Dr. Slaa amsimamisha kazi Katibu wa CHADEMA Nzega | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa amsimamisha kazi Katibu wa CHADEMA Nzega

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by nngu007, Apr 20, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Wednesday, April 20, 2011

  Na Mustapha Kapalata, Nzega

  KATIBU MKUU wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)Dkt,Willibrod Slaa amemsimamisha kazi katibu wa wilaya ya Nzega wa chama hicho Sunny Yohana katika kikao kilichofanyika jana katika ukumbi wa chanel one uliopo wilayani hapa.

  Dkt,Willibrod Slaa ambaye yupo mkoani Tabora akiendelea na Ziara yake ya kikazi ya Chama hicho akianzia Tabora mjini,Bukene,Nzega na leo akiwa hutubia wananchi wa wilaya ya Igunga na kuendelea na wilaya zilizo salia Mkoani hapa.


  Dkt,Willibrod amefikia maamuzi hayo ya kumsimamisha kazi katibu huyo wa wilaya baada ya kupokea malalamiko mengi yautendaji kazi wake katika kikao hicho cha wanachama wa chama hicho ambacho kilikuwa kama hukumu ya katibu huyo kufuatia uongozi wake katika Ngazi ya wilaya.


  Mambo ambayo yalichangia kuenguliwa kwa muda katika kiti hicho nipamoja na kutokuwa na ushirikiano na umoja wa vijana na baadhi ya wanachama ambao walikuwa wakimshutumu kwa kuwa na ubinafisi.


  Wanachama hao walisema mbele ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt,Willibrod kuwa katibu huyo amekuwa akiukataza umoja wa vijana kufanya mikutano ya ndani na hata ile ya nje jambo ambalo lilimshangaza Katibu huyo Mkuu wa chama hicho.


  Wakiendelea kubainisha wanachama hao juu ya utawala wa Sunny Yohana walisema alisubutu hata kusimamisha michango ambayo ilikuwa akitolewa na wanachama hao ilikupata mfuko wa chama hicho,hata hivyo chama hicho kwa sasa hakina hata akaunti ya kutunzia fedha.


  Pamoja na hayo jambo ambalo liliochangia kwa kiasi kikubwa kumsimamisha katibu huyo nipale aliwasilisha hati ya bajeti ambayo ilighalimu maandalizi ya ujio wa msafara wa Katibu Mkuu wa chama hicho.


  Akikabidhi hati hiyo yenyezaidi ya Tsh, laki 4 kwa mkurugezi wa msafara huo ndipo alipo anza kuuwasirisha kwa wanachama hao na kuonekana kunaubadhirifu mkubwa wa fedha hali ambayo ilimfanya Dkt,Willibrod kutoa tamko hilo la kumsimamisha kazi kwa muda usiofahamika mpaka pale tume ya taifa itakapo kuja kufanya uchunguzi zaidi juu ya tuhuma hizo.


  Kwa upande Sunny alisema ameyapokea vizuri maamuzi hayo ya Katibu Mkuu kuwa ilichama kiendelee mambo kama hayo hutokea kuajibishana katika chama,akiendelea kusema kuwa bado yumwana chama na anamapenzi na chama hicho.


  Alisema kwa Tamko hilo ingawa hakupewa hata muda kidogo wa kujitetea juu ya tuhuma hizo na kuuangushia mzigo kwa umoja wa vijana kumuundia njama za kumtengua cheo hicho.


  Dkt,Willibrodi alimteua Peter Piusi kuwa katibu kaim wilaya wa Chama hicho mpaka pale tume maalumu itakapo fanya uchunguzi.


  Katibu kaim wa chama hicho alisema ameipokea vizuri nafasi hiyo na ameahidio kutoa ushirikiano mkubwa kwa wanachama,hata hivyo aliuomba ushirikiano wa kutosha kwa wadau hao ilikuweza kukiweka sawa chama hicho ambacho kilionekana kukosa muelekeo katika medani ya kisiasa wilayani hapa.


  Kwaupande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Omary Shaabani Omary alisema kusimamishwa kwa katibu hiyo nimoja ya pengo kwa chama hicho kulingana na utendaji kazi wake,


  Amemtaka kaim Katibu wilaya kujitolea kwa nyakati zote ilikurudisha imani kwa wanachama pamoja na wananchi akiongezea alisema kuwa kuachana na makundi ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kukigawa chama hicho.


  Katibu Mkuu akitoa maagizo kwa wana Chama wake ni pamoja na kuachana na mambo ya kukigawa chama kwa njia ya udini ama ukabila hali ambayo inaweza kuhatarisha amani hapa nchini.


  Alisema kwa kashifa hiyo ambayo ilikuwa imeenezwa na baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini na sumu hiyo kuenea kote nchini ni vema ikatoweka mara moja na wananchi wakaendelea na mapenzi na vyama vyao kama jinsi ilivyo kuwa hapo awari.


  Akiendelea kutoa maagizo hayo alisema kanda ya Mkoa wa Tabora nimoja ya kanda zilizo pangwa kuzishugulikia na kukieneza chama hicho hasa katika ngazi ya vijiji na ngazi ya kata huko ndipo kwenye mapungufu.


  Alliwataka wana Chama hao kutoa ushirikiano kwa viongozi wa liowachagua na kuwa kitu kimoja ilikujenga chama bora na kuwa na imani kwa wananchi ambao wanatazama kujiunga na chama hicho.
   
 2. Du Bois ideas

  Du Bois ideas JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Najua Dr. haangalii magamba kwanza, yeye huwa ni makini wakati wote. Endelea kujenga chama Dr. Hasa Tabora!!!
   
 3. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Safi dr fanya kazi tuko nyuma yako,.asante kwa taarifa hii,mkuu:A S 465:
   
 4. z

  zamlock JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  safi sana maamzi mazuri ndani ya chama awekwe pendeni uchunguzi ndiyo ufanyuke akuna mjadala dr pambana ujenge chana ndiyo kazi uliyibaki nayo uku tukikusubiria uingue ikulu ufanye mambo zaidi
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Naweza kuwa na fikra tofauti kidogo na uamuzi wa Katibu Mkuu wa Chadema kumsimamisha Katibu wa Chadema wa wilaya ya Nzega. Si vizuri kutumia jukwaa kutolea maamuzi mazito ni hatari kwa uhai wa wanachana na viongozi wao. Bora angetulia na kuvumilia kidogo hadi ujumbe wa kitaifa kuja kufanya uchunguzi na kumpa nafasi ya kujitetea. Sina maana ya chama kufuga wabadhilifu wa mali za chama au wanaoweka mipasuko ndani ya chama, bali kutumia taratibu nzuri za kisheria zinazokubalika na kulinda heshimna ya mtu.

  Kuna matukio kadhaa hata kipindi cha kampeni alifanya hivyo kutolea maamuzi jukwaani kitu ambacho kisaikoloji inaweza kumharibu mhusika hata kabla ya kufanya uchunguzi kwa taratibu za kichama. Katika hilo Katibu Mkuu Dr. Slaa anatakiwa kuwa mwangalifu maana busara inatakiwa kutumika zaidi katika nafasi kama hiyo. Na tujue binadamu si 100% ni kamili la hasha, kila mtu ana mapungufu yake, na kwa hilo mimi namshauri kuwa mwangalifu kadiri ya mtazamo wangu.
  Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko
   
 6. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Candid Scope,
  Leo tunamtuhumu JK kwa kuwataka watuhumiwa wa ufisadi wajivue magamba ndani ya siku 90. Ni kushindwa kwa uongozi kuwa na uamuzi. Yaani ufisadi ufanyike mbele yangu, licha ya tuhumu zilizoelezwa na waliolaklamika. Kisha nimwache aendelee kuua chama? Uongozi ni kufanya maamuzi kwa wakati kuepuka mdhara zaidi au kulenga manufaa ya uamuzi huo. Ndivyo nilivyofundishwa uongozi. Uongozi legelege usio na maamuzi ndio uliotufikisha hapa tulipo. Mhusika alipata nafasi ya kujieleza hapo hapo, lakini maelezo yake hayakuridhisha hasa kwa kuwa ufisadi ni "documentary" na kwa kawaida kwa documentary evidence huhitaji ushahidi zaidi.

   
 7. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Haya maamuzi ya ghafla yamekuwa ya kawaida. Shitambala alituhumiwa akaweka kando baadae akarejeshwa. Upo uwezekano wa mtu yoyote kuzushiwa majungu na kuwekwa kando. Hivi katiba ya chama inasema juu ya mtu kuvuliwa au kusimamishwa madaraka? Ukiangalia jamaa analalamika kuwa hata nafasi ya kujitetea hakupewa. Huu ulikuwa ni mchezo wa Lowasa pia kwa ajili ya popularity. Kwamba tuhuma zinafikishwa kisha mtu anavuliwa hapo hapo. Ndio demokrasia kweli hii. Huenda hii ikawa inapatikana Tanzania tu. Na hapa ndio watu wanakuwa wanakituhumu CHAMA kuwa ni cha watu wachache maana too centralised. Hivi Mkoa maamuzi yake yanaanzia wapi!!!
   
 8. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #8
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Anfaa,
  Get your facts correct. Shitambala "hakuwekwa pembeni na baadaye kurudishwa". Shitambala alijiuzulu kwa hiari yake kupisha "uchunguzi wa Tuhuma ya kuiuza jimbo". Kwa mujibu wa Katiba uongozi una mamlaka ya kukubali au kukataa kujiuzulu kwake na kumrejesha wakati uchunguzi unaendelea. Ni mazingira tofauti sana. Soma pia maelezo yangu katika reply ya awali.


   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa vile mimi siijui katiba ya Chama cha Chadema nafyata mkia, maana nafikiria jambo kama hilo alihitaji kupata ushirikiano toka kwa viongozi wengine, isije kesho wakasema mwenye maamuzi ni Slaa kutokana na matuko kama haya, na hivi baadaye mambo yakienda kinyume atabeba lawama peke yake.
  Na katika nafasi kama ile huwa watu wana jazba na kumbe ukitulia na kufuatilia baadaye unaweza kugundua kwamba si yote yaliyosemwa ni kwali ingwa kuna baadhi yenye ukweli.

  Tunapenda mabadiliko ila Dr. jaribu kuwa flaxable kupata maoni ya watu kwa ajili ya kujenga chama chenye nguvu kwa busara zaidi na umoja wa hali ya juu.

  Labda ungetumia nafasi ya kumsimamisha kwa ustaarabu baada ya kuongea naye ukimwita ofisini, lakini katika halaiki kama ile hapana Dr. inaumiza na pengine inaweza toa picha ambayo si sahihi.
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Dr. W. Slaa heshima kwako na hongera kwa jitihada kubwa unazofanya kuelimisha umma. Ushauri tunaokupa ni kutoka kwenye moyo mwema kabisa ili kusaidia kujenga zaidi chama cha Chadema.

  Mtakatifu Benedicto alipokuwa anawafundisha wanafunzi wake juu ya kusahihishana katika jamii alisema. Kuweni na uangalifu katika kusahihi maana vyombo vingine vina kutu na hivyo ukiparuza sana vitatoboka.

  Kumbuka viongozi wengi wa vyama vya upinzani hawana uzoefu wa uongozi, kwa maana hiyo unatakiwa uzungukie huko kuwapa darasa, na ni matumaini yangu wengi watajifunza mengi kutokana na uzoefu wako katika masuala mambalimbali ya kijamii, kisheria, kiutamaduni na kisiasa.  Walipo wawili au watatu wamekusanyika kwa jina langu ................
   
 11. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Scope

  Ukiwa nje huwezi kujua nini kilichopo ndani. Nzega ilitakiwa siku nyingi iangukie upinzani. Katika mikoa ambayo cdm hawakuinvest lakini wamepata viti vya udiwani ni Tabora. Ninaamini kuwa Dr. Slaa angeweza kufanya kama unavyofikiria kama angekuwa mkweli. Baada ya kuiona hii post nimepigia jamaa yangu mwanaharakati wa pale NzEGA tena hupo Mgodini;
  • aliambiwa alisema wachangiaji wa chama kutoka mgodini ni mafisadi, ushahidi hana kisa Caspian inamilikiwa na RA,
  • Kwenye ujio huu wa jumatatu anaomba gharama zilizotumika ilhali hizo gharama wanachama wa pale ndo wamechanga. Hizo laki nne ni za wapi?
  Haya mawili pamoja na mabango yalioanzia kwenye mkutano wa hadhara pamoja na zile shutuma kwamba anakataza vikao vya ndani kwa nini asichukuliwe hatua? Mpaka chama kife? bora hio timu ije na hata mimi nitaenda nzega kutoa ushahidi wangu wa madudu wakati wa uchaguzi mkuu.

  Kwanza kabisa aniambie ile form ya matokeo ya urais ipo wapi????
   
 12. G

  Guraa Member

  #12
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Excellent!!!!!!!!!!!!!!!! Hiyo ndiyo falsafa ya nguvu ya umma, ili tusije tukawa na viongozi miungu watu kama mapacha watatu
   
 13. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Dr. huyu huyu alimsimamisha KAFULILA....! kumbe wana ajenda ya SIRI...! SISI YETU MACHO
   
 14. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  nimeipenda signature byako tu mkuu!

  BILA RUSHWA..HAKI HAIPATIKANI....TOA RUSHWA UPATE HAKI.....(?)
  RUSHWA NA TANZANIA DAM-DAM.....!
  TAASISI IPI RUSHWA KWAO MWIKO?
  NASEMA KWA KUWA YAMENIKUTA......!
   
 15. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Dr ni vizuri ukafuata utawala wa Sheria na sio ubabe. Kwani huyo katibu alikuwa na haki kabisa kisheria kupewa nafasi ya kujitetea mbele yako au kamati kabla kufikiwa maamuzi ya kusimamishwa.

  Kwa staili hiyo ya Ubabe na kutofata Utawala wa Sheria unanitia mashaka sasa kama nchi utaiweza.
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu hebu msome Dr hapa chini....
   
 17. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #17
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,246
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono kwa asilimia zote dr Slaa na rais makini mtarajiwa! Huruma za kijinga na siasa zakimakundi/uswahiba ndivyo vinavyo mtafuna kikwete leo hii! Nasema Slaa usisikilize mashinikizo ya vibaraka wa chama cha magamba! Tumia taratibu na kanuni za cdm. P....poweeeeeerrrr!
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hivi ukiwa kiongozi na mtu anakuambia wametumia mamilioni kujenga barabara ya Bagamoyo (Waziri Nalaila Kiula?) utabaki bado unasema kuwa mtu ajitetee?

  Mtu ananunua Kivuko kibovu, Rada mbovu, Ndege mbovu nk na unataka mtu eti apewe muda ajitete?

  Kuna vitu vya kujitetea ila kuna vingine hakuna haja ya kumpa muda ajitetee.

  Alitakiwa kuwa ameshaanza kufuatilia hilo jambo zamani na siyo anakumbuka shuka wakati kumekucha na anaomba apewe muda ajitetee kwanini hakutumia shuka.

  Sasa wee mtu anadai maandalizi ya sherehe katumia laki nne na ukiangalia hakuna kilichofanywa............

  Hebu ona hawa yaliyowakuta:

  JUKWAA LAO LAANGUKA
  Wakati huo huo, Chiligati na Nape wamejikuta wakipigwa butwaa baada ya wao na viongozi wengine wa Chama hicho Mkoa wa Iringa kudondoka chini baada ya jukwaa walilokuwa wamekaa kuanguka.
  Mkasa huo ulitokea katika Kata ya Mgama Iringa Vijijini majira ya saa 7:10 jana mchana wakati viongozi hao walipokwenda kukagua ujenzi wa chuo cha makada wa chama hicho katika eneo la Ihemi.
  Haikueleweka mara moja kama jukwaa hilo lilikaguliwa na oganaizesheni ya Chama hicho kabla ya kukaliwa na viongozi hao.
  Ujumbe wa viongozi hao ukiwa katika harakati za kutia saini kitabu cha wageni, jukwaa hilo liliachia sehemu ya chini na kuanguka jambo ambalo lilisababisha kizaazaa cha nani ajiokoe na nani aokolewe.
  Baadhi ya viongozi waliokuwepo katika jukwaa hilo ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Asery Masangi; Mbunge wa Kalenga, William Mgimwa na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Iringa, Abed Kiponza.
  Muda mfupi baada ya tukio hilo, wanachama wa CCM na watu wengine waliokuwepo walishuhudia viongozi hao wakiamka na kuhutubia bila kutumia jukwaa.
  Inadaiwa kuwa ujenzi wa jukwa hilo uligharimu Sh. 800,000.
   
 19. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa mimi hili la kutolea maamuzi ya ghafla jukwani ni sawa na zoezi la wananchi kujichukulia sheria mkononi, au polisi kuchukua uamuzi anapomshika mhalifu bila kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

  Ukiwa kiongozi wa nchi ufanye maamuzi kama hayo utaambiwa ni Dikteta, ndio maana mambo haya bora yawe na utaratibu wa kichama bila kumvunjia mtu heshima yake mbele ya hadhara, na lo lote litokealo ni jukumu la chama si mmoja tu wa viongozi wa chama.

  Kumbuka kutolea maamuzi ya ghafla jukwaani bila kukaa ofisini pamoja kujadiri na kupata hints baada ya kutulia kunamvunjia heshima yule anayetolewa kafara bila tuhuma kuthibitishwa, ni kumdhalilisha mbele ya hadhara na madhara yake kisaikolojia ni makubwa kuliko kama ingejengea radhi ya kuvumilia hadi suala liamuliwe katika kikao cha pamoja au angeitwa na kuambiwa hivyo ofisini kwako.
   
 20. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #20
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Candid, ukifikilia siasa za namna hii utaona kazi ya kuchukua nchi ilivyokuwa ngumu. Yaani hawataki wao kuwa ni alternative. Hivi ni demokrasia gani ipo hivyo? Wapi duniani kuna vituko vya hivi? Hapa wanataka gavana au watendaji wengine wathibitishwe na bunge ili kumpunguzia madaraka Rais lakini vitendo wafanyavyo ni vya kujilimbikizia madaraka.
  Kuna haja ya kunijanusua katika baadhi ya vitanzi, kwamba wenye maamuzi katika chama ni watu wachache. Kesho akisafiri Mbowe au Arfi na yeye anaweza kufanya hivyo? Hivi ziko wapi taratibu na kanuni za CHAMA. Kule Nzega hakuna uongozi kabisa. Yaani kesi inasikilizwa hapo na utetezi unafanyiwa tathmini kisha maamuzi. Huyu bwana angekuwa hakimu huenda wengi hata wasio na hatia wangejaa magerezani na kinyume chake.
   
Loading...