Dr. Slaa anatafutwa kujibu maswali yafuatayo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa anatafutwa kujibu maswali yafuatayo.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Gwallo, Nov 9, 2010.

 1. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,319
  Likes Received: 840
  Trophy Points: 280
  Jana nillikuwa katika jimbo la uchaguzi la karatu na nilikutana na watu wengi wenye maswali yafuatayo.

  1.Je matokeo yaliyotangazwa na tume nec yanatofauti gani na matokeo kwenye vituo?

  2.Je Dr. Slaa alishindwa ktk uchaguzi uliopita? kama ndiyo jibu ni ndiyo kwa kiasi gani cha kura kama ni laa kwa kiasi gani cha kura?

  3.Je wachungaji na maaskofu walioenda kumpoza Dr. Slaa ndiyo wapiga kura pekee yao? na je nani anayehitaji kupozwa ni wananchi waliathirika na matokeo hayo au Dr.Slaa?

  4.Je Dr.atazungumza na wanachi lini? kauli yake ndiyo jibu pekee la kutufariji katika wakati huu wa majonzi makuu ya janga la matokeo ya uchaguzi.

  Pamoja na kujitahidi kuwaelimisha wananchi hao walioonekana wana jazba kuwa Dr.Slaa anajipanga namna ya kukabiliana na hili bado hawakuridhika. Kitakacho weza kupoza mioyo ya wananchi hawa ni Dr. Slaa kutoa ufafanuzi juu ya yaliyojiri kipindi cha uchaguzi na namna ya kupita katika kipindi hiki kigumu cha miaka 5.............Wadau nawasilisha.


   
 2. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli mie binafsi nimekata tamaa nasubiri tamko lale bila mafanikio
   
 3. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama hawataki makubwa wawaulize wazee wa NEC hayo maswali 2 ya juu
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,173
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. K

  Kachest Senior Member

  #5
  Nov 9, 2010
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani wewe hujui kuwa 61.17% alizopata JK ndo zilikuwa za Dr. Slaa
   
 6. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,319
  Likes Received: 840
  Trophy Points: 280
  This is more serious that you think.
   
 7. S

  SUWI JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wavute subira...... za mwizi 40!!!
   
 8. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
 9. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,319
  Likes Received: 840
  Trophy Points: 280
  Wale watu huwezi kwenda kuwaambia ushauri unaotoa hapa kwenye hiyo attachment hawatakuelewa, wanajua jambo moja kwamba Dr.Slaa alijitokeza kwenye vyombo vya habari kusema kura zinazotangazwa na tume haina uhusiano na matokeo ya kura ya vituoni,wanachota ni kuambiwa tofauti hiyo imetoka wapi na nini hatima ya tofauti hiyo.
   
 10. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hapo kweli pamekuwa pagumu. Sasa ndugu yetu Slaa hakuna kingine zaidi ya kwenda kuongea nao kwa sababu inaonekana yeye wanamuamini na watamsikilize akiwapa mwongozo.
   
 11. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Inawezekana kabisa hiyo 61% ilikuwa ni ya SLAA ila Kiruvi alichanganya majina kama alivyokili mwanzo kuwa alichanganya pia kutaja badala ya Nyangwale akatanganza ya Geita..lol.Ila tukimkumbusaha anaweza akabadili na kutoa matokeo yaliyo halisi zaidi na yaliyomategemeo ya wengi zaidi.:israel:
   
 12. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #12
  Nov 9, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ukweli ni kwamba tume ya uchaguzi kwa makusudi kabisa imeamua kutuchagulia viongozi. Baada ya kuona majimbo mengi ya awali yananyakuliwa na chadema, tume iliamua kwa makusudi kuchelewa kutangaza matokeo ya majimbo mengine. Jimbo la segerea licha ya vituo 36 kutohusishwa katika kuhesabu kura, bado matokeo ya msingi yalipotoshwa na tume bila woga ilisema wanaopinga waende mahakamani. Hali imekuwa hivyo kwa majimbo yote yaliyocheleweshwa matokeo, yote yameangukia kwa ccm. Kuthibitisha kwamba tume ilifanya kusudi kuharibu matokeo, majimbo ya musoma mjini na musoma vijijini, matokeo ya kura za uraisi yanazidi za wagombea ubunge kwa zaidi ya kura 20,000. Kwa tume hii na katiba hii, haki haitokuwepo ni bora jeshi lichukue nchi.
   
Loading...