Dr Slaa atingisha Kigoma Kaskazini

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Msafara wa Gwiji wa siasa Tanzania na Katibu mkuu CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa ndo unakatiza hapa Kigoma mjini, ishara ya vidole viwili inatanda kila mahali na maneno ya ''Dkt. Slaa huyo huyo...Chademaaaa....Chademaaaa''.

Msafara unaelekea Jimbo la Kigoma Kaskazini Mkutano wa Kwanza utakuwa Nyarubanga, kisha utaelekea mkutano wa pili.

Updates.....

Ndo twawasili Nyarubanga hapa. Akina mama wamejipanga barabarani pembeni kdg ya uwanja wanaimba kumpokea Katibu Mkuu Dkt. Slaa. Msafara umeshaingia uwanjani.

Red Brigade wako imara kweli kweli leo hapa. Wananchi wanasogea sogea. Naona ngoma hapa inachezwa na akina mama.

Updates No 2:

Dkt. Slaa anaingia kucheza ngoma na wenyeji hapa. Ngoma hii inachezwa na kikundi cha ngoma cha akina mama wa CHADEMA kuhamasisha wananchi kujiunga na CHADEMA hasa akina mama na vijana.

Naambiwa inaitwa Denga. Wananchi wanashangilia kumuona Dokta anaungana na akina mama kucheza Denga!

Updates No 3.....

Mkutano umeshafunguliwa na Mkiti Issa Kibaba. Waitara amemkaribisha Mratibu wa Kanda ambaye amezungumzia namna Kanda inavyojipanga kuhudumia wanachama na wananchi kwa ujumla.

Sasa anapanda Mkiti wa Kanda Shaaban Mambo, anazungumza kidogo kwa sbb ya dalili ya mvua kubwa. Sasa amepanda Dkt. Slaa.

Mvua imekuwa kubwa hapa. Wav wamevumilia kumsikiliza Dkt, ambaye ameamua kubadili kubadili mbinu ya mkutano badala ya kuendelea kuhutubia, anatoa nafasi ya maswali kwa wananchi ili wasiende mbali

Updates No 4.....

Watu 4 hadi sasa wameshauliza maswali na Dkt. Slaa anaendelea kujibu maswali yote 5, 3 yanayuhusu maamuzi ya Kamati Kuu kuwavua madaraka Zitto, Kitila na Mwigamba

Mengine 2 yanayuhusu Chadema na misingi yake. Dkt, anaendelea kufafanua, masuala yote yaliyoulizwa.

Mvua inazidi kuwa kubwa hapa. Dkt. Slaa anawauliza wananchi aendelee au afunge mkutano, wananchi wanasema aendelee. Anaendelea hapa.

Mvua kubwa iliyotanguliwa na ukungu mkubwa sana ktk eneo la mkutano imezidi kuongezeka.

Sehemu ya umati wa wananchi wametafuta miamvuli na kubaki karibu na jukwaa. Wengine wako jukwaa kuu, wengine wamekimbilia upenuni mwa nyumba kuendelea kusikiliza.

Mvua ktk eneo hili la mkutano ni kubwa sana, ingawa mbali kdg tu kutoka hapa hakuna ukungu wala mvua.

Updates No 5....

Kutokana na mvua kuzidi kuwa kubwa Wananchi wamemruhusu Dkt. Slaa ashuke jukwaani baada ya kuhutubia kama dkk 45.

Msafara unalazimika kuondoka kwenda mkutano wa pili.

Kuna utani unazungumzwa na baadhi ya wananchi kwamba ''wameshindwa njia zote sasa wameamua kujaribu hii...''.

Lakini Dkt. Slaa kabla hajaondoka jukwaani, aliwaambia wananchi kuwa mvua ni baraka, hivyo wasilaumu!

Picha chini ni kabla mvua haijaanza kunyesha:
attachment.php



Source: Afisa Habari Mkuu CHADEMA Tumaini Makene
 
Umbea utawatoa mishipa ya Shingo.
Kama anajiamini Brigade ya nini?
 
...

....Nguvu za Mungu zimeshuka Kigoma ..

...Mji umetikisika Matunguri yanaendela kulipuka...

Mungu na Chadema...Chadema na Mungu...
 
Mafala wa Zitto na MACCM walifanya wananchi wawe sympathetic na DR Slaa it was a very poor calculation ya kutumia watu wa Mwanza na ndugu wa damu kufanya fujo wangeacha natural justice it take place pengine ingekuwa vingine sasa hivi inaonyesha kama vile wananchi wanasema hatutaki kubandikwa maneno, kwamba sisi ndio baadhi ya wananchi walianzisha mageuzi hongereni wananchi wa Mwandiga , Zitto nyumba yake pale kona ya barabara hata hajaiezeka manake anaonyesha yeye ni mpita njia
 
Jamani mwenye sifa tumpe sifa yake wakuu, Mimi toka nimefatilia kwa karibu hekima, maarifa na siasa za Dr.Slaa, ninathubutu kusema huyu Mzee ni miongoni mwa Simba(Wakombozi) wa Africa, Dr.Slaa ni mwanasiasa hasa, Ni jemedari na Kamanda mpiganaji aliye jasiri mithili ya Steve Biko na mwenye muono mithili Cout Camilo cavour wa Italy.

Mungu ampe maisha marefu sana Kamanda wetu na hakika Historia itakuandika na kukumbuka kama shujaa wa haki mwenye ujasiri na kweli aliyeshuka zama hizi.
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom