiiforums.com watakuelekeza kirahisi hawa jamaa. Nashindwa kukuelekeza mimi
 
mi natamani kupiga ukunga nilieeeeeee.aaaaah hivi ni kweli haya mambo au?eeeh baba yetu uliye mbinguni wewe ni muweza wa yote ulikuwa wapi kumleta mkombozi huyu wa kweli???? napiga kura yangu kwa kishindo kwa maana nakuwa miongoni mwa watanzania tunaoandika historia ya kuigaragaza CCM...
 
thanks mugumu, asante sana na sana, leo nimefarijika sana , na huu umati wa mbeya, yaani ni balaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Nimependa bango, Khanga, Tshirt, Kofia na POMBE si mahitaji ya watanzania! Hahahahahahaahha Kiwete lazima aanguke
 
Nashukuru picha hizi zinazidi kutupa matumaini ila kazi ni kuhamasishana, kupiga na kulinda kura. Ninasema Vyama vya Ushindani lazima kudai haki ya kulinda kura vituoni. Hivyo watu wakiisha kupiga kura wasogee nyuma kidogo na kukifanya kituo kiwe eneo la tukio na hivyo kulilinda mpaka kura zimetangazwa na kubandikwa rasmi.

CCM zamani walikuwa wakiiamini kwa matendo kauli ya Joseph Stalin kuwa mtu wa maana katika uchaguzi si mpiga kura bali mhesabu kura. Hivi sasa wamekwenda mbali zaidi na kuungana na Kibaki kuwa mtu wa maana katika uchaguzi ni mtangaza matokeo hivyo ni lazima kuhakikisha njama chafu za CCM, Shimbo na wenzake wote zinashindwa kwa nguvu ya watu.
 
Huuuuu! Mungu awabariki watu wa Mbeya! mikoa yote waige kutoka mbeya, mwaka huu mabadiliko ni lazima!
 
Majjid anasemaje kuhusu umati huu?

Kweli bwana, tunataka Maggid atoe tathimini yake tena, maana alisema Slaa hakubaliki mikoa ya kusini. Atwambie wakati wa Kikwete kulikuwa na umati huo? Na ukizingatia hawa hawakuletwa na magari. Kazi ipo kwa CCM mwaka huu.
 
Mkusanyiko huo unaweza kuvunja rekodi iliyowekwa na wanaIringa na Moshi. Inapendeza sana kwa kweli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom