Dr. Slaa atazishinda propaganda dhidi yake!

Malova

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
784
228
Katika Nchi hii na pengine hata nchi nyingine sijawahi kumwona au kumsikia kiongozi wa kisiasa anayetajwa mambo yake mengi hadharani kama Dr. Slaa.

Wapinzani wake wana/wamemwongelea sana mambo yake mengine hadi ya ndani ya zipu lakini Babu amehilimi na kukabiliana nayo vizuri kabisa. Kwahiyo hata hizi propaganda za sasa nina uhakika Dr. Slaa atazishinda.

Kwasababu anajua uwezo wa kufikiri na kutenda na hata mbinu za wapinzani wake. Sina shaka kabisa na hili. Na huu unaweza kuwa mmoja ya mipango ambayo mtu mmoja aliiandika...

Kwamba ili CCM iendelee kuongoza ni:
1. Au wakiue CHADEMA
2. Au Wakiue CCM na kuanzisha chama kingine
3. Watumie Demokrasia.

Hili la kwanza lilipewa kipaumbele sana. LAKINI KWA TAARIFA YENU (MAGAMBA) HAMTAWEZA HATA KIDOGO. Uwezo wa Dr. Unaweza kuwa sawa au hata zaidi ya Sekretariati nzima ya CCM.
 
Ninakubaliana na wewe. Katibu mkuu huyu anafikiri saana na akili yake nafikiri ni akili za wana CCM 50 waliomstari wa mbele. Nawaza sana kwa nini mti huu wa matunda unapopolewa sana? Kumbe ni kwa sababu matunda yake yameiva na ni ya kupendeza kwa kila mtu.

Dr. ana technique nyingi saana za kupambana na wapinzani wake, hata sasa najua anawavutia pumzi tu akianza watakiona cha moto. itabidi waitishe kamati ya sekretariet tena kupanga uchafu mwingine.
 
Usihangaike na akina NAPE. Karume ameshafanya hesabu za INTEGRATION na kuja na jibu hili......
1845918e723ad0b5874fa2fb77870925.png
=
CCM-Samaki.jpg
 
Slaa ni homa kwa CCM, kumpaka matope, kumtukana, kumzulia uongo na fitina juu yake hakutaisaidia CCM, dawa ni moja tu kwa CCM, kuacha ufisadi,kutowakumbatia mafisadi, kujali wananchi kwa kutekeleza ahadi zao ipasavyo hiyo ndio salama ya CCM.

Haya mambo ya kadi, sijui mke wa mtu, sijui babu huo ni woga na CCM ya leo haina tofauti na Mbwa koko, wala haitutishi tena, popote kwenye mechi (uchaguzi) tunaingia nao uwanjani pamoja na kwamba wanashinda kwa kubebwa lakini wakitoka wanasimuliana hali ilivyokuwa ngumu.
 
Dk. Slaa ni jiwe la pembeni walilolikataa waashi, ccm inapelekwa puta sana na dr slaa,binafsi naamini chadema wana la kujivunia kupitia dr.
 
Nape anaona ametimiza aliyoyapanga ndio maana yupo kimya. Lakini mipango kama hii ni mirahisi sana. Hata mtot wa darasa la pili anaweza kukuona hufikirii kwa propaganda kama hizi. Hata kama ukatumia watu waliopo CHADEMA bado mziki ni mkubwa sana.
 
Dr slaa ni kichwa, watasema uwongo wao wote watamaliza akija kuibuka na sera zake utasikia haziwezekani baada ya siku chache

utawasika inawezekana. Wanapinga kila siku na bila mda kupita wanaaibika kwa kuukubali ukweli.
 
Hii ni makala ya Deusdedit Jovin kwenye gazeti la raiamwema.

MAELEZO kutoka kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kuhusu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa kuendelea kumiliki kadi ya CCM ni propaganda zinazokiuka misingi ya ukweli, uhuru na haki. Nitaeleza kwa nini.

Kwanza, kulingana na ibara ya 8 ya Katiba ya CCM, Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi ndio hufikiria na kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu maombi ya uanachama.

Pili, kulingana na ibara ya 12 (1), baada ya mtu kukubali kuwa mwanachama inabidi atekeleze mambo yafuatayo, kabla ya kusajiliwa kwenye rejesta ya wanachama wa CCM: lazima atoe kiingilio cha uanachama; lazima alipe ada ya uanachama kila mwezi; na lazima atoe michango yoyote inayoamuliwa na viongozi wa CCM.

Tatu, kulingana na ibara ya 13(1) ya Katiba ya CCM (2010) uanachama wa mtu katika CCM unakwisha kutokana na sababu mojawapo kati ya sababu sita zifuatazo: kufariki, kujiuzulu, kuachishwa kwa mujibu wa Katiba, kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba, kutotimiza masharti ya uanachama, au kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa.

Na nne, kulingana na ibara ya 13(4) mwanachama aliyejiuzulu akitaka kuingia tena katika CCM ataomba upya kwa kufuata utaratibu wa kuomba uanachama kwa mujibu wa Katiba ya CCM.

Kwa kuzingatia vifungu hivi vinne vya katiba ya CCM (2010), mambo kadhaa yanafuata kimantiki.

Kwanza, ni wazi kuwa ibara hizi zinawakataza viongozi watendaji katika CCM kupokea kiingilio cha uanachama au ada ya uanachama kutoka kwa mtu ambaye ni mwanachama wa Chama kingine chochote cha siasa mbali na CCM. Yaani, kiongozi wa CCM anayepokea kiingilio cha uanachama au ada ya uanachama kutoka kwa mtu ambaye sio mwanachama wa CCM anakuwa ni kiongozi mwenye asiyefikiri sawasawa.

Na pili, kwa kuzingatia vifungu hivi vinne vya katiba ya CCM, ni wazi kuwa, mwanachama wa CCM ambaye anathibitika kuwa, baada ya kujiunga na CCM, ameamua kuwa mwanachama wa Chama kingine chochote cha siasa mbali na CCM, anapaswa ama kuachishwa kwa mujibu wa Katiba au kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba ya CCM.

Hii maana yake ni kwamba, kiongozi wa CCM anayefahamu kuwa kuna mwanachama wa CCM ambaye amefanikiwa kuwa Katibu Mkuu au mbunge kupitia chama kingine chochote cha siasa lakini akasita kusimamia mchakato wa mtu huyo kuachishwa kwa mujibu wa Katiba ya CCM au mtu huyo kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba hiyo hiyo, anakuwa ni kiongozi asiyefikiri sawasawa. Anakuwa ameisahau katiba yake.

Kwa kuzingatia mahitimisho haya mawili muhimu, sasa tunaweza kutambua kwa kurejea kauli ya Nape dhidi ya Slaa kuwa na kadi ya CCM, yeye (Nape) ni kiongozi wa namna gani.

Nape Nnauye, Katibu Mwenezi na Itikadi (CCM), amesema na kuandika katika mitandao ya kijamii maneno yafuatayo:
“Katika matamshi yangu hakuna mahali nilipohusisha kuwa na kadi na uanachama wa mtu.....hivyo wanaojaribu kubwabwaja kuwa sijui Katiba ya CCM wanakurupuka kwa sababu ndogo sana… nilichosema (ni kuwa) Dk. Slaa na baadhi ya vigogo wa (CHADEMA) wana kadi za (uanachama wa) CCM na baadhi yao wanazilipia mpaka leo.

Sijazungumzia uanachama wao...najua kuwa kwa katiba ya CCM ukishakuwa mwanachama wa chama kingine uanachama wako CCM unakufa hapo hapo.

Kwa mujibu wa nukuu hii, Nape Nnauye amejenga hoja mbili tata ambazo nakusudia kuzipa muundo wa kimantiki na kisha kuzihakiki kwa lengo la kumpa somo. Hoja ya kwanza ambayo Nnauye ameijenga kwa njia ya mzunguko ni hii hapa:

“Kwa mujibu wa katiba ya CCM, kila mwanachama hai anapaswa kulipa kiingilio cha uanachama na ada ya uanachama; Dk. Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA na baadhi ya vigogo wenzake katika CHADEMA wana kadi za uanachama wa CCM na baadhi yao wanafanya malipo haya mpaka leo; Kwa hiyo wao ni wanachama hai wa CCM. Hata hivyo, haya matamshi yangu dhidi yao hayahusianishi kadi za CCM walizonazo kina Dk. Slaa na uanachama wao katika CCM.”

Katika hoja yake hii, Nape Nnauye ananishangaza mambo mawili. Kwanza anajaribu kutuambia kuna wanaCCM ambao ni wanaCHADEMA pia. Lakini pili, anatuambia kwamba, yeye haijui katiba ya CCM. Nitaanza na hili la pili nikiwa nimefanya dhahania (assumption) kwamba, siku ile Nnauye anatoa kauli zake inawezekana, angalau kimantiki, kwamba Dk. Slaa na wenzake wanaotajwa naye tayari walikuwa wameamua kuchukua uanachama wa CCM lakini wakasitisha nia yao baadaye kidogo.

Katika mtazamo wake kuhusu katiba ya CCM, tatizo liko hivi: Nnauye amemwongelea Dk. Slaa pamoja na “vigogo wengine” wa CHADEMA katika sentensi yenye kiunganishi cha “na.” Hivyo, anachokiongelea kitaalamu tunakiita “mazingira ya kitu hiki pamoja na kitu kile” (both/and scenario), ambapo kuna Dk. Slaa kwa upande mmoja na “vigogo wengine” wa CHADEMA kwa upande mwingine. Anasema kwamba wote wanazo kadi za CCM na baadhi yao wanazilipia mpaka sasa.

Ni wazi kuwa, Dk. Slaa kama Katibu Mkuu wa CHADEMA anayo kadi ya uanachama wa CHADEMA tangu alipohamia katika chama hiki karibu miaka 15 iliyopita. Kwa hiyo, kiunganishi cha “na” katika sentensi ya Nnauye kinamaanisha kuwa, baadhi ya wale “vigogo wengine” wa CHADEMA anaowataja wana kadi za CHADEMA pia.

Na maneno “baadhi yao wanalipia kadi” katika sentensi yake yanamaanisha kuwa ama Dk. Slaa au mmojawapo kati ya hao vigogo wengine wa CHADEMA waliotajwa analipia ada ya uanachama wa CCM. Huwezi kulipa ada ya uanachama wa CCM kama sio mwanachama wa CCM. Kwa hiyo, kwa kuzingatia ukweli huu, inafuata kimantiki kuwa kauli ya Nnauye kuwa “baadhi yao wanalipia kadi” za CCM inaongelea uanachama wa kina Dk. Slaa katika CCM.

Hivyo, ni kinyume cha kanuni za mantiki, kwa Nnauye kusema kwamba, matamshi yake haya “hayahusianishi kadi za CCM walizonazo kina Dk. Slaa na uanachama wao katika CCM.” Huu ni usahaulifu.

Kuna hoja ya pili ambayo imesanifiwa na Nape Nnauye na ambayo inakoleza zaidi mtazamo wangu huu dhidi yake na wenzake. Katika nukuu yake hapo juu, kwa njia ya mzunguko, Nnauye pia amejenga hoja ifuatayo:

“Kwa mujibu wa katiba ya CCM, kila mwanachama hai anapaswa kulipa kiingilio cha uanachama na ada ya uanachama; Dk. Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA na baadhi ya vigogo wenzake katika CHADEMA wana kadi za uanachama wa CCM na wanafanya malipo haya mpaka leo; Kwa hiyo, viongozi watendaji wa CCM wanapokea kiingilio cha uanachama na ada ya uanachama kutoka kwa wanachama wa vyama vingine vya siasa! Hii maana yake ni kwamba, baadhi ya wanachama wa vyama vingine vya siasa ni wanachama wa CCM pia, jambo ambalo ni kinyume cha katiba ya CCM.”

Huyo ndiye Nape Nnauye katika rangi zake halisi! Ameivua nguo CCM! Alichofanya hapa ni kulitangazia taifa na dunia nzima kwamba, CCM inaendeshwa nje ya utaratibu wa kikatiba!

Ni hivi: Kama anachokisema ni kweli, basi jambo hili ilipaswa kuwa sababu ya kutosha ya vikao husika ndani ya CCM kuanzisha mchakato wa kikatiba ili kufanikisha kuachishwa au kufukuzwa kwa kina Dk. Slaa kutoka CCM. Vinginevyo, vikao vya juu vinapaswa kuisambaratisha sekretarieti ya CCM ya sasa kwa kuvunja katiba ya CCM!

Nape Nnauye na sekretarieti yake lazima washughulikiwe kwa sababu wao wamethibitisha kwamba ni viongozi wenye kusumbuliwa na tatizo la kutokujipanga na kusimamia katiba ya chama chao.

Na kwa kuhitimisha basi, nataka niseme kwamba, Nape Nnauye, Katibu Mwenezi wa CCM, pamoja na sekretarieti yake yote inayofanya madudu haya aliyoyatangaza kwa dunia nzima tayari wamepoteza sifa ya kubaki katika ofisi wanazoziongoza.

Tutawashangaa sana kina Jakaya Kikwete (Mwenyekiti CCM), kama wataendelea kuwakumbatia viongozi hawa wanaosumbuliwa na tatizo la usahaulifu wa kiwango hiki kuhusu katiba ya chama chao, wakati ndani ya chama chao kuna watu wenye umakini mkubwa wa kushika nafasi hizi za uongozi.
 
The ultimate measure of a man is not where he stands in the moment of confort,but where he stands the moment of challenge and controversy
 
Acha uongo wewe yaani watu kuhoji kuwa na kadi mbili na kwa nini katelekeza watoto wake ndio kumuongelea sana...
 
Ritz, Inawezekana kweli sisi waongo au tunamtetea babu. Lakini kwa haya yanayoendelea yaliyoanzishwa na Nape nyinyi ndio mtakaofedheeka. Maana inaonesha hata vichwa vyenu havifikiri sawasawa. Hapo ndipo ukweli utakapoonekana.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom