Dr. Slaa asema maandamano ya wananchi kudai kura zao yapo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa asema maandamano ya wananchi kudai kura zao yapo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kalunguine, Nov 19, 2010.

 1. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Dr Slaa amesema kupitia mahojiano yaliyonukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari leo kuwa maandamano nchi nzima yapo na yatatumiwa na wananchi kama njia ya kudai kura zao zilizoibiwa na CCM na JK. Yatatumika kudai mfumo bora ili wapiga kura wasiendelee kuibiwa kura zao. Njia ya maandamano ambayo ni People power itatumika kama njia za awali za majadiliano zitashindikana kupata ufumbuzi wa wizi wa kura za wananchi.

  My take: CCM wana kawaida ya kuafiki majadiliano halafu wanapiga danadana. Wanaweza kufanay usanii katika majadiliano hadi uchaguzi wa mwaka 2015 huu hapa. Kwa hiyo ni vema CHADEMA wasikawie kumaliza hizo njia zingine ili people power ifanye kazi yake kudai kura za wananchi. Inafaa ufumbuzi uwe umepatikana si zaidi ya miezi miwili kuanzia leo tarehe 18.11.2010.
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  watajadiliana na nani kama Rais hawamtambui?
   
 3. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo wewe unataka maandamano leoleo?
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  this thing is getting out of control
   
 5. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Unajua nadharia ya majadiliano? hutumika kwa pande zenye mvutano mkubwa kama ilivyo sasa kati ya wananchi walioibiwa kura na JK, CCM na NEC. Kama wananchi wangemtambua hakuna haja ya majadiliano
   
 6. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Wananchi walioibiwa kura ni kina nani? Kuna kidhibiti chochote kimetolewa?
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Thanks for the information. Your source please??????????
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  si alikwenda kenya kuchekacheka? basi na kibaki aje kununanuna
   
 9. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #9
  Nov 19, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  hapo kama umefuatilia kwa karibu utaona kuwa hakuna mvutano. Chadema wanalalamika peke yao. Uchaguzi ulikuwa na vyama 7. so it 6-1. chadema ndio wanataka kuvuta ila mvutano haupo.
   
 10. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wananchi wanajua idadi ya kura walizopiga na kusainiwa vituoni na zile zlizotangazwa na NEC zimepishana sana, pia website kumbukumbu ya website ya NEC inavyoonyesha walivyochakachua hadi wanatoa kura zinazofanana kwa vitua vya kupigia kura kwa wagombea wote
   
 11. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Soma kwenye Post, pia sikiliza exclusive
   
 12. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #12
  Nov 19, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Wananchi wa wapi kwa mfano? idadi ya walizopiga wao ni ngapi na NEC imetangaza ngapi?
   
 13. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #13
  Nov 19, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Unatarajiwa kuwa great thinker. Kwa kuanzi soma hapa

  Dk. Slaa: Uchaguzi wizi mtupu | Gazeti la MwanaHalisi  Dk. Slaa: Uchaguzi wizi mtupu


  [​IMG]
  Na Saed Kubenea - Imechapwa 10 November 2010

  [​IMG][​IMG] [​IMG]


  MATOKEO ya uchaguzi mkuu yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), yamejaa utata, MwanaHALISI limegundua.
  Taarifa kutoka ndani ya NEC, vyama vya siasa na baadhi ya wagombea, zinasema matokeo yaliyotolewa yanatofautiana na kura halisi zilizopigwa.
  Kwa mujibu wa baadhi ya mawakala wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), matokeo mikononi mwao yanatofautiana sana na yale yaliyotangazwa na Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC).
  Matokeo mikononi mwa mawakala kutoka mikoa 18 ya Tanzania Bara na mitatu ya Zanzibar, hadi juzi Jumatatu, yanathibitisha kuwepo tofauti kati ya idadi ya vituoni na ile iliyotangazwa na NEC.
  Uchaguzi mkuu nchini ulifanyika Jumapili iliyopita kwa kuchagua madiwani, wabunge na rais, kwa upande wa Tanzania Bara na masheha, wawakilishi na rais Visiwani.
  Katika jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro, matokeo yaliyotangazwa na NEC yanaonyesha kuwa CCM imepata kura za urais 35,910, huku CHADEMA ikionyeshwa kupata kura 18,513.
  Lakini matokeo ambayo yamekusanywa na mawakala wa CHADEMA yanaonyesha CCM imepata kura 20,120, huku CHADEMA ikipata kura 26,724.
  Katika jimbo la Karatu, mkoani Arusha, hesabu za NEC zinaonyesha CCM imepata kura za urais 24,382, huku CHADEMA ikipata kura 41 tu; angalau kwa mujibu wa matangazo ya televisheni.
  Bali kwa mujibu wa matokeo yaliyokusanywa na mawakala na ambayo yamesainiwa na mawakala wa vyama vilivyoshiriki uchaguzi na msimamizi wa uchaguzi katika jimboni hilo, CCM imepata kura 24,364 na CHADEMA imepata kura 43, 137.
  Jimbo jingine ambalo matokeo yake yamejaa utata ni Geita, mkoani Mwanza. Matokeo yaliyotangazwa na NEC katika jimbo hilo, yanaonyesha kuwa CCM imepata kura 17,792, na CHADEMA imeambulia kura 3,989.
  Lakini matokeo mikononi mwa mawakala yanaonyesha kuwa CCM imepata kura 30,960 na CHADEMA kimepata kura 15, 736. NEC ilikiri kuwapo kwa kasoro katika jimbo la Geita na ilikubali kufanyia marekebisho.
  Katika jimbo la Ubungo, mkoani Dar es Salaam, matokeo ya NEC yameipa CCM kura 68,727 na CHADEMA kura 65,450.
  Hata hivyo, kwa mujibu wa matokeo mikononi mwa mawakala katika jimbo hilo yanaonyesha kuwa CHADEMA imepata kura 72,252 na CCM kura 70,472.
  Kuvuja kwa taarifa hizi kumekuja wiki moja baada ya NEC kumtangaza Jakaya Kikwete kuwa mshindi wa kiti cha urais.
  Kwa mujibu wa NEC, Kikwete alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 5,276,827 ambazo ni sawa na asilimia 61.17 ya kura zote halali zilizopigwa. Tume imesema kura zizopigwa zilikuwa 8,626,283.
  Mshindani mkuu wa Kikwete, ambaye ni mgombea wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa alitangazwa kuwa amepata kura 2,271,941 zilizo sawa na asilimia 26.34 ya kura zote halali zilizopigwa.
  Katika mpangilio huo, Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF alipewa kura 695,667 ambazo ni sawa na asilimia 8.06 ya kura zote halali.
  Uchunguzi wa MwanaHALISI umebaini kuwa licha ya tofauti ya matokeo ya vituoni na yale ya NEC, matokeo katika baadhi ya maeneo hayakurekodiwa kwenye karatasi za tume, rasmi kwa shughuli hiyo.
  Gazeti hili limeona matokeo yaliyorekodiwa kwenye karatasi za kawaida na magamba magumu ya makasha, ingawa zimegongwa mihuri inayoonekana kuwa ya tume.
  Matokeo ya aina hii yanashurutisha kuwepo ujenzi wa shaka juu ya usalama wa kura na uwezekano wa matokeo kugushiwa.
  Kwa mfano, katika jimbo la Segerea, mkoani Dar es Salaam, matokeo ya kura za urais yaliandikwa kwenye karatasi ya kawaida ya rangi ya khaki. Karatasi hiyo inaonyesha kuwa imetoka katika kituo Na. B – 2.
  Katika kituo B – 4 ambako matokeo yameandikwa kwenye karatasi ya kawaida, CCM imepata kura 90 na CHADEMA kura 55.
  Matokeo katika kituo hicho, kwa mujibu wa karatasi hiyo, yanaonyesha kuwa CCM imepata kura 94 na CHADEMA kura 90.
  MwanaHALISI limeelezwa kuwa mbali na kasoro hiyo ya kutokuwapo kwa fomu za kurekodia matokeo, katika baadhi ya majimbo yaliyofanya uchaguzi, majumuisho ya kura za urais hayakufanyika.
  Gazeti hili lilitaka kujua maoni ya Dk. Slaa juu ya taarifa kuwa kuna maeneo ambako majumuisho ya kura za urais hayakufanyika.
  Naye alijibu, "Wewe unazungumzia hilo; matatizo yaliyopo katika uchaguzi huu ni makubwa sana. Kuna uchafu mwingi. Ndiyo maana sisi tunasisitiza kuwa hatuwezi kukubaliana na matokeo yaliyotangazwa."
  Amesema, "Tunaendelea kukusanya nyaraka zote za uchaguzi na si muda mrefu ujao, tutaeleza dunia ni kitu gani kilifanyika, wapi na akina nani walihusika. Tutaeleza pia hatua gani itakayofuata baada ya hapa."
  Gazeti lina taarifa kuwa baadhi ya majimbo ambako matokeo ya urais hayakutangazwa, ni Kiteto, Segerea, Muheza, Kibakwe, Kinondoni, Ilala na Moshi Vijijini.
  "Huku kwetu hatukupewa nafasi ya kushuhudia zoezi la kuhesabu kura. Kazi hiyo ilifanywa na msimamizi wa uchaguzi ambaye alisema kura za rais zitahesabiwa wilayani," anasema John Mrema ambaye aligombea ubunge katika jimbo la Vunjo kupitia CHADEMA.
  Anasema, "Lakini tulipofika katika ofisi ya mkurugenzi wa uchaguzi kule wilayani, tulimkuta msimamizi wa uchaguzi akiwa tayari na matokeo yake ya urais. Tulipomuuliza amepataje matokeo hayo wakati kura hazijajumlishwa, alikasirika na kuamua kuchana karatasi zote alizokuwa nazo."
  Akiongea kwa kujiamini, Mrema amesema, kwa ufahamu wake, mpaka sasa matokeo ya urais katika jimbo la Moshi Vijijini hayajatangazwa.
  Mbali na kuwapo kwa kasoro za majumuisho, taarifa zinasema zaidi ya majimbo 25 yaliyoshiriki uchaguzi hayakuwa na fomu za matokeo Na. 21 (A) na 24 (A).
  Aidha, masanduku 36 yaliyosheheni kura za urais, yalikutwa yamehifadhiwa katika shule binafsi ya Biafra iliyopo katika manispaa ya Kinondoni, mkoani Dar es Salaam.
  Masanduku hayo yalikutwa yakiwa na karatasi zake halisi za kupigia kura na yalikuwa bado yamefungwa kwa lakiri. Katika orodha ya masanduku hayo kulikuwa na yale yaliyotolewa kwa Kata za Tandale, Makumbusho, Mwananyamala, Kigogo na Hananasif.
  Kwa kata ya Tandale yalikuwa na namba: 162452, 162495, 1624586, 162489 na 162401. Makumbusho Na. 161330, Hananasif Na. 16871, 161051, 160958, 160165 na Kigogo Na. 160665.
  Kutoka Morogoro, taarifa zinaeleza utata wa aina yake. Kati ya wapigakura 422 waliotarajiwa kupiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Msufini, kata ya Msufini, manispaa ya Morogoro, hakuna hata mmoja aliyekuwa na shahada ya kupigia kura.
  Taarifa hizi ni kwa mujibu wa daftari la wapigakura PDF Na. 00434524.
  Katika kituo cha Shule ya Msingi Misufini B – 2, Na. 00006226 kilichopo kata ya Mafinga, kati ya wapigakura 422 ni wapigakura 192 tu ambao walikuwa na sifa ya kupigakura. Hii ni kwa mujibu wa daftari la wapigakura PDF Na. 00434425.
  Mbali na kasoro hizo, baadhi ya watu wanaonekana mara mbili katika daftari la wapigakura. Inaonyeshwa pia kuwa wana shahada mbili tofauti za kupigia kura.
  Hapa ndipo zinachipuka taarifa zinazodai kuwa kwa kupitia majina hayo, na mengine ya ambao hawakujitokeza kupigakura, ulifanyika uchakachuaji matokeo.
  Madai yamezagaa kuwa uchakachuaji kwa njia ya wale ambao hawakujitokeza kupiga kura, ama ulifanyika kupitia mawakala wa vyama vya siasa wasiowaaminifu au wasimamizi wa uchaguzi.
  Katika jimbo la Babati Mjini pekee, yamekutwa majina zaidi ya 2,000 ya wapigakura wa aina hiyo. Miongoni mwao ni Ali Khera Sumaye ambaye amekutwa na shahada mbili.
  Shahada ya kwanza ya Sumaye ambaye aliwahi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya chama cha NCCR- Mageuzi kabla ya kurejea CCM, ina Na. 12539414 na nyingine ni Na. 49947458. Taarifa nyingine zote za Sumaye, ikiwamo tarehe ya kuzaliwa zinafanana.
  Shahada zote mbili zinamuonyesha Sumaye kuwa amezaliwa 17 Agosti 1952. Taarifa zake zinapatikana katika PDF Na. 00400518 ya daftari la kudumu la wapiga kura.
  Naye Amina Abdallah Soono anatumia shahada Na. 1255139 na Na. 12557140; Anna Yakobo Masay, shahada Na. 1255831 na 12558205; Elinake Joseah, shahada Na. 26314248 na 49716656 na Jumapili Ramadhani Moromba mwenye shahada Na. 41226061.
  Katika orodha hiyo, wapigakura wengine waliokutwa na shahada mbili ni Mariam Saidi Mohamed ambaye shahada zake ni Na. 12566932 na 49773838 na Ibrahim Richard Shalua Na. 32298659 na 12557313.
  Taarifa za wapigakura hawa zinapatikana katika PDF, Na.004000518, Na.004000537 na Na. 00400534.
  MwanaHALISI limegundua pia kwamba kuna baadhi ya wapigakura ambao majina yao yamekutwa katika daftari la wapigakura, lakini picha zao zinakosekana.
  Haijaweza kufahamika iwapo wapigakura wanaoonyeshwa kuwa na shahada mbili walifanikiwa kupiga kura mara mbili au hata zaidi katika uchaguzi uliomalizika wiki iliyopita.
  Lakini katika daftari la wapigakura kunaonyesha pia kuwa katika kituo cha Serikali ya Mt. Mbuyuni – 1 Na. 00006218, kata ya Mafisa, wapigakura 57 kati ya 410 hawakuwa na shahada za kupigia kura.
  Miongoni mwa ambao hawakuwa na shahada ni Abas Ali Dunda, Abdallah Ali Matoto na Abas Majemba.
  Mbali na kasoro hizo, MwanaHALISI limegundua mkanganyiko katika idadi ya walioandikishwa kupiga kura. Kwa mfano, Mkurugenzi wa NEC, Rajabu Kilavu alinukuliwa akisema tume yake imeandikisha jumla ya watu 21,210,187.
  Hata hivyo, idadi hiyo ilipungua hadi kufikia wapigakura 19,686,608. Lakini Mwenyekiti wa Tume, Jaji mstaafu Lewis Makame alisema tume yake iliandikisha wapigakura 20,137,303.
  Aidha, imefahamika kuwa timu ya wataalamu wa teknoljia ya habari (IT) ya CHADEMA ilitembelea mtambo wa kupokea matokeo ya uchaguzi siku mbili kabla ya uchaguzi.
  Katika ziara hiyo, wataalamu hao waligundua kuwa mtambo huo haukuwa umejaribiwa kwa ajili ya kazi iliyokusudiwa.
  "Tulipowaeleza kwamba ni makosa kitaalamu kutojaribu mtambo kama huu, ndipo walipoamua kuujaribu; na mara baada ya kuujaribu, ulikwama palepale," anaeleza Mashinda Mtei, mmoja wa wataalamu wa CHADEMA waliokwenda kukagua mtambo wa NEC.
  Anasema wakati wanafanya majaribio waligundua kuwapo kwa kasoro kubwa ya kura za mgombea mmoja kuhamia kwa mgombea mwingine.
  Mara baada ya kugundua kasoro hizo, anaeleza Mtei, NEC waliahidi kurejesha Dar es Salaam kompyuta zote zilizokuwa zimesambazwa mikoani na kwamba waliahidi kufanya kazi hiyo na kuikamilisha haraka.
  Tume iliahidi kuifahamisha CHADEMA juu ya maendeleo kuhusu kompyuta hizo.
  Hata hivyo, katika hali ambayo haijaeleweka, siku hiyohiyo, tarehe 28 Oktoba 2010, Kiravu alimuandikia barua katibu mkuu wa CHADEMA akikiri kuwapo kwa ujumbe wake katika ofisi za NEC.
  Barua ya NEC yenye Kumb. Na. EA.75/162/08/99 ya tarehe 28 Oktoba inasema, "Napenda kukujulisha kwamba jana tarehe 27/10/2010, wataalam wa chama chako wa IT walikuja na kuruhusiwa kukagua mfumo wa kujumlisha kura.
  Wataalamu hao waliridhika na mfumo huo na ni matumaini yangu kwamba wamekupatia taarifa kamili."
  Barua ya Kiravu ilipokelewa CHADEMA terehe 4 Novemba 2010, siku sita baada ya uchaguzi kumalizika.
  Gazeti hili ambalo linaendelea kutunga taarifa za uchaguzi kwa makini zaidi, limeshindwa kumpata Kiravu kueleza mapungufu haya na kwa nini barua kutoka NEC kwenda CHADEMA ilichukua zaidi ya siku tano kuwafikia.
  Wakati NEC ikisema wataalamu wa IT waliotumwa na CHADEMA wameridhika na mfumo wa kuhesabia kura, taarifa kutoka ndani ya chama hicho na ambazo zimethibitishwa na Dk. Slaa zinasema wataalamu wake waliupinga mfumo huo kwa maelezo kwamba haufahamiki kwa watendaji wa NEC.
  Anasema kuthibitisha kwamba watalaamu wa chama walikuwa sahihi, zoezi la kuhesabu kura za rais na hata kumjulisha kura za wabunge ili kupata idadi ya wabunge wa viti maalum, limechukua zaidi ya wiki moja.
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Nov 19, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  uchaguzi ulikua kati ya ccm, chadema, kafu na nccr tu

  1. ccm wameshinda
  2. kafu ni wa pili visiwani - wapo tayari ndani ya mwafaka, na mtu wao kapewa kile cheo cha kukata utepe
  3. nccr in viti vichache sana
  4. chadema - ni ya pili bara... hawakati utepe wala kukagua bei za futari kama mwenzetu madevu --- wanadai wameibiwa

  hii loggerhead ni kati ya chadema na ccm na si 6-1 wala 1-1

  Nijuacho mimi, chadema si kama ilivyokua nccr wala kafu... tehy have a rather clearer strategy for this... it is just sad kwamba watanzania hatujazoea
   
 15. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #15
  Nov 19, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Isingekuwa Chadema kupoza moto wa wananchi sasa hivi wangeshadai kura zao barabarani kwa maandamano
   
 16. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #16
  Nov 19, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Acid,
  I see your point. Lakini tukumbuke hii ni siasa. Chadema wameamua kuisolve kisiasa. Hiyo 6-1 ndio jinsi mwanasiasa anayepinga uamuzi huu atakavyoichukulia. Hii strategy udhaifu wake ni kwamba lazima utafikia ukingoni. Iwapo CCM waki ignore tamko la Chadema, basi Chadema watajikuta wakirudi Bungeni huku wakiitambua serikali ya Kikwete. Hiyo itakuwa ni blow ambayo ni unnecessary, ingeweza kuepukika.
  Halafu umesema ukweli kuwa watanzania hawajaizoea hii strategy inayotumika, maana yake ni kwamba kuna risk ya kuwa na mgawanyiko kati ya wanaounga mkono Chadema, jambo ambalo nimeshaliona.
   
 17. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #17
  Nov 19, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Naona wewe unapata "great thinking capacity" kwa kusoma gazeti la mwanahalisi. Haya kila la heri, ila mimi huheshimu mawazo ya wote, great thinkers and ordinary thinkers.
   
 18. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #18
  Nov 19, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
 19. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #19
  Nov 19, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Kidhibiti ni hiki ZeMarcopolo;Kura zaidi ya 6,000 za mgombea wa TLP Augustino Lyatonga Mrema kule Vunjo ZILIINGIZWA kwenye kapu la mgombea wa CCM wakati wa majumlisho;TLP wakalalamika kuwa wana ushahidi kuwa kura za Mrema zilizo ripotiwa na MAWAKALA wao ni nyingi kuliko kura zilizotangazwa kuwa TLP wamezipata hapa Vunjo;NEC juzi wakaomba msamaha kama ni kweli "walikosea kwenye kujumlisha"

  Wakamrudishia Mrema kura zake 6,000 na kuongeza asilimia 4 zaidi kwenye ushindi wake;Kama walikosea kura za jimbo la Vunjo na hata Geita na NEC kukiri baadae kuwa"walikosea kujumlisha";Je haiingii akilini kuwa madai ya Dr Slaa yana ukweli ndani yake?

  Na kinachonisikitisha zaidi ni kuwa hadi sasa sijasikia hata Jimbo moja walilotwaa CCM then NEC ikasema"ilikosea kujumlisha"
   
 20. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #20
  Nov 19, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180

  kwa hiyo hapo inathibitisha kuwa Dr. Slaa kaibiwa kura na Rais Kikwete? Sorry, ila kidhibiti hicho kama ndio msingi wa kutokumtambua Rais basi Tanzania tusingekuwa na Rais hata mmoja.
   
Loading...