Katika hali inayoonekana Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa anatikisa anga la siasa za Tanzania jana wabaya wake wamemzushia kifo.
Katika SMS zilizokuwa zinasambazwa kwa watu mbalimbali ilidaiwa Dr Slaa amepata ajali ya gari na kufariki dunia.
Hali hiyo ilisababisha hofu kubwa kwa watu mbalimbali na kwa muda mfupi simu zilikuwa zikipigwa kila kona huku Taifa likiwa na tahuruki kubwa kwa muda mfupi.
Akizungumza na Nipashe Dr Slaa alisema yeye ni mzima wa afya bali kinachofanywa ni mchezo mchafu.Dr Slaa alisema maadui wa CHADEMA wanaweweseka na wanadhani wakizusha hivyo wanamtakia mabaya.Kiongozi huyo shupavu aliongeza kuwa kumzushia kifo ni kumuombea mema ambapo siku zake za kuishi zinaongezeka.
Source: Nipashe Jumapili.