Dr.Slaa apewa kazi nzito

nickname

nickname

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2009
Messages
524
Likes
66
Points
45
nickname

nickname

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2009
524 66 45
Elvan Stambuli na Makongoro Oging'
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa (pichani) amepewa kazi mpya ya kuhakikisha kuwa mwaka 2015, Tanzania inaingia katika uchaguzi mkuu ikiwa na katiba mpya ya nchi.

Habari kutoka ndani ya Chadema zinasema mkakati huo ndiyo aliopangiwa Dk. Slaa ambaye alikuwa mgombea urais na kwamba, atatakiwa kuanza mara moja kwa kuhamasisha wananchi kudai katiba mpya kupitia mikutano ya hadhara, taasisi zisizo za kiserikali na hata katika vikundi vya dini.

"Ni mkakati ambao utamfanya Dk. Slaa kuwa ‘bize' pengine kuliko hata wakati wa kampeni za kuwania urais, atashirikiana na wabunge ile sehemu yenye wabunge katika mikutano na ni lazima katiba mpya ya nchi ije, mapambano haya yatakuwa nje na ndani ya bunge," alisema mpashaji wetu wa habari aliye ndani ya chama hicho aliyeomba jina lake kutotajwa kwa kuwa si msemaji.

Hata hivyo, msaidizi mkuu wa Dk. Slaa, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amethibitisha kuwepo kwa mikakati hiyo ya kushughulikia uwepo wa katiba mpya ya nchi wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

"Tunajenga ajenda moja kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu ujao (2015), unafanyika kwa mujibu wa katiba mpya na mfumo mpya wa uchaguzi… sijawahi kusimamia ajenda ikaishia njiani," alitamba Zitto.

Naye Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alithibitisha Jumamosi iliyopita kuwa, suala la kudai katiba mpya na mfumo mzuri wa uchaguzi ni moja ya ajenda yao kuu na watataka ikamilike kabla ya mwaka 2015.

"Watu wengi wanalalamikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi na hii imetokana na katiba ya nchi, tutatumia nguvu ya umma kuhakikisha katiba mpya inatengenezwa na kutumika mwaka 2015.

"Uzoefu umeonesha kuwa hata katika majimbo tuliyoshinda, nguvu za umma zilitumika, tutahamasisha watu, taasisi zisizo za kiserikali, dini mbalimbali na watu, kudai katiba mpya na mfumo mzuri wa uchaguzi," alisema Mbowe.

Alifafanua kuwa hata alipokuwa Dodoma kuapishwa aliwaambia wabunge wa Chama Cha Mapinduzi kuwa, wao (Wapinzani) wamefika hapo walipo kwa njia iliyojaa miba, milima, kokoto na mashimo, tofauti na wenzao ambao walitumia barabara ya lami.

Baadhi ya wachambuzi wa mambo ya kisiasa nchini walisema iwapo Chadema watafanikiwa katika kampeni yao ya kuandikwa kwa katiba mpya ya nchi, itakiumiza Chama Cha Mapinduzi ambacho kama chama tawala kimepewa mamlaka tena kama vile Mwenyekiti wake ambaye pia ni rais kuchagua wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi inayolalamikiwa na wapinzani.

Juzi Jumapili, Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa Chadema, Tundu Lissu alidai kuwa Jeshi la Polisi lina mkakati wa kudhoofisha chama chake baada ya kuwakatalia wabunge wao kufanya mikutano ya hadhara sehemu mbalimbali nchini na kusisitiza kuwa watafanya mikutano hiyo hata kama jeshi hilo litakataa kuruhusu, jambo lililotafsiriwa na wachambuzi wa siasa kuwa ni jino kwa jino.

Alisema jeshi la polisi katika kuwazuia kukutana na wapiga kura wao limetumia visingizio vya ‘taarifa ya intelijensia' au kwamba kuna baadhi ya vyama vya siasa ‘havina nia njema', kama sababu ya kupiga marufuku mikutano yao ya hadhara.

Aliwataja baadhi ya wabunge aliodai wamenyimwa kufanya mikutano na majimbo yao katika mabano kuwa ni Mhe. Saidi Arfi (Mpanda mjini), Annamary Stella Mallack (Viti Maalum, Rukwa), Mch. Peter Msigwa( Iringa mjini), Mhe. Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) na Mhe. Ezekiah Wenje (Nyamagana, Mwanza).

Source : Global Publishers(GPL)
 
K

KERENG'ENDE

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2010
Messages
398
Likes
2
Points
35
K

KERENG'ENDE

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2010
398 2 35
Mchakato huu ni mzuri lakini sithani kama taarifa hizi ni rasmi.......nadhani hizi ni tetesi! mungu ibariki CDM na watu wake
 
zoeca

zoeca

Senior Member
Joined
Nov 24, 2010
Messages
124
Likes
1
Points
35
zoeca

zoeca

Senior Member
Joined Nov 24, 2010
124 1 35
embu tungoje taarifa rasmi ili tumpe kampani kamanda wetu wa mabadiliko:whoo:
 
Kigogo

Kigogo

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2007
Messages
20,562
Likes
1,583
Points
280
Kigogo

Kigogo

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2007
20,562 1,583 280
aaah Dr.bana hivi tamko lako utatoa lini mi niko standbye muda wote nasubiria tu utoe tamko ....maana kuna jizi limeiba kura na inafahamika hivyo
 
Mabel

Mabel

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2010
Messages
1,029
Likes
35
Points
145
Mabel

Mabel

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2010
1,029 35 145
Ni kweli tusubiri taarifa rasimi ya Chadema, maana kuanza kujadili hoja ambayo bado haiko rasimi sio vizuri sana. Lakini katiba mpya tunaihitaji sana watanzania japo serikali haiko tayari kuruhu hili litokee
 
Mongoiwe

Mongoiwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
522
Likes
101
Points
60
Mongoiwe

Mongoiwe

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
522 101 60
Dr. Slaa yupo Mwanza ngoja tutamuuliza kama ni kweli
 
TUKUTUKU

TUKUTUKU

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2010
Messages
11,841
Likes
49
Points
145
TUKUTUKU

TUKUTUKU

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2010
11,841 49 145
Hili ni jambo zuri sana!Mungu ibariki CHADEMA iendelee kuwepo,ikiwa na nguvu kubwa kuliko ilivyo kwa sasa,iepushe na migogoro kama iliyoikumba NCCR MAGEUZI,iepushe na mapandikizi ili ifikapo 2015 iwe CHADEMA yenye nguvu!
 
M

mama kubwa

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
2,730
Likes
2,422
Points
280
M

mama kubwa

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2010
2,730 2,422 280
kila la heri sie tunataka kazi acha wenyewe wagombanie u kuu wa mikoa chadema nyie chapeni kazi italipa tu.
 
G

Gad ONEYA

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Messages
2,641
Likes
8
Points
135
G

Gad ONEYA

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2010
2,641 8 135
Ni jambo zuri kwa Tanzania na raia wake wote, tuombe Mungu atutangulie mbele.
 
GeniusBrain

GeniusBrain

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
4,321
Likes
20
Points
135
GeniusBrain

GeniusBrain

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2010
4,321 20 135
Elvan Stambuli na Makongoro Oging'
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa (pichani) amepewa kazi mpya ya kuhakikisha kuwa mwaka 2015, Tanzania inaingia katika uchaguzi mkuu ikiwa na katiba mpya ya nchi.

Habari kutoka ndani ya Chadema zinasema mkakati huo ndiyo aliopangiwa Dk. Slaa ambaye alikuwa mgombea urais na kwamba, atatakiwa kuanza mara moja kwa kuhamasisha wananchi kudai katiba mpya kupitia mikutano ya hadhara, taasisi zisizo za kiserikali na hata katika vikundi vya dini.

"Ni mkakati ambao utamfanya Dk. Slaa kuwa ‘bize' pengine kuliko hata wakati wa kampeni za kuwania urais, atashirikiana na wabunge ile sehemu yenye wabunge katika mikutano na ni lazima katiba mpya ya nchi ije, mapambano haya yatakuwa nje na ndani ya bunge," alisema mpashaji wetu wa habari aliye ndani ya chama hicho aliyeomba jina lake kutotajwa kwa kuwa si msemaji.

Hata hivyo, msaidizi mkuu wa Dk. Slaa, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amethibitisha kuwepo kwa mikakati hiyo ya kushughulikia uwepo wa katiba mpya ya nchi wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

"Tunajenga ajenda moja kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu ujao (2015), unafanyika kwa mujibu wa katiba mpya na mfumo mpya wa uchaguzi… sijawahi kusimamia ajenda ikaishia njiani," alitamba Zitto.

Naye Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alithibitisha Jumamosi iliyopita kuwa, suala la kudai katiba mpya na mfumo mzuri wa uchaguzi ni moja ya ajenda yao kuu na watataka ikamilike kabla ya mwaka 2015.

"Watu wengi wanalalamikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi na hii imetokana na katiba ya nchi, tutatumia nguvu ya umma kuhakikisha katiba mpya inatengenezwa na kutumika mwaka 2015.

"Uzoefu umeonesha kuwa hata katika majimbo tuliyoshinda, nguvu za umma zilitumika, tutahamasisha watu, taasisi zisizo za kiserikali, dini mbalimbali na watu, kudai katiba mpya na mfumo mzuri wa uchaguzi," alisema Mbowe.

Alifafanua kuwa hata alipokuwa Dodoma kuapishwa aliwaambia wabunge wa Chama Cha Mapinduzi kuwa, wao (Wapinzani) wamefika hapo walipo kwa njia iliyojaa miba, milima, kokoto na mashimo, tofauti na wenzao ambao walitumia barabara ya lami.

Baadhi ya wachambuzi wa mambo ya kisiasa nchini walisema iwapo Chadema watafanikiwa katika kampeni yao ya kuandikwa kwa katiba mpya ya nchi, itakiumiza Chama Cha Mapinduzi ambacho kama chama tawala kimepewa mamlaka tena kama vile Mwenyekiti wake ambaye pia ni rais kuchagua wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi inayolalamikiwa na wapinzani.

Juzi Jumapili, Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa Chadema, Tundu Lissu alidai kuwa Jeshi la Polisi lina mkakati wa kudhoofisha chama chake baada ya kuwakatalia wabunge wao kufanya mikutano ya hadhara sehemu mbalimbali nchini na kusisitiza kuwa watafanya mikutano hiyo hata kama jeshi hilo litakataa kuruhusu, jambo lililotafsiriwa na wachambuzi wa siasa kuwa ni jino kwa jino.

Alisema jeshi la polisi katika kuwazuia kukutana na wapiga kura wao limetumia visingizio vya ‘taarifa ya intelijensia' au kwamba kuna baadhi ya vyama vya siasa ‘havina nia njema', kama sababu ya kupiga marufuku mikutano yao ya hadhara.

Aliwataja baadhi ya wabunge aliodai wamenyimwa kufanya mikutano na majimbo yao katika mabano kuwa ni Mhe. Saidi Arfi (Mpanda mjini), Annamary Stella Mallack (Viti Maalum, Rukwa), Mch. Peter Msigwa( Iringa mjini), Mhe. Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) na Mhe. Ezekiah Wenje (Nyamagana, Mwanza).

Source : Global Publishers(GPL)
Kweli Chama hakina hata watu wanao fikiria. Suala la katiba mpya ni mchakato na haiwezekani 2015 tukawa na katiba mpya hata malaika washuke. Hakuna nchi duniani iliyo anza mchakato wa kutengeneza katiba mpya na ndani ya miaka 5 ikawa tayari. Mtamzeesha bure mzee watu na ana machungu ya kushindwa Urais
 
GeniusBrain

GeniusBrain

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
4,321
Likes
20
Points
135
GeniusBrain

GeniusBrain

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2010
4,321 20 135
Hili ni jambo zuri sana!Mungu ibariki CHADEMA iendelee kuwepo,ikiwa na nguvu kubwa kuliko ilivyo kwa sasa,iepushe na migogoro kama iliyoikumba NCCR MAGEUZI,iepushe na mapandikizi ili ifikapo 2015 iwe CHADEMA yenye nguvu!
Waepushe viongozi wake waache Uzinifu, waache ukabila na waache udini ambao wako nao hivi sasa
 
N

Ngandema Bwila

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2010
Messages
999
Likes
5
Points
135
N

Ngandema Bwila

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2010
999 5 135
Kweli Chama hakina hata watu wanao fikiria. Suala la katiba mpya ni mchakato na haiwezekani 2015 tukawa na katiba mpya hata malaika washuke. Hakuna nchi duniani iliyo anza mchakato wa kutengeneza katiba mpya na ndani ya miaka 5 ikawa tayari. Mtamzeesha bure mzee watu na ana machungu ya kushindwa Urais
kwa ubongo huo hata ufikiri mara saba hata mara sabini hutafanikiwa. lakini kwa watu makini wanao ona mbele katiba ni swala miaka hata miwili. Zanzibar wamechukua muda gani? Umeona FFU na mabomu yao wanalinda masanduku ya kura zanzibar? . Shida ni hao wanaojua hawakubaliki lkn wanataka washinde kwa kishindo kwa kutumia TUME YAO, ASKARI WAO, MABOmu YA MACHOZI, WAKURUGENZI walio wateua wao kusimamia uchaguzi.
 
Mtumishi Wetu

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
5,142
Likes
500
Points
280
Age
66
Mtumishi Wetu

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
5,142 500 280
Kweli Chama hakina hata watu wanao fikiria. Suala la katiba mpya ni mchakato na haiwezekani 2015 tukawa na katiba mpya hata malaika washuke. Hakuna nchi duniani iliyo anza mchakato wa kutengeneza katiba mpya na ndani ya miaka 5 ikawa tayari. Mtamzeesha bure mzee watu na ana machungu ya kushindwa Urais
Think Twice kama lilivyo jina lako unaishi dunia gani? Huo muda unatosha tena saana. Usikatishe watu tamaa, kama tumedhamilia inawezekana.
Tutoe taadhari kuwa hatukwenda kwenye uchaguzi mpya 2015, bila katiba mpya, huo uwe mkakati wa Watanzania wote!!!!!!!!!!!!!
Wewe unajiweka wapi unaonekana kama haikuhusu vile?
 
L

LAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2010
Messages
4,411
Likes
17
Points
0
L

LAT

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2010
4,411 17 0
Yes sasa Chadema wanamuvuzisha mambo ...... step by step....nashukuru
 
K

Kishalu

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
948
Likes
307
Points
80
K

Kishalu

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
948 307 80
mimi nasema tu ni KATIBA KATIBA ndiyo siri ya mafanikio kwa watanzania wote

jamani watanzania tuamke kutetea maslahi ya wote walio na uelewa jaribu kuwaelimisha wale ambao hawajapata uelewa wa uhalisia wa uongozi wa serikali yetu

moz-screenshot.png
 
mfarisayo

mfarisayo

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2010
Messages
5,067
Likes
420
Points
180
mfarisayo

mfarisayo

JF-Expert Member
Joined Nov 23, 2010
5,067 420 180
Uzinifu, Ukabila na Udini vinaye yeye JK-Mteule wa NEC
 
K

Kishalu

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
948
Likes
307
Points
80
K

Kishalu

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
948 307 80
@nickname

tunataka katiba mpya na hamna anayelazimisha mchakato uishe mapema swala ni kuanza kwa mchakato wa KATIBA mpya na kuundwa tume huru ya uchaguzi ambayo haitachaguliwa na rais aliye madarakani

kuanza kwa mchakato wa kuunda katiba ndiyo mwanzo wa mafanikio na matarajio ya watanzania na kuchelewa kwa mchakato wa katiba ni kuchelewa kwa maendeleo ya watanzania jaribu kutafakari kwa makini na kuangalia baada ya miaka kumi tutakuwa wapi?
 
K

Kishalu

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
948
Likes
307
Points
80
K

Kishalu

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
948 307 80
Waepushe viongozi wake waache Uzinifu, waache ukabila na waache udini ambao wako nao hivi sasa

hapa ni ni kuelimishana na kutetea maslahi ya taifa letu acha mambo ya ubinafsi na kuongelee mtu
 
Forum statistics

Threads 1,235,846
Members 474,742
Posts 29,238,336