nickname
JF-Expert Member
- Dec 20, 2009
- 544
- 147
Elvan Stambuli na Makongoro Oging'
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa (pichani) amepewa kazi mpya ya kuhakikisha kuwa mwaka 2015, Tanzania inaingia katika uchaguzi mkuu ikiwa na katiba mpya ya nchi.
Habari kutoka ndani ya Chadema zinasema mkakati huo ndiyo aliopangiwa Dk. Slaa ambaye alikuwa mgombea urais na kwamba, atatakiwa kuanza mara moja kwa kuhamasisha wananchi kudai katiba mpya kupitia mikutano ya hadhara, taasisi zisizo za kiserikali na hata katika vikundi vya dini.
"Ni mkakati ambao utamfanya Dk. Slaa kuwa ‘bize' pengine kuliko hata wakati wa kampeni za kuwania urais, atashirikiana na wabunge ile sehemu yenye wabunge katika mikutano na ni lazima katiba mpya ya nchi ije, mapambano haya yatakuwa nje na ndani ya bunge," alisema mpashaji wetu wa habari aliye ndani ya chama hicho aliyeomba jina lake kutotajwa kwa kuwa si msemaji.
Hata hivyo, msaidizi mkuu wa Dk. Slaa, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amethibitisha kuwepo kwa mikakati hiyo ya kushughulikia uwepo wa katiba mpya ya nchi wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
"Tunajenga ajenda moja kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu ujao (2015), unafanyika kwa mujibu wa katiba mpya na mfumo mpya wa uchaguzi… sijawahi kusimamia ajenda ikaishia njiani," alitamba Zitto.
Naye Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alithibitisha Jumamosi iliyopita kuwa, suala la kudai katiba mpya na mfumo mzuri wa uchaguzi ni moja ya ajenda yao kuu na watataka ikamilike kabla ya mwaka 2015.
"Watu wengi wanalalamikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi na hii imetokana na katiba ya nchi, tutatumia nguvu ya umma kuhakikisha katiba mpya inatengenezwa na kutumika mwaka 2015.
"Uzoefu umeonesha kuwa hata katika majimbo tuliyoshinda, nguvu za umma zilitumika, tutahamasisha watu, taasisi zisizo za kiserikali, dini mbalimbali na watu, kudai katiba mpya na mfumo mzuri wa uchaguzi," alisema Mbowe.
Alifafanua kuwa hata alipokuwa Dodoma kuapishwa aliwaambia wabunge wa Chama Cha Mapinduzi kuwa, wao (Wapinzani) wamefika hapo walipo kwa njia iliyojaa miba, milima, kokoto na mashimo, tofauti na wenzao ambao walitumia barabara ya lami.
Baadhi ya wachambuzi wa mambo ya kisiasa nchini walisema iwapo Chadema watafanikiwa katika kampeni yao ya kuandikwa kwa katiba mpya ya nchi, itakiumiza Chama Cha Mapinduzi ambacho kama chama tawala kimepewa mamlaka tena kama vile Mwenyekiti wake ambaye pia ni rais kuchagua wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi inayolalamikiwa na wapinzani.
Juzi Jumapili, Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa Chadema, Tundu Lissu alidai kuwa Jeshi la Polisi lina mkakati wa kudhoofisha chama chake baada ya kuwakatalia wabunge wao kufanya mikutano ya hadhara sehemu mbalimbali nchini na kusisitiza kuwa watafanya mikutano hiyo hata kama jeshi hilo litakataa kuruhusu, jambo lililotafsiriwa na wachambuzi wa siasa kuwa ni jino kwa jino.
Alisema jeshi la polisi katika kuwazuia kukutana na wapiga kura wao limetumia visingizio vya ‘taarifa ya intelijensia' au kwamba kuna baadhi ya vyama vya siasa ‘havina nia njema', kama sababu ya kupiga marufuku mikutano yao ya hadhara.
Aliwataja baadhi ya wabunge aliodai wamenyimwa kufanya mikutano na majimbo yao katika mabano kuwa ni Mhe. Saidi Arfi (Mpanda mjini), Annamary Stella Mallack (Viti Maalum, Rukwa), Mch. Peter Msigwa( Iringa mjini), Mhe. Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) na Mhe. Ezekiah Wenje (Nyamagana, Mwanza).
Source : Global Publishers(GPL)