Nyakageni
JF-Expert Member
- Feb 1, 2011
- 15,045
- 5,104
Mwaka 2015 Dr. Slaa alifanya kazi kubwa sana ya kuibomoa UKAWA na kutuaminisha kuwa '' mwenye heri '' ni bora kuliko '' shetani'' aliyemkaribisha nyumbani na baadaye kumkimbia kwa kigezo kuwa '' kinyesi kimepakuliwa na kuhamishiwa sebuleni ''
Muda ni jibu zuri sana na nashukuru Mungu kuwa tunaona kuwa shetani yule hata mahakama ya mafisadi hajapelekwa na mahakama aliyoisifu kuwa ingemuweka hatiani shetani yule mwenye Nywele nyeupe na roho ya unyenyekevu.
Na kwa sasa Lowassa (shetani kwa tafsiri ya Slaa) anazidi kutakasika siku baada ya siku. Mungu atusaidie tuishi miaka mingi. Na upande wa pili wa shilingi '' mwenye heri '' (sitataja jina kwa sababu siwezi kujificha bungeni usiku kucha kama Zitto) anafanya baadhi ya vitu ambavyo yeye Dr. Slaa hajavikemea licha ya kuahidi kukemea pepo linapojitokeza popote pale. SILENCE MEANS YES. Tafsiri yake ni kuwa Dr. Slaa anakubaliana na anayoyafanya mwenye heri kwa 100% (mutatis mutandis)
1. Dr. Slaa anafurahia yanayofanyika kwa Godbless Lema (mbunge wa Arusha mjini). Ukizingatia baba yangu Slaa ni msomi mzuri wa sheria
2. Anafurahia kunyang'anywa mashamba kwa Sumaye (adui yake aliyemuita Mr. Zero akataka na sisi tumchukie lakini tunampenda)
3. Dr. Slaa anacheka sana kwa Lissu kuburuzwa usiku usiku toka Dodoma hadi Dar huku kapigwa pingu kama jambazi la Meremeta na tangold
4. Anarukaruka kwa furaha kuona Zitto Kabwe analala bungeni kama mlinzi kwa kuhofia usalama wake na kukamatwa kwa makosa ya uchochezi (na moyoni mwake atakuwa anasema wachochezi sana hao wakome!!)
5. Kukatazwa kwa mikutano ya kisiasa nadhani moyoni Dr. Slaa atakuwa anafurahia sana na kugonga cheers ya mvinyo wa kifaransa akiwa ughaibuni na Josephine Mushumbusi Slaa (mke wake) huku akiwaza bora wapigwe wavunjwe mkono kama yeye au watolewe damu kama Josephine kule Arusha
6. Anachekelea sana kukamatwa kwa mbunge Lijualikali na kufungwa miezi sita na kusema mwenye heri anaiweka ardhi ya Tanganyika wakfu
7. Kukataza mchakato wa katiba mpya (aliyoililia sana Dr. Slaa) kwa sasa atasema haina haja yuko mwenye heri anatosha na naamini atakuwa anafunga novena kumuombea ili 'akamatie chini' na akaze uzi
8. Swala la Kagera ulisema ni ushamba wetu kwani nchi zote zilizoendelea majanga kama hayo bima ya majengo ndiyo hufidia
Binafsi kama Nyakageni nakuombea sana Dr. Slaa ili wanao warudi kuishi Tanzania hapo baadaye na nakupongeza sana kwa kusababisha haya yanayoendelea na yatakayokuja. Msimamo wako kuhusu jambo la Kagera lilinipa mwanga kuwa 'usiamini mtoto aliyezaliwa na mwanamke'. Nakusalimia sana na nakuomba urudi tena pale Serena Hotel na kumpongeza mwenye heri na kumbariki ili aendelee na kazi 'njema' aliyoianza
Msalimie sana mdogo wangu Junior na mama yake. Wasalaaam