Dr. Slaa apewe PhD ya heshima

kuna watu wana hawatumii akili ya kuzaliwa! Sasa wewe Ustaadh DSM Phd ya siasa ina uhusiano gani na mambo binafsi? Au watu wote wenye Phd za heshima vitanda vyao ni visafi? Na wewe Ahamadnejad feki, hivi unautumia ubongo wako kufanya nini? Msituletee vituko vya Sokomoko na Tedi hapa. Hiki sio kigenge cha ulanzi au kijiwe cha gahawa ebo!
 
Ile ya kupora mke wa mtu inamvunjia sifa ya "heshima". Sasa vipi apewe Phd ya heshima?

Tehetehe ? kaka unafurahisha,hujui kuna viongozi wa serikali nao ndio vinara wa kupora wake za watu hadi wanawapa madaraka .Lakini Phd wanapewa za heshima. Au kwa kuwa ni wa chama chetu? au nikutajie kwa majina. Na wengine wanafumaniwa na kulipa mabilioni .
 
Dr. Wilbroad Slaa ameonyesha ukomavu wa kisiasa, uzalendo na moyo wa Upendo kwa Taifa letu. Watu wengi walidhani kuwa angekuwa mtu mwenye tamaa ya madaraka, taifa letu leo lingelikuwa kwenye vita kali.

Dr. Wilbroad Slaa, alisema, yeye si mdini, na kweli haja hubiri udini wowote wakati wa kampeni zake. Amesakiziwa mambo mengi, akaambiwa ataleta vita, akasema hayuko tayari kuingia Ikulu kupitia damu ya wa Tanzania. Mengi yalisemwa juu yake lakini yaonekana yote ni uzushi.

Kwa mara ya kwanza ktk historia ya Tanzannia, mwanaume alijitokeza kusema ameporwa mke na Dr. Slaa lakini inaonyesha alipandikizwa, kwani ilikuwaje miaka 3 asijue mke wake yuko wapi! Yaonekana alishaaachana na mkewe huyo, au ni mhuni au mtu asiyejali familia, etc.

Dr. Slaa alionekana akicheka na kufurahi pamoja na Mh. Pinda nje ya Bunge kuonyesha kuwa hana uadui na wapinzani wake, bali sera zao. Dr. Slaa amesema anamtambua mh. Kikwete lakini hatambui taratibu zilizompa ushindi. This is very moving. Mambo ya siasa si lazima yatatuliwe kisheria, (Ref. Kenya, etc). Huu ni ustaarabu wa hali ya juu, kwani hata kama anaweza kuwa anatofautiana na mimi hapo, lakini kaonyesha ukomavu mkubwa kisiasa.

Nampenda Slaa,, nampenda Kikwete.... Mungu ibariki Tanzania. Naomba Slaa apewe Digrii ya Udaktari wa Heshima na Muungano wa Vyuo Vikuu vyote Afrika. NAWASILISHA


Dr Slaa tayari ana phd yake ya kusomea darasani, sasa nashindwa kukuelewa unapoleta hoja nyepesi namna hii.:embarrassed:
 
Back
Top Bottom