Dr. Slaa anasema atauza saruji kwa shilingi elfu tano…kiwanda anacho? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa anasema atauza saruji kwa shilingi elfu tano…kiwanda anacho?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngurudoto, Sep 26, 2010.

 1. N

  Ngurudoto JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 208
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wasira: Msiuze urais kwa 20,000/-

  MG O M B E A ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Bunda, Steven Wasira amewataka Watanzania wasifanye majaribio na kubahatisha katika kuchagua urais kwa sababu mamlaka hayo ni makubwa na yanastahili kukabidhiwa kwa mtu mwenye akili timamu na chama cha maana.

  Aidha, amehoji kwa vipi Watanzania wanaweza kununua urais kwa Sh 20,000, akihusisha na kauli ya mgombea urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa aliyekaririwa akisema akishinda, atafuta ada katika shule nchini.

  Kwa sasa, ada kwa shule za sekondari za kutwa za serikali ni Sh 20,000 wakati elimu ya msingi hakuna ada. Kwa elimu ya chuo kikuu, serikali inatoa mikopo.

  Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni mjini Bunda mbele ya mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, Wasira alisema urais ni mamlaka makubwa ambayo Watanzania hawapaswi kuyafanyia majaribio.

  “Mwisho nataka kutoa ushauri kwa watu wa Bunda, Mkoa wa Mara na kwa Watanzania wote. Kwa mujibu wa Katiba yetu, mamlaka ya kiongozi wa serikali huchaguliwa na wananchi.

  Rais ni mamlaka makubwa,” alisema. “Ndiye anayetangaza vita, kwa hiyo usiende kubahatisha, wala msifanye mambo ya kubahatisha, kujaribu.

  Ni lazima mchague mtu mwenye akili timamu, anayetoka chama cha maana. Mwalimu Nyerere alisema Rais anaweza kutoka chama chochote, lakini Rais bora atatoka CCM.”

  Huku akishangiliwa na wananchi, mwanasiasa huyo ambaye pia ni maarufu kwa jina la Tyson, alisema Watanzania ifikapo Oktoba 31, mwaka huu, hawapaswi kuchagua Rais wa kubahatisha, wa kudanganya na msema uongo.

  “Mtu anasema atauza saruji kwa shilingi elfu tano…kiwanda anacho?

  Bei ya mafuta inapangwa duniani na ina uhusiano na mataifa mengine katika masuala ya uchumi, yeye atamudu vipi,” alihoji Wasira ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika.
   
 2. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Kuna kazi sana ktk upinzani hapa Tanzania,Baada ya mwaka na NGAI ndo bei itapunguaaaa...
   
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #3
  Sep 26, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Wasira, mbona saruji kutoka Pakistani ni bei rahisi sana hata kutishia kuua viwanda vya nyumbani, Inakuwaje iwe bei poa na hapa nyumbani tushindwe kuuza kwa elfu tano. Kutoka Pakistani hadi Dar kuna freight charges, tax, and other associated cost, lakini mfuko bado ni rahisi kuliko Twiga cement, hujiulizi tu mheshimiwa!
  Tangu mwaka 1978 hatujapigana vita tena, sasa Wasira unaposema ndiye anatangaza vita, vipi hivyo unavyohisi au kujua vitatokea. Kwanini usiseme Rais ndiye anasimamia uchumi wa nchi unaohusu maisha ya watu kila siku. Hapa unataka kuwatisha watu,maana hata JK alisema Moshi watu wakichagua upinzani ni vita, akarudia Tarime watu waangalie nchi jirani, akimanisha vurugu za kenya zimeletwa na wapinzani.
  Hizi ni siasa za maji taka, kuwatisha watu wazidi kuteseka baada ya miaka 49. Kuwadanganya watu amani na utulivu wakati Wake zao wakijifungulia juu ya matenga ya baiskeli ili hali wake zao na watoto wao wakizunguka na ndege za serikali Kutafuta kura. Amani na utulivu upo wapi kwa mtu anayeshindia uji usio na sukari, kupewa panadol kwa kugongwa na nyoka, kuacha shule ili mtoto ateke maji na wakiume akimbize ndezi kama kitoweo.
  Kenya imewezekana, Zambia imewezekana, Malawi imezekana, Tanzania is next if we all stand together and say enough is enough.
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kikwete anamwita Wassira ni TYSON yaani mpiganaji asiyetumia akili. hata wanawake dhaifu anawaweka masumbwi tu!
   
 5. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2010
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Hamjagundua,Tyson ni CHADEMA halisi.Ndio maana alisisitiza achaguliwe mtu mwenye afya na akili timamu.Hapo kuna mwingine zaidi ya Dr.Slaa?Hatudanganyiki mwaka huu.Chadema hoyeeeeee?
   
 6. B

  Bibi Ntilie JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 245
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wassira hajui kwamba wako wananchi Tanzania hii ambao hata hiyo 20,000/= kuipata ni kwa mbinde. Yale yale ya mwenye shibe...?
   
 7. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sikufahamu, kumbe mjomba wangu anatudanganya ni sisiemu kumbe chadema!, Kesho nitamuuliza, asiponijibu.........!?'*:;?
   
 8. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Wasira ni ndumila kuwili alipotoka CCM akawa anaikandia vibaya sana, leo kapewa ulaji anakandia upinzani.Hana lolote zaidi ya kuwa mnafiki, mlafi , mchoyo na mbinafsi. Kwanza sura yenyewe...mmm!..,.. from Congo forets!
   
 9. Z

  Zhu Senior Member

  #9
  Sep 26, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Opposition is to go against;taking weakness of the otherside.
  A politician always takes advantage of that. Put any negative post to any party. They usualy become mad becouse they expect positive towards themselves and negative towards other party.
   
 10. c

  chambuyar New Member

  #10
  Sep 26, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi ni porojo za uchaguzi ambazo Kikwete ndiyebingwa zaidi wakuzitoa.Tumwulize Kikwete hela kuwajengea waathirika wa mafurikio Kilosa atazitoa wapi? Na "Je hii ina maana wale wote watakaoathirika na majanga takuwa anafanya hivyo?
  . Mbona Kigamboni bado wanalia hadi leo.
   
 11. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ndiyo wale wale wanaopinga sera ya elimu bure eti wakisema itaifilisi Serikali, watu hao hao hawajawahi kukaa chini na kujiuliza ni kiasi gani cha pesa serikali inahitaji ili Elimu yetu iwe bure mpaka form six
   
 12. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  TzPride umenichekesha sana hapo kwenye red! Dah, ni kweli kabisa. Anatisha!!
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Fedha za mbwembwe na majigambo zipo mingi, lakini ukitamka mambo ya shule wanaona kama unawatukana!...Wanaogopa sana mtu akiongelea elimu bure,maana wanahofia watz wakielimika watajua haki zao, na kuwamwaga!./..
  Bei ya sementi inaweza kushuka kabisa na kukaribia kwenye 5000,maana material zote zipo nchini!..wasione hiyo ni hatari!...hiyo ni mbinu ya kuwablind watu kwa kukwepa kuwa holistic katika kuelezea mambo!....shame on them!
   
 14. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #14
  Sep 26, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  yaani nimemdharau sana wasira kama ni kweli katoa kauli hiyo, nilikuwa naamini ni msomi mwenye utashi wa kupambunua mambo kwa kina lakini kumbe nilikuwa nakosea sana.

  Kauli yake ya kugusia suala la vita na mamlaka ya rais ni dhahiri alikuwa na nia ya kutumia unyonge wa wananchi kielimu kuwapandikizia hofu katika kufanya maamuzi yao. Na hii ni silaha kubwa ambayo ccm inajitahidi kwa nguvu zote kuieneza.
  Pili suala la saruji kuuzwa shs. 5000 linawezekana kabisa endapo serikali ina nia madhubuti ya kuwasaidia wananchi wake, wassira ajiulize kwanini cement ya kutoka pakistani inauzwa kwa bei rahisi ndani ya nchi yetu kuliko cement yetu?
   
 15. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  tuwaache hao wapige debe tu hapo....

  Tanesco unanunua nguzo ya umeme wewe kwa TShs 1,500,000/= halafu eti siyo yako, akija mtu hapo pembeni anapewa umeme bure je huo sio utawala mbovu... Nguzo hizo hizo zinaenda Kenya na kule ni Tshs. 250,000/= je huo sio wizi?????

  sukari inatoka Brazil inauzwa TZ Tshs 850/= ya hapa Tshs. 1600/= kwa nini?

  JK ameweka kodi nyingi sana ndiyo maana bidhaa za hapa bei ziko juu......

  Jeshini bia ni Tshs. 600 / = uraiani ni 1,500/= kwa nini??? kodi nyingi kwa watanzania...


  Tanzania bila ya CCM inawezekana....
   
 16. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  Yale yale ya VIJISENTI
   
 17. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,461
  Likes Received: 789
  Trophy Points: 280
  Wagombea ubunge walio wengi wa CCM roho zao ni za CHADEMA lakini mkate wanataka kwa CCM ,watose waache unafiki,hawana lolote la kuendeleza taifa letu,ni mizigo mizito kama zebaki (mercury).Hakisha wapinzani wa dhati wananyakua viti vya ubunge asilimia 55,Kuwakumbatia hawa watu ni kukumbatia ufukara ujinga,ulimbukeni,ulofa,unafiki.Miaka mingine mitano itapotea.Nguzo ya bunge ni muhimu kwa mabadiliko ya kuleta maendeleo ya dhati kwa wananchi walio wengi.Tumeonewa kiasi cha kutosha,tumenyonywa na wakoloni weusi kiasi cha kutosha,tumenyanyaswa kiasi cha kutosha,tumedanganywa kiasi cha kutosha,sasa tunasema basi,siraha yetu muhimu ni kura yako.
   
 18. Mntambo

  Mntambo Member

  #18
  Sep 26, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Yale yale ya mwenye shibe hamjui mwenye njaa. Imeandikwa kwamba kilio cha mnyonge humfikia Mungu naye humsikia. Tuboreshe maisha yetu watanzania kwa kuchagua upinzani!
   
 19. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #19
  Sep 26, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Huyo nae ni mgonjwa hamuioni sura yake kama nanasi!!
   
 20. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #20
  Sep 26, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  waomi wa CCM wengi wanaganaga njaa zao tu ,wala hawajali masilahi ya taifa,
  Ni aibu sana kuwa na wasomi kama hawa
  ni bora kabisa kutokuwa nao
   
Loading...