Dr Slaa ana kwa ana na Mama Salma Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa ana kwa ana na Mama Salma Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Jun 16, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Mama Kikwete akihutubia.
  [​IMG]
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, akiwa amemshika mtoto mchanga baada ya kukabidhiwa na wazazi wake baada ya ushuhuda walioutoa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya Fistula- Tanzania. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT, Dk. Wilbroud Slaa.
  [​IMG]
  Shuhuda wa ugonjwa wa FISTULA, Beatrice Mlunga (kulia) akitoa ushuhuda wa matatizo aliyoyapata ya ugojwa Fistula wakati wa uzinduzi huo. Kushoto ni mume wake, Hosea Sanga.
  [​IMG]
  Mke wa Rais NaMwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete (mwenye miwani ) akiponyeza kitufe kuzindua kampeni hiyo.
  [​IMG]
  Mjomba Mpoto akiwatumbuiza waalikwa wakati wa Uzinduzi.
  [​IMG]
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa na wasanii wa Kikundi cha Mrisho Mpoto pamoja na wafanyakazi wa CCBRT wakati wa uzinduzi.
  [​IMG]
  Wasanii wa kikundi Mpoto wakifanya maigizo.
  [​IMG]
  Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi huo.Picha na Mwanakombo Juma-MAELEZO
  Hii ilikuwa ni Uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya FISTULA Tanzania, uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar eSalaam Juni 15 2012, Uzinduzi rasmi umefanywa na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete. Mradi wa Fistula kwa mwaka inakadiriwa wastani wanawake wapya 2,500 hadi 3000 hupatwa na ugojwa huo wakati wanapojifungua. Kwa sasa wanawake zaidi ya 31,000 inasemekana wanalo tatizo la Fistula hapa nchini, Hivyo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametoa wito wakina mama wenye matatizo ya Fistula kumuacha kujificha kwani unatibika .hivyo waende katika matibabu ambayo hupatikana ktk hosp. ya CCBRT jijini DSM na hosp, ya Kilutheli ya Selian.


   
 2. T

  Tewe JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  So what?
   
 3. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Tupo pamoja kuijenga nchi yetu, ila tuwe na dhamira za dhati katika mioyo yetu.
   
 4. M

  Masabaja Senior Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna tatizo mbona wote ni watanzania kama kuna jambo la kufanya pamoja ni sawa lakini ikifika mahali kutofautiana na kwa maslai ya taifa siyo tatizo kutofautiana, na kutofautiana kwa itikadi siyo uadui tudumishe umoja lakini tusiache kutofautiana kwa fikra ndiyo chimbuko la maendeleo. Kwa hiyo Slaa kuwa na mama Kikwete hakuna tatizo.
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  mbona leo sio mara ya kwanza!
   
 6. B

  Bob G JF Bronze Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Dr Slaa Uongozi ni kuwatumia watu kwa moyo endelea kuwa mfano Kamanda
   
 7. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,732
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Ubarikiwe dk' jaman nani kama dk' tz hii,. Watanzania wote tunakupenda dk unaemchkia dk ikifika 2015 uame nchi urudi tena 2025,. Hahahahaaa
   
 8. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  cha ajabu ni nini?
   
 9. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,746
  Trophy Points: 280
  Tanganyika kwanza vyama baadae, vyama vitapita bali Tanganyika itaendelea kuwepo.
   
 10. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Afya ya Doctor inapendeza! tunakutegemea sana 2015 doctor!
   
 11. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Nadhani mtoa mada alikuwa na dhamira safi kuelezea uma kuwa pindi inapokuja kwenye suala la watanzania tunaweka upinzani kando tunaungana pamoja, big up dk n salma
   
 12. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Duuu mama Salma Kikwete hongera wewe pamoja na Mzee mlipima ingiwa majibu bado ni kitendawili!!
   
 13. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Sawa iyo..DR ur alwayz on ma mind.
   
Loading...