Gembe
JF-Expert Member
- Sep 25, 2007
- 2,483
- 164
Habari za usiku huu wana Bodi,
Kwa mujibu wa habari toka Karatu,Dr Wilbroad slaa amepokelewa kwa ndiriomo na vifijo jimboni mwake nbaada ya kushinda kesi ya uzushi iliyotolewa na watu watatu ambao walikuw wanapinga matokeo yake.Kulikuwa na Msululu mrefu wa magari,pikipiki na basikeli ambapo kwa baadaye yalifanyika maandamano .
Akizungumza katika Mkutano huo Dr. Slaa aliwahaidi watu wa jimbo lake ataendelea kukemea UFISADI na kuhakisha wale wote waliochukua pesa ya EPA wanatajwa kwa majina kabla ya kikao cha Bajeti hakijaisha.
Pia alisisitiza kuwafunga wale wote ambao walifungua kesi hiyo,na amemshangaa Tsere kuwatumia watu ili aanguke.
Watu waliokuwapo hapo ni pamoja na Tundu Lissu ambaye aliwaambia wananchi kuwa,wale wote ambao walimfungulia Dr. Slaa Kesi walikuwa wana nia ya kuwatoboa wanachi wa Karatu macho ili wasione na kuwaibia,na akasisitiza Dr. Slaa ni macho ya watanzania.

Last edited by a moderator: