Elections 2010 Dr.Slaa ANATAKIWA AANZE KUWANDAA WATANZANIA KISAIKOLOJIA KUPOKEA UTAWALA WAKE MPYA

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,780
3,227
Dr. Slaa ametuelimisha vya kutosha umuhimu wa kufanya mabadiliko ya uongozi wanchi ili kulikomboa kiuchumi, kijamii na kiuongozi taifa la Tanzania.
Mimi binafsi nimemuelewa sana na tayari nimejiandaa kupigia CHADEMA, Rais, mbunge na Diwani nimeandaa pia wapiga kura 34 watapiga chadema.Usiulize napigia kituo gani NI SIRIIIIII MOYONI.
Laikini ninaomba mnisaidie kufikisha ujumbe huu kwa Dr.Slaa na wadau wote;

  • Dr.SlAA anatakiwa kuwaweka bayana watanzania, kuhusiana na ajira zao walizonazo kwa sasa hasa serikalini, aondoe dhana iliyoanza kujengwa na CCM kwamba akiingia madarakani wakurugenzi, mameneja, wahasibu na KADA zingine watapoteza kazi. Hawa ni wapiga kura wanahitaji kuhakikishiwa usalama wa ajira zao.
  • Dr. Slaa aseme chochote ajira za askari, je muundo wa majeshi(polisi, Mmagereza, Ulinzi na usalama, usalama wa Taifa) yetu utakuwaje, na wale walioko kwenye ajira ya askari wataendelea au watapunguzwa? Hii ni muhimu kwani askari hawajaguswa na kampeni za wagombea wote.Mfano OBAMA alitoa msimamo wake kuhusu majeshi ya Iraq na AFGHAN. Kwa hiyo SLAA aachane na dhana potofu kuwa JESHI NI SIRI anatakiwa aseme askari watafaidika vipi na ujio wake na serikali mpya
  • Msimamo wake kuhusu kupeleka majeshi nje ya nchi, akumbuke kuna wanajeshi wa Tanzania wa Nchi za nje
  • Sera ya Mambo ya nje anatakiwa kusema chochote itakuwaje ndani ya siku 100 akumbuke kuna mabalozi na watumnishi wengine wote hawa wana ndugu zao TZ ambao ni wapiga kura
  • Yawezekana Luteni SHIMBO anachokoza baada ya kuona Dr.Slaa hajaongelea majeshi you never know, may be they want to hear the position of Dr.Slaa on ARM MATTERS
Naamini akigusa na haya atakuwa ametukonga zaidi.

Let him set the ball rolling
 
watanzania bila kuandaliwa wanaonekana wapo tayari kabisaaaaaaa
 
Mawazo mazuri sana haya, thank you,huu ujumbe ni muhimu sana, nani aufikishe directly kwa Dr ili aanze kuweka wazi maeneo hayo?

Walio karibu naye please act!
 
Asante kwa mada nzuri, Mnjika na kundi lake najua mnasoma humu. Naomba pelekeni kwa Dr. Slaa suala hili.
 
Jamaa ameongea kitu ni lazima haya mambo yafahamike mapema ili watu wajipange!
 
Hayo yanapaswa kuja siku ya mwisho ya kampeni yake ili kutokuwapa CCM nafasi ya kupindisha ukweli na kuhadaa wapigakura.

CCM kwa mkakati anaondolea nao Dr. Slaa umewapagaisha na hawajui wafanye nini. Inabidi aendelee vivyo hivyo. Watumishi wengi serikalini wameichoka CCM kuna dhuluma kubwa inaendelea nadi ya watumish serikalini na wengi wao wala hawahitaji kubwa zaidi ya kumwona JK anadhalilishwa ka vile alivyozoea kuwadhalalisha.

Hata kuna makatibu wakuu wanne niliosoma nao wameniumasikio ya kuwa watashukuru CCM ikiondolewa madarakani hata kama na wao wataathirika potelea mbali.

Tatizo la kuwahakishia watu ajira ni ngumu kwani CCM watasema hivi ni mageuzi gani anaahidi wakati anataka kulamba makombo ya CCM?
 
Back
Top Bottom