Dr. Slaa Apokelwa na Maelfu ya watanzania huko Karatu

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
159
Habari za usiku huu wana Bodi,

Kwa mujibu wa habari toka Karatu,Dr Wilbroad slaa amepokelewa kwa ndiriomo na vifijo jimboni mwake nbaada ya kushinda kesi ya uzushi iliyotolewa na watu watatu ambao walikuw wanapinga matokeo yake.Kulikuwa na Msululu mrefu wa magari,pikipiki na basikeli ambapo kwa baadaye yalifanyika maandamano .

Akizungumza katika Mkutano huo Dr. Slaa aliwahaidi watu wa jimbo lake ataendelea kukemea UFISADI na kuhakisha wale wote waliochukua pesa ya EPA wanatajwa kwa majina kabla ya kikao cha Bajeti hakijaisha.

Pia alisisitiza kuwafunga wale wote ambao walifungua kesi hiyo,na amemshangaa Tsere kuwatumia watu ili aanguke.

Watu waliokuwapo hapo ni pamoja na Tundu Lissu ambaye aliwaambia wananchi kuwa,wale wote ambao walimfungulia Dr. Slaa Kesi walikuwa wana nia ya kuwatoboa wanachi wa Karatu macho ili wasione na kuwaibia,na akasisitiza Dr. Slaa ni macho ya watanzania.
 
Last edited by a moderator:

Maneno machache sana lakini carries heavy weight .Hivi wale walio fungua kesi wako wapi sasa ? Watalipa fidia za kuendesha kesi ?Tundu kawa shujaa maana kaonyesha moto mkali .
 
Kanyaga twende Wakuu lazima kufikia 2010 tunahesabu wamebakia FISADI wangapi. Hata wale wazuri kutoka CCM tutakuwa nao tu
 
anastahili hayo mapokezi. Hongereni wana karatu kwa kujua kuchuja baina ya mchele na chuya. Wanabariadi watajifunza kutoka kwenu kuwa kura inathamani kubwa sana na hainunuliwi kwa tshirt wala pilau wala kwa noti ya elfu kumi.
 
Na nadhani nia ya Dr. Slaa Kuwataja Mafisadi katika kikao cha bajeti kitakachoanza mwezi juni ndiyo sababu hasa ya wao kumtafuta balali,sasababu wamepanga kumpakazia kuhusiana na yote yanayohusu EPA,kuna watu wataathirika ambao ni papa wadogo tu ila wana pesa na walizipata kupitia EPA.
 
Hii ni habari nzuri kwa Dr. Slaa na wapiga kura wa Karatu kwa ujumla. Hii ni tofauti sana kwa wale wananchi wa Monduli na Bariadi waliopoteza muda wao kwenda kuwashangilia watuhumiwa wa ufisadi. Kanyaga twende Dr. na kundi lako, tuko nyuma yako mkuu, hongera sana.
 
Maneno machache sana lakini carries heavy weight .Hivi wale walio fungua kesi wako wapi sasa ? Watalipa fidia za kuendesha kesi ?Tundu kawa shujaa maana kaonyesha moto mkali .

Of course wtalipa gharama za kesi na watafunguliwa kesi kama Dr. slaa alivyosema watafunga.JF mnasemaje?wawasamehe??
 
Hawa CCm walishazoea wakishindwa katika uchaguzi wanaenda mahakamani wanawanunua mahakimu wanashida kesi uchaguzi unarudiwa wanafanya ujambazi wa kura wa hali ya juu wanashinda. Na hii isiwe mwisho hakuna mtu kuenguliwa na mahakama kama ameshinda.

Congrats Dr Slaa.
 
Pamoja na kumpongeza Dr. Slaa na Shujaa Tundu Lissu, nawapongeza pia mahakimu walio endesha kesi hii ambao hawakuwa tayari kupokea peremende kwa ajili ya matumbo yao kwa garama ya haki ya wana Karatu. Bravo majaji wahusika!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom