Dr. Slaa anasa nyaraka za siri za CCM za kuingiza silaha nchini

Naona machine ya Lister Peter (Tanzania daima) inaendelea kumwaga pumba, hivi ni kweli Dr Slaa anaweza kutamka uupzi wa aina hii au wakati anazungumza sukari ilikuwa imepanda?
Tulia dogo mbona unaweweseka na mipovu kukutoka kila kona
 
Hii hali inatishia sana usalama wa nchi. Kama siasa chafu zinaendelea kushamiri hapa nchini, basi hatuwezi kuhepuka vita vya wenyewe kwa wenyewe pasipo msingi.
 
Nashauri Dr apelekwe haraka sana India au German kwa wale wafadhili wetu ili tatizo la Epilepsy lipatiwe tiba. Haki ya nani Dr anaanza kuwehuka..
 
huu ni ujinga,uongo na uzushi mtakatifu.mwenye uwezo wa kuagiza silaha hapa nchini ni jeshi na polisi tu.yale makontena ya CUF yaliyokuwa na VISU yako wapi??yale makontena yalikuwa na kura kutokea msumbiji uako wapi???slaa acha cheap popularity,umechuja wewe.
Hivi ile sinema ya Darwins nightmare iliwahusu polisi na jw?
 
uongo wa kwanza ni pale alipodanganya kanisa kuwa atatii sheria za mungu matokeo yake akaasi.
pili alipoaminiwa na ROSE kamili matokeo yake akamtelekeza yeye pamoja na watoto akaanza uzinifu na Josephine

uongo mwingine ni huu kwamba CUF wameingiza kontena la visu na lile la kura kule mpakani na msumbiji

Policcm mnaufinyu wa kufikiri,hayo ni matatizo ya mazoea.
 
Tunataka kweli mabadiliko lakini si kwa watu wa namna hii kuanzia katibu,wabunge ,mpaka wajumbe wenyewe.
 
Wakuu,
Gazeti la Tz daima leo limeibuka na taarifa ya Dr Slaa kudai kuwa anazo nyaraka za siri za ccm kuagiza na kuingiza silaha kwa ajili ya vijana wa ccm waliowekwa ktk makambi mbali mbali hapa nchini. Lengo la vijana hao ni kudhibiti Chadema. Dr Slaa anasema tunaposema kuwa ccm imedhamiria kufanya vurugu hatutanii, tuko serious.
wakati huo huo,
Gazeti limeelezea pia kwa urefu maelezo ya Dr Slaa na msafara wake kufuatiliwa ktk operesheni yake ya M4C na gari lisiloeleweka. Kufuatilia hali hiyo Dr Slaa aliwaagiza idara ya ulinzi kutoa taarifa polisi ktk wilaya husika lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyiwa kazi.
Gazeti pia lilimpigia simu Nape Nnauye kuhusu madai hayo naye akakana. Akifafanua Nape alisema, Dr Slaa mwongo mbona makontena ya kura za wizi alizosema zimeingizwa nchini hazijaonekana?

My take.
Nape, absence of evidence is not evidence for absence of evidence. Kutokuonekana kwa ushahidi si ushahidi wa kubatilisha mashitaka. Je, kama makontena hayo yamefichwa baada ya siri kuvuja ni nani ajuaye? Ukizingitia kuwa polisi wetu wameshakuwa policcm.

Mkuu Aweda unajua kwanini idara ya ulinzi ya CDM haijachukua hatua yeyote? ebu tafakari na fuatilia maneno ya mtu mzima siku hizi.
 
hawa chadema sasa wanaboa...kila kukicha wana habari hii mara wana ushahidi mara wana majina ya watu flani kama hamuwezi kusema hivi vitu hadharani basi ni bora mkae kimya...mnaogopa nini...maana kama kuonewa mtaendelea kuonewa tu hata mkikaa kimya so ni bora muongee tajeni majina leteni ushahidi kama hamuwezi basi kaeni kimya....
 
slaa anazeeka vibaya sasa,ona uzushi wake mwingine huu.

Hivi umekosa Id huru ya kutumia hadi utumie ubongo wa mwenzako T2015 CDM kupata ID!
Sasa watakuja wengine na T2015 CUF, T2015 TLP, T2015 UDP nk nk.
Mtatuchanganya wasomaji wenu.
 
UPDATE,
HABARI KAMILI HII HAPA KWA UREFU NIMEI UDATE MAIN THREAD AS WELL.

Aituhumu kuingiza nchini silaha kimyakimya
*Asema lengo lake ni kutaka kuihujumu Chadema
KATIBU Mkuu wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, kwa mara nyingine tena ameibua tuhuma nzito dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dk. Slaa amedai kuwa, anazonyaraka zinazoonyesha namna chama hicho tawala kinavyoingiza silaha nchini zikiwamo bunduki bila vibali wala kuzikatia leseni.

Dk. Slaa alisema, CCM inaingiza silaha hizo na kuwapatia vijana wake waliowekwa katika kambi maalumu, kwa ajili ya kufundishwa mbinu za kuwashughulikia wapinzani wao kisiasa hususan
Chadema.

Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana mjini Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea tathmini ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), pamoja na Operesheni Sangara iliyoanza mkoani hapa Agosti 8 mwaka huu.

“Kwa hapa Morogoro mjini tunazo taarifa, tumeshaambiwa kuna vijana kama 10-20 wa CCM wanaandaliwa kufanya njama za kuhujumu CHADEMA.

“Watavalishwa kombati kama hizi za kwetu, watafanya fujo ili ionekane ni sisi, wamepewa sumu, tindikali na sindano kwa ajili ya kukamilisha hizo hujuma wanazopanga dhidi yetu.

“Kwa baadhi yetu tunaowafahamu CCM, hili si suala jipya, walifanya hivyo hivyo wakati wa uchaguzi mdogo Igunga, moja ya kambi yao ilikuwa Ilemo na Iramba.

“Huu ndio mtindo wao, wana tabia ya kuingiza hata bunduki nchini bila kibali wala leseni wanapatia vijana, kisha wakishafanya hivyo wanajiandaa kuhamishia tuhuma
CHADEMA.

“Mtakumbuka Wilson Mukama (katibu mkuu CCM) aliwahi kutamka wakati ule tukiwa Igunga kuwa, tumeingiza makomandoo nchini, alisema hadharani.

“Kumbe wao tayari wameshaweka vijana kambini na wanafundisha, tena waliohusika kufundisha ni polisi na usalama wa taifa. Tulitoa taarifa polisi juu ya masuala yote na ushahidi tukawapatia wafuatilie, lakini mpaka leo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa,” alisema Dk. Slaa.

Dk. Slaa alisema kuwa, chama chake hakitatoa taarifa polisi juu ya njama hizo za vijana kuandaliwa na wala hakina mpango wowote wa kuishitaki CCM kwa njama za kukihujumu.

Dk. Slaa alisema, kufanya hivyo ni sawa na kupeleka kesi ya nyani kwa ngedere, ingawa alisisitiza kuwa wakati utakapofika wataweka hadharani nyaraka hizo.

Aliongeza kuwa, kudhihirisha CCM hawatanii katika kutaka kufanya vurugu, hivi karibuni kumekuwa na matukio ya msafara wao kuandamwa na watu wasiojulikana.

Dk. Slaa alisema, watu hao wamekuwa wakitumia magari tofauti na kueleza kuwa, juzi wakiwa wanatoka Gairo, Gari lenye namba T886 AVS aina ya Prado lilikuwa likiwafuatilia.

“Juzi walifanya hivyo tukiwa Mvomero tukatoa taarifa Polisi jana na leo asubuhi tumepata taarifa ambazo hatuwezi kuzipuuza kuwa, kuna vijana kuanzia 10-20 wakiwa na Sumu Sindano pamoja na visu, wanawawinda watu walio katika operesheni kwa ajili ya kuwadhuru, ”alisema Dk Slaa.
 
uongo wa kwanza ni pale alipodanganya kanisa kuwa atatii sheria za mungu matokeo yake akaasi.
pili alipoaminiwa na ROSE kamili matokeo yake akamtelekeza yeye pamoja na watoto akaanza uzinifu na Josephine

uongo mwingine ni huu kwamba CUF wameingiza kontena la visu na lile la kura kule mpakani na msumbiji

Policcm mnaufinyu wa kufikiri,hayo ni matatizo ya mazoea.
 
Slaa amesahau hao ni poiliccm wakishirikiana na usalama wa taifa?Unajua kwa wenzetu warusi na nadhani waisrael huwa wanaselect watu wao kwa kuangalia hata uwezo wa kiakili sio huku mtoto wa mjomba,shangazi alifeli peleka huko naye apate kazi.Shida sana.
 
Wasomjua dr slaa wanitafute,sisi huwa tunamwita slahama ,maaana yake ni aina ya wazimu ktk lugha ya kwao .kwasababu ya kuzusha mambo na kuchonganisha jamii.na kumbuka kisa kimmoja aliwahi kuzusha karatu kuhusu maji,watu wakataka kuuana mungu kaweka mkono wake.hatufui mtu huyu hata kidogo.ebu fikiri wasomi wote wana kazi zakufanya ,kina profesa lipumba,prof mwandosya,mabere marando nk ni wasomi na wanatumikia taaruma zao siasa kwao kama ziada,huyu bwana udoctor wake umesaidia nini watanzania ?.yeye kila kukicha uongo ,visa,mikasa mtafutieni kazi .
 
Nashauri Dr apelekwe haraka sana India au German kwa wale wafadhili wetu ili tatizo la Epilepsy lipatiwe tiba. Haki ya nani Dr anaanza kuwehuka..

Mkuu umenichanganya hapa,
kati ya mtu anayesema kuna xx ameingiza silaha kijambazi na huyo jambazi ambaye tuliwahi kumjua kuwa ni mtu mwenye heshima huko nyuma, ni nani wa kupima epilepsy?
 
huu ni ujinga,uongo na uzushi mtakatifu.mwenye uwezo wa kuagiza silaha hapa nchini ni jeshi na polisi tu.yale makontena ya CUF yaliyokuwa na VISU yako wapi??yale makontena yalikuwa na kura kutokea msumbiji uako wapi???slaa acha cheap popularity,umechuja wewe.

duh..shule ya kata hizi.SASA NDO HAO WAMEAGIZA AFU WASEME NI CHADEMA.AKILI UMEWEKA PEMBENI KWA AJILI YA KUUTETEA MFUMO UNAOKUPA KULA.
 
Wasomjua dr slaa wanitafute,sisi huwa tunamwita slahama ,maaana yake ni aina ya wazimu ktk lugha ya kwao .kwasababu ya kuzusha mambo na kuchonganisha jamii.na kumbuka kisa kimmoja aliwahi kuzusha karatu kuhusu maji,watu wakataka kuuana mungu kaweka mkono wake.hatufui mtu huyu hata kidogo.ebu fikiri wasomi wote wana kazi zakufanya ,kina profesa lipumba,prof mwandosya,mabere marando nk ni wasomi na wanatumikia taaruma zao siasa kwao kama ziada,huyu bwana udoctor wake umesaidia nini watanzania ?.yeye kila kukicha uongo ,visa,mikasa mtafutieni kazi .

Hapo kwenye Red umezusha kupita kiasi,

Sema lingine, wakati huo nilikuwepo Mbulu jirani kabisa. Hilo sakata nalifahamu. Maji yalimpa umaarufu Dr Slaa karatu ccm wakafanya ujuha wao wa kutaka kuhujumu mabomba ya maji ili kumpunguzia umaarufu. Walishindwa.
Pili, katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani hana kazi - atafute kazi? Chama chenye waajiriwa kibao? Chenye madiwani na wabunge!
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kimedai kukamata nyaraka za siri za uingizwaji wa silaha kutoka nje unaodaiwa kufanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwadhuru, huku wakieleza kuwa na taarifa zaidi ya vijana 20 wakiwa na sumu,tindikali,sindano wamepangwa pia kuwadhuru viongozi wa chama hicho wanaofanya operesheni sangara inayoendelea nchi nzima.

Akizungumza na Waandishi wa habari mkoani Morogoro jana, Katibu mkuu wa Chadema Dk. Willbrod Slaa, alidai kuwa silaha hizo zimeingizwa nchini kwa kushirikiana na vyombo vya usalama kwa lengo la kuwafanyia vitendo vya kinyama viongozi wa chama hicho.

Alitaja baadhi ya silaha hizo ni bastola ambazo watapewa kundi la vijana linaloandaliwa na CCM ili kuwadhuru viongozi wa Chadema ambao watakaokuwa katika mikutano mbalimbali ya M4C ikiwa ni njia mojawapo ya kukidhoofisha chama hicho.

Alisema Chadema kupitia kitengo chake cha Interejinsia wamebaini kuwa CCM wameingiza silaha bila kulipia ushuru na kwamba nyaraka wanazo pindi zitakapohitajika watazitoa.

Alitolea mfano njama kama hizo ziliwai kufanywa katika uchaguzi wa jimbo la Igunga mkoani Tabora ambapo moja ya kambi hizo za vijana iliwekwa Iramba Magharibi na kwamba vijana waliandaliwa ili kufanya vurugu katika mikutano ya kampeni ya Chadema.

“Hivi sasa Morogoro, tumepata taarifa kuwa kuna kundi la vijana zaidi ya 20 ambao watavalia sare kama za Chadema wakiwa na sumu, tindikali, sindano na visu ili kuwadhuru viongozi na wanachama wa Chadema ili wananchi wajue kuwa waliofanya hivyo ni wafuasi wa Chadema,” alisema Dk. Slaa.

my take

Tanzania tumefika huko kweli????No I dont believe, sumu,tindikali,visu, bastola?????
 
jamani hebu tuache haya mambo hivi watu mnaomba vita eeh! haya wengi watakufa kwa stail manake kila siku njama za kuuwawa anjama za kudhoofishwa wewe ni nani hadi uuwawe? na kwanini tutumie hadi visu na bastola za kauagiza zilizopo nchini hazitosh kuwachinja na kuwaua ? tindikali zilizopo kwenye ma duka ya vifaa vya maabara hazitosh hadi tuagize?
 
Back
Top Bottom