Dr. Slaa anasa nyaraka za siri za CCM za kuingiza silaha nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa anasa nyaraka za siri za CCM za kuingiza silaha nchini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, Aug 21, 2012.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Aug 21, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  Gazeti la Tz daima leo limeibuka na taarifa ya Dr Slaa kudai kuwa anazo nyaraka za siri za ccm kuagiza na kuingiza silaha kwa ajili ya vijana wa ccm waliowekwa ktk makambi mbali mbali hapa nchini. Lengo la vijana hao ni kudhibiti Chadema. Dr Slaa anasema tunaposema kuwa ccm imedhamiria kufanya vurugu hatutanii, tuko serious.
  wakati huo huo,
  Gazeti limeelezea pia kwa urefu maelezo ya Dr Slaa na msafara wake kufuatiliwa ktk operesheni yake ya M4C na gari lisiloeleweka. Kufuatilia hali hiyo Dr Slaa aliwaagiza idara ya ulinzi kutoa taarifa polisi ktk wilaya husika lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyiwa kazi.
  Gazeti pia lilimpigia simu Nape Nnauye kuhusu madai hayo naye akakana. Akifafanua Nape alisema, Dr Slaa mwongo mbona makontena ya kura za wizi alizosema zimeingizwa nchini hazijaonekana?

  My take.
  Nape, absence of evidence is not evidence for absence of evidence. Kutokuonekana kwa ushahidi si ushahidi wa kubatilisha mashitaka. Je, kama makontena hayo yamefichwa baada ya siri kuvuja ni nani ajuaye? Ukizingitia kuwa polisi wetu wameshakuwa policcm.

  UPDATE,
  HABARI KAMILI HII HAPA KWA UREFU

  Aituhumu kuingiza nchini silaha kimyakimya
  *Asema lengo lake ni kutaka kuihujumu Chadema
  KATIBU Mkuu wa
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, kwa mara nyingine tena ameibua tuhuma nzito dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Dk. Slaa amedai kuwa, anazonyaraka zinazoonyesha namna chama hicho tawala kinavyoingiza silaha nchini zikiwamo bunduki bila vibali wala kuzikatia leseni.

  Dk. Slaa alisema, CCM inaingiza silaha hizo na kuwapatia vijana wake waliowekwa katika kambi maalumu, kwa ajili ya kufundishwa mbinu za kuwashughulikia wapinzani wao kisiasa hususan
  Chadema.

  Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana mjini Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea tathmini ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), pamoja na Operesheni Sangara iliyoanza mkoani hapa Agosti 8 mwaka huu.

  "Kwa hapa Morogoro mjini tunazo taarifa, tumeshaambiwa kuna vijana kama 10-20 wa CCM wanaandaliwa kufanya njama za kuhujumu CHADEMA.

  "Watavalishwa kombati kama hizi za kwetu, watafanya fujo ili ionekane ni sisi, wamepewa sumu, tindikali na sindano kwa ajili ya kukamilisha hizo hujuma wanazopanga dhidi yetu.

  "Kwa baadhi yetu tunaowafahamu CCM, hili si suala jipya, walifanya hivyo hivyo wakati wa uchaguzi mdogo Igunga, moja ya kambi yao ilikuwa Ilemo na Iramba.

  "Huu ndio mtindo wao, wana tabia ya kuingiza hata bunduki nchini bila kibali wala leseni wanapatia vijana, kisha wakishafanya hivyo wanajiandaa kuhamishia tuhuma
  CHADEMA.

  "Mtakumbuka Wilson Mukama (katibu mkuu CCM) aliwahi kutamka wakati ule tukiwa Igunga kuwa, tumeingiza makomandoo nchini, alisema hadharani.

  "Kumbe wao tayari wameshaweka vijana kambini na wanafundisha, tena waliohusika kufundisha ni polisi na usalama wa taifa. Tulitoa taarifa polisi juu ya masuala yote na ushahidi tukawapatia wafuatilie, lakini mpaka leo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa," alisema Dk. Slaa.

  Dk. Slaa alisema kuwa, chama chake hakitatoa taarifa polisi juu ya njama hizo za vijana kuandaliwa na wala hakina mpango wowote wa kuishitaki CCM kwa njama za kukihujumu.

  Dk. Slaa alisema, kufanya hivyo ni sawa na kupeleka kesi ya nyani kwa ngedere, ingawa alisisitiza kuwa wakati utakapofika wataweka hadharani nyaraka hizo.

  Aliongeza kuwa, kudhihirisha CCM hawatanii katika kutaka kufanya vurugu, hivi karibuni kumekuwa na matukio ya msafara wao kuandamwa na watu wasiojulikana.

  Dk. Slaa alisema, watu hao wamekuwa wakitumia magari tofauti na kueleza kuwa, juzi wakiwa wanatoka Gairo, Gari lenye namba T886 AVS aina ya Prado lilikuwa likiwafuatilia.

  "Juzi walifanya hivyo tukiwa Mvomero tukatoa taarifa Polisi jana na leo asubuhi tumepata taarifa ambazo hatuwezi kuzipuuza kuwa, kuna vijana kuanzia 10-20 wakiwa na Sumu Sindano pamoja na visu, wanawawinda watu walio katika operesheni kwa ajili ya kuwadhuru, "alisema Dk Slaa.
   
 2. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,120
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  dhuluma haiwezi kuishinda haki
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Slaa achana na kuitegemea Polisi wala usalama wa Taifa kwa usalama wako na familia yako mimi ni mmoja wa watu ambao siwategemei tena Polisi na usalama wa Taifa kwa usalama wangu na Familia yangu, nimeamua kuwategemea na kuwekeza zaidi katika ulinzi binafsi, wee unategemea mtu kama Dr Ulimboka asingebweteka kuwategemea Polisi kwa ulinzi wake yangemkuta yaliyomkuta? Au nchi ingekuwa kweli ina watu wa usalama leo hii ingeshindwa kuyakamata mabilioni yaliyowekwa na mafisadi Uswisi?
   
 4. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,634
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Naona machine ya Lister Peter (Tanzania daima) inaendelea kumwaga pumba, hivi ni kweli Dr Slaa anaweza kutamka uupzi wa aina hii au wakati anazungumza sukari ilikuwa imepanda?
   
 5. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Magazeti ifikie hatua muwe mnaelewa aina ya majibu mtakayopata wakati wa kuthibitisha habari kabla hata ya kuuliza. Ukimuuliza Nape issue yoyote ya Dr Slaa lazima ataweweseka na kutoa majibu ya ku-panic, heri wangeruka kwa mwenye mbwa Mukama mwenyewe aliyewahi kutuletea ushahidi wa maghaidi toka Libya na Pakistani walioingia Igunga.
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Sipati picha Chama cha Mabwepande wakiwa wapinzani,sasa unapita pale mnazi mmoja unakuta wale waganga njaa wamekaa wanasubiri amri waende kupiga domo mitaani na kuzua mikutano kwa kuwabeba wananchi na pesa ndogo ndogo(kama wataweza tena)....watakimbiana hawa wanafiki wote tutawaona live maana sasa wanajificha kwenye kutoa povu
   
 7. MZIMU

  MZIMU JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 4,080
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  MAWEEEEEEEEEE!!!! Jamani haya sio yale Mambo ya Mstaafu NGUNGURI Kua chama cha kina YAKHEEE KIMEINGIZA MAKONTENA YA MAJAMBIA KUVURUGA AMANI. NA SAMPLE TUKA ONYWESHWA. YAANI WAO MAJAMBIA POLISI BUNDUKI. JAMANI?
  LEO TENA CHICHIEM WANAANDAA VIJANA WOA. YAANI WAPAMBANE NA JW AU POLISI? MMMMHHHH! AMAKWELI SISI WADANGANYIKA.
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Aug 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu jana aliibuka na thread humu kwamba kuna silaha zimeletwa kwa ajili ya kuwabambikia CDM. Naona Mods waliifuta. Haya mambo ya kutishana na silaha si mazuri. Dr. weka mambo hadharani isije ikawa ni kama ile signature ya Ritz hapa JF
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #9
  Aug 21, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  It's beleavable.
   
 10. t

  thatha JF-Expert Member

  #10
  Aug 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  slaa anazeeka vibaya sasa,ona uzushi wake mwingine huu.
   
 11. t

  thatha JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  yule mzee wa vimwana ana uchu sana na urais,yaani hadi leo haamini kuwa alishindwa kwenye uchaguzi mkuu uliopita kwa hiyo kila siku anaibuka na uzushi mpya.wajinga ndio wadanganyikao
   
 12. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kurasa 1 kati ya 3
  [​IMG]Dk. Wilbrod Slaa

  *Aituhumu kuingiza nchini silaha kimyakimya
  *Asema lengo lake ni kutaka kuihujumu Chadema
  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, kwa mara nyingine tena ameibua tuhuma nzito dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Dk. Slaa amedai kuwa, anazonyaraka zinazoonyesha namna chama hicho tawala kinavyoingiza silaha nchini zikiwamo bunduki bila vibali wala kuzikatia leseni.

  Dk. Slaa alisema, CCM inaingiza silaha hizo na kuwapatia vijana wake waliowekwa katika kambi maalumu, kwa ajili ya kufundishwa mbinu za kuwashughulikia wapinzani wao kisiasa hususan Chadema.

  Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana mjini Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea tathmini ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), pamoja na Operesheni Sangara iliyoanza mkoani hapa Agosti 8 mwaka huu.

  “Kwa hapa Morogoro mjini tunazo taarifa, tumeshaambiwa kuna vijana kama 10-20 wa CCM wanaandaliwa kufanya njama za kuhujumu CHADEMA.

  “Watavalishwa kombati kama hizi za kwetu, watafanya fujo ili ionekane ni sisi, wamepewa sumu, tindikali na sindano kwa ajili ya kukamilisha hizo hujuma wanazopanga dhidi yetu.

  “Kwa baadhi yetu tunaowafahamu CCM, hili si suala jipya, walifanya hivyo hivyo wakati wa uchaguzi mdogo Igunga, moja ya kambi yao ilikuwa Ilemo na Iramba.

  “Huu ndio mtindo wao, wana tabia ya kuingiza hata bunduki nchini bila kibali wala leseni wanapatia vijana, kisha wakishafanya hivyo wanajiandaa kuhamishia tuhuma CHADEMA.

  “Mtakumbuka Wilson Mukama (katibu mkuu CCM) aliwahi kutamka wakati ule tukiwa Igunga kuwa, tumeingiza makomandoo nchini, alisema hadharani.

  “Kumbe wao tayari wameshaweka vijana kambini na wanafundisha, tena waliohusika kufundisha ni polisi na usalama wa taifa. Tulitoa taarifa polisi juu ya masuala yote na ushahidi tukawapatia wafuatilie, lakini mpaka leo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa,” alisema Dk. Slaa.

  Dk. Slaa alisema kuwa, chama chake hakitatoa taarifa polisi juu ya njama hizo za vijana kuandaliwa na wala hakina mpango wowote wa kuishitaki CCM kwa njama za kukihujumu.

  Dk. Slaa alisema, kufanya hivyo ni sawa na kupeleka kesi ya nyani kwa ngedere, ingawa alisisitiza kuwa wakati utakapofika wataweka hadharani nyaraka hizo.

  Aliongeza kuwa, kudhihirisha CCM hawatanii katika kutaka kufanya vurugu, hivi karibuni kumekuwa na matukio ya msafara wao kuandamwa na watu wasiojulikana.

  Dk. Slaa alisema, watu hao wamekuwa wakitumia magari tofauti na kueleza kuwa, juzi wakiwa wanatoka Gairo, Gari lenye namba T886 AVS aina ya Prado lilikuwa likiwafuatilia.

  “Juzi walifanya hivyo tukiwa Mvomero tukatoa taarifa Polisi jana na leo asubuhi tumepata taarifa ambazo hatuwezi kuzipuuza kuwa, kuna vijana kuanzia 10-20 wakiwa na Sumu Sindano pamoja na visu, wanawawinda watu walio katika operesheni kwa ajili ya kuwadhuru, ”alisema Dk Slaa.
   
 13. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #13
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kama tunakaribisha siasa chafu, basi tutegemee vita mbaya ya wenyewe kwa wenyewe.
   
 14. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #14
  Aug 21, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  Umeenda vituo vya polisi ktk wilaya husika ili kujua kama ni kweli taarifa hizo zimepelekwa au la!
  Je, una uhakika kiasi gani kwamba hizo nyaraka hana! Nyaraka za EPA mlisema hivyo, hivyo, mkaumbuka baadaye.
  Hebu tupe, ameshasema kweli mara ngapi na uwongo mara ngapi ili ushawishi jukwaa hili likuamini wewe.
  Unadhani kwanini watz wanamwanini sana mpaka akachakachuliwa kura? je, kwa kuwa ni mkweli au ni mzushi?
   
 15. Ally Kanah

  Ally Kanah JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 1,433
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  ZZK kweli ni jembe aliwahu kuwaambia viongozi wenzake wa CHADEMA wabakize akiba ya maneno sasa leo inaonekana KIBABU KIBACHELA kimeishiwa hakina jipya hii single ya leo inabidi akaifanyie remix
   
 16. t

  thatha JF-Expert Member

  #16
  Aug 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  huu ni ujinga,uongo na uzushi mtakatifu.mwenye uwezo wa kuagiza silaha hapa nchini ni jeshi na polisi tu.yale makontena ya CUF yaliyokuwa na VISU yako wapi??yale makontena yalikuwa na kura kutokea msumbiji uako wapi???slaa acha cheap popularity,umechuja wewe.
   
 17. Ally Kanah

  Ally Kanah JF-Expert Member

  #17
  Aug 21, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 1,433
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Ajipange akaifanyie hii single remix kwa kweli haijatubamba SLAA hoiii au ndio Mama Jounior kampa hii Single
   
 18. d

  danizzo JF-Expert Member

  #18
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  LAANA ZA MKE WAMTU ZINA MSUMBUA MR SILAHA! Tehe!
   
 19. t

  thatha JF-Expert Member

  #19
  Aug 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  uongo wa kwanza ni pale alipodanganya kanisa kuwa atatii sheria za mungu matokeo yake akaasi.
  pili alipoaminiwa na ROSE kamili matokeo yake akamtelekeza yeye pamoja na watoto akaanza uzinifu na Josephine

  uongo mwingine ni huu kwamba CUF wameingiza kontena la visu na lile la kura kule mpakani na msumbiji
   
 20. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #20
  Aug 21, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Majibu ya Nape ni swadakta Dr Slaa ni muongo mkubwa, mwizi, mnafiki, msaliti, na ugonjwa wa kisukari umeathiri ubongo wake kwa sehemu kubwa.
   
Loading...