Elections 2010 Dr. Slaa anguruma BBC redioni: Nimeshinda Uraisi kwa kura milioni 15...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Katika mahojiano kati ya BBC na Dr. Slaa leo jioni Raisi wetu Mtarajiwa Dr. Wilbard Slaa ametuhakikishia ya kuwa ameshinda Uraisi kwa kura zaidi ya milioni 15.........

Akitoa mfano wa uchakachuajii wa CCM alisema lipo jimbo ambalo amepata kura 15,000 lakini NEC yadai alipata kura 3,000 tu.........

Dr. Slaa ameimuru NEC iache mara moja kuendelea kutangaza matokeo hayo ya Uraisi kama wanaitakia nchi hii mema..................

BBC walipomuuliza nini kifanyike Dr. Slaa alidai uchaguzi wa Uraisi ni lazima urudiwe haraka iwezekanavyo...............

Mimi hapo nipo na Dr. Slaa kwa asilimia mia moja kwa sababu uongozi unaoingia madarakani kwa dhuluma utaendesha nchi kwa dhuluma tu ni kheri tupate shida kidogo ili wapigakura tupewe heshima yetu tunayostahili ya kubadili serikali kila mara tunapoona uhaja wa kufanya hivyo....................
 
Yani mi nawashangaa sana wanaoitukuza CCM,nawaonaga hawana akili hata kidogo wala upeo wa kufikiria ni wanyang'anyi wa haki za wananchi, lakini ipo siku yatawatokea puani, mambo ya duniani tu ipo day watayaacha yote na watakufa,je wataenda wapi km si motoni?
 
rutashubanyuma usimwekee dr slaa maneno mdomoni nimesikiliza mahojiana ya dr slaa na media na sijasikia aki claim atashinda kwa kura milioni 15 and remember watanzania waliojitokeza kupiga kura wanaweza kuwa that number or bellow due to some ambao hawakujitokeza kupiga kura kutokana na majina yao kutoonekana na wenye sababu zao binafsi na wale walioharibu kura zao pls naomba tuwe tunaripoti kikamilifi mimi binafsi naamini kuna uchakachuaji matokeo ila tukianza kuzua ambayo hayajasemwa na viongozi wetu kwanza kabisa hatuwatendei haki wao binafsi na wafuasi wao!
 
Mimi nauliza hivi kuna balozi zipo Tanzania kweli?? Hawa watu wanasubiri watu waanze vurugu ndio waanze kuongea au hawaoni ni nini kinaendelea Tz. mimi nashindwa kabisa kuelewa?? Wanasubiri watu waende The Hague au ni aje?
 
Watanzania waliopiga kura mwaka huu hawafiki hata milioni 15, ina maana kura zote kazoa yeye tu. Kweli wanasiasa wetu hawako makini!
 
rutashubanyuma usimwekee dr slaa maneno mdomoni nimesikiliza mahojiana ya dr slaa na media na sijasikia aki claim atashinda kwa kura milioni 15 and remember watanzania waliojitokeza kupiga kura wanaweza kuwa that number or bellow due to some ambao hawakujitokeza kupiga kura kutokana na majina yao kutoonekana na wenye sababu zao binafsi na wale walioharibu kura zao pls naomba tuwe tunaripoti kikamilifi mimi binafsi naamini kuna uchakachuaji matokeo ila tukianza kuzua ambayo hayajasemwa na viongozi wetu kwanza kabisa hatuwatendei haki wao binafsi na wafuasi wao!
Huyu rutashubanyuma huwa ana ka unafiki fulani huwa anajifanya anamtetea Slaa kwa mlengo wa nyuma, angalia hapa kuweka figare hiyo ya uongo makusudi lengo lake likiwa Slaa aonekane anadai madai ambayo hayapo.

rutashabanyuma badailisha hiyo figure haraka.
 
Dr. Slaa anguruma BBC redioni:Nimeshinda Uraisi kwa kura milioni 15..................
Katika mahojiano kati ya BBC na Dr. Slaa leo jioni Raisi wetu Mtarajiwa Dr. Wilbard Slaa ametuhakikishia ya kuwa ameshinda Uraisi kwa kura zaidi ya milioni 15.........

Akitoa mfano wa uchakachuajii wa CCM alisema lipo jimbo ambalo amepata kura 15,000 lakini NEC yadai alipata kura 3,000 tu.........

Dr. Slaa ameimuru NEC iache mara moja kuendelea kutangaza matokeo hayo ya Uraisi kama wanaitakia nchi hii mema..................

BBC walipomuuliza nini kifanyike Dr. Slaa alidai uchaguzi wa Uraisi ni lazima urudiwe haraka iwezekanavyo...............

Mimi hapo nipo na Dr. Slaa kwa asilimia mia moja kwa sababu uongozi unaoingia madarakani kwa dhuluma utaendesha nchi kwa dhuluma tu ni kheri tupate shida kidogo ili wapigakura tupewe heshima yetu tunayostahili ya kubadili serikali kila mara tunapoona uhaja wa kufanya hivyo....................

Nimemsikia Dr BBC na ameitisha kurudiwa kwa uchaguzi wa urais kwamba kumetokea kwa udanganyifu na tuma ya uchaguzi ikome kutangaza matokeo ya uraisi kwa kuwa yanayotangazwa ni tofauti na yaliyohesabiwa maeneo yaliyopigiwa kura. pia DR anasema kila kona anapigiwa simu na wananchi wakisema waanza kuchoma matairi na akatoa mfano kule shinyanga Iringa Pia amesisitiza kuwa akiruhusu wananchi kuingia mitaani kudai haki yao nani atabaki?haitabaki CCM wala chadema wala nani kwa hiyo tume iache mara moja kutangaza kura za urais
 
Katika mahojiano kati ya BBC na Dr. Slaa leo jioni Raisi wetu Mtarajiwa Dr. Wilbard Slaa ametuhakikishia ya kuwa ameshinda Uraisi kwa kura zaidi ya milioni 15.........

Akitoa mfano wa uchakachuajii wa CCM alisema lipo jimbo ambalo amepata kura 15,000 lakini NEC yadai alipata kura 3,000 tu.........

Dr. Slaa ameimuru NEC iache mara moja kuendelea kutangaza matokeo hayo ya Uraisi kama wanaitakia nchi hii mema..................

BBC walipomuuliza nini kifanyike Dr. Slaa alidai uchaguzi wa Uraisi ni lazima urudiwe haraka iwezekanavyo...............

Mimi hapo nipo na Dr. Slaa kwa asilimia mia moja kwa sababu uongozi unaoingia madarakani kwa dhuluma utaendesha nchi kwa dhuluma tu ni kheri tupate shida kidogo ili wapigakura tupewe heshima yetu tunayostahili ya kubadili serikali kila mara tunapoona uhaja wa kufanya hivyo....................
Ukweli ni kwamba Tume inatangaza kura tofauti na zile zilizopatikana majimboni. Hii ni kutokana na ukweli wasimamizi wa uchaguzi hutuma ripoti tofauti na zile zilizotangazwa vituoni hiyo yote ni mikakati ya kuchakachua matokeo. Ningeshauri Chadema kwenda mahakamani kupinga kuendelea kutangazwa matokeo kwa haraka ili zoezi zima lirudiwe.
 
Watanzania waliopiga kura mwaka huu hawafiki hata milioni 15, ina maana kura zote kazoa yeye tu. Kweli wanasiasa wetu hawako makini!

wapiga kura mil 19.7 (source nec), Dr slaa kapata kura nyingi halali (ushaidi: mabomu yaliyopigwa nchi nzima mfano dar, mwanza, Arusha, mbeya, kigoma, kilombero, shy nk). kikwete kapata zilizobaki,nyingi zikiwa ni za kuchakachua. NEC itamtangaza kikwete rais wa JMT, what a waste of time and resources! maisha yataendelea hivyo hivyo kama yalivyokuwa kabla ya uchaguzi,wanaofuraia au kupinga wizi wa ccm wote tupo jahazi moja la ufukara, elimu mbovu, matihabu hafifu, umeme wa mgao, usafiri mbovu nk. Kama wewe unanufaika na ufisadi na unaakili angalau kidogo tu zaidi ya bata, jiulize unafurahia nini, je ni kuendesha benzi kwenye mitaa ya vumbi isiyo na taa ndani ya jiji kuu la nchi liitwalo dar? je nikumiliki nyumba ya mabilioni lakini ndani ya geti unakisima cha maji au septic tanks sababu hayo ya bomba hayaaminiki na jiji halina drainage system? je ni kumpeleka mtoto wako shuleni na hela za kununua chips maana shule haitoi lunch kwa wanafunzi wa shule za misingi? je ni kukimbilia india kutibiwa sababu nchi yako ni duni kifikira na haiwezi kutibu wananchi wake yenyewe? je ni kuwaona ndugu zako uliowaacha uswekeni bado wakitembea pekupeku bila viatu, wakiishi ndani ya nyumba za udongo na vikoroboi/vibatali? je ni kuwaona raia wema na heshima zao wakigombania dala dala au wale wanaotembea kwa miguu kwa sababu hawezi kulipa nauli?
 
Huyu rutashubanyuma huwa ana ka unafiki fulani huwa anajifanya anamtetea Slaa kwa mlengo wa nyuma, angalia hapa kuweka figare hiyo ya uongo makusudi lengo lake likiwa Slaa aonekane anadai madai ambayo hayapo.

rutashabanyuma badailisha hiyo figure haraka.

mods wanaweza kubadili hii heading kama wakitaka (i guess hawataki for now).
 
The citizen ya leo inaonyesha wapiga kura wamezidi millioni ishirini! Hebu bofya uone kwenye ukurasa wa matokeo! Ni uchakachuaji au....
 
Nakubaliana na ukweli wa kuchakachuliwa matokeo ya Dr Slaa, tuungane kupinga matokeo hayo feki ya nec na ccm yao!
 
Ndugu zangu Watanzania,Kwanza kabisa nampongeza sana Dr.Slaa kwa hatua hii ingawa wengi wanaipinga kwa sababu tayari wamekwisha fikia maamuzi ya kutokea vita au vurugu kwa sababu tu ametangaza kutokubaliana na matokeo.

Ikumbukwe tu kwamba Dr.Slaa anaitumia nafasi na haki yake ya kidemokrasia kupinga matokeo yanayototangazwa kwani hata sisi wananchi tunaosoma mafgazetini tunashindwa kuelewa ukweli ni upi. Kwa mfano, nenda mtazame mwananchi elections utakuta kura halia au waliojiandikisha ni wachache kuliko jumla ya kura zilizopigwa ktk sehemu nyingi tu na sababu haifahamiki.

Kisha tazama pia Urais ktk mkoa wa Manyara utaona jumla ya JK against Dr.Slaa lakini ukienda kwenye majimbo yake utakuta tofauti yao ni ndogo sana pengine asilimia 51 kwa 49 baina yao. Sasa ikiwa vyombo hivi wanashindwa kutoa takwimu zinazoridhisha mlitegemea vipi wananchi watakubali matokeo kwa kusikiliza NEC wanavyotangaza..

Na ikumbukwe tu kwamba wananchi wengi wamepiga kura zao AGAINST - Kikwete na sii wabunge wa CCM kama walivyomchagua Dr.Slaa zaidi na sii Wabunge wawakilishi. Kwa hiyo upo uwezekwano mkubwa wa wapiga kura kuchagua Dr.Slaa na wakamchagua mbunge wa chama kingine kuliko kumchagua mbunge wa Chadema na kumpa kura za Urais Kikwete. Huu ni ukweli ambao hauwezi kuepukika kirahisi.

Kwa hiyo ni muhimu sana kwa Dr.Slaa kuweka madai yake leo hii ili kurekebisha utaratibu mzima wa kupiga kura na uhesabuji wake uchaguzi ujao. kwani akiacha kama alivyoacha Seif Sharrif Hamad ambaye baada ya uchakachuaji amepata kura asilimia 41.1 basi mwaka 2015 mchezo wa CCM utaendelea kuwahivyo hivyo madhari Seif amekubali uchaguzi huu kuwa halali na wenye haki hali akifahamu fika kwamba uchakachuaji umetumika. Mbona mwaka 2005 alishindwa kwa asilimia kubwa zaidi na bado alipinga iweje leo kaahidiwa wadhifa iwe rahisi kwake kukubali matokeo!.

Hivyo nawaomba tuwe na mtazamo wa mageuzi badala ya kufikiria vita na Uadui baina ya vyama hivi bali ni ktk process ya kutengeneza mazingira bora zaidi kesho ktk uchaguzi ujao kwani kama tusiporekebisha leo basi mwaka 2015 mchezo utakuwa huo huo..Sina imani kubwa na ushindi wa Dr.Slaa na hata kama ameshinda CCM na system hawawezi mkubali kwa leo. Dr.Slaa kifupi anatisha! na hawako tayari kukubali kuanikwa madhambi yao, hivyo tatizo hapa linatokana na makosa ya wazi ya CCM kutafuta ushindi wa kshindo hali inajulikana wazi kwamba ushindi huo haupo.

Nitazidi kumpongeza Dr.Slaa kwa nguvu na uwezo wake kutetetea maslahi ya nchi hii kwani fundisho kwa viongozi na chama tawala hauwezi kwisha baada tu ya matokeo hata kaa yamefanyiwa uchakachuaji. Mapambano yanaendelea hadi kuhakikisha utaratibu unawekwa wazi na wenye kutoa haki kwa wananchi wanapomchagua kiongozi wao na sii chama au chombo cha serikali kuchukua dhamana ya utoaji ridhaa kwa niaba yao. Hatua hii ya Dr. ni kwa manufaa ya wagombea miaka ijayo...
 
Back
Top Bottom