Dr. Slaa amrarua Dr. Kamara: Elimu yako umeshindwa kuitumia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa amrarua Dr. Kamara: Elimu yako umeshindwa kuitumia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Oct 21, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Katika mkutano wa jana ambao haujawahi kuonekana katika historia ya nchi hapo Mwanza, Dr.Slaa alimtolea uvivu Dr. Deriodoris Kamala ambaye alidai bei ya simenti kuwa shilingi 5,000/= haiwezakani na kutaingila makubaliano ya Afrika mashariki na kudhoofisha viwanda hapa nchini.

  Dr. Kamala ambaye hata sifa za udaktari wake zimekuwa zikitiliwa mashaka sana hivi sasa anamalizia uwaziri wake wa Afrika ya mashariki na ameshindwa hata kwenye kura za maoni ndani ya chama chake na hivyo hatakuwa waziri tena.

  Dr. Slaa alijibu hizo kombora kwa kuhoji kuwa Dr. kamala ameshindwa kutumia elimu yake katika kusaidia katika kuleta chachu ya maendeleo hapa nchini na ya kuwa bei ya shilingi elfu tano kwa mfuko wa simenti yawezakana.

  Linalohitajika ni kuondoa kodi zote kwenye mfuko huo wa simenti na kuwaagiza wahusika kuiuza kwa bei ambayo inazingatia hali hiyo.

  Habari za nyongeza soma majira ya leo
   
Loading...