Dr. Slaa apewe PhD ya heshima

We can

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
678
47
Dr. Wilbroad Slaa ameonyesha ukomavu wa kisiasa, uzalendo na moyo wa Upendo kwa Taifa letu. Watu wengi walidhani kuwa angekuwa mtu mwenye tamaa ya madaraka, taifa letu leo lingelikuwa kwenye vita kali.

Dr. Wilbroad Slaa, alisema, yeye si mdini, na kweli haja hubiri udini wowote wakati wa kampeni zake. Amesakiziwa mambo mengi, akaambiwa ataleta vita, akasema hayuko tayari kuingia Ikulu kupitia damu ya wa Tanzania. Mengi yalisemwa juu yake lakini yaonekana yote ni uzushi.

Kwa mara ya kwanza ktk historia ya Tanzannia, mwanaume alijitokeza kusema ameporwa mke na Dr. Slaa lakini inaonyesha alipandikizwa, kwani ilikuwaje miaka 3 asijue mke wake yuko wapi! Yaonekana alishaaachana na mkewe huyo, au ni mhuni au mtu asiyejali familia, etc.

Dr. Slaa alionekana akicheka na kufurahi pamoja na Mh. Pinda nje ya Bunge kuonyesha kuwa hana uadui na wapinzani wake, bali sera zao. Dr. Slaa amesema anamtambua mh. Kikwete lakini hatambui taratibu zilizompa ushindi. This is very moving. Mambo ya siasa si lazima yatatuliwe kisheria, (Ref. Kenya, etc). Huu ni ustaarabu wa hali ya juu, kwani hata kama anaweza kuwa anatofautiana na mimi hapo, lakini kaonyesha ukomavu mkubwa kisiasa.

Nampenda Slaa,, nampenda Kikwete.... Mungu ibariki Tanzania. Naomba Slaa apewe Digrii ya Udaktari wa Heshima na Muungano wa Vyuo Vikuu vyote Afrika. NAWASILISHA
 
Ile ya kupora mke wa mtu inamvunjia sifa ya "heshima". Sasa vipi apewe Phd ya heshima?
 
Siamini kama kuna Chuo chochote hapa Bongo kinachoweza kuwa na ujasiri kama huo maana sasa vyuo vikuu vimeshaingiliwa na siasa! wanajua wakifanya hivyo nini kitatokea baada ya hapo maana vyuo vikuu vingi bado ni vichanga so vinaendeshwa kwa kutegemea ada za wanafunzi wao zaidi na siyo utafiti, serikali itakacho wafanyie ni kutafuta sababu yoyote na kugoma kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wanaoenda kusoma katika vyuo hivyo na huo ndo utakuwa mwisho wa hicho chuo.
 
Hilo nalo kaka! Unajua katika hali ya kawaida ni vigumu sana kwa mtu kugundua umuhimu wa Dr Slaa katika nchi yetu. Ni mtu muhimu na atakumbukwa sana na watanzania wenye kuipenda nchi yao! Tatizo letu tuna mawazo pandikizi ambayo huwa hatuyafanyii umbembuvi yakinifu. Suala la DR Slaa kusingiziwa kiupora mke wa mtu hilo haliingiii akilini mwa mtu mtu anaeitwa mpembuvi wa mambo! Kabla hujaanza kumhukumu jihukumu mwenyewe unatembea na wake za watu wangapi? au unafanya uzinzi? Suala la mapenzi ni suala la mtu bunafsi.Mkuu naungana na wewDr Slaa apewe PHD ya heshima na Africa.Nawakilisha.
 
Samahani mimi napenda kuuliza tu kaswali haka kadogo kabla Dokta Slaa hajatunukiwa hiyo PhD ya heshima!

Hivi kwanini Dr. Slaa anapoulizwa alikosana nini na wale viongozi wa kanisa hata akatoka huko huwa anakuwa mkali na kutotoa maelezo yanayojitosheleza?

Ahsante natumai nitapata jibu kwa kaswali hako kadogo!
 
Hajakosana na kiongozi yeyote na hilo lilishajibiwa na Dr. Slaa mara nyingi. Ila kama unajua alikosana nao nini basi wewe tuambie.
 
Hivi kesi imeishia wapi? Wakati wa kampeni ilikuwa inazungumza kila siku

sijui sheria hivi ukiwa mwanaume kweli mentally fit, mkeo ataondoka nyumbani kwako for over two years, can you still say she is my wife?
 
sijui sheria hivi ukiwa mwanaume kweli mentally fit, mkeo ataondoka nyumbani kwako for over two years, can you still say she is my wife?

Ungemuuliza Dr Slaa sheria za kikatoliki zinasemaje kwenye hilo?
 
Hajakosana na kiongozi yeyote na hilo lilishajibiwa na Dr. Slaa mara nyingi. Ila kama unajua alikosana nao nini basi wewe tuambie.

Je unaweza kutukumbusha alizungumziaje hilo jambo? Utakuwa umefanya jambo la mbolea sana mkuu.
 
Ile ya kupora mke wa mtu inamvunjia sifa ya "heshima". Sasa vipi apewe Phd ya heshima?

Kwa sababu amejitokeza mwenye mke au kwa sababu kapora mke wa mtu???

Anyang'anywe mtu dola alafu walioporwa mabinti na wake zao wakjitokeze tuone mtakimbilia wapi
 
Samahani mimi napenda kuuliza tu kaswali haka kadogo kabla Dokta Slaa hajatunukiwa hiyo PhD ya heshima!

Hivi kwanini Dr. Slaa anapoulizwa alikosana nini na wale viongozi wa kanisa hata akatoka huko huwa anakuwa mkali na kutotoa maelezo yanayojitosheleza?

Ahsante natumai nitapata jibu kwa kaswali hako kadogo!

Hajakosana na kiongozi yeyote na hilo lilishajibiwa na Dr. Slaa mara nyingi. Ila kama unajua alikosana nao nini basi wewe tuambie.
Nimekubadilishia rangi labda utanielewa kiini cha swali langu ili unisaidie jawabu :teeth:
 
.... Tatizo letu tuna mawazo pandikizi ambayo huwa hatuyafanyii umbembuvi yakinifu.

Naamini hata yale yaliyozungumzwa na Mhe Ben pamoja na JK kuhusu Dr. S, siku ya kuhitimisha Kampeni Jangwani yanaangukia kwenye category hiyo.
 
Back
Top Bottom