Dr. Slaa ataka Sofia Simba ajiuzulu au awajibishwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa ataka Sofia Simba ajiuzulu au awajibishwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mfamaji, Feb 1, 2010.

 1. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,572
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Doctor Slaa amemtaka Sofia Simba ajiuzulu na asipofanya hivyo awajibishwe na Rais kwa kuitia serikali aibu kwa kuleta mbele ya Bunge mswada usio na mashiko. Sofia Simba anataka kumpunguzia Amiri Jeshi Mkuu madaraka. Je hili litafanyika ? Na kwa nini lisifanyike? Does this amount to insurbordination ? Kwa nini Sofia hakuseek advise from the state house, security Organs, etc kabla hajaleta unproffesiopnal bill bungeni? Au anafikiri security issues ni mchiriku, rusha roho au mipasho ya akina Pembe la Ngombe? Wakuu mnasemaje ?
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Feb 1, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Kama wewe huna cha kusema wengine tutasema,

  mwambie Dr. Slaa kama amesema hivyo amefulia, Sofia Simba hajiuzulu, wala JK hamfanyi chochote! wala serikali haijapata aibu, walichopitia miaka hii minne kama ingekuwa serikali ya ibu tungeijua! mwambie slaa mshipa wa aibu serikali ya JK haina!!

  Yeye Slaa aangalie kuiondoa CCM na sio kujificha chini ya JK, anaposema hivyo ina maana JK ni safi, poa, mchapa kazi n.k

  Sofia Simba ameonyesha uwezo wa CCM, Slaa badala ya kuchukua kama point ya kupatia kura anataka kujikomba! aache kujikomba kwa JK; kutaja jina la JK kuwawajibisha mawaziri aliowateua ni ujinga!!! mna hakika gani kama hakupitia huko state house na vyombo vya usalama kupata ushauri? kwani hawana sheria zao kuwa kabla ya mswada upitiwe? SS hana tatizo baba! ni sanamu robot lingine next to JK akiambiwa simama anasimama

  nani kawaroga jamani?? JK has nothing to do in this country, JK alitaka ujiko tu wa urais hana analoliweza na hakuna atakaloliweza achilia mbali kumuwajibisha SS!!

  Huyo slaa naye kama amesema hivyo ajiuzulu upinzani; I am sick and tired mentioning the name of JK as if he is innocent!

  wapinzani my foot! JK akimchukulia hatua Sofia Simba si ndio anapata kura yeye! halafu mnasema kuna upinzani 'nji' hii

  Wapinzani wa Tanzania ukiwasikiliza sana unaweza ukaugua ukichaa, wapole, wanajikomba, statement zao sio za kipinzani, they dont take opportunity, yaani wapinzani nchi hii ni kama mabaraza ya wazee wa CCM!! au tume fulani za bunge!
   
 3. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,482
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Duh!!!
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,572
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Well, Slaa should have said something . This is his stand kama mpinzani, angalau pale mswada umepingwa hata na CCM wenyewe.

  He could have a different stand and perhaps use it as opposition stick if the same could have gone through the perliament.

  Kama aliupitisha kwenye sehemu husika zikiwemo Security na baraza la Mawaziri nao wakaukubali, then were are borne to suffer more and more and forever until we uproot this pumkin CCm from the reign. Bora hata wangeuleta kwanza hapa Jf kablaya kuleta aibu kama hiyo. Tungewasidia zaidi. Great Thinkers.
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Feb 1, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Sure my friend ndani ya bunge angesema bila woga kuwa "nadhani wananchi wanaona bomu lingine la CCM, hawafikiri usalama wa nchi n.k"

  ange-wablast CCM wote, hapo ndio angewasha moto mzuri, kwanza unawadharau chama chote wapigane huko huko, lakini huku umejiwekea credit kuwa 'you see chadema wazuri'' kuongea sentensi yoyote itakayoonyesha utatuzi wa tatizo hilo ni CCM ni kuweka upinzani mbali na wananchi!

  CCM has to go! msiwapambe pambe na kuwatenga 'wasafi' na wachafu, woote kuanzia JK mpaka madiwani wao wachafu sina cha kulinganisha!
   
 6. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2010
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Kweli kuna vimeo lakini huyu kimeo cha juu kabisa mara apigane mara mipasho mara mswada usiokua na kichwa wala miguu akini JK KIMYAAAAAA!
   
 7. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,329
  Likes Received: 3,914
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Mfamaji.

  Dr W Slaa ni miongoni mwa wabunge wa bunge la JMT ambao wanajua kilichowapeleka pale mjengoni [Bungeni].Anasimamia vyema maslahi ya taifa pia anawawakilisha vizuri wapiga kura wake wa Karatu.Natamani mbunge wetu wa jimbo la Arusha angekuwa kama alivyo mheshimiwa W Slaa,natamani Tanzania ingekuwa na wabunge kumi wa aina ya Dr W Slaa.

  Maoni/mapendekezo ya Mheshimiwa Dr W Slaa kwa Mheshimiwa S Simba na kwa Muungwana ni muhimu sana kuzingatiwa hasa kwa nchi inayozingatia sheria,kanuni na taratibu.Nafasi ya uwaziri anayoshikilia Simba ni kubwa sana kwake pengine muungwana angecreate wizara ya mipasho/blah blah ingemfaa sana mama Simba.Mama Simba ameidhalilisha sana serekali laiti ingekuwa mambo haya yamefanyika kwenye nchi za wenzetu wanaojua nini maana ya bunge,serekali na wananchi tungesha msahau mama mipasho.

  Nakubaliana na maelezo ya waberoya kwamba hakuna kitakachofanyika labda niongezee sababu moja kubwa ni uchaguzi mkuu.Mama Simba ni mwenyekiti wa UWT ambayo ni muhimu sana kumhakikishia Muungwana anapita kwa kishindo ndani ya CCM.Muungwana hajali maslahi ya kitaifa sana sana anaangalia term ya pili ya urais ni kina nani watamsaidia kufikia lengo lake.
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,494
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Richmond wameikataa mara ngapi? Kuna aliyejiuzuru?
   
 9. N

  Nanu JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  This is a lesson that the MPs are not always on opposite sides when it comes to issues pertinent to our country. I think, we need a more balanced parliament in terms of opposition and the ruling party.

  The Committee which prepared the bill may have not done their work thoroughly but again Hon. S.Simba must have taken the bill to the cabinet meeting before tabling it. How did it go through the cabinet which is chaired by His Excellency President of URT?

  There may be a good motive for the bill but it was not well addressed or some flaws were left uncemented. This also send signals to the ministers to be well prepared for their bills before tabling to the parliament.
   
 10. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  huyu mama naamini wamemuingiza mkenge wa kisiasa tu, nadhani kuna watu wanatumiwa katika ofisi yake kisiasa. kimantiki tunafahamu kabisa, kama waziri hapa nchini kwetu si mtendaji (professinal) kuna watu na kamati maalumu zinazofanya michakato kama hii,akiwemo katibu mkuu, pia kabla ya kufika Bungeni, Mwanasheria mkuu lazima apitie na kuridhishwa na jambo lolote linalohusu sheria, Pia ikumbukwe kwamba, muswada huu ulisharudishwa bungeni, ili ufanyiwe marekebisho, Je timu ya mwanasheria mkuu iliji evaluate vipi pale kazi yao waliyo ibariki kurudishwa? na walichukua hatua gani mpaka wanarudisha utumbo ule ule? Sophia atapata aibu na ikibidi kuwajibika kwa wajibu wake kama waziri (accountability)

  Mnataka JK alie kama ilivyokuwa kwa Pinda Jamani? kuna tatizo hapa kwenye ofisi ya MAMA huyu,
  Kwa matatizo yaliyompata, SS nadhani amejitahidi kujirekebisha, kwani simsikii kuropoka siku hizi. wamemtafutia mitego mingine ya kiutendaji, anakuwa dhalili tena.lakini hadhaliliki, anapoteza umakini wake, na credibility kwa nafasi yake.

  Nashauri. kuna watu hapa badala ya kuisaidia Tanzania isonge mbele, wanatumiwa na wanasiasa kurudisha nyuma tanzania, haiwezekani watu wenye professional zao wafanye madudu kama haya. washughulikiwe haraka watu wabaya hawa

  JK, Baba hizi ndizo hasara za wewe kutokaa hapa nyumbani na kufuatilia na kujua nini kinaendelea. Nadhani umeshatambua kwamba wasaidizi wako si lolote si chochote. kaa chini ufanye kazi mwenyewe, ikiwezekana kazi hata za wakuu wa mikoa na wilaya, hakuna kinachofualitiliwa na hao watu wako. wanafanya siasa na majungu ili udondoke.walimdondosha EL kwa malengo ya kukudondosha wewe. umeanguka baba.

  Inuka, futa mavumbi, Usiogope lawama, cc wa Tz ni wa pole na wenye kusamehe.

  Umetukosea sana,
  tuonyeshe na wewe umesikitika na umefahamu kwamba umetukosea, tuonyeshe si kwa maneno, bali kwa vitendo kwamba, umeikosea tanzania na sasa unatubia makosa yako.
   
 11. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 965
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Hiyo ndio hasara ya kuteua waziri mbumbumbu! Hata kama yeye si mtendaji lazima ahoji na kujiridhisha kabla ya kuleta bill itakayotia aibu. Yeye ndie aneyebeba dhamana ya wizara hata kama anoo wataalam na ndio maana anombwa kujiuzuru!
   
 12. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 2,020
  Likes Received: 717
  Trophy Points: 280
  Ninavyofahamu, muswada unaopelekwa Bungeni na Serikali unakuwa umejadiliwa na kupitishwa na Baraza la Mawaziri (Cabinet) ambalo mwenyekiti wake ni Rais. Aidha, kabla ya hapo, Wizara zote na taasisi husika hupewa nafasi ya kutoa maoni yao kwa maandishi. Hivyo, nimeumia kichwa sana kuwaza nini hasa kilichotokea hapa.

  Je, ni kwamba kuna watu wanataka kumpunguza uzito Rais? Lakini yeye ndiye bosi wa mchakato wa Waraka huo Serikalini! Au ni yeye ndiye anayetafuta namna ya kukwepa majukumu nyeti? And why? Au hana uwezo tena wa kudhibiti mambo Serikalini; kuna watemi wengine ambao ndio Serikali yenyewe zaidi yake?

  In any case, kilichotokea Bungeni ni dalili mbaya sana kwa taifa. Na huyo Mh. S. Simba awe katumwa, au mjinga, au mkorofi ni kielelezo cha aibu (embarassment) kwa uongozi wa taifa letu. CCM watake wasitake wanayo aibu hiyo hadi hapo watakapojipambanua na makada uozo.
   
 13. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2010
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wakati wa u-Rais wa Mwalimu Nyerere, Muswada wowote uliokuwa unaletwa kwa majadiliano Bungeni ulikuwa umekwisha pitishwa na Baraza la Mawaziri na kukubaliwa na Rais. In any case, the President will have to assent to Bill, and so all Bills submitted to Parliament by a Minister must have the approval of the President.

  Kama utaratibu huu unafuatwa hadi leo, basi ni Baraza lote lingetakiwa kujiuzulu, kwa vile Bunge limeonyesha halina imani na Baraza la Mawaziri, Rais akiunganishwa nao.

  Mheshimiwa Dk Slaa waunganishe wote hawa wababaishaji, waondoke kabla ya Oktoba 2010.
   
 14. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Dk Slaa ana uelewaa mkubwa tuu kwamba uelewaa wa SS unalindwaa na serikali iliyomteuaaa..Hapa ni kwamba muswada huu umejadiliwaa na vyombo vyotee achilia mbalii kamati husika ya bunge kuhusu masuala ya ulinzi na KATIBA...SHAME ON THEM ALL!!!!

  SS aliwajibika tuu kuusomaa bungeni kwani ndo mhusikaa na kazi yake ya msingii. wapi wajumbe na mwenyekiti wa kamati husikaaaaaaaaaaaaaaa???

  Pia Raisi na baraza lake waliupitia na natumaii kwa undani zaidi TISS na wenzao wakikacherooo ndo waliousomaa kwa undani zaidiiii na kumshaurii Wazirii Husikaa.

  Bunge wamefanya kazi yao ila nawalaumuu huwa wanachelewaa sanaa kufanya kazi yao na mara nyingi wako bias na ushabikii wa kipuuuziiiiiiiiiii...WAACHEE WAENDELEE KUPIGA CHINI MISWADA MINGI ZAIDI (MINGI HUWA MIBOVUUU) na wasichague wala kutishiaa na kutafuta umaarufuu wa kisiasa.
  Tayari ni maarufuu kwa wapiga KURA WAO..WAWATEEE NA KUWALETEAA MAENDELEOOOOO..
   
 15. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2010
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  You really dont have to react that way at all.., also dont condem people without facts, argue with fact ,listen to the loud and stupid, they too have their story, what you have quoted above everyone knows about it, what we dont know is why she mentioned what she did, you could start from there, but vuta pumzi kwanza..kunywa maji pia...
   
 16. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #16
  Feb 1, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,636
  Likes Received: 2,704
  Trophy Points: 280
  Me nadhani ingekuwa poa tu huo mswada nugepita halafu tuone kama Muungwana angeupitisha kabla haujawa sheria au la.....wakina Slaa wamekurupuka,wangeuchunia waone Muungwana atasema nini,by then Kumpunguzia majukumu Muungwana ingekuwa poa tu..maaana mambo yamemzidia sana,huu mswada upite akiingia madarakani mtu mwingine zaid ya Muungwana then sheria inapigwa chini..
  Wangemuacha Muungwana waone angefanya nini..angeupitisha au angeuchunia
   
 17. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kazi zote hizi ndio kwanza zimeanza maana kipindi hiki tunahitaji viongozi makini sana katika zama hivi za harakati
   
 18. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 8,013
  Trophy Points: 280
  Inawezekana muswada huu ulipitiwa na baraza la mawaziri na mkuu mwenyewe. Haingii akilini kwamba Muswada unaweza kuibukia bungeni bila kupitiwa na kujadiliwa kwanza.

  Hii ndio product ya kuchaguana kishkaji bila sifa.

  Ni aibu kwa serikali nzima. Wabunge nao wasiogope mikwara na wakaze buti mpaka kieleweke
   
 19. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #19
  Feb 1, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  I totally agree with you! Tunataka kuona upinzani wa kweli ambapo kila kosa la kiongozi wa CCM linakuwa 'mtaji' wenye manufaa kwa the opposition. Hakuna lolote la maana wanalofanya haw wanaojiita ni wapinzani wa Chama tawala!
   
 20. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #20
  Feb 1, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 38,087
  Likes Received: 9,747
  Trophy Points: 280
  I actually support the general idea of clipping presidential wings. Na sielewi what's this hoopla is all about - at least from the little info we have-. Tukiwa na madikteta tutashangaa kweli?

  Tuna rais kama papa bwana.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...